
35
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Shughuli nyingine zisizo rasmi zinazopendekezwa kuchangia ujifunzaji
a) Wanafunzi wanafanya mazoezi ya kuimba nyimbo, vitanzandimi, mashairi nje
na ndani ya darasa.
b) Wanafunzi wanafanya mazoezi ya kutamka heru na wenzao ndani na nje ya
darasa.
ch) Wanafunzi wanafanya mazoezi kutoa maombi mepesi katika njia ya maandishi.
d) Kusomea maktabani wakati wao wa ziada.
Tathmini zinazopendekezwa
a) Zoezi la kutenganisha silabi na sauti katika maneno.
b) Kuunda maneno na sentensi.
ch) Tathmini za wenzake, maswali/majibu, kusoma hadithi.
Nyenzo za ujifunzaji zinazopendekezwa
Rekodi za sauti, chati kwenye karatasi ngumu, nyenzo za kusikia na video, vitabu
vya hadithi, chati, picha, vitabu vya kusoma, magazeti, majarida, kanda za sauti, kadi
mulishi za maneno, vitabu n.k.
Kuwashughulikia wanafunzi wenye mahitaji maalum
Usaidizi kwa wanafunzi wenye
uwezo mbalimbali
Usaidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji
maalum
• Himiza wanafunzi wenye uelewa
wa polepole kushiriki katika
mazungumzo kama maigizo na
kusimulia hadithi.
• Wape wanafunzi wenye uelewa
wa haraka kazi nyingi ili kuepuka
kuwachosha na kuzubaa darasani.
• Wape wanafunzi wenye uelewa
wa polepole na haraka nafasi
za kutosha katika shughuli
za darasani. Una jukumu
la kuhakikisha kwamba
wanafurahiana na kufurahia
kukaa pamoja licha ya tofauti
zao.
• Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kuona,
wape breli, picha za kugusa na wale
wasioweza kuona vizuri wape maandishi
makubwa.
• Kwa wanafunzi wasio sikia vizuri tumia
lugha ishara au kumleta mtaalamu wa lugha
ishara kufasiri.
• Wanafunzi ambao hawawezi kuona mbali
wakae mbele darasani na wenye uwezo wa
kuona mbali wakae nyuma.
• Wape wanafunzi wenye ulemavu majukumu
wanayoweza kutekeleza kama vile kuigiza
nafasi ya mwalimu mkuu au balozi wa kijiji.
Wape usaidizi wa kutosha na kuhakikisha
kwamba wanafunzi wengine wanafanya
hivyo, kwa mfano, kuwasaidia katika
kusukuma kitimaguru kwa mwanafunzi
mlemavu.