
141
akimtibu (muktadha rasmi).
b) Chifu anawahutubia wanakijiji
(muktadha rasmi). c) Mwalimu
mkuu anawahutubia wanafunzi
kwenye gwaride (muktadha rasmi).
d) Wanafunzi wawili wanazungumza
(muktadha usio rasmi). Waelekeze
wanafunzi kutambua miktadha rasmi
na isiyo rasmi kutokana na michoro
waliyojadili.
• Wapange wanafunzi katika vikundi
vinne kisha kila kikundi kiigize
mazungumzo yanayoendelea katika
kila mchoro. Kila kikundi kiigize
mbele ya wanafunzi wenzao darasani.
Shughuli hii itakuza ujasiri wa
wanafunzi wa kuongea mbele ya watu
hivyo kujiamini na kujithamini zaidi.
Tathmini uigizaji wa kila kikundi.
Rekebisha matamshi na lugha isiyo
sahihi.
• Katika shughuli ya 2, waelekeze
wanafunzi katika vikundi vyao
wajadili kuhusu magonjwa matano
wanayofahamu, dalili zao, kinga zao
pamoja na hospitali wanazofahamu
zilizo karibu na shule yao. Tathmini
majadiliano ya wanafunzi.
• Waongoze wanafunzi wawiliwawili
kushiriki maigizo ya mazungumzo
katika miktadha waliyopewa
vitabuni mwao katika shughuli ya
3. Wanafunzi hawa waigize mbele ya
wenzao darasani. Tathmini uigizaji
na lugha yao. Hakikisha wanatumia
lugha rasmi kwa sababu miktadha
waliyopewa ni rasmi. Wanafunzi
wajadili maigizo ya wenzao pamoja
na lugha wanayotumia.
• Hitimisha somo hili kwa kumhimiza
mwanafunzi afanye kazi ya ziada
akisaidiwa na mzazi au mlezi wake.
Mwanafunzi atafiti kuhusu njia za
kuambukizwa ugonjwa wa korona,
dalili zake, kinga yake na njia za
kuudhibiti ugonjwa huo. Mwanafunzi
awasomee wenzake darasani maelezo
yake ili wayatathmini na kujifunza.
Majibu tarajiwa:
1. Njia za kuambukizwa ugonjwa wa
korona ni kama vile: Mgonjwa wa
korona anapokohoa au kupiga chafya
karibu nawe (iwapo hujavaa maski ya
uso), kugusa sehemu zilizo na virusi
vya korona kisha kujigusa kwenye
macho, mdomo au pua, kumgusa
mgonjwa wa korona kisha kujigusa
kwenye macho, mdomo au pua n.k.
2. Dalili za ugonjwa wa korona ni
kama vile: kuwa na joto jingi mwilini,
kukohoa, kupiga chafya, kuumwa
na kifua, kuumwa na koo, kupata
matatizo ya kupumua n.k.
3. Kinga za ugonjwa wa korona ni kama
vile: kunawa mikono kila wakati kwa
kutumia maji safi na sabuni, kutumia
kieuzi (‘sanitaiza’), kuvalia barakoa
(maski ya uso), kujizuia kuyagusa
macho yako, mdomo na pua, kukaa
mbali na watu, kutotangamana na
makundi ya watu wengi n.k.
4. Njia za kudhibiti ugonjwa wa korona
ni kama vile: kufika kwenye kituo cha
afya haraka iwezekanavyo ili kupata
dawa za kusaidia kupumua na kudhibiti
joto mwilini, kujitenga (kujikarantini)
na watu ili usiwaambukize virusi vya
korona, kupata ushauri nasaha n.k.