Kusoma na Kuandika
katika Kiswahili
Gredi ya 1
Mwongozo wa Mwalimu
Henry T. Indindi
Danstone Khasiani
ii
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kimechapishwa na:
Longhorn Publishers Ltd.,
Barabara ya Funzi, Eneo la Viwandani,
S.L.P. 18033-00500,
Nairobi, Kenya.
Longhorn Publishers (Uganda) Ltd.,
Ploti 4, Eneo la Vubyabirenge, Ntinda,
S.L.P 24745
Kampala, Uganda.
Longhorn Publishers (Tanzania) Ltd.
Barabara Mpya ya Bagamoyo/Garden,
Mikocheni B, Ploti Namba: MKC/MCB/81
S.L.P 1237, Dar es Salaam, Tanzania.
Longhorn Publishers (Rwanda) Ltd.,
Remera mkabala na benki ya COGE
S.L.P 5910
Kigali, Rwanda.
© H. T. Indindi, D. Khasiani, 2018
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kupigisha chapa, kutafsiri au kukitoa
kitabu hiki kwa jinsi yoyote ile bila idhini, kwa maandishi, kutoka kwa Longhorn (K) Ltd.
Chapa ya kwanza 2018
ISBN978-9966-64-017-8
Kimepigwa chapa na Ramco Printing Works Ltd,
Unit 2, Ramco Industrial Complex,
Barabara ya Mombasa, Eneo la Viwandani,
S. L. P. 27750 - 00506, Nairobi.
iii
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Yaliyomo
Utangulizi ........................................................................................................... vii
Maazimio ya kazi..............................................................................................................ix
Mpangilio wa funzo .......................................................................................................... x
Sura ya 1: Ninajua maneno .................................................................................. 1
Wiki ya 1 ............................................................................................................... 4
Kipindi cha 1: Sikiliza maagizo........................................................................................ 4
Kipindi cha 2: Sikiliza na utende..................................................................................... 5
Kipindi cha 3: Imba wimbo wa vitendo ......................................................................... 6
Kipindi cha 4: Fanya mazoezi .......................................................................................... 8
Kipindi cha 5: Tambua na utamke heru....................................................................... 9
Wiki ya 2 .............................................................................................................10
Kipindi cha 1: Tambua sauti........................................................................................... 10
Kipindi cha 2: Unganisha sauti na maneno halisi....................................................... 11
Kipindi cha 3: Tenganisha silabi.................................................................................... 12
Kipindi cha 4: Soma kwa sauti.......................................................................................13
Kipindi cha 5: Tambua sauti na uzitumie.....................................................................14
Wiki ya 3 ..............................................................................................................16
iv
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 1: Andika heru kubwa na ndogo ........................................................... 16
Kipindi cha 2: Jinsi ya kuketi vizuri na kuandika........................................................17
Kipindi cha 3: Angalia tofauti........................................................................................ 18
Kipindi cha 4: Andika na utamke neno........................................................................19
Sura ya 2: Mwalimu Musa ...................................................................................20
Wiki ya 4 ..............................................................................................................23
Kipindi cha 1: Tambua na utamke sauti zifuatazo ...................................................... 23
Kipindi cha 2: Kuunganisha sauti ili kuunda maneno................................................25
Kipindi cha 3: Cheza mchezo ........................................................................................ 26
Kipindi cha 4: Kutenganisha na kubadilisha sauti ......................................................28
Kipindi cha 5: Mazungumzo na watu wengine ........................................................... 31
Wiki ya 5 ..............................................................................................................32
Kipindi cha 1: Kutambua heru na sauti...................................................................... 32
Kipindi cha 2: Mazungumzo na watu wengine ........................................................... 33
Kipindi cha 3: Unda maneno kutokana na silabi ........................................................ 34
Kipindi cha 4: Kuunda sentensi.....................................................................................35
Kipindi cha 5: Mchezo wa kutunga sentensi................................................................37
Sura ya 3: Kwa nini batamzinga ana madoadoa meupe.....................................39
Wiki ya 6 ..............................................................................................................42
Kipindi cha 1: Sikiliza hadithi........................................................................................ 42
v
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 2: Sikiliza na uigize..................................................................................... 43
Kipindi cha 3: Kuungana na watu wengine..................................................................45
Kipindi cha 4: Salamu .....................................................................................................46
Kipindi cha 5: Soma vifungu vifupi ..............................................................................48
Wiki ya 7 ..............................................................................................................49
Kipindi cha 1 na 2: Kuandika heru vizuri.................................................................. 49
Kipindi cha 3: Njia nzuri ya kukaa unapoandika........................................................50
Kipindi cha 4: Kutambua na kuweka heru kwenye makundi.................................. 51
Kipindi cha 5: Andika vyema......................................................................................... 52
Sura ya 4: Koome na magari yake .......................................................................54
Wiki ya 8 ..............................................................................................................57
Kipindi cha 1: Mazungumzo..........................................................................................57
Kipindi cha 2: Tamka maneno.......................................................................................58
Kipindi cha 3: Kusoma.................................................................................................... 59
Kipindi cha 4: Kujibu maswali ya hadithi ...................................................................60
Kipindi cha 5: Kutambua sauti ...................................................................................... 61
Wiki ya 9 ..............................................................................................................62
Kipindi cha 1: Tuzungumze ...........................................................................................62
Kipindi cha 2: Kuunda na kusoma maneno................................................................. 63
Kipindi cha 3: Tuzungumze ...........................................................................................65
Kipindi cha 4: Kutunga maneno....................................................................................66
vi
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 5: Kutazama picha na kusoma.................................................................. 67
Sura ya 5: Simba na panya...................................................................................69
Wiki ya 10 ............................................................................................................72
Kipindi cha 1: Kushiriki katika mazungumzo............................................................. 72
Kipindi cha 2: Shughli zangu za kila siku..................................................................... 73
Kipindi cha 3: Kusoma kwa sauti ..................................................................................74
Kipindi cha 4: Kujibu maswali kutoka kwa hadithi .................................................... 75
Kipindi cha 5: Kupimania muda....................................................................................76
Wiki ya 11 ............................................................................................................77
Kipindi cha 1: Kuzungumza kujihusu .......................................................................... 77
Kipindi cha 2: Kupangia siku yangu ............................................................................. 77
Kipindi cha 3: Kupanga mawazo................................................................................... 78
Kipindi cha 4: Kusoma.................................................................................................... 79
Kipindi cha 5: Maneno ya kuunganisha....................................................................... 80
Wiki ya 12 ............................................................................................................81
Kipindi cha 1: Kuzungumza na maraki......................................................................81
Kipindi cha 2: Kurekodi mawasiliano...........................................................................82
Kipindi cha 3: Kuandika sentensi.................................................................................. 83
Kipindi cha 4: Jinsi ya kupanga mambo....................................................................... 84
Kipindi cha 5: Kusoma sentensi ....................................................................................85
vii
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
UTANGULIZI
Lugha ya Kiswahili imepita mipaka ya Uswahilini, kusambaa na kutambaa katika
Afrika Mashariki, Kati na kwingineko. Ni wajibu wa mwalimu kuwahamasisha
wanafunzi wake kuipenda lugha ya Kiswahili kwani ina matumaini ya siku za usoni.
Mwalimu awahimize wanafunzi wake kuwa wanaweza kujiendeleza katika somo la
Kiswahili katika bahari pana ya maisha kama vile: redio, runinga, magazeti, ualimu,
tafsiri miongoni mwa nyanja anuwai.
Jukumu la lugha ya taifa ni kuweza kutambulisha watu wa taifa moja na kuwatia
hisia kuwa wanaungana na kutambulika. Lugha ni kitambulisho muhimu sana cha
watu wa jamii fulani. Lugha ya Kiswahili, kwa sababu ya kusambaa kwake kama moto
nyikani, msamiati wake ulio mzuri, utati uliofanyiwa lugha hii na idadi kubwa ya
watu wanaoizungumza ni thibitisho tosha kuwa lugha hii inapaswa kupewa nafasi
mwafaka kwani ndiyo lugha ya kutambulisha bara la Afrika katika ramani ya dunia.
Isitoshe, lugha ya Kiswahili inao wajibu wa kuleta mabadiliko ya kijamii, kisiasa
na kiuchumi katika bara la Afrika, ingawa Afrika ni bara ambalo limekumbwa na
matatizo si haba yakiwemo usadi, Ukimwi, ukabila, madeni ya kimataifa, umaskini
na kadhalika.
Malengo ya kufundisha Kiswahili katika shule za msingi
Malengo ya kufundisha Kiswahili katika shule za msingi kama
yanavyofafanuliwa na silabasi mpya ni kumwezesha mwanafunzi:
1. Kusikiliza na kuitikia vilivyo kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kuongea lugha ya Kiswahili kwa ufasaha.
3. Kusoma na kuelewa lugha ya Kiswahili.
4. Kujieleza kikamilifu kwa kuandika kwa lugha ya Kiswahili.
5. Kutunga kazi za kisanii kulingana na kiwango cha mwanafunzi.
6. Kuimarisha mazoea ya usomaji bora.
7. Kupenda na kujiendeleza katika somo la Kiswahili baada ya shule ya msingi.
8. Kuionea fahari na kuikuza lugha ya Kiswahili katika mawasiliano.
9. Kutukuza na kuendeleza Kiswahili sanifu maishani.
10. Kutathmini, kufurahia na kujivunia Kiswahili kama lugha ya taifa na kimataifa.
11. Kutambua na kushiriki katika kupata suluhisho la masuala ibuka yanayohusu
na kuathiri jamii kama vile: afya na Ukimwi, uadilifu, jinsia, mazingira na
teknolojia.
Jukumu la mwalimu katika kutimiza malengo haya
Ili kutimiza malengo haya, mwalimu wa Kiswahili ana wajibu muhimu. Mwalimu
viii
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
azingatie mazingira ya shule na kutoa mifano halisi ya vitu au watu wanaopatikana
katika mazingira ya shule. Kuna mazingira ya mjini na ya mashambani.
Mwalimu ana wajibu wa kujitayarisha mapema kabla ya somo lake kwa kuhakikisha
ana vifaa vya kutumia darasani ili kufanikisha somo lake. Vifaa hivi viwe vinapatikana
kwa urahisi au kwa bei rahisi iwapo ni vya kununuliwa.
Mwalimu anapaswa kutumia mwongozo huu na kitabu cha wanafunzi na rasilimali
yoyote itakayofanikisha kipindi chake. Mwalimu asitumie mwongozo huu kisisisi bali
awe mbunifu kulingana na uwezo wa wanafunzi wake na vifaa vinavyopatikana.
Mwalimu aanze kwa kufundisha dhana sahili kabla ya kufundisha zile changamano
zaidi. Si lazima afuate ukurasa hadi ukurasa. Lazima azingatie uwezo wa wanafunzi
wake.
Mwalimu anapaswa kuwashirikisha wanafunzi wake kadiri iwezekanavyo katika
somo la Kiswahili. Kwa kuwashirikisha, watakuza stadi zao za kusikiliza, kuongea,
kusoma na kuandika. Nyakati za kufundisha lugha ya Kiswahili ikiwa kavu zimepita
na yamkini hazitarudi!
Mifano anayotoa darasani iwe rahisi, sahihi, ya hali ya kila siku na inayoeleweka
kwa wanafunzi kuhusu mazingira yao na kuihusisha na masuala ibuka kama vile:
uadilifu, haki za watoto, Ukimwi, jinsia na teknolojia. Jukumu kubwa la mwalimu
ni kuwahamasisha wanafunzi kuongea, kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili kwa
ufasaha. Hili ni jukumu ambalo mwalimu yeyote wa Kiswahili hawezi kuepuka.
Lazima mwalimu awe kielelezo kwa wanafunzi wake kwa sababu wanafunzi
hupenda sana kuiga. Awe ni mtu anayeipenda lugha ya Kiswahili na kuionea fahari
ili awatie ari wanafunzi wake kuipenda lugha ya Kiswahili.
Mwalimu mwema ni yule anayejaribu kuwa katika kiwango cha wanafunzi.
Kama ni kuimba, wote wanaimba, kama ni kuigiza naye anaigiza. Mwalimu sharti
awe mchangamfu ili awachangamshe wanafunzi wake. Asifunze mambo au mada
kidhahania tu. Ataje matukio halisi maishani mwa wanafunzi huku akiwahusisha
katika kila hatua darasani. Mwongozo huu ni kama dira kwa mwalimu katika
kutekeleza mambo haya.
Mwalimu ajaribu kutumia rekodi za redio pamoja na video ili kuwavutia
wanafunzi mbali na kuendeleza stadi za kusikiliza na matamshi bora. Mwalimu
awahusishe wanafunzi katika kuchora picha, kuigiza darasani, kuimba, mijadala ili
somo la Kiswahili liwe hai. Mwalimu anaweza kuwaalika shuleni watu waliobobea
katika Kiswahili ili kuwahamasisha wanafunzi kuipenda na kuionea fahari lugha ya
Kiswahili.
Mbinu za kufundisha Kiswahili
Kuna mbinu kadhaa zinazoweza kutumiwa kufundisha somo la Kiswahili. Mwalimu
anashauriwa atumie mbinu kulingana na kiwango cha wanafunzi wake, uwezo wao,
ix
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
mazingira, rasilimali na vifaa vinavyopatikana. Kuna mbinu kama kuigiza, mjadala,
kuwaalika watu wenye ujuzi wa lugha ya Kiswahili (kama waandishi wa habari,
wahadhiri, malenga, watangazaji) na kadhalika. Mbinu ya jadi ni maswali na majibu
lakini bado inatumiwa hasa kutathmini wanafunzi darasani. Michoro au kuunda
picha za vitu mbalimbali na kuwapanga wanafunzi katika vikundi ni mbinu nyingine.
Mwalimu akumbuke kuwa kila mbinu ina faida na upungufu wake. Mwalimu atumie
mbinu inayofaa zaidi na rahisi kwa wanafunzi ili kueleza dhana inayohusika.
Kazi za wanafunzi
Sharti mwalimu awashirikishe wanafunzi katika somo la Kiswahili. Baadhi ya
shughuli za wanafunzi ni:
Kujibu na kuuliza maswali darasani.
Kusoma makala katika kitabu.
Kujadiliana darasani, kusimuliana hadithi na kukariri mashairi.
Kuchora vifaa mbalimbali.
Kuigiza watu mbalimbali.
Kusikiliza wenzao wakisoma, wakiongea au wataalamu walioalikwa.
Kuandika majibu ya maswali mbalimbali.
Vifaa vya kufundisha lugha ya Kiswahili
Mwalimu anaweza kutumia vifaa kama vile:
Kadi Mabango Vifaa halisi vinavyoweza kupatikana
kwa urahisi
Michoro Picha Tarakilishi
Redio Vitabu
Maazimio ya kazi
Kwa kawaida, mwalimu huandaa maazimio ya kazi baada ya kupokea silabasi
inayoeleza mada zinazotakiwa kufunzwa katika darasa fulani kwa mwaka mmoja.
Mwalimu sharti ajue sehemu mbalimbali za silabasi na malengo ya somo la Kiswahili
kwa ujumla. Kisha apange mada zake kwa mtiririko kutoka sahili hadi changamano.
Mwalimu apange na kutayarisha maazimio yake ya kazi mwanzo wa muhula hasa
wiki ya kwanza au hata wakati wa likizo.
Maazimio ya kazi humwezesha mwalimu kuandaa vifaa vyake na kupanga
ufundishaji wake kimantiki bila kuhangaika. Isitoshe, maazimio ya kazi humwezesha
mwalimu wa Kiswahili kuhitimisha mada zilizopo katika silabasi kwa muda
zilizotengewa.
x
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Mfano wa maazimio ya kazi
Darasa: Gredi ya
Kwanza
Somo: Kiswahili Jina: YOHANA
MKUKI
Muhula: Wa kwanza Mwaka: 2017
Wiki Kipindi Mada Malengo Nyenzo Shughuli
za darasani
Tathmini Marejeleo Maoni
1 3 Msamiati Mwanafunzi
aweze:
a) Kutaja
vifaa vya
darasani.
b) Kutunga
sentensi
kwa
kutumia
majina ya
vifaa vya
darasani.
Michoro
Vifaa
halisi
Kutaja vifaa
Kutunga
sentensi
Kujibu
maswali
Kutunga
sentensi
Kitabu cha
Mwanafunzi
ukurasa
11-15
Mpangilio wa funzo
Kwa kawaida, mpangilio wa funzo hutayarishwa kutoka kwenye maazimio ya
kazi. Huu ni uandalizi wa awali kabla ya kuingia darasani kufundisha. Mwalimu
anayeingia darasani kufundisha bila mpangilio wa funzo hawezi kutekeleza wajibu
wake ipasavyo kwani hajui aanzie wapi na amalizie wapi. Mpangilio wa funzo ni dira
inayomwongoza mwalimu darasani. Humwezesha mwalimu kukamilisha mada yake
kwa muda uliotengwa bila kwenda kombo, pia huchangia katika kujiamini akiwa
darasani. Aidha, humwezesha kutafuta vifaa na vielelezo vingine atakavyotumia na
kuhusisha somo na lile lililopita iwapo panahitajika.
Wakati wa utayarishaji wa mpangilio wa funzo, sharti mwalimu akumbuke uwezo
wa wanafunzi wake, vifaa vinavyopatikana na muda uliotengewa kipindi fulani.
Aidha, sharti awashirikishe wanafunzi katika shughuli mbalimbali huku akionyesha
kazi zake zitakazofanikisha kipindi. Kazi za mwalimu na wanafunzi ziende sambamba.
Kwa mfano, mwalimu akitaja mifano, nao wanafunzi washirikishwe kutaja.
Mwalimu atumie ubao ipasavyo kwa kuelezea hoja muhimu katika somo. Ufuatao
ni mfano tu wa mpangilio wa funzo katika darasa la kwanza.
xi
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Mfano wa mpangilio wa funzo
TAREHE WAKATI GREDI SOMO IDADI
12.10.17 8.00 - 8.30 1 KISWAHILI 30
Funzo: Msamiati
Mada: Vifaa vya darasani
Malengo: Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze:
(a) Kutambua vifaa vya darasani.
(b) Kutunga sentensi akitumia majina ya vifaa vya darasani.
Marejeleo: Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 11-15
Mwongozo wa Mwalimu, ukurasa 10-14.
Maendelezo ya funzo
Mwalimu awaulize wanafunzi
majina ya vifaa darasani. Mwalimu
awaambie wataje vifaa wanavyoona
kwenye mchoro.
Mwalimu awape wanafunzi fursa ya
kutunga sentensi kuhusu vifaa vya
darasani.
Mwalimu arejelee somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali.
Awape mazoezi zaidi kuhusu vifaa
vya darasani.
Wanafunzi wataje vifaa
wanavyoona darasani, kwa
mfano: rula, ubao n.k.
Wanafunzi watunge sentensi
sahihi wakitumia majina ya
vifaa vya darasani.
Wanafunzi wajibu maswali.
Wanakili mazoezi zaidi katika
madaari yao.
Dakika 5Hitimisho
Kiini Dakika
20
Hatua Muda Kazi ya Mwalimu Kazi ya Mwanafunzi
Ufundishaji wa mada mbalimbali
(i) Ufahamu
Kufunza somo la ufahamu barabara kama yalivyo masomo mengine kunahitaji
mwalimu afanye matayarisho ya kutosha kabla ya kipindi. Mwalimu anapaswa
kufahamu barabara maana ya maneno au msamiati unaotumiwa katika taarifa.
Utangulizi Dakika
5
xii
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Mwalimu anaweza kuanza kwa kuwauliza wanafunzi maana ya baadhi ya maneno
kabla ya kusoma makala yenyewe. Kisha anaweza kuwaeleza maneno magumu
watakayokumbana nayo katika kifungu. Wanafunzi washirikishwe kutunga sentensi
wakitumia maneno hayo. Mwalimu asahihishe makosa pindi yanapotokea.
Mwalimu anaweza kuanza kusoma sentensi za kwanza mbili au tatu hivi.
Mwalimu daima akumbuke kuwa yeye ni kielelezo na hana budi kujizatiti katika
matamshi bora. Kisha awaongoze wanafunzi kuisoma taarifa, kwa makini huku kila
mwanafunzi akipata nafasi ya kuisoma. Mwalimu aandike maneno magumu ubaoni
huku akiwaongoza kuyatamka. Kisha awaeleze maana na matumizi yake.
(ii) Saru
Saru kwa ujumla ni utaratibu, kanuni au sheria zinazotawala matumizi na matamshi
ya maneno, maumbo ya maneno na miundo ya sentensi katika lugha fulani. Saru
ya Kiswahili ni pana, yamkini imetawaliwa na ngeli. Ngeli ni kundi moja la majina
yaliyo na upatanisho sawa wa kisaru na viambishi sawa vya umoja na wingi. Kwa
mfano:
Mtu anakuja
Watu wanakuja
Mara nyingi, wanafunzi hawalichangamkii somo la saru, lakini likifunzwa kwa
kuhusishwa na masomo mengine na kutumia vifaa halisi na michoro, linaweza kuwa
somo la kuvutia mno.
(iii) Msamiati
Msamiati ni jumla ya maneno yanayopatikana katika lugha fulani. Msamiati unaweza
kufunzwa kwa kuhusishwa na masomo mengine kama vile saru au ufahamu.
Mwalimu anapofundisha msamiati sharti akumbuke kuwa neno moja linaweza kuwa
na maana zaidi ya moja. Kwa hivyo, ni vyema kuliweka neno katika muktadha wa
matumizi yake.
(iv) Kusoma na kuandika
Kusoma ni stadi moja ambayo inatiliwa mkazo mno katika silabasi mpya, kusoma
kwa ufasaha ni tathmini ya kuonyesha kuwa mtu ameimudu lugha husika. Mwalimu
awaongoze wanafunzi kusoma makala ya kila aina kama ufahamu, magazeti na
mashairi.
Mwalimu awaeleze wanafunzi maana ya ushairi. Anaweza kuanza kwa kuwauliza
wataje mifano ya wimbo au nyimbo wanazozifahamu. Kisha anaweza kuwaelezea
shairi kama mtungo wa kisanaa ni kama wimbo wenye mpangilio maalum wa lugha
unaoelezea wazo fulani kuhusu maisha ya binadamu.
xiii
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Tathmini
Kutathmini ni shughuli inayoendelea katika mfumo wa elimu. Kutathmini ni jambo
lisiloepukika katika elimu kwa sababu ufundishaji wa Kiswahili au somo jingine
hauwezi kuwa kamilifu bila kutathmini. Kupitia tathmini mwalimu anaweza kuelewa
udhaifu na uwezo wa wanafunzi wake. Kuna mbinu kadhaa za kutathmini kama
kuuliza na kujibiwa maswali darasani, kusoma, kuandika na kusimulia hadithi.
Katika kutathmini, mwalimu atumie mbinu inayofaa wanafunzi wake ili kupima
stadi husika kama kusoma, kuandika, kusikiliza, ufahamu, saru na kuzungumza.
Tunatarajia kuwa mwongozo huu utakuwa dira mufti kwa mwalimu
anapowaongoza wanafunzi katika safari ya kuiendeleza na kuikuza lugha ya Kiswahili.
xiv
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
1
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Sura ya
1
Ninajua maneno
(Kitabu cha mwanafunzi ukurasa 1–34)
Matokeo yanayotarajiwa ya mafunzo
KUSIKILIZA KUZUNGUMZA KUSOMA KUANDIKA
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kusikiliza kwa
makini maagizo na
maswali mbalimbali
yanayotolewa.
b) kujibu ifaavyo
na kwa ujasiri
maagizo na maswali
yaliyotolewa.
c) kutumia maneno
na kauli mwafaka
za kimaadili katika
kutoa na kujibu
maagizo na maswali.
d) kutumia msamiati
aliojifunza kutoa
maagizo na kuuliza
maswali.
e) kutambua umuhimu
wa kutoa na kujibu
maagizo na maswali
ifaavyo.
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kujibu kwa
ujasiri maswali
na maagizo
ya kuongea
kutoka kwa vifaa
mbalimbali.
b) kutumia maneno
mwafaka katika
kutoa maagizo
na maswali.
c) kutambua
umuhimu wa
kujibu maagizo
na maswali
ifaavyo.
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kufanya mazoezi
ya kupeleka macho
kushoto na kulia
kwa makini.
b) kutenganisha sauti
katika maneno.
c) kutenganisha
maneno
yanayoanza kwa
sauti zinazofanana.
d) kutambua heru
zote za abjadi/
alfabeti katika
uwanja wa lugha.
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kuandika heru
kubwa na ndogo
ifaavyo.
b) kutofautisha
heru
zinazoonekana
kufanana (bdp
(w, vym) (k)(ch)
na makundi ya
konsonanti.
d) kupenda
kuandika majina
katika heru
kubwa na ndogo
ifaavyo.
e) kuandika kwa
mkono heru,
namba na ishara.
2
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Umilisi mkuu unaokuzwa:
Mawasiliano na ushirikiano:
a) Wanafunzi wanafanya mazoezi ya kupeana maagizo mepesi na kujibu maagizo
na maswali katika vikundi au wakiwa wawili wawili.
b) Wanafunzi wanachanganya na kutenganisha maneno mapya.
Umilisi wa kidijitali:
a) Wanafunzi wanajirekodi kwa kutumia vifaa vya kidijitali kama vile simu.
Masuala ya mtambuko:
a) Stadi za maisha zinaendelezwa wanapojifunza kujithamini na kuwa jasiri.
Aidha, wanapata ujuzi wa kukaa na kuwasiliana na wenzao katika kazi za
pamoja.
b) Wanafunzi katika vikundi wanacheza michezo itakayowasaidia kuimarisha
afya zao na viungo vya mwili.
Uhusiano na thamani za kitaifa:
Kunajengwa heshima na uwajibikaji
Uhusiano na masomo mengine:
Wakijigawa katika idadi maalumu za vikundi, wanadhihirisha uhusiano na
somo la Mathematical Activities.
Mapendekezo ya Huduma za Kijamii za Ujifunzaji
1. Wanafunzi wanatoa na kujibu maagizo mepesi kutoka kwa wanajamii.
2. Wanafunzi wanafanya mazoezi ya kusoma sauti na kuandika maneno na
wenzao walio nyumbani.
3. Wanafunzi wanafanya mazoezi ya kuandika wakiwa nyumbani.
4. Wanafunzi wanafanya mazoezi ya kuuliza maswali na kupeana maagizo na
wenzao nyumbani.
Shughuli nyingine zisizo rasmi zinazoweza kuchangia ujifunzaji:
1. Wanafunzi wanajifunza kupeana na kujibu maagizo mepesi na wenzao.
2. Wanafunzi wanajifunza kutamka maneno wakicheza na wenzao.
3. Wanafunzi wanashirikiana kutazama maandishi yao pamoja na wenzao.
4. Wanafunzi wanajifunza kupeana na kupokea maagizo mepesi wakiwa na
wenzao.
3
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Tathmini zinazopendekezwa:
1. Maswali na majibu katika kuongea.
2. Wanafunzi wanajifunza kusoma sauti, silabi na maneno huku wakizingatia
matamshi bora.
3. Kujenga familia za maneno kama vile maneno ya silabi mbili au tatu.
4. Kushiriki kwa kucheza.
Nyenzo za kujifunzia:
Chati zilizo na maneno ya maagizo na maswali, vifaa vya rekodi za sauti au video
(kanda, video, simu), chati za maneno, sauti kutoka kwa mazingira, penseli, vitabu,
kadi, majedwali ya maneno, penseli za rangi, kadi za maandishi, kanda za sauti na
video, wageni waalikwa, viongozi wa kijamii.
Kuwashughulikia wanafunzi wenye mahitaji maalum
Usaidizi kwa wanafunzi wenye uwezo
mbalimbali
Usaidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji
maalum
Himiza wanafunzi wenye uelewa
wa polepole kushiriki katika
mazungumzo kama maigizo na
kusimulia hadithi.
Wape wanafunzi wenye uelewa
wa haraka kazi nyingi ili kuepuka
kuwachosha na kuzubaa darasani.
Wape wanafunzi wenye uelewa wa
polepole na haraka nafasi za kutosha
katika shughuli za darasani. Una
jukumu la kuhakikisha kwamba
wanafurahiana na kufurahia kukaa
pamoja licha ya tofauti zao.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa
kuona, wape breli, picha za kugusa
na wale wasioweza kuona vizuri
wape maandishi makubwa.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa
kusikia vizuri tumia lugha ishara au
kumleta mtaalamu wa lugha ishara
kufasiri.
Wanafunzi ambao hawawezi kuona
mbali wakae mbele darasani na wenye
uwezo wa kuona mbali wakae nyuma.
Wape wanafunzi wenye ulemavu
majukumu wanayoweza kutekeleza
kama vile kuigiza nafasi ya mwalimu
mkuu au balozi wa kijiji. Wape
usaidizi wa kutosha na kuhakikisha
kwamba wanafunzi wengine
wanafanya hivyo, kwa mfano, kusaidia
katika kusukuma kitimagurudumu
cha mwanafunzi mlemavu.
4
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Wiki ya 1
Mpangilio wa vipindi
Kipindi cha 1: Sikiliza maagizo
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kusikiliza kwa makini maagizo na
maswali mepesi yakitolewa.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza, hasa
zile zilizo chini ya (Somo 1.1 (kusikiliza maagizo na maswali). Mwalimu awape
wanafunzi kauli na vifungu vinavyotoa maagizo kisha wanafunzi wamuige katika
vikundi, wakiwa wawili wawili au akiwa peke yake. Jitahidi kuunganisha kusoma na
kuandika katika kipindi kwa kutumia mikutadha ya kufaa.
Nyenzo za kujifunzia
Chati zilizo na maneno ya maagizo na maswali.
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwauliza wanafunzi kutazama picha katika Kitabu cha
Mwanafunzi ukurasa wa 1.
Tandaza chati zilizo na maneno ya maagizo na maswali.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kutazama picha katika Kitabu cha Mwanafunzi. Katika
vikundi, wanafunzi wajadiliane wanachokiona.
2. Waweke wanafunzi katika vikundi na uwaelekeze kusoma mazungumzo kati ya
Annet na mwalimu.
3. Waelekeze wanafunzi kupeana maagizo huku ukirekodi.
4. Waelekeze wanafunzi kusikiliza kanda iliyorekodiwa.
Baadhi ya majibu
Jaza mapengo
2. Jaza mapengo kwa maneno sahihi.
a. {Jina} langu ni ……………………..(mwanafunzi aseme jina lake)
5
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
b. Babako anaitwa nani?
Jina {la} babangu ni ………………… (mwanafunzi aseme jina la babake)
c. Mamako anaitwa nani?
Mamangu anaitwa…………………… (mwanafunzi aseme jina la mamake)
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Hili litakuza mawasiliano na kushirikiana miongoni mwa wanafunzi ili kutoa sifa za
heshima na umoja wakishirikiana na wenzao katika shughuli za darasani.
Tathmini
Zoezi la nyumbani
Waambie wenzako au wazazi kukupa maagizo na maswali katika kuongea na
kubadilishana nafasi.
Kwa mfano: Gusa kichwa chako.
Gusa masikio yako.
Inua mikono yako.
Kipindi cha 2: Sikiliza na utende
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi mwanafunzi aweze kujibu ifaavyo na kwa ujasiri aina
mbalimbali za maagizo mepesi na maswali.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kiwawezeshe wanafunzi kujua nyenzo mbalimbali za kusikiliza. Wape
wanafunzi muda wa kutosha kufanya mazoezi ya kutoa majibu tofauti tofauti kwa
maagizo na maswali ifaavyo kutumia njia ya mazungumzo au ishara ya ana kwa ana
kisha uwasahihishe ipasavyo. Kipindi hiki kinashughulikia stadi za kusikiliza na
kuzungumza chini ya Somo 1.1. Hata hivyo, juhudi zifanyike kuunganisha stadi za
kusoma na kusikiliza katika kipindi kwa kutumia mikutadha mwafaka.
Nyenzo za ujifunzaji
Chati
Vifaa vya kurekodi za sauti na video
6
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwauliza wanafunzi kuiangalia picha kisha kutoa maagizo
ambayo wao husikia yakitolewa shuleni.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kuangalia Kitabu cha Mwanafunzi na uwaagize kusoma
mazungumzo kati ya baba na mwanawe.
2. Katika vikundi vya wawili wawili, wanafunzi waigize mazungumzo baina ya
baba na mwanawe.
3. Wanafunzi wasikilize rekodi ya seneta wao wa darasa akipeana maagizo.
Majibu sahihi
1. Tafadhali
2. Letea
3. Asante
4. Hapa
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Kipindi hiki kitakuza stadi ya maisha katika kujua jinsi ya kuishi na wanafunzi wengine
kutokana na mawasiliano mema. Hivyo basi, hakikisha kwamba kila mwanafunzi
anashiriki katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha mawasiliano, ushirikiano na umoja.
Tathmini
Waagize wanafunzi kujibu maswali ya zoezi la kufanyia nyumbani katika Kitabu cha
Mwanafunzi.
Kipindi cha 3: Imba wimbo wa vitendo
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi hiki, mwanafunzi aweze kujibu kwa ujasiri maswali mepesi
katika mazungumzo na maagizio kutoka kwa kifaa chochote cha mawasiliano.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza, hasa
zile zilizo chini ya (Somo 1.1 (kusikiliza maagizo na maswali). Mwalimu awape
7
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
wanafunzi kauli na vifungu vinavyotoa maagizo kisha wanafunzi wamuige katika
vikundi, wakiwa wawili wawili au akiwa peke yake. Jitahidi kuunganisha kusoma na
kuandika katika kipindi kwa kutumia mikutadha ya kufaa.
Nyenzo zinazopendekezwa
Vifaa vya kurekodi sauti na video
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kucheza rekodi au kuimba wimbo ulio katika Kitabu cha
Mwanafunzi ukurasa wa 6
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kuelekeza kidole kwenye namba huku ukikariri au
kuimba wimbo.
2. Katika vikundi vya wawili wawili, waruhusu wanafunzi kuweka kidole
kwenye sauti huku ukiwasomea sauti katika zoezi la 1(2).
3. Huku ukiwaelekeza, waruhusu wanafunzi katika vikundi vya wawili wawili
kusoma sauti na maneno.
4. Waelekeze wanafunzi kutambua sauti na kusoma maneno.
5. Waelekeze wanafunzi wakilishughulikia zoezi hilo katika vikundi vya wawili
wawili.
6. Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Kipindi hiki kitakuza stadi ya maisha katika kujua jinsi ya kuishi na wanafunzi wengine
kutokana na mawasiliano mema. Hivyo basi, hakikisha kwamba kila mwanafunzi
anashiriki katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha mawasiliano, ushirikiano na umoja.
Tathmini
Zoezi la nyumbani
Waagize wanafunzi kujibu maswali ya zoezi la nyumbani katika Kitabu cha Mwanafunzi.
Waagize wanafunzi kufanya mazoezi ya kutamka sauti na kusoma maneno na watu
walio nyumbani.
8
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 4: Fanya mazoezi na urekodi
Kusikiliza maagizo
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kutumia maneno mwafaka katika kutoa
na kujibu maagizo na majibu.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza, hasa
zile zilizo chini ya (Somo 1.1 (kusikiliza maagizo na maswali). Mwalimu awape
wanafunzi kauli na vifungu vinavyotoa maagizo kisha wanafunzi wamuige katika
vikundi, wakiwa wawili wawili au akiwa peke yake. Jitahidi kuunganisha kusoma na
kuandika katika kipindi kwa kutumia mikutadha mwafaka.
Nyenzo za kujifunzia
Vifaa vya kurekodi sauti na video
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuwaagiza wanafunzi kuimba wimbo ulio katika Kitabu
cha Mwanafunzi ukurasa wa 9 huku wanafunzi wakijirekodi.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kuimba wimbo katika Kitabu cha Mwanafunzi ukurasa
wa 9.
2. Cheza wimbo uliorekodiwa darasani huku wakisikiliza.
3. Wahimize wanafunzi kuuliza maswali ikihitajika.
Tathmini
Wanafunzi wafanye zoezi la nyumbani katika Kitabu cha Mwanafunzi.
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Kipindi hiki kitakuza mawasiliano na ushirikiano miongoni mwa wanafunzi na
kukuza maadili kama vile heshima na umoja wanapotangamana katika kazi za
makundi darasani.
9
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 5: Tambua na utamke heru
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kufanya mazoezi ya kutembeza jicho
kushoto na kulia kwa uangalifu.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza, hasa
zile zilizo chini ya (Somo la 3.1 (kusikiliza maagizo na maswali). Jitahidi kuunganisha
kusoma na kuandika katika kipindi kwa kutumia mikutadha mwafaka.
Nyenzo zinazopendekezwa
Vifaa vilivyorekodiwa vya sauti na video
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kusoma sauti na maneno huku wanafunzi wakiiga.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kutamka maneno ifaavyo.
2. Katika vikundi vya wawili wawili, waruhusu wanafunzi kuweka alama zao
kwenye maneno huku ukisoma shairi katika zoezi la 2.
3. Huku ukiwaelekeza, waruhusu wanafunzi katika vikundi vya wawili wawili
kutambua maneno huku wenzao wakisoma shairi.
4. Waelekeze wanafunzi kutambua maneno huku wakisoma shairi.
5. Waelekeze wanafunzi kulishughulikia zoezi katika vikundi vya wawili wawili.
6. Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Hitimisho
Kipindi hiki kitakuza stadi ya maisha katika kujua jinsi ya kuishi na wanafunzi wengine
kutokana na mawasiliano mema. Hivyo basi, hakikisha kwamba kila mwanafunzi
anashiriki katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha mawasiliano, ushirikiano na umoja.
Tathmini
Wanafunzi wafanye mazoezi ya kusoma na wenzao wakiwa nyumbani.
10
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Zoezi la nyumbani
Waagize wanafunzi kujibu maswali ya zoezi la nyumbani katika Kitabu cha Mwanafunzi.
Waagize wanafunzi kufanya mazoezi ya kutamka sauti na kusoma maneno na watu
walio nyumbani.
Wiki ya 2
Kipindi cha 1: Tambua sauti
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, wanafunzi waweze kutenganisha sauti na silabi katika
neno.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kiwawezeshe wanafunzi kupata umilisi mbalimbali wa hijai na maendelezo
ya maneno. Wanafunzi waelekezwe kutenganisha sauti katika maneno.
Nyenzo za kujifunzia
Chati ya maneno
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kutandaza chati ya maneno, na katika chati hiyo ya maneno
tambua maneno mepesi na sauti zake. Hakikisha kwamba inaonekana na kuvutia hata
kwa mbali.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waagize wanafunzi kujaribu kusoma chati.
2. Omba wanafunzi kutambua konsonanti na vokali katika chati.
3. Himiza kushiriki kwa wanafunzi.
4. Katika vikundi vya wawili wawili, waelekeze kushughulikia zoezi la 2 na 3.
5. Hakikisha kwamba wanafunzi wote wanashiriki.
11
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Hitimisho
Uliza wanafunzi kueleza walichojifunza katika kipindi. Waeleze wanafunzi kuwa
sauti na silabi huunda maneno ambayo sisi hutumia kwa mazungumzo na hivyo
kuwa na lugha. Kipindi hiki kitakuza stadi ya maisha katika kujua jinsi ya kuishi na
wanafunzi wengine kutokana na mawasiliano mema. Hivyo basi, hakikisha kwamba
kila mwanafunzi anashiriki katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha mawasiliano,
ushirikiano na umoja.
Tathmini
Waulize wanafunzi kufanya mazoezi ya utamkaji wa sauti na kusoma maneno wakiwa
na watu wengine nyumbani.
Kipindi cha 2: Unganisha sauti na maneno halisi
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi hiki, mwanafunzi aweze kutenganisha na kupanga maneno
yanayoanza kwa sauti zinazofanana.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kiwawezeshe wanafunzi kupata umilisi mbalimbali wa hijai na maendelezo
ya maneno. Wanafunzi waelekezwe kutenganisha sauti katika maneno na kutambua
maneno yanayoanza kwa sauti sawa.
Nyenzo za ujifunzaji
Chati ya maneno
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kutandaza chati ya maneno, na katika chati hiyo ya maneno
tambua maneno mepesi na sauti zake. Hakikisha kwamba inaonekana na kuvutia hata
kwa mbali.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waagize wanafunzi kujaribu kusoma chati.
2. Omba wahisani kutambua konsonanti na vokali katika chati.
12
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
3. Himiza kushiriki kwa wanafunzi.
4. Katika vikundi vya wawili wawili, waelekeze kufanya zoezi la 2.
5. Hakikisha kwamba wanafunzi wote wanashiriki.
6. Waelekeze wanafunzi kuchunguza na kusoma sentensi zinazoambatana na
picha.
Zoezi la nyumbani
Katika Kitabu cha Mwanafunzi ukurasa wa 18.
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Kipindi hiki kitakuza mawasiliano na ushirikiano miongoni mwa wanafunzi na
kukuza maadili kama vile heshima na umoja wakitangamana katika shughuli za
darasani.
Kipindi cha 3: Tenganisha silabi
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kutenganisha sauti katika neno.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kiwawezeshe wanafunzi kupata umilisi mbalimbali wa hijai na maendelezo
ya maneno. Wanafunzi waelekezwe kutenganisha sauti katika maneno.
Nyenzo za ujifunzaji
Chati ya maneno
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kutandaza chati ya maneno, na katika chati hiyo ya maneno
tambua maneno mepesi na sauti zake. Hakikisha kwamba inaonekana na kuvutia ata
kwa mbali.
Mwalimu anaweza kutumia jedwali katika Kitabu cha Mwalimu kama mfano.
13
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Shughuli za ujifunzaji
1. Waagize wanafunzi kujaribu kusoma chati.
2. Omba wanafunzi kutambua konsonanti na vokali katika chati.
3. Himiza kushiriki kwa wanafunzi.
4. Katika vikundi vya wawili wawili, waelekeze kufanya zoezi la 1–4.
5. Hakikisha kwamba wanafunzi wote wanashiriki.
Hitimisho
Waulize wanafunzi kutaja walichojifunza katika kipindi hicho. Waeleze wanafunzi kuwa
sauti huunda maneno tunayozungumza na hivyo ndivyo lugha huundwa. Kipindi hiki
kitakuza stadi ya maisha katika kujua jinsi ya kuishi na wanafunzi wengine kutokana
na mawasiliano mema. Hivyo basi, hakikisha kwamba kila mwanafunzi anashiriki
katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha mawasiliano, ushirikiano na umoja.
Tathmini
Wanafunzi wafanye zoezi la nyumbani katika Kitabu cha Wanafunzi ukurasa wa 21.
Mwagize mwanafunzi kufanya mazoezi ya kutamka sauti na kusoma maneno pamoja
na wenzake nyumbani.
Kipindi cha 4: Soma kwa sauti
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kufanya mazoezi ya kutembeza macho
kushoto na kulia kwa makini.
Hadithi za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza,
hasa zile zilizo chini ya (Somo la 3.1 (kusikiliza maagizo na maswali). Jitahidi
kuunganisha kusoma na kuandika katika kipindi kwa kutumia mikutadha mwafaka.
14
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Nyenzo zinazopendekezwa
Vifaa vya kurekodi sauti na video
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuandika ubaoni sentensi zinazofanana na zile zilizo katika
Kitabu cha Mwanafunzi, kuzisoma huku wanafunzi wakiigiza.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kusoma sentensi ifaavyo.
2. Katika vikundi vya wawili wawili, waruhusu wanafunzi kusoma sentensi.
3. Waelekeze wanafunzi katika vikundi vya wawili wawili kusoma shairi.
4. Waelekeze wanafunzi kutambua maneno huku wakisoma shairi.
5. Waelekeze wanafunzi kulishughulikia zoezi hilo katika vikundi vya wawili
wawili.
6. Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Hitimisho
Kipindi hiki kitakuza stadi ya maisha katika kujua jinsi ya kuishi na wanafunzi wengine
kutokana na mawasiliano mema. Hivyo basi, hakikisha kwamba kila mwanafunzi
anashiriki katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha mawasiliano, ushirikiano na umoja.
Zoezi la nyumbani
Waagize wanafunzi kufanya zoezi la nyumbani katika Kitabu cha Mwanafunzi ukurasa
wa 24.
Tathmini
Wanafunzi wafanye mazoezi ya kusoma na wenzao wakiwa nyumbani.
Kipindi cha 5: Tambua sauti na uzitumie
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kutambua heru zote za abjadi/alfabeti
katika lugha ya mazingira yao.
15
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Habari za kimsingi
Tambua heru za alfabeti/abjadi katika lugha ya eneo husika.
Nyenzo za kujifunzia
Chati ya maneno
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kutandaza chati ya maneno, na katika chati hiyo ya maneno
tambua maneno mepesi na sauti zake. Hakikisha kwamba inaonekana na kuvutia hata
kwa mbali.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waagize wanafunzi kujaribu kusoma chati.
2. Omba wanafunzi kutambua konsonanti na vokali katika chati.
3. Himiza kushiriki kwa wanafunzi.
4. Katika vikundi vya wawili wawili, waelekeze kufanya mazoezi yaliyo katika
Kitabu cha Mwanafunzi.
5. Hakikisha kwamba wanafunzi wote wameshiriki.
Hitimisho
Waulize wanafunzi kutaja walichojifunza kutoka katika kipindi hicho.
Waeleze wanafunzi kwamba sauti huunda maneno tunayozungumza na hivyo basi
kuunda lugha.
Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Kipindi hiki kitakuza stadi ya maisha katika kujua jinsi ya kuishi na wanafunzi
wengine kutokana na mawasiliano mema. Hivyo basi, hakikisha kwamba kila
mwanafunzi anashiriki katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha mawasiliano,
ushirikiano na umoja.
Tathmini
Mwagize mwanafunzi kufanya mazoezi ya kutamka sauti na kutamka maneno na
wenzake walio nyumbani.
16
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Wiki ya 3
Kipindi cha 1: Kuandika heru kubwa na ndogo
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, wanafunzi waweze kuandika heru kubwa na ndogo
ifaavyo.
Habari za kimsingi
Katika kipindi hiki, wanafunzi waweze kutekeleza maarifa ya kuandika heru ili
waweze kuandika heru kwa njia sa na kuonekana vizuri.
Nyenzo za kujifunzia
Penseli Vitabu Kadi Penseli za rangi Chati
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kutandaza chati iliyo na heru zote za abjadi/alfabeti katika
heru kubwa na ndogo.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waagize wanafunzi kusoma heru katika chati.
2. Waelekeze wanafunzi kufanya zoezi la 1 na 2 wakiwa katika vikundi vidogo au
wawili wawili.
3. Katika kipindi hiki, wanafunzi watajifunza kuhusu mwandiko.
Hitimisho
Kwanza, hakikisha wanafunzi wameandika majina. Kipindi hiki kitakuza stadi ya
maisha katika kujua jinsi ya kuishi na wanafunzi wengine kutokana na mawasiliano
mema. Hivyo basi, hakikisha kwamba kila mwanafunzi anashiriki katika kazi hii ya
darasa ili kuimarisha mawasiliano, ushirikiano na umoja.
Tathmini
Waagize wanafunzi kuandika majina yao katika heru kubwa na ndogo kama zoezi la
nyumbani.
17
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 2: Jinsi ya kuketi vizuri na kuandika
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, wanafunzi waweze kujenga umilisi wa kuandika.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitakuza umilisi wa wanafunzi katika kuandika hati nadhifu na kazi ya
kuonekana vizuri.
Nyenzo za kujifunzia
Penseli Vitabu Kadi Penseli za rangi Chati
Utangulizi
Anza kwa kumwomba mmoja kati ya wanafunzi kujitokeza na kuonyesha wenzake
njia nzuri ya kukaa wanapokuwa wakiandika.
Waelekeze wanafunzi kuangalia picha katika Kitabu cha Mwanafunzi.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kutazama picha katika Kitabu cha Mwanafunzi.
2. Wape wanafunzi muda wa kutosha kutazama tofauti.
3. Jadili kinachofanyika katika kila picha.
4. Waelekeze wanafunzi kuhusu njia nzuri ya kuketi.
Hitimisho
Fika mwisho wa kipindi hiki kwa kuwaeleza wanafunzi kwamba mkao wetu au njia
yetu ya kukaa huathiri mwandiko. Kipindi hiki kitakuza stadi ya maisha katika kujua
jinsi ya kuishi na wanafunzi wengine kutokana na mawasiliano mema. Hivyo basi,
hakikisha kwamba kila mwanafunzi anashiriki katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha
mawasiliano, ushirikiano na umoja.
Tathmini
Mwanafunzi afanye mazoezi ya mkao mzuri nyumbani na maraki zake.
18
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 3: Angalia tofauti
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, wanafunzi waweze kujenga umilisi wa kutofautisha heru
zinazowiana.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitakuza umilisi wa wanafunzi katika kuandika hati nadhifu na ya
kuonekana vizuri.
Nyenzo za kujifunzia
Penseli Vitabu Kadi Penseli za rangi Chati
Utangulizi
Waelekeze wanafunzi kuangalia picha katika Kitabu cha Mwanafunzi.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kutazama picha katika Kitabu cha Mwanafunzi.
2. Wape wanafunzi muda wa kutosha kutazama tofauti.
3. Jadili wanachoona katika kila picha.
4. Hakikisha wanafunzi wanaunda heru kama walivyotazama.
Hitimisho
Kipindi hiki kitakuza stadi ya maisha katika kujua jinsi ya kuishi na wanafunzi wengine
kutokana na mawasiliano mema. Hivyo basi, hakikisha kwamba kila mwanafunzi
anashiriki katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha mawasiliano, ushirikiano na umoja.
Tathmini
Wanafunzi watafanya mazoezi ya kuandika wakiwa na maraki zao.
19
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 4: Andika na utamke neno uliloandika
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, wanafunzi waweze kujenga umilisi wa sauti na makundi
ya konsonanti.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitakuza ubunifu wa mwanafunzi kuandika kwa hati nadhifu, inayosomeka
na sahihi.
Nyenzo za kujifunzia
Penseli Vitabu Kadi Penseli za rangi Chati
Utangulizi
Anza kwa kuomba wanafunzi wanaohiari kujitokeza na kuonyesha wenzao mkao wao
wanapoandika.
Waelekeze wanafunzi kuangalia picha katika Kitabu cha Mwanafunzi.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kutazama picha katika Kitabu cha Mwanafunzi.
2. Wape wanafunzi muda wa kutosha kutazama tofauti.
3. Jadili kinachofanyika katika kila picha.
4. Waelekeze wanafunzi kuhusu makundi ya konsonanti katika kila fungu na
kufanana kwake.
5. Wasaidie wanafunzi katika zoezi la pili na tatu.
Hitimisho
Kamilisha kipindi hiki kwa kuwaeleza wanafunzi kwamba maendelezo ya maneno
huathiri mawasiliano. Kipindi hiki kitakuza stadi ya maisha katika kujua jinsi
ya kuishi na wanafunzi wengine kutokana na mawasiliano mema. Hivyo basi,
hakikisha kwamba kila mwanafunzi anashiriki katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha
mawasiliano, ushirikiano na umoja.
Tathmini
Waelekeze wanafunzi kufanya mazoezi ya kuandika ruwaza katika Kitabu cha
Mwanafunzi pamoja na wazazi wake.
20
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Sura ya
2
Mwalimu Musa
(Kitabu cha mwanafunzi ukurasa 35–49)
Matokeo yanayotarajiwa ya mafunzo
Mada 1.0
Kusikiliza
Mada 2.0
Kuzungumza
Mada 3.0
Kusoma
Mada 4.0
Kuandika
Somo la 1.2
Utambuzi wa sauti
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kutamka,
kuunganisha
silabi katika
maneno
yanayosemwa
na kutiririsha
maneno ya silabi
mbili.
b) kuvunjavunja
silabi katika
maneno semwa
na kutiririsha
maneno ya silabi
mbili.
c) kutenganisha
sauti za mwanzo,
kati na mwisho
katika maneno
kwa matamshi
sahihi.
d) kuongeza au
kuubadilisha
sauti moja katika
maneno ya silabi
Somo la 2.3
Utambuzi wa sauti
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kutaja na
kutamka heru
zinazowakilisha sauti.
b) kuunganisha heru
za sauti kuunda silabi
na silabi kuunda
maneno.
c) kuvunjavunja silabi
kuunda sauti na
heru na maneno
kuunda silabi.
d) kutambua ujenzi
wa maneno
katika shughuli ya
kuunganisha na
kutenganisha heru
za sauti na silabi.
Somo 3.2
Mpangilio wa sauti
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kupata ufahamu
wa kutambua
heru na sauti.
b) kuunganisha
fonimu au sauti
kujenga silabi.
c) kusoma na
kutamka silabi.
d) kuhusisha silabi
na sauti zake.
Somo la 4.2
Uundaji wa
neno, silabi
na sentensi
Kukia mwisho
wa somo,
mwanafunzi
aweze:
a) kuvunjavunja
maneno
katika silabi.
b) kuunda
maneno
kutokana na
silabi.
c) kuandika
silabi, maneno
na sentensi
zinazotumika
mara kwa
mara.
d) kujenga ari
ya kuunda
maneno na
sentensi.
21
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
mbili ili kuunda
maneno mapya.
e) kutambua
na kutamka
sauti na silabi
zinazotumika
mara kwa mara.
f) kutambua sauti
na silabi katika
mtiririko,
nyimbo,
mashairi,
vitanza ndimi na
vitendawili.
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa
a) Wanakuza ushirikiano na mawasiliano katika kushirikiana katika vikundi.
Aidha, wanakuza uwezo wao wa kujieleza ama kwa kuandika au kuzungumza.
b) Uwezo wa kukiri na kutatua matatizo unakuzwa kutokana na kubuni na
kujieleza na vilevile kupanga mawazo vizuri kwa uwasilishaji.
c) Uwezo wa kidijitali unahimizwa wanapotumia vifaa vya kidijitali kusikiliza
mazungumzo.
Uhusiano na masuala mtambuko
a) Ujuzi wa kujua jinsi ya kuishi na watu wengine katika jamii unakuzwa kutokana
na kushirikiana vyema na wenzao katika makundi na mawasiliano bora.
b) Hamu ya kusoma inakuzwa kutokana na kusoma hadithi na kuzifurahia
hadithi zenyewe.
c) Stadi ya maisha inakuzwa ya kujua kuishi na watu wengine kwa kushirikiana
na wenzao na kudumisha mawasiliano bora.
Uhusiano na desturi na maadili ya jamii
a) Heshima itahimizwa wakifanya kazi pamoja na wanafunzi wenzao kwa
kuheshimiana.
b) Umoja utahimizwa kutokana na ushirikiano na wenzao katika vikundi.
c) Uwajibikaji unakuzwa kwa kuwa wanajifunza kuwajibika wakitekeleza
majukumu waliyopewa ya kusoma.
22
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
d) Uadilifu unakuzwa katika himizo la kuwa raia wema wanaowajali wenzao.
Uhusiano na masomo mengine
a) Mathematical activities wanapojigawa katika vikundi.
b) Religious activities katika himizo la kuthamini na kujali hali na hisia za
wenzao.
Shughuli za kijamii zinazopendekezwa kuchangia ujifunzaji
a) Wanafunzi wanakariri maneno na vitanza ndimi.
b) Wanafunzi wanafanya mazoezi ya kutamka maneno kwa wanajamii wengine.
c) Wanafunzi wanawasomea watu wa nyumbani silabi za maneno.
d) Wanafunzi wanajenga mazoea ya kuandika ndani na nje ya shule.
Shughuli nyingine zisizo rasmi zinazopendekezwa kuchangia ujifunzaji
a) Wanafunzi wanaimba maneno ya kutiririka huku wakicheza.
b) Wanafunzi wanafanya mazoezi ya kuwatamkia wenzao maneno.
c) Wanafunzi wanafanya mazoezi ya kusoma sauti, silabi na maneno huku
wakicheza.
d) Wanafunzi wanaandika majina kwenye vitu.
Tathmini zinazopendekezwa
a) Maswali na majibu
b) Kulinganisha sauti katika matashi na picha
c) Kuchunguza matamshi na kasi ya kusoma wanafunzi wanaposoma sauti, silabi
na maneno.
d) Kuunda jamii ya maneno
Nyenzo za ujifunzaji zinazopendekezwa
Mkusanyiko wa vitendawili na vitanza ndimi, wajuzi waalikwa, rekodi za sauti, chati,
kadi za heru, kikasha cha silabi, penseli, kitabu, kadi za maneno na jedwali la maneno.
23
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kuwashughulikia wanafunzi wenye mahitaji maalum
Usaidizi kwa wanafunzi wenye uwezo
mbalimbali
Usaidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji
maalum
· Himiza wanafunzi wenye uelewa wa
polepole kushiriki katika mazungumzo
kama maigizo na kusimulia hadithi.
· Wape wanafunzi wenye uelewa
wa haraka kazi nyingi ili kuepuka
kuwachosha na kuzubaa darasani.
· Wape wanafunzi wenye uelewa wa
polepole na haraka nafasi za kutosha
katika shughuli za darasani. Una
jukumu la kuhakikisha kwamba
wanafurahiana na kufurahia kukaa
pamoja licha ya tofauti zao.
· Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa
kuona, wape breli, picha za kugusa na
wale wasioweza kuona vizuri wape
maandishi makubwa.
· Kwa wanafunzi walio na shida ya
kusikia vizuri tumia lugha ishara au
kumleta mtaalamu wa lugha ishara
kufasiri.
· Wanafunzi ambao hawawezi kuona
mbali wakae mbele darasani na wenye
uwezo wa kuona mbali wakae nyuma.
· Wape wanafunzi wenye ulemavu
majukumu wanayoweza kutekeleza
kama vile kuigiza nafasi ya mwalimu
mkuu au balozi wa kijiji. Wape usaidizi
wa kutosha na kuhakikisha kwamba
wanafunzi wengine wanafanya
hivyo, kwa mfano, kuwasaidia katika
kusukuma kitimagurudumu cha
mwanafunzi mlemavu.
Wiki ya 4
Mpangilio wa vipindi
Kipindi cha 1: Tambua na utamke sauti zifuatazo
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kutambua na kutamka heru za sauti
na silabi.
Habari za kimsingi
Mada hii ndogo itawasaidia wanafunzi kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza.
Mwanafunzi atashirikishwa katika shughuli inayomhitaji kusikiliza kwa makini
heru na sauti. Hili litamsaidia katika kukuza stadi ya kusikiliza.
24
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Nyenzo za ujifunzaji
Chati za karatasi ngumu
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwauliza wanafunzi kusikiliza kwa makini huku ukisoma
heru na sauti katika Kitabu cha Wanafunzi. Andika heru kama hizo kwenye chati
ya karatasi ngumu.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kusoma kwa sauti heru katika Kitabu cha Mwanafunzi.
2. Wakiwa wawili wawili, waagize wanafunzi kutamka heru hizo tena.
3. Waelekeze wanafunzi kutamka sauti katika heru kwenye chati za karatasi
ngumu.
4. Waruhusu wanafunzi kutamka sauti kwa mara ya pili.
5. Zunguka darasani kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anashiriki katika
kutamka heru na kuhakikisha kwamba wanafunzi wanatamka sauti sahihi.
Warekebishe wanafunzi inapohitajika.
6. Waweke wanafunzi katika vikundi vya watatu watatu. Lipe kila kundi kikapu/
boksi/ndoo lililo na konsonanti 10 zilizochongwa na kukatwa vizuri kutokana
na karatasi ngumu na karatasi 10 za vokali zilizokatwa kutoka kwa karatasi
ngumu.
7. Waagize wanafunzi kucheza mchezo wa kuvua heru ambapo kila mwanafunzi
atahitajika kuchagua heru mbili kutoka kwenye kikapu/sanduku/ndoo.
8. Waulize wanafunzi kutaja kila heru waliyochagua.
9. Waagize wanafunzi kusoma sauti za heru walizochagua. Warekebishe
wanafunzi inapohitajika.
Tathmini
Waulize wanafunzi kukamilisha mazoezi katika vitabu vyao kwa kunakili au kuandika
heru zilizo katika kitabu cha wanafunzi kwenye madaari yao. Wanafunzi waandike
heru hizo kwa jinsi zinavyoonekana katika kitabu cha mwanafunzi (anza kwa heru
ndogo kisha heru kubwa).
25
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwaagiza wanafunzi kusoma sauti za heru na silabi kutoka
kwa kitabu cha wanafunzi au vifaa vya kiteknohama.
Zoezi la nyumbani
Waambie wanafunzi kuwaomba wazazi/walezi wao kuwapa vifaa vya kiteknohama
wanavyoweza kutumia kusikiliza na kusoma sauti za heru.
Kipindi cha 2: Kuunganisha sauti ili kuunda maneno
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kutenganisha sauti za mwanzo, kati na
mwisho katika kutamka maneno ya heru nne.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kinalenga utahiji wa maneno ya heru nne. Kuza ujuzi waliopata
wanafunzi katika kutambua sauti za heru na silabi ili kuwasaidia kutahiji maneno
yenye heru nne kwa njia sahihi.
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuandika maneno ya heru nne ubaoni. Waambie wanafunzi
kutumia ujuzi wao wa kutamka sauti za heru na maneno.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kutenganisha sauti katika maneno ya heru nne kwa
kutenganisha sauti za mwanzo, kati na mwisho.
2. Waelekeze wanafunzi kusoma maneno ya heru nne katika kitabu cha wanafunzi.
Sikiliza na usahihishe matamshi ya wanafunzi.
Maneno yanayopendekezwa kusoma:
a) Paka
b) Kaka
c) Dada
d) Gari
e) Pini
26
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
3. Wagawe wanafunzi katika vikundi vya watatu watatu. Lipe kila kundi kadi
tatu mulishi zilizo na heru zinazoweza kuunda neno jepesi la heru nne
zikiunganishwa.
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwahimiza wanafunzi kutumia rangi na vifaa vilivyo karibu
nao kutenganisha na kuchanganya sauti za mwanzo, kati na mwisho katika maneno ya
heru nne ili kufanya mazoezi ya matamshi na kutahiji.
Zoezi la nyumbani
Wape wanafunzi orodha ya maneno ya heru nne na uwaulize wanafunzi kusaidiwa
na wazazi/walezi wao katika kuzisoma.
Maneno yanayopendekezwa
1. paka 6. kipa
2. dada 7. futa
3. baba 8. leta
4. mama 9. cheza
5. rula 10. panya
Kipindi cha 3: Cheza mchezo
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi hiki, mwanafunzi aweze:
1. Kutamka, kuunganisha silabi katika maneno na maneno ya silabi mbili.
2. Kutambua sauti na silabi katika maneno ya mtiririko, nyimbo, mashairi, vitanza
ndimi na vitendawili.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kushiriki katika michezo mbalimbali ya lugha
k.v. mchezo wa kuvua. Hili linawasaidia wanafunzi kutazama heru zilizotandazwa
huku wakisikiliza sauti. Hili hatimaye huwasaidia wanafunzi kuunda maneno mepesi
kutokana na sauti watakazokuwa wamejifunza kutamka.
27
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Nyenzo za ujifunzaji
Chati kwenye karatasi ngumu, kadi mulishi na masanduku/ndoo
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuwaagiza wanafunzi kusoma maneno waliyojifunza
kutamka katika kipindi kilichopita. Hakikisha kwamba wanafunzi wanapata matamshi
sahihi kwa kila neno.
Shughuli za ujifunzaji
a) Wagawe wanafunzi katika vikundi vya watatu watatu. Kipe kila kikundi
kadi tatu mulishi zilizo na heru zinazoweza kuunda maneno ya heru nne
zikiunganishwa.
b) Muulize kila mwanafunzi katika kikundi kusoma kwa sauti, sauti ya heru
katika kadi yake mulishi.
c) Waulize wanafunzi kujaribu kuunda maneno mengi kiasi cha haja ya heru nne
kutokana na kadi zao.
d) Teua vikundi bila mpangilio maalum na uwaruhusu wanakundi kusoma kwa
sauti maneno ya heru nne waliyounda darasani. Hakikisha kwamba vikundi
vyote vinashiriki na kila mwanakundi anasoma neno kwa sauti.
e) Waelekeze wanafunzi kurejelea Kitabu cha Mwanafunzi kwenye ukurasa 40.
Wasomee wanafunzi mtiririko huo mara mbili huku wakisikiliza.
Huyu ni Paka.
Paka huyu mkubwa ni wa kaka.
Paka wa kaka amekaa kwenye mkeka.
Paka anasubiri panya anayeshuka.
f) Waagize wanafunzi kusoma maneno ya mtiririko baada yako. Wapeleke
wanafunzi taratibu, neno kwa neno na sentensi baada ya sentensi huku
ukihakikisha kwamba kuna utamkaji mzuri wa maneno.
28
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Tathmini
Waagize wanafunzi kuandika maneno ya heru nne ambayo wamesikiliza na
kusoma kutoka kwenye mtiririko. Hakikisha kwamba una maneno yafuatayo yote
yanayopatikana katika mtiririko.
Kaka Pika Fuata
Paka Bata
Fika Futa
Mkeka Andika
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwaagiza wanafunzi kuandika upya maneno waliounda kwa
kadi mulisi katika vikundi.
Kipindi hiki kitakuza stadi ya maisha katika kujua jinsi ya kuishi na wanafunzi
wengine kutokana na mawasiliano bora. Hivyo basi, hakikisha kwamba kila
mwanafunzi anashiriki katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha mawasiliano,
ushirikiano na umoja.
Tathmini
Waagize wanafunzi kuandika maneno yaliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi ukurasa
40 mara tatu. Waandike kwa kuelekezwa na walezi/wazazi wao nyumbani.
Kipindi cha 4: Kutenganisha na kubadilisha sauti
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi hiki, mwanafunzi aweze kutenganisha na kubadili sauti.
Wafanye hivi kwa kuunda maneno mapya baada ya kubadili sauti hizi na sauti nyingine.
Habari za kimsingi
Wawezeshe wanafunzi kujua maneno na kuyaandika ubaoni. Waagize wanafunzi
kutenganisha sauti na kutamka sauti mahususi k.m. kutofautisha PAKA kutoka kwa
P-A-K-A. Wakimaliza, andika maneno machache ubaoni. Wape sauti wanazoweza
kutumia kubadili na nyingine hivyo kupata maneno mapya k.v. katika maneno kama
29
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
vile pata na kuibadilisha heru ya mwanzo kwa sauti ya heru ba ya mwanzo ili kupata
neno bata. Wanafunzi watamke sauti na maneno kwa uwazi. Hili litakuza stadi za
mawasiliano.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu
Vibango vilivyo na maneno mbalimbali yaliyoandikwa juu yake.
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwapa wanafunzi vibango vilivyoandikwa maneno.
Maneno hayo hayo yawe ya herufi nne. Waagize kuzigawa herufi hizo katika sauti
mahususi. Wafanye kazi katika vikundi.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waagize wanafunzi kutamka sauti na maneno wakiwa katika kikundi chao.
2. Waelekeze wanafunzi kufanya zoezi la 1.
Majibu yanayotarajiwa
a) M-a-m-a
b) B-a-b-a
c) K-a-k-a
d) P-a-p-a
e) D-a-d-a
3. Sahihisha makosa ya matamshi.
4. Waagize wanafunzi kusoma kwa sauti maneno katika zoezi la 2. Katika
vikundi, wanafunzi wabadili sauti ya kwanza katika kila neno. Waagize
wanafunzi kusoma maneno mapya yaliyoundwa.
5. Waelekeze wanafunzi katika kujibu swali la nne, tano, sita na saba. Katika
kila hali, waagize wanafunzi kusoma maneno mapya. Hili litakuza stadi za
kusikiliza na kuzungumza katika wanafunzi.
30
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Majibu yanayotarajiwa kwa swali 4 katika zoezi la 2
a. bata
b. basi
c. babu
d. bao
e. bati
Majibu yanayotarajiwa kwa swali 6 katika zoezi la 2
a. paka
b. ka
c. shika
d. kaka
e. toka
Hitimisho
Katika vikundi, waagize wanafunzi kuandika maneno ya heru nne au silabi mbili ya
vitu vinavyopatikana katika mazingira yao ya karibu.
1. Wanyama wa pori au wa kufugwa
2. Majina ya watu
Waulize wawakilishi wachache wa vikundi kusoma maneno waliyounda.
Tathmini
Waagize wanafunzi kukamilisha zoezi la nyumbani kwa ushauri na uelekezi wa wazazi
au walezi k.v. kuandika maneno ya heru nne ya vitu vifuatavyo vinavyopatikana
katika mazingira yao ya karibu (vyakula na vyombo).
31
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 5: Mazungumzo na watu wengine
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi hiki, mwanafunzi aweze kushiriki kwa ujasiri katika
mazungumzo na wenzake katika mikutadha mbalimbali na kuzingatia ubadilishanaji
wa nafasi.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kufanya mazoezi ya stadi za kusikiliza na
kuzungumza. Mwalimu achukue hali halisi ya maisha ambapo mazungumzo
yanafanyika ili kuwaonesha wanafunzi. Fanya juhudi kuunganisha stadi za
kusoma na kuandika katika kipindi hiki kwa kurejelea mikutadha mwafaka.
Nyenzo za ujifunzaji
Chati kwenye karatasi ngumu
Rekodi ya sauti za mazungumzo
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwauliza wanafunzi kusikiliza kwa makini na kutazama kwa
uangalifu na kusoma kuhusu Mwalimu Musa.
Unaweza pia kuwaagiza kusikiliza mazungumzo yaliyorekodiwa.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kusoma shughuli ya kwanza kwa sauti.
2. Waagize wanafunzi kuigiza mazungumzo kuhusu masuala yanayohusiana na
mada Nyumbani kwetu.
3. Wanafunzi warekodi sauti za mazungumzo na kuwasikiliza, kwa kuwa kadiri
wanavyoshiriki katika mazungumzo wanakuza stadi za mawasiliano na
ushirikiano. Aidha, wanapata ujuzi wa kuishi na wenzao.
Majibu yanayotarajiwa
Zoezi la 1 na 2
Kubali majibu yoyote faafu.
32
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Hitimisho
Sisitiza umuhimu wa kubadilishana nafasi za uhusika na ujasiri katika mazungumzo.
Tathmini
Waagize wanafunzi kujaribu kushughulikia zoezi la kufanyia nyumbani.
Wiki ya 5
Kipindi cha 1: Kutambua heru na sauti
Tokeo maalum la ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kutambua na kutamka heru na silabi
zinazotumika mara kwa mara.
Habari za kimsingi
Kipindi kitawasaidia wanafunzi kutamka heru wanazoona. Kipindi kinahusu stadi
ya kusikiliza na kuzungumza. Hata hivyo, jaribu kujumuisha stadi za kusoma na
kuandika kwenye kipindi ukitumia muktadha ufaao.
Nyenzo za ujifunzaji
Chati Karatasi ngumu Vitabu Kadi za heru
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuonesha kadi ya heru mbalimbali na kusoma kwa sauti huku
wanafunzi wakisikiliza na kurudia baada ya kusema.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waambie wanafunzi watazame kadi za heru.
2. Wanafunzi watambue sauti zinazosomwa na mwalimu.
3. Kwa makundi ya wanafunzi watatu watatu, mmoja ataje sauti huku wengine
wawili wakionesha heru kwenye kadi. Hili litakuza uwezo wa kukiria
wanafunzi wanapolinganisha sauti na heru.
4. Sikiliza matamshi mbalimbali huku ukihakikisha kuwa kila mwanafunzi
anashiriki.
33
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Baadhi ya majibu
Zoezi la 2
B, CH, D, F, G
1. Beba
2. Chai
3. Dawa
4. Funga
5. Gari
Majibu mengine yakubaliwe
Hitimisho
Kamilisha kipindi kwa kusoma sauti na kuonyesha heru zake.
Tathmini
Wape wanafunzi heru zaidi na kuwaambia waunde maneno wakitumia heru.
Kipindi cha 2: Mazungumzo na watu wengine
Tokeo maalum la ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kutamka maneno na kuzitumia silabi
katika maneno ya kutamkwa, maneno yanayofanana ya kutokea ghaa na yenye
kufanana ya maneno ya silabi moja.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kinahusu stadi ya kusikiliza na kuzungumza. Mwalimu awaelezee
wanafunzi kuhusu silabi.Wanafunzi wapate muda wa kuelewa ujumbe. Hata hivyo, kila
hatua ichukuliwe kujumuisha stadi za kusoma na kuandika kwenye kipindi, kulingana
na muktadha.
Nyenzo za ujifunzaji
Chati Karatasi ngumu Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwahusisha wanafunzi kuteua idadi sawa ya konsonanti na
vokali.
34
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Shughuli za ujifunzaji
1. Waambie wanafunzi watazame konsonanti na irabu zilizoteuliwa.
2. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, wanafunzi wajifunze kuunganisha
heru kuunda silabi. Hili litahakikisha kuwa wamejifunza kutumia silabi na
kuunda maneno.
3. Waongoze wanafunzi kusoma silabi walizounda kwa sauti. Hili litaimarisha stadi
ya mawasiliano.
4. Waongoze wanafunzi kutumia konsonanti na vokali zote kuunda silabi. Mifano:
ba be bi bo bu
cha che chi cho chu
Hitimisho
Kamilisha kipindi kwa kusoma silabi kwa sauti darasani kisha usome sauti na
kuonyesha heru zake.
Tathmini
Teua baadhi ya wanafunzi kusoma silabi mbele ya wanafunzi huku wengine wakirudia.
Kipindi cha 3: Kuunda maneno kutokana na silabi
Tokeo maalum la ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kuunda maneno akitumia silabi teule.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kinahusu stadi ya kuandika na kumsaidia mwanafunzi kupata msamiati
mpya na kuimarisha stadi za mawasiliano. Mwalimu amsaidie mwanafunzi kuelewa
maana ya maneno yaliyoundwa kwa kuunganisha silabi na jinsi ya kuzitumia katika
sentensi.
Nyenzo za ujifunzaji
Chati Karatasi ngumu Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuonyesha wanafunzi silabi mbalimbali na kuwaambia wasome
kwa sauti.Waonyeshe jinsi ya kuunda maneno kutoka kwa silabi.
35
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Shughuli za ujifunzaji
1. Waambie wanafunzi watazame silabi zilizoonyeshwa.
2. Wakiwa katika makundi ya wanafunzi watatu unganisha silabi kuunda
maneno. Hili litaleta uwazaji wa kina na stadi ya kuunda na kutenga
maneno
3. Waongoze wanafunzi kusema maneno waliyounda kwa sauti. Hili
litaimarisha stadi ya mawasiliano.
4. Waongoze wanafunzi kueleza maana ya maneno waliyounda.
Majibu yanayotarajiwa
Zoezi la 1 Zoezi la 2
1. Wali 1. Paka
2. Kula 2. Kiti
3. Chakula 3. Kaka
4. Wacha 4. Meza
Jawabu lingine lolote 5. Babu
6. Somo
Jawabu lingine lolote sahihi
Hitimisho
Kamilisha kipindi kwa kuwaambia wanafunzi wawaambie wenzao maneno waliyounda.
Tathmini
Wape wanafunzi silabi kadhaa na uwaambie waziunganishe ili kuunda maneno yafaayo
ya Kiswahili.
Kipindi cha 4: Unda sentensi
Tokeo maalum la ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kuandika sentensi kutokana na
mengine aliyopewa.
36
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Habari za kimsingi
Wanafunzi wataunda sentensi mbalimbali wakitumia maneno waliyopewa.
Wanafunzi wapewe maneno mengi na kuambiwa waunde sentensi wakiyatumia.
Angalia kuwa wanatumia alama za uakishi vyema.Wanaposoma, hakikisha kuwa
wanatamka maneno ifaavyo.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu
Kadi zikiwa na maneno mengi
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwaambia wanafunzi kutazama na kujadili maana ya
maneno yaliyoandikwa ubaoni.Wafanye kazi katika makundi.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waambie wanafunzi wachache wafafanue maana ya maneno waliyojadili
kwenye vikundi. Sahihisha inapowezekana.
2. Waambie wanafunzi kuunda sentensi kutokana na maneno waliyopewa.
Wakumbushe sheria za uakishi. Angalia wanafunzi wanapoandika sentensi
na kuwasaidia wasioweza.
3. Wanafunzi wabadilishane vitabu na kusoma sentensi za wenzao. Hili litakuza
stadi za ushirikiano na mawasiliano wanafunzi wanaposhirikiana.
4. Waongoze wanafunzi kutazama picha kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
Waambie wanafunzi waandike sentensi chini ya picha.
5. Soma sentensi na uwaulize wanafunzi kurudia. Wasome kimakundi ili
kukuza ubora.
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwaambia wanafunzi wajaze mapengo katika sentensi
zifuatazo.Watoe majibu kwenye picha za Kitabu cha Mwanafunzi.
Tathmini
Waambie wanafunzi waandike sentensi tano kuhusu walioketi nao darasani.
37
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 5: Mchezo wa kutunga sentensi
Tokeo maalum la ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kuandika sentensi kutokana na
maneno waliyopewa. Wanafaa waunde maneno mapya kutokana na maneno
waliyopewa.
Habari za kimsingi
Wanafunzi watunge sentensi mbalimbali wakitumia maneno waliyopewa. Wanafunzi
wapewe maneno mengi na kuunda sentensi wakiyatumia. Pia, andika maneno
machache ubaoni na uwaambie wanafunzi waunde maneno mapya kutokana na
yaliyo ubaoni. Kuza stadi ya kusoma kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanasoma
sentensi wanazoandika.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu
Kikapu cha karatasi ndogo kilicho na maneno
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwaambia wanafunzi wachukue karatasi tano zikiwa na
maneno yaliyoandikwa.Wanafunzi wasome katika makundi.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waambie wanafunzi wajadili maana ya maneno waliyopata kwenye kikapu.
Sahihisha inapofaa.
2. Waambie wanafunzi kuunda sentensi tano kutokana na maneno waliyopata.
Wakumbushe kuhusu sheria za uakishaji.Waangalie wanapoandika sentensi.
3. Wanafunzi wachache wa makundi wasome sentensi zao darasani.
Wanapofanya kazi pamoja katika makundi, wanakuza stadi za ushirikiano
na mawasiliano. Maadili kama umoja na heshima pia yanakuzwa.
4. Andika neno KARATASI ubaoni. Waambie waunde maneno mapya kutokana
na neno hilo. Wasomee wenzao kukuza stadi ya kusoma.
Baadhi ya majibu
1. Sita
2. Kata
3. Kasi
38
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
4. Taka
5. Karata
Hitimisho
Waambie wanafunzi waandike maneno matano. Waambie waunde maneno mapya
kutokana na maneno waliyoandika. Wafanye kimakundi.
Tathmini
Waambie wanafunzi waandike sentensi tano kuhusu familia zao. Wawasomee wazazi
au walezi wao.
39
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Sura ya
3
Kwa nini bata mzinga ana madoadoa
meupe
(Kitabu cha mwanafunzi ukurasa 50–68)
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Mada ya 1.0
Kusikiliza
Mada ya 2.0
Kuzungumza
Mada ya 3.0
Kusoma
Mada ya 4.0
Kuandika
Somo la 1.3:
Masimulizi
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kusikiliza kwa
makini na kujibu
hadithi hizo kwa
ujasiri.
b) kutumia
msamiati wa
kimaudhui.
c) kufurahia
kusikiliza hadithi
za simulizi.
d) kufurahia desturi
na tamaduni zao
kupitia hadithi
za kisimulizi.
e) kuwahurumia
watu walio
na sifa kama
hizo katika
masimulizi.
f) kukuza ubunifu
na uwezo
wakijenga picha
akilini kuhusu
hadithi za
kisimulizi.
Somo la 2.1:
Kuiga
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kupata msamiati
wa mawasiliano
katika muktadha
tofauti.
b) kutumia msamiati
mwafaka kujieleza
katika mikutadha
mbalimbali.
c) kujibu kwa ujasiri
mawasiliano
katika mikutadha
tofauti.
d) kudhihirisha
mienendo
mwafaka katika
mazungumzo ya
mikutadha tofauti.
Somo la 3.3:
Kusoma kauli na
sentensi
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kusoma kwa sauti
kauli na sentensi
fupi kwa njia
sahihi.
b) kusoma maneno
ya kawaida
kutokana na sauti
unazojua.
c) kufurahia kusoma
maneno mapya,
kauli na sentensi
mpya.
Somo la 4.3:
Mwandiko
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kutumia alama
za uakishaji
kuwasilisha maana
iliyokusudiwa.
b) kutumia mwandiko
unaosomeka vizuri
kwa mawasiliano
mwafaka.
c) kuimarisha kasi na
wepesi wa kusoma.
d) kupata ujuzi wa
kuchonga silabi,
maneno na sentensi
katika njia sahihi.
e) kuandika kwa mkono
heru, nambari na
ishara.
40
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Umilisi mkuu unaokuzwa
1. Ujasiri unaendelezwa katika wanafunzi wanapojieleza katika mikutadha mbalimbali.
2. Wanakuza ushirikiano na mawasiliano katika kushirikiana katika vikundi.
3. Uwezo wa kukiri unakuzwa kutokana na kubuni na kujieleza katika visa.
4. Uwezo wa kidijitali unahimizwa wanapotumia vifaa vya kidijitali.
Uhusiano na masuala ya mtambuko
a) Uraia wa Kenya unahimizwa kutokana na kuheshimiana katika makundi na umoja
katika ushirikiano.
b) Stadi za maisha zinakuzwa za kujua jinsi ya kuishi na watu kutokana na kushirikiana
katika makundi.
Uhusiano na desturi
a) Heshima itaendelezwa wakifanya kazi pamoja na wanafunzi wenzao.
b) Umoja utahimizwa kutokana na ushirikiano na wenzao au katika vikundi.
c) Wanajifunza kuwajibika wakitekeleza majukumu waliyopewa.
Uhusiano na sehemu nyingine za ujifunzaji
a) Mathematical Activities zinadhihirika katika kujigawa katika vikundi.
Ujifunzaji wa Huduma kwa Jamii
1. Wazazi wanashiriki kwa kuwasimulia watoto wao hadithi.
2. Wanafunzi wanajiunga na makundi ya kukusanya na kusimulia hadithi za kiasili
katika jamii.
3. Wanafunzi watawauliza wazazi/walezi wao kuhusu maadili katika mawasiliano.
4. Wanafunzi wanawasomea watu wa familia zao jumbe fupi fupi.
5. Wanafunzi wanashiriki katika shughuli za kuimarisha uwezo wao wa kiutendaji
kama vile kuandika kwa kutumia samadi, kukusanya nyenzo za kuezekea nyumbani.
Shughuli nyingine zisizo rasmi zinazopendekezwa kuchangia ujifunzaji:
1. Wanafunzi wanawaeleza wenzao hadithi hizi upya.
2. Wanafunzi wanawasiliana ifaavyo na wenzao katika mikutadha mbalimbali.
3. Kusoma maktabani.
4. Wanafunzi wanajifunza utendaji katika shughuli za kucheza kama vile kushika vitu.
41
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Tathmini zinazopendekezwa
1. Kuzisimulia hadithi upya, maswali na majibu
2. Maswali ya kuongea
3. Kusoma maneno na kauli fupi fupi
4. Kunakili au kuandika heru, maneno na sentensi katika miandiko yao bora
Nyenzo za ujifunzaji zinazopendekezwa
Vifaa vya hadithi za kusimuliwa, kadi za picha, chati, madaari, vitabu vya hadithi,
hadithi zilizorekodiwa katika sauti na video, nyenzo, mzazi/mlezi, vifaa kusikilizia sauti
zilizorekodiwa au kutazamia vilivyo na mazungumzo mepesi kwa mfano, ‘Habari? U hali
gani? Unaitwa nani?’
Kutilia maanani mahitaji maalum ya kielimu
Usaidizi kwa wanafunzi wenye uwezo
mbalimbali
Usaidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji
maalum
· Himiza wanafunzi wenye uelewa
wa polepole kushiriki katika
mazungumzo kama maigizo na
kusimulia hadithi.
· Wape wanafunzi wenye uelewa
wa haraka kazi nyingi ili kuepuka
kuwachosha na kuzubaa darasani.
· Wape wanafunzi wenye uelewa wa
polepole na haraka nafasi za kutosha
katika shughuli za darasani. Una
jukumu la kuhakikisha kwamba
wanafurahiana na kufurahia kukaa
pamoja licha ya tofauti zao.
· Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa
kuona, wape breli, picha za kugusa na
wale wasioweza kuona vizuri wape
maandishi makubwa.
· Kwa wanafunzi walio na shida ya
kusikia vizuri tumia lugha ishara au
kumleta mtaalamu wa lugha ishara
kufasiri.
· Wanafunzi ambao hawawezi kuona
mbali wakae mbele darasani na wenye
uwezo wa kuona mbali wakae nyuma.
· Wape wanafunzi wenye ulemavu
majukumu wanayoweza kutekeleza
kama vile kuigiza nafasi ya mwalimu
mkuu au balozi wa kijiji. Wape
usaidizi wa kutosha na kuhakikisha
kwamba wanafunzi wengine
wanafanya hivyo, kwa mfano,
kuwasaidia katika kusukuma
kitimagurudumu cha mwanafunzi
mlemavu.
42
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Mpangilio wa vipindi
Wiki ya 6
Kipindi cha 1: Sikiliza hadithi
Matokeo maalumu ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze:
1. Kusikiliza masimulizi kwa makini na kujibu kwa ujasiri.
2. Kutumia msamiati mbalimbali wa kimaudhui.
Habari za kimsingi
Mada hii ndogo itawasaidia wanafunzi kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza. Wahimize
wanafunzi kushiriki katika shughuli za usimulizi wa hadithi huku wakisikiliza na kusimulia
hadithi.
Nyenzo za ujifunzaji
Vifaa vya usimulizi wa hadithi, kadi za picha, vitabu vya hadithi, hadithi zilizorekodiwa katika
kanda za sauti na video, na mjuzi mwalikwa.
Utangulizi
Waagize wanafunzi kutazama picha katika Kitabu cha Mwanafunzi ukurasa 50 na kutaja
wanachokiona. Waruhusu wanafunzi kutoa maelezo ya picha katika maneno yao wenyewe.
Wanaweza kueleza hisia, umbo, vitendo na mandhari ya picha.
Shughuli za ujifunzaji
Zoezi la 1
Majibu utakayotarajia kutoka kwa wanafunzi ni pamoja na:
a) Kuna picha ya msichana.
b) Msichana ana mkoba
c) Msichana amevaa sare ya shule.
d) Msichana huyo amevaa viatu.
e) Msichana huyu ana nywele refu.
f) Rangi ya sare ya shule ni samawati na manjano.
43
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Zoezi la 2
1. Wasomee wanafunzi hadithi hii hapa chini.
2. Katika vikundi vya wawili wawili, waruhusu wanafunzi kusimulia upya hadithi hiyo kwa
maneno yao.
Hii ni picha ya Adamba. Ana umri wa miaka saba. Yuko katika daraja ya kwanza.
Mamake anaitwa Pendo. Mamake Adamba ni mkulima. Yeye hupanda mimea kama
vile karoti, dengu na viazi. Adamba humsaidia mamake kunyunyizia mimea maji kila
asubuhi. Babake Adamba anaitwa Bwana Wasike. Yeye ni seremala. Yeye hutengeneza
viti, meza na vitanda. Adamba hukalia kibago chini ya mti kusoma kitabu cha hadithi
kila jioni.
Zoezi la 3
Wanafunzi wajibu swali lililo katika Kitabu cha Mwanafunzi kwa maongezi.
Hitimisho
1. Waagize wanafunzi kusimulia hadithi kuhusu maisha yao.
2. Wanafunzi wanaweza kutumia kifaa cha kiteknolojia kujirekodi.
Zoezi la kufanyia nyumbani
Waagize wanafunzi kuwaambia wazazi kuwasimulia hadithi kuhusu familia yao.
Kipindi cha 2: Sikiliza na uigize
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze:
1. Kupata ari ya kusikiliza masimulizi.
2. Kufurahia desturi na utamaduni kama zinavyofunzwa katika masimulizi.
3. Kukuza ubunifu wanapojenga picha za akilini kuhusu matukio na wahusika
katika masimulizi hayo.
4. Kujihusisha na watu wanaodhihirika katika masimulizi hayo.
44
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuwaeleza wanafunzi kuhusu umuhimu wa hadithi au masimulizi
katika jamii.
Shughuli za ujifunzaji
Zoezi la 1
1. Waulize wanafunzi kutazama picha katika kitabu cha mwanafunzi na kuzungumza
kuzihusu.
2. Mwalike mtu mwingine kuwasomea wanafunzi hadithi inayofuata. Hakikisha
kwamba yuko katika hali nzuri ya kuweza kusimulia (akiwa katika mavazi ya
kitamaduni).
3. Msimulizi azingatie koma, kikomo na kuiga sauti za wanyama na halihamasa ya
masimulizi.
Mbwa Mla
Hapo zamani kulikuwa na mbwa. Aliitwa Mbasi. Mbasi alikuwa mla na asiye na
shukrani. Jioni moja, Mbasi alihisi njaa na akapata mfupa kutoka kwa muuzaji wa
nyama wa hapa karibu. Alikula mfupa huo kwa ula huku akitikisa mkia wake kwa
furaha. Alipokuwa akifurahia mfupa wake, alimwona raki yake, Mulwa, akitafuna
mfupa mwingine. Mbasi aliangusha mfupa wake na akamkimbilia Mulwa. Bwe!
Bwe! Bwe!” alibweka. Mbwa mwingine alipita hapo na akauchukua mfupa wa Mbasi.
Mbasi alipogeuka kuangalia alipata mfupa wake haupo. Mulwa alibweka, Bwe! Bwe!”
kwa furaha akiondoka na mfupa wake. Mbasi aligundua kwamba alikuwa amepoteza
mfupa wake na ule wa Mulwa. Muda ulikuwa umeenda. Alikuwa amepoteza mfupa
wake kwa sababu ya ula. Sasa hakuwa na budi kulala njaa.
Zoezi la 2
1. Waagize wanafunzi kukaa katika nusu ya duara na kumsikiliza msimulizi kwa
makini.
2. Waambie wanafunzi kusimulia upya hadithi ya Mbwa Mla katika maneno yao
wenyewe.
3. Waagize wanafunzi kufanya kazi katika vikundi kuigiza hadithi hii.
Zoezi la 3
1. Waagize wanafunzi kujibu maswali yaliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi kwa njia ya
maongezi.
45
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Zoezi la kufanyia nyumbani
1. Waambie wanafunzi kusimulia wazazi au walezi wao kisa cha mbwa mla.
2. Wazazi wao wawasomee hadithi, Kwa nini bata mzinga ana madoadoa meupe.
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kuendelea kusoma na kufurahia kusoma.
Kipindi cha 3: Kuungana na watu wengine
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze:
1. Kutumia msamiati mwafaka kujieleza katika mikutadha mbalimbali.
2. Kupata msamiati wa mawasiliano katika mikutadha mbalimbali.
Utangulizi
Anza kipindi kwa kuwaeleza wanafunzi kuhusu umuhimu kuiga mambo na tabia
chanya kutoka kwa watu walio karibu nao.
Shughuli za ujifunzaji
Zoezi la 1
1. Waelekeze wanafunzi kutazama picha kwa makini na kueleza kinachofanyika
katika picha hiyo.
2. Wasomee wanafunzi mazungumzo katika kitabu cha wanafunzi.
3. Soma mazungumzo huku wanafunzi wakifuata au kurudia baada yako.
4. Waulize wanafunzi kutaja wakati ambao mazungumzo kati ya mama na
mwanawe yanafanyika.
5. Waulize wanafunzi wawe katika vikundi vya wawili wawili na kuiga shughuli
zinazofanyika katika picha waliyotazama.
Zoezi la 2
1. Watajie wanafunzi maneno ya lugha ya kunyenyekea yaliyotumiwa katika picha
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
46
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
a) Shikamoo
b) Marahaba
c) Asante
d) Nashukuru
e) Naomba
f) Unisaidie
g) Tafadhali
2. Waagize wanafunzi kurudia msamiati uliopo hapo juu baada yako.
3. Waelekeze wanafunzi kutumia msamiati waliojifunza katika mazungumzo. Fanya
hivi kwa kushiriki katika mazungumzo na wanafunzi huku mkitumia msamiati
wa kunyenyekea.
4. Waagize wanafunzi kuiga matumizi ya lugha hiyo ya kunyenyekea.
Hitimisho
Waagize wanafunzi kujumuisha lugha ya kunyenyekea katika mawasiliano yao ya kila siku.
Zoezi la nyumbani
1. Waagize wanafunzi kufanya mazoezi ya kutumia lugha ya kunyenyekea.
2. Waagize wanafunzi kuwaambia wazazi au walezi wao kuwaonesha jinsi lugha ya
kunyenyekea inavyotumiwa katika jamii yao wakati wa salamu.
Kipindi cha 4: Salamu
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze:
1. Kujibu kwa ujasiri mawasiliano katika mikutadha mbalimbali;
2. Kuonyesha mienendo ifaayo wakati wa mazungumzo katika mikutadha
mbalimbali.
Habari za kimsingi
Katika shughuli hii ya ujifunzaji jumuisha kadi zinazoonesha wakati wa siku
(asubuhi, adhuhuri, jioni na usiku). Wanafunzi wataimba wimbo kulingana na
wakati wa siku utakaoonyeshwa kwenye kadi.
47
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuwauliza wanafunzi kutaja nyakati mbalimbali za siku
(asubuhi, adhuhuri, jioni na usiku). Kariri shairi lolote kuhusu nyakati tofauti za siku.
Shughuli za ujifunzaji
Zoezi la 1
1. Waagize wanafunzi kutazama picha katika vitabu vyao vya kusoma.
2. Waimbie wanafunzi wimbo ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi.
3. Waagize wanafunzi kurudia wimbo huo baada yako.
4. Katika vikundi vya wawili wawili, wanafunzi waimbe wimbo huo.
5. Waonyeshe wanafunzi kadi za maandishi moja baada ya nyingine. Waulize wajibu
kwa kuimba salamu kulingana na wakati ulioonyeshwa kwenye kadi.
6. Katika vikundi, wanafunzi wafanye mazoezi ya kutumia maneno ya salamu
kutegemea nyakati mbalimbali za siku.
7. Waelekeze wanafunzi huku ukiangalia wanavyoendelea katika kazi za vikundi.
Zoezi la 2
1. Waelekeze wanafunzi katika kutazama picha kuhusu mienendo katika vitabu vyao vya
kusoma.
2. Waulize wanafunzi kuzungumza kuhusu mienendo inayodhihirishwa na watu walio
katika picha hiyo.
3. Waweke wanafunzi katika vikundi na kuwaelekeza kuigiza vitendo vilivyo katika picha.
Zoezi la kufanyia nyumbani
Waulize wanafunzi kutambua mienendo mbalimbali inavyofanyika katika jamii.
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwauliza wanafunzi kudhihirisha mienendo miema katika
mawasiliano.
48
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 5: Soma vifungu vifupi
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze:
1. Kusoma maneno wasiyoyazoea kutokana na ufahamu wa kimatamshi.
2. Kujenga ari ya kusoma maneno mapya, vifungu na sentensi.
Utangulizi
Waoneshe wanafunzi maneno mapya na uwaulize kuyatamka.
Shughuli za ujifunzaji
Zoezi la 1
1. Tamka sauti za heru, vokali na silabi zilizo katika Kitabu cha Mwanafunzi.
2. Waagize wanafunzi kurudia baada yako sauti na silabi.
3. Waelekeze wanafunzi katika kutamka maneno yaliyoundwa kwa vokali, konsonanti na
silabi.
Zoezi la 2
1. Waulize wanafunzi kutazama vitabu vyao vya kusoma na uwasomee maneno
yaliyoonyeshwa.
2. Wahimize wanafunzi kusoma maneno uliyo nayo kwenye chati.
3. Waelekeze wanafunzi katika kusoma vifungu na kauli katika vitabu vyao vya kusoma.
4. Waagize kuunda na kutamka vifungu na kauli zao wenyewe kutokana na maarifa
waliyopata darasani.
5. Waelekeze wanafunzi katika kusoma sentensi zilizo katika Kitabu cha Mwanafunzi na
kutunga sentensi zao nyepesi kwa kuzingatia sentensi walizosoma.
Zoezi la kufanyia nyumbani
Waagize wanafunzi kutumia sentensi katika vitabu vyao vya kusoma kufanya mazoezi ya
matamshi.
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kufanya mazoezi ya heru, maneno na sentensi katika hadithi.
49
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Wiki ya 7
Kipindi cha 1 na 2: Kuandika heru vizuri
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze:
1. Kusoma kauli na sentensi fupi fupi katika njia sahihi.
Utangulizi
Andika kauli hizo ubaoni na uwaagize wanafunzi kuzisoma kwa sauti.
Shughuli za ujifunzaji
Zoezi la 1
1. Waelekeze wanafunzi katika kucheza mchezo wa kuvua.
2. Katika vikundi vidogo vidogo, mwanafunzi mmoja avue kadi kutoka kikapuni na
kuwasomea wanakikundi.
3. Wanafunzi waseme maana ya neno.
4. Waelekeze wanafunzi katika kutamka maneno katika njia sahihi.
Zoezi la 2
1. Katika vikundi waagize wanafunzi kukamilisha mazoezi katika Kitabu cha Mwanafunzi.
Majibu
a) Huyu ni paka.
b) Mimi ni mvulana.
c) Huu ni mpira.
d) Duka hili limefunguliwa.
e) Sasha gari hili.
2. Muulize mmoja katika kila kundi kuwasomea wanafunzi darasani sentensi zilizopangwa
upya.
3. Wape wanafunzi kadi zilizo na maneno mbalimbali. Waelekeze wanafunzi katika
kutunga sentensi kamlifu wakitumia kadi huku wenzao darasani wakisoma sentensi.
50
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Zoezi la 3
1. Wape wanafunzi hadithi fupi zilizo na sentensi fupi fupi. Waagize wanafunzi kusoma
sentensi zilizowekwa rangi katika kitabu cha hadithi wakiwa wawili wawili.
2. Waelekeze wanafunzi kutoka katika kundi moja hadi lingine na kuwasomea
wanafunzi wa makundi hayo mengine hadithi zao fupi.
Zoezi la kufanyia nyumbani
Waulize wanafunzi kuwaambia wazazi/walezi wao kuwapa maandishi ili waendelee kusoma.
Hitimisho
Waagize wanafunzi kusoma ifaavyo nyenzo walizo nazo ili kuboresha uwezo na ujuzi wao wa
matamashi.
Kipindi cha 3: Njia nzuri ya kukaa unapoandika
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze:
1. Kupata stadi za kimsingi za kuandika heru mbalimbali vizuri ili kupata silabi,
maneno na sentensi zilizopangwa nadhifu.
2. Andika kwa mwandiko wako heru, nambari na alama.
Habari za kimsingi
Masomo haya yanalenga kumhami mwanafunzi kwa ujuzi wa kushughulikia uandishi.
Makinikia kusisitiza mkao mzuri wakati wa kusoma na jinsi ya kuweka vitabu na penseli
mezani wakati wa kuandika.
Nyenzo za kujifunzia
Vitabu
Utangulizi
Andika heru ubaoni na uwaagize wanafunzi kuziandika katika vitabu vyao.
51
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Shughuli za ujifunzaji
Zoezi la 1
1. Waulize wanafunzi kuzungumza kuhusu anachokifanya msichana aliye katika picha.
2. Waelekeze wanafunzi kuhusu jinsi ya kuketi, kushika kalamu na kuweka madaari
yao katika nafasi nzuri wakiandika.
Zoezi la 2
1. Waambie wanafunzi wakutazame ukiandika na kupanga heru a, b, ch, d, e, f, g ubaoni.
2. Tumia matendoishara kuwaonesha wanafunzi maumbo ya heruf za abjadi/alfabeti.
3. Wanafunzi waigize mwendo wa mkono hewani unapoandika heru za abjadi/alfabeti
ubaoni.
4. Waruhusu wanafunzi kufanya mazoezi ya kuandika abjadi/alfabeti wakiwa katika
vikundi vya wawili wawili.
5. Waambie wanafunzi kuandika heru za abjadi/alfabeti katika madaari yao.
Zoezi la 3
1. Waweke wanafunzi katika makundi, waandike heru za kwanza za vifaa vilivyo
katika picha kwenye karatasi nzito.
2. Wanafunzi watumie mkasi kukata heru walizoandika.
3. Wanafunzi waoneshe darasani heru walizokata.
Zoezi la kufanyia nyumbani
Waambie wanafunzi kufanya mazoezi ya kuandika nambari 1-10 na heru za abjadi/alfabeti
nyumbani.
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kufanya mazoezi ya kuandika na kupanga nambari na heru ifaavyo ili
kuboresha mwaandiko wao.
Kipindi cha 4: Kutambua na kuweka heru kwenye makundi
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze:
1. Kuandika kwa hati nadhifu inayosomeka kuwasiliana ifaavyo.
2. Kuimarisha kasi na wepesi wa mwandiko.
52
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Utangulizi
Waulize wanafunzi kutaja shughuli zinazoweza kuimarisha usongeshaji wao wa mikono na
vidole. Wanafunzi wanaweza kutaja aina yoyote ya mchezo unaohusisha ujuzi wa kusongesha
sehemu zao za mwili.
Shughuli za ujifunzaji
Zoezi la 1
1. Waagize wanafunzi kutazama picha katika kitabu chao cha kusoma.
2. Wanafunzi wazungumze kuhusu wanachokiona.
Zoezi la 2
1. Wanafunzi wakutazame ukipanga punje kwa makini kwa kutumia heru kubwa za
abjadi/alfabeti.
2. Waagize wanafunzi wakiwa katika vikundi vya wawili wawili wapange punje za heru
tano za kwanza za alfabeti/abjadi.
3. Mwanafunzi apange punje zake peke yake za heru sita na saba za abjadi/alfabeti.
Zoezi la kufanyia nyumbani
1. Waagize wanafunzi kukata picha, maumbo ya heru na nambari kutoka katika majarida
au magazeti kwa kutumia mkasi.
2. Waelekeze wanafunzi kuzibandika katika vitabu vya sanaa.
Hitimisho
Waagize wanafunzi kutumia zoezi lao la nyumbani ili kuimarisha utendaji wa viungo vya
mwili.
Kipindi cha 5: Andika vyema
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kutumia alama za kimsingi za
uchapishaji ili kuwasilisha maana iliyokusudiwa.
Utangulizi
Andika heru za abjadi/alfabeti ubaoni na uwaulize wanafunzi kutaja heru za kwenda juu,
53
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
zenye mkia na zenye mkunjo.
Shughuli za ujifunzaji
Zoezi la 1
1. Waagize wanafunzi kuandika heru za abjadi/alfabeti, vokali na maneno vitabuni.
Hakikisha kwamba wanaweka maumbo ifaavyo kwenye vitabu vyao.
2. Wape wanafunzi heru zilizokatwa katika boksi au kikapu. Wanafunzi waweze kupanga
na kuweka heru katika makundi ya heru za kwenda juu, zenye mkia na zenye mkunjo.
Zoezi la 2
1. Waagize wanafunzi kusoma maneno katika vitabu vyao vya kusoma na kuyaandika
katika madaari yao.
2. Waelekeze wanafunzi katika kusoma sentensi zilizo katika vitabu vyao vya kusoma.
Waagize kuandika sentensi hizo katika madaari yao. Hakikisha kwamba wanaanza
sentensi kwa heru kubwa na kukamilisha kwa kikomo.
Zoezi la kufanyia nyumbani
Waagize wanafunzi kuandika katika madaari yao sentensi zilizo katika Kitabu cha
Mwanafunzi ukurasa 69.
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kufanya mazoezi ya kuandika huku wakitumia alama za kuakisha.
54
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Sura ya
4
Koome na Magari yake
(Kitabu cha mwanafunzi ukurasa 69–87)
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Mada ya 1.0
Kusikiliza
Mada ya 2.0
Kuzungumza
Mada ya 3.0
Kusoma
Mada ya 4.0
Kuandika
1.4 Mawasiliano
bora
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kupata msamiati
mbalimbali wa
kutumia kuelezea
hali yake na hali za
watu wengine.
b) kutumia matendo
ishara katika
maongezi kuelezea
hisia na hali zao.
c) kuonyesha
kujali hisia na
hali za wenzake
wanapozielezea.
2.4 Zungumzia
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kutumia msamaiti
alioupata ifaavyo
katika kujieleza.
b) kujihusisha na
watu, vitu na
sehemu katika
mazingira.
c) kuonyesha ari ya
kutumia majina ya
watu, mahali na
vitu vilivyo katika
mazingira hayo.
d) kuonyesha hisia za
kibinafsi, na maoni
kuhusu watu,
mahali na vitu.
3.4 Kusoma
ufahamu
Kukia mwisho
wa somo,
mwanafunzi
aweze:
a) kusoma
maandishi mepesi
kwa ufasaha na
kwa kuelewa.
b) kusoma kwa sauti
maandishi mepesi
na hadithi kwa
njia sahihi.
c) kusoma kwa kasi
inayostahili na
kufurahia.
d) kujenga ari ya
kusoma hadithi
fupi na vifungu.
4.4 Maagizo ya
kuendeleza
maneno
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kutumia ujuzi
wa kukusanya
na kuunganisha
kuandika maneno.
b) kutumia umbo
linalofaa la heru na
utengaji wa nafasi
ya kutosha kuandika
maneno ipasavyo.
c) kujenga ari ya
kutahiji/kuendeleza
na kuandika
maneno mapya.
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa
a) Ujasiri unaendelezwa katika wanafunzi wanapojieleza mbele ya wenzao.
b) Wanakuza ushirikiano na mawasiliano katika kushirikiana katika vikundi.
Aidha, wanakuza uwezo wao wa kujieleza ama kwa kuandika au kuzungumza.
c) Uwezo wa kukiri na kutatua matatizo unakuzwa kutokana na kubuni na
kujieleza na vilevile kupanga mawazo vizuri kwa uwasilishaji.
d) Uwezo wa kidijitali unahimizwa wanapotumia vifaa vya kidijitali kusikiliza
mazungumzo.
e) Wanajifunza umilisi wa kusoma kwa kasi na mawasiliano bora ili wasisitesite
wakati wa kusoma.
55
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Uhusiano na masuala mtambuko
a) Ujuzi wa kujua jinsi ya kuishi na watu wengine katika jamii unakuzwa kutokana
na kushirikiana vyema na wenzao katika makundi na mawasiliano bora.
b) Uraia unakuzwa kutokana na kuwajibikia maadili.
c) Hamu ya kusoma inakuzwa kutokana na kusoma hadithi na kuzifurahia
hadithi zenyewe.
d) Stadi ya maisha inakuzwa ya kuweza kuwa raia mwema wa kushirikiana na
wengine.
Uhusiano na desturi na maadili ya jamii
a) Heshima itahimizwa wakifanya kazi pamoja na wanafunzi wenzao.
b) Upendo unakuzwa kutokana na wanafunzi hawa kushirikiana na wenzao
vizuri katika kufanya kazi.
c) Umoja utahimizwa kutokana na ushirikiano na wenzao katika vikundi.
d) Uwajibikaji unakuzwa kwa kuwa wanajifunza kuwajibika wakitekeleza
majukumu waliyopewa ya kusoma.
e) Uadilifu unakuzwa katika himizo la kuwa raia wema wanaowajali wenzao.
Uhusiano na masomo mengine
a) Mathematical activities wanapojigawa katika vikundi.
b) Religious activities katika himizo la kuthamini na kujali hali na hisia za
wenzao.
Shughuli za kijamii zinazopendekezwa kuchangia ujifunzaji
a) Wanafunzi wanawaeleza watu wa nyumbani kwao kuhusu hali zao.
b) Wanafunzi wanawashirikisha watu walio karibu nao katika mazungumzo.
c) Wanafunzi wanawasomea wazazi /watu wa nyumbani kwao na kujadili kuhusu
maana ya kinachosomwa.
d) Wanafunzi wanashiriki katika mashindano yanayowaleta pamoja wanafunzi
kutoka shule mbalimbali katika jamii hiyo.
Shughuli nyingine zisizo rasmi zinazopendekezwa kuchangia ujifunzaji
a) Wanafunzi wanashiriki katika mazungumzo na wenzao kuhusu hali zao.
b) Wanafunzi wanahimizwa kujieleza hisia zao kwa wanafunzi wenzao.
c) Wanafunzi wanafanya mazoezi ya kuwasomea wenzao maandishi mepesi.
d) Wanafunzi wanacheza mchezo wa matamshi na maendelezo ya maneno nje ya
darasa.
56
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Tathmini zinazopendekezwa
a) Maswali na majibu
b) Kutazama matendo ishara huku wanafunzi wakizieleza hali zao walizopitia
c) Maigizo
d) Mawasilisho ya kisimulizi
e) Imla
f) Mashindano ya kutahiji au kuendeleza maneno
Nyenzo za ujifunzaji zinazopendekezwa
Vifaa vya kurekodi sauti, rekodi za sauti na video, nyenzo za kusoma za wanafunzi,
kadi za picha, maktaba, vitabu vya kusoma, chati zilizo na majina ya watu, mahali na
vitu, tarakilishi, kadi mulishi zilizo na maneno, penseli, chati za kusoma.
Kuwashughulikia wanafunzi wenye mahitaji maalum
Usaidizi kwa wanafunzi wenye uwezo
mbalimbali
Usaidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji
maalum
· Himiza wanafunzi wenye uelewa wa
polepole kushiriki katika mazungumzo
kama maigizo na kusimulia hadithi.
· Wape wanafunzi wenye uelewa wa haraka
kazi nyingi ili kuepuka kuwachosha na
kuzubaa darasani.
· Wape wanafunzi wenye uelewa wa
polepole na haraka nafasi za kutosha
katika shughuli za darasani. Una jukumu
la kuhakikisha kwamba wanafurahiana
na kufurahia kukaa pamoja licha ya
tofauti zao.
· Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa
kuona, wape breli, picha za kugusa na
wale wasioweza kuona vizuri wape
maandishi makubwa.
· Kwa wanafunzi walio na shida ya
kusikia vizuri, tumia lugha ishara au
kumleta mtaalamu wa lugha ishara
kufasiri.
· Wanafunzi ambao hawawezi kuona
mbali wakae mbele darasani na wenye
uwezo wa kuona mbali wakae nyuma.
· Wape wanafunzi wenye ulemavu
majukumu wanayoweza kutekeleza
kama vile kuigiza nafasi ya mwalimu
mkuu au balozi wa kijiji. Wape
usaidizi wa kutosha na kuhakikisha
kwamba wanafunzi wengine wanafanya
hivyo, kwa mfano, kuwasaidia katika
kusukuma kitimagurudumu cha
mwanafunzi mlemavu.
57
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Wiki ya 8
Mpangilio wa vipindi
Kipindi cha 1: Mazungumzo
Tokeo maalum la ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kufanya mazungumzo kikamilifu.
Habari za kimsingi
Wanafunzi wawezeshwe kuwa na mazingira ambamo wanaweza kushiriki mazungumzo
siku baada ya siku maishani. Waeleze wanafunzi kwamba mazungumzo ni hali ya
watu kuzungumziana. Sisitiza haja ya unyenyekevu wakati wa kuzungumza na watu.
Waruhusu wanafunzi kuigiza mazungumzo kwa uwazi wakati wa kipindi hiki.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu
Penseli
Penseli za rangi
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuwaagiza wanafunzi kusoma kimya kimya mazungumzo
katika Kitabu cha Mwanafunzi.
Shughuli za ujifunzaji
1. Wagawe wanafunzi katika vikundi. Waambie kuteua wanafunzi watakaosoma
mazungumzo, mmoja awe mwalimu mkuu, mwingine awe Moraa na wengine
katika kundi wawe wanafunzi.
2. Wasome mazungumzo hayo katika vikundi. Waangalie ili kuhakikisha
kwamba wanafanya kazi nzuri.
3. Pata wanafunzi wawili kujitokeza kuigiza mazungumzo. Mmoja awe
mwalimu mkuu na mwingine Moraa. Wanaosalia wawe wanafunzi. Kwa
kufanya kazi pamoja, wanafunzi hawa wanakuza stadi za ushirikiano na
mawasiliano.
4. Waagize wanafunzi kuandika vitu viwili vinavyowafurahisha na viwili
visivyowafurahisha.
5. Waagize kubadilishana vitabu na kusoma sentensi walizoandika wenzao.
58
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwasisitizia wanafunzi kutumia maneno yenye unyenyekevu
katika mazungumzo, wasichachawizane au kukatizana kauli wakati wa mazungumzo
na kwamba wanapaswa kusikiliza kwa makini wanapokuwa katika mazungumzo.
Tathmini
Waagize wanafunzi kuchora michoro ya nyuso zenye furaha na huzuni. Waagize
kuwaonesha wazazi au walezi wao nyumbani michoro waliyochora.
Kipindi cha 2: Tamka maneno
Tokeo maalum la ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kutumia msamiati mbalimbali katika
mahusiano yao ya kila siku.
Habari za Kimsingi
Kipindi hiki kunanuiwa kuwawezesha wanafunzi kupata misamiati mbalimbali
wanayoweza kutumia katika mahusiano yao ya kila siku. Tanguliza dhana za nomino
na vitenzi. Waambie wanafunzi kwamba kuna maneno yanayotaja vitu (nomino) huku
mengine yakizungumza kuhusu vitu tunavyofanya (vitendo). Wape wanafunzi kadi
mulishi zilizo na maneno mbalimbali na kueleza maana za maneno hayo. Waagize
wanafunzi kusoma maneno hayo kwa sauti baada yako. Shughuli hizi zitamsaidia
mwanafunzi kupanua msamiati wake.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu
Kadi mulishi zilizo na maneno
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuwaagiza wanafunzi kutaja maneno yaliyo kwenye kadi
mulishi baada yako. Waeleze maana ya maneno hayo.
Shughuli za ujifunzaji
1. Eleza dhana za nomino na vitenzi k.v. maneno yanayotaja vitu huitwa
nomino huku maneno yanayozungumza kuhusu vitendo vyetu yanaitwa
vitenzi.
59
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
2. Waelekeze wanafunzi kufanya zoezi la 1. Waulize kutambua maneno
yanayotaja vitu na yale yanayotaja vitendo vya Maria. Waangalie wanafunzi ili
kuhakikisha kwamba wanafanya kazi sahihi.
3. Waonyeshe wanafunzi jinsi ya kufanya zoezi la 2. Waagize wanafunzi
kujiunga nawe. Kifanye kipindi kiwe cha kuvutia kabisa.
Hitimisho
Hitimisha kwa kuwaeleza wanafunzi kwamba sehemu hizo walizogusa wakiimba
wimbo katika zoezi la 2, zinaitwa sehemu za mwili.
Tathmini
Waulize wanafunzi kuwaimbia wazazi wao wimbo waliojifunza katika zoezi la 2
nyumbani.
Kipindi cha 3: Kusoma
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kusoma maandishi mepesi na hadithi
nyepesi kwa njia sahihi na kwa kasi inayofaa.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kinashughulikia umilisi wa kusoma. Mwanafunzi aelekezwe kuepuka
mienendo mibaya ya kusoma kama vile kurudiarudia na kuelekeza kidole kwenye
maandishi ili kuimarisha kasi yao ya kusoma. Juhudi zifanyike kujumuisha stadi za
kusikiliza na kuandika katika kipindi hiki kwa kurejelea mikutadha mwafaka.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu vya wanafunzi
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuwauliza wanafunzi ikiwa wanajua wanyama wowote wa
mwituni na howa (wa kufugwa nyumbani).
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kutazama na kusoma picha zilizo katika Kitabu cha
Mwanafunzi.
2. Washirikishe wanafunzi katika mjadala darasani kuhusu kilicho katika picha
ili kuimarisha stadi ya mawasiliano.
3. Wagawe wanafunzi katika vikundi kurahisisha ujifunzaji na usaidizi
unaowaelekeza wanafunzi kushirikiana.
4. Katika vikundi, waulize wanafunzi kusoma hadithi iliyo katika zoezi la 2 kwa
sauti.
60
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Hitimisho
Waelekeze wanafunzi kuelewa umuhimu wa wanyama wa kufugwa nyumbani na wale
wa mwituni. Isitoshe, waeleze umuhimu wa kutunza mazingira.
Tathmini
Waagize wanafunzi kueleza ujumbe wa hadithi ambayo wamesoma.
Kipindi cha 4: Kujibu maswali ya ufahamu
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kutoa majibu sahihi kwa maswali
kutokana na hadithi. Aidha, waweze kutumia msamiati mpya waliojifunza katika
kutunga sentensi sahili.
Habari za Kimsingi
Kipindi hiki kinahusu stadi ya umilisi. Mwanafunzi ahimizwe kujenga ari ya kusoma
hadithi fupi kikamilifu ili aweze kutoa majibu sahihi kwa maswali. Juhudi zifanywe
kujumuisha stadi za kusikiliza na kuandika kwa kutumia mikutadha mwafaka.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu vya wanafunzi
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuwaagiza wanafunzi kukumbuka hadithi waliyosoma
katika kipindi kilichopita. Waulize wanafunzi wahusika katika hadithi hiyo na kurejelea
hadithi hiyo kwa ufupi.
Shughuli za ujifunzaji
1. Wanafunzi kusoma hadithi; Wanyama
2. Waulize wanafunzi kueleza maana ya maneno mapya.
Hitimisho
Wakumbushe wanafunzi kuhusu jinsi ya kujibu maswali ya ufahamu.
Tathmini
Waagize wanafunzi kujibu maswali ya ufahamu kibinafsi pamoja na zoezi la kufanyia
nyumbani katika Kitabu cha Mwanafunzi.
61
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 5: Kutambua sauti
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kutambua na kutamka sauti za heru
zinazotumiwa mara kwa mara.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kufanya mazoezi ya stadi za kusikiliza na
kuzungumza. Mwanafunzi atahusishwa katika shughuli zinazomhitaji kusikiliza kwa
makini heru na sauti. Hili litasaidia katika kuimarisha stadi ya kusikiliza.
Nyenzo za ujifunzaji
Chati kwenye karatasi ngumu
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuwauliza wanafunzi kusoma maneno katika Kitabu cha
Mwanafunzi. Andika maneno yanayofanana kwenye chati ya karatasi ngumu.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kusoma maneno kwa sauti katika Kitabu cha Wanafunzi
kutoka kushoto hadi kulia.
Jibu linalotarajiwa
Zoezi la 1
Kinachofanana ni kwamba vikundi fulani vya maneno vinaanza kwa konsonanti na
heru sawa.
2. Wakiwa wawili wawili, waagize wanafunzi kutamka maneno hayo tena.
3. Zunguka darasa ili kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi anatamka maneno
na kuhakikisha kwamba wanatoa matamshi sahihi. Wasahihishe wanafunzi
ikihitajika.
4. Waelekeze wanafunzi kuimba wimbo wa mchezo mchezo.
5. Wakiwa wawili wawili, waagize wanafunzi kurudia wimbo huo kwa maneno
yaliyotolewa katika Kitabu cha Mwanafunzi.
62
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Majibu yanayotarajiwa
Zoezi la 2
1. /b/a/t/a/
2. /b/a/t/i/
3. /da/wa/ti/
4. /k/a/l/a/m/u/
Hitimisho
Hitimisha kwa kuwauliza wanafunzi kufanya mazoezi ya kusoma sauti za heru na
silabi katika maneno kutoka kwa wimbo, mchezo mchezo’.
Tathmini
Waagize wanafunzi kukamilisha kazi ya zoezi la 2 katika vitabu vyao vya kibinafsi.
Wiki ya 9
Kipindi cha 1: Tuzungumze
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kutumia msamiati alioupata kuzungumza
kuhusu watu, maeneo au vifaa katika mazingira yao.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitamsaidia mwanafunzi kufanyia mazoezi stadi ya kusikiliza na
kuzungumza. Mwanafunzi atajihusisha katika shughuli zinazomhitaji kutazama kwa
makini picha kisha kueleza kwa kuzungumza kile alichokiona, ili kuinua stadi ya
mawasiliano na ubunifu.
Nyenzo za ujifunzaji
Chati
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza somo kwa kumwambia mwanafunzi atazame picha kwenye Kitabu cha
Mwanafunzi kwa makini.
63
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kutambua kilicho kwenye picha.
2. Waweke katika makundi, kisha uwaambie wajibu maswali kwenye Kitabu cha
Mwanafunzi. Majibu yoyote yanayohusiana na somo yakubalike.
3. Wakiwa wawili wawili, waambie wanafunzi wafanye jambo fulani huku
wengine wakieleza kinachotendeka.
4. Zunguka darasani ili uhakikishe kuwa kila mwanafunzi anahusika ili kukuza
umoja na ushirikiano.
Hitimisho
Kamilisha kipindi kwa kurudia maelezo ya picha kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
Tathmini
Waambie wanafunzi wajaribu kufanya zoezi la nyumbani kwenye Kitabu cha
Mwanafunzi.
Kipindi cha 2: Kuunda na kusoma maneno
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kufanya mazoezi ya kuunda maneno
na kuendeleza ifaavyo na aunde maneno kwa kucheza mchezo wa maendelezo.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kinawezesha wanafunzi kutambua njia mbalimbali za kuunda maneno
mapya wakiwa peke yao, wakiwa wawili wawili au katika makundi wakitumia
mikakati kama vile maneno ya ghaa, manaeno yanayofanana na uhusiano wa
heru na sauti. Hili litamsaidia mwanafunzi kukuza maarifa ya kutambua na kuishi
na wengine kupitia mawasiliano bora. Litasaidia pia kukuza maadili ya heshima na
uwajibikaji.
Nyenzo za ujifunzaji
a. Vitabu vya kusoma
b. Kadi na chati za alfabeti
c. Wanafunzi
64
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuonyesha heru za alfabeti kwenye chati ubaoni. Cheza
rekodi ya heru za alfabeti. Baada ya wanafunzi kumaliza kusikiliza rekodi, andika
heru kubwa na ndogo.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waambie wanafunzi waandike heru za alfabeti kwa kuangalia jinsi
zilivyoandikwa ubaoni.Waongoze kuandika heru kubwa huku ukizunguka
na kusahihisha inapobidi.
2. Waambie wanafunzi waandike heru ndogo.Waambie wabadilishane vitabu
na kuangalia jinsi wenzao walivyofanya.Waangalie wanafunzi wanaouliza
maswali na kujibu maswali yao huku ukiwaongoza kuandika heru vyema.
3. Waambie wanafunzi waandike majina yao kwa heru kubwa na ndogo.
Waambie wanafunzi wawasomee walioketi nao majina yao. Zunguka darasani
kuhakikisha kuwa wanafunzi hawachanganyi heru kubwa na ndogo
wanapoandika majina yao.
4. Someni maneno kwenye Kitabu cha Mwanafunzi pamoja na wanafunzi.
Waongoze kuandika upya kwa kuandika jinsi yalivyo kwenye Kitabu cha
Mwanafunzi. Sahihisha ifaavyo unapoweza ukizunguka darasani.
5. Rudia kazi hiyo kwa kuwasomea wanafunzi sentensi kitabuni mwao. Soma
sentensi pamoja na wanafunzi.Waambie waandike sentensi upya. Angalia kazi
kwa kuzunguka na kusahihisha inapohitajika.
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwaambia wanafunzi watambue na kuandika heru
za alfabeti ambazo zimerudiwa zaidi ya mara moja katika majina yao. Kipindi
hiki kitaimarisha stadi za maisha za kutambua na kuishi na wengine kupitia
kwa mawasiliano bora.
Tathmini
Waambie wanafunzi wakiwa katika makundi wapange kadi zilizo na heru
ya kwanza ya majina yao. Waruhusu wanafunzi wapate ruhusa ya wazazi wao
kusoma vifungu na sentensi kutoka kwenye magazeti na vitabu.
65
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 3: Tuzungumze
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze:
1. Kufuata sheria za uhusiano wa kijami(kufuatana katika matendo).
2. Kuhusika katika mazungumzo ya kujieleza(jina na jinsia).
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitasaidia wanafunzi kujiboresha ifaavyo kwa kuwasaidia kutaja watu,
vifaa na mahali.Wanafunzi wakiwa wawili wawili watasaidika kuimarisha uwezo wa
mawasiliano na ushirikiano.
Nyenzo za ujifunzaji
Vifaa
Chati za majina ya watu, mahali na vifaa
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwaambia wanafunzi wasalimiane wakiwa wawili.
Wanaposalimiana, wahimize wawaambie wenzao jambo lolote kuwahusu. (Sisitiza
kwamba wanafunzi wajitambulishe kwa kutaja majina yao, jinsia, darasa na umri)
Waambie watazame picha kwenye Kitabu cha Mwanafunzi na kusema kinachotendeka
pichani. Waulize wanafunzi waeleze kinachofanyika pichani. Kubali majibu yote kama
njia ya kupongeza ushiriki wao, kisha usahihishe majibu yenye makosa ifaavyo.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waambie wanafunzi wakiwa katika makundi wajaribu kuigiza mazungumzo
yanayoendelea pichani. Waongoze kwa kuwaruhusu kutumia maneno yao
wanapoigiza.
2. Wahimize wanafunzi wawili wawili waende mbele ya darasa na kuwasilisha
mazungumzo yoyote wanayoona kuwa wameelewa vyema. Hakikisha kuwa
mazungumzo tofauti tofauti yameigizwa. Wahimize wanafunzi wengine
wawapongeze hao wawili baada ya wasilisho.
3. Uliza maswali yaliyo katika zoezi la 1 katika ya Kitabu cha Mwanafunzi.
Baadhi ya majibu
a. Tafadhali, nisaidie penseli.
66
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
b. Nashukuru mama
c. Asante sana kwa zawadi
d. Asante mwalimu
Hitimisho
Kamilisha kipindi kwa kuwaambia wanafunzi wajibu maswali kwenye Kitabu cha
Mwanafunzi.Tathmini jinsi wanafunzi walielewa majibu uliyowapa.
Tathmini
Tathmini uelewa wa kipindi kwa wanafunzi kwa kuwauliza watunge sentensi nyepesi
wakitumia maneno yaliyo kwenye kitabu.
Kipindi cha 4: Kutunga maneno
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze:
a. Kusoma vifungu mbalimbali.
b. Kusoma sentensi kwa sauti akipata maana.
c. Kutambua maana kutoka kwa picha.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kinafaa kumfanya mwanafunzi apate maneno na sentensi nyepesi za
kutumia wanapojieleza katika mazungumzo ya kila siku. Wape wanafunzi muda wa
kutosha kutumia maumbo tofauti ya maneno kisha usahihishe ifaavyo. Kipindi hiki
kinahusisha stadi ya kusikiliza, kutokana na Mawasilano bora(Somo la 1.4) Hata
hivyo, jaribu kujumuisha stadi za kusoma na kusikiliza katika kipindi katika muktadha
ufaao.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu vya kusoma
Utangulizi
Tanguliza somo kwa kuwaambia wanafunzi watazame na kusoma maneno kwenye
picha katika Kitabu cha Mwanafunzi.
67
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Shughuli za ujifunzaji
1. Waongoze wanafunzi kutambua maneno kwenye mti. Waruhusu watambue
na kusoma maneno wanayoweza kuona kwenye mti katika picha iliyo kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi.
2. Waweke wanafunzi katika makundi ya watatu watatu na kuwaruhusu
kutambua maneno yaliyo na sauti zinazofanana.Waongoze wanafunzi ifaavyo
kwa kuzunguka kwenye makundi na kuona kile wanafunzi wanafanya.
3. Ukitambua kikundi kilicho na maneno yenye sauti zinazofanana zilizo bora,
wahimize wawasomee wenzao kwa sauti.
4. Waongoze wanafunzi kutumia jedwali kwenye Kitabu cha Mwanafunzi
kujaribu kuandika maneno yanayofanana na heru za kwanza kwenye jedwali.
5. Waongoze wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kujaribu
kusoma maneno kutoka kwenye jedwali. Waruhusu kubadilishana vitabu na
kuwasomea wenzao maneno watakayochagua.
baba chapati dada kiti yetu shati
beba chaki daari kisu yatima shule
bahari cheti dawati kiatu yangu shuka
bata chura darasa kidole yote shimo
Hitimisho
Waongoze wanafunzi kutumia maneno mepesi waliyojifunza kuunda sentensi
nyepesi. Wanaweza kufanyia nyumbani.
Tathmini
Tathmini uelewa wa mwanafunzi wa kipindi kwa kuwaambia watunge sentensi nyepesi
wakitumia maneno rahisi kwenye picha ya mti kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
Kipindi cha 5: Kutazama picha na kusoma
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kutambua maana ya kifungu kutoka
kwenye picha.
68
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kinawaonyesha wanafunzi jinsi ya kutumia picha kuelewa ujumbe.
Kitawasaidia wanafunzi kutambua na kuelewa vitu na majina kwenye picha.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu vya kusoma
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwaambia wanafunzi watazame picha na kusoma kisa kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waambie wanafunzi wakiwa wawili wawili wasome hadithi kwenye Kitabu
cha Mwanafunzi. Hakikisha kuwa kila mwanafunzi anahusika vilivyo katika
usomaji. Zunguka darasani kuthibitisha kuwa kila mwanafunzi anasoma
hadithi.
2. Wahimize wanafunzi kuambiana walichokielewa kwenye hadithi. Himiza
wanafunzi wakiwa wawili wawili kuzungumziana wakisikilizana. Hili litakuza
stadi za kimaisha za kujua jinsi ya kukaa na wengine kupitia kwa mawasiliiano
bora na kukuza heshima miongoni mwao.
3. Waambie wakiwa wawili wawili wasonge mbele ya darasa na kuwasomea
wengine hadithi kwa sauti. Sikiliza kwa makini wanafunzi wakisoma hadithi
na usahihishe inapofaa.
4. Wape wanafunzi majibu ya maswali kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
Majibu
1. Bluu, kijani, nyekundu
Hitimisho
Waongoze wanafunzi kutumia msamiati kwa kutambua maana kutoka kwa picha na
kuunda sentensi nyepesi.
Tathmini
Waambie wanafunzi wawambie wenzao hadithi ya Paka Mkubwa. Waambie wanafunzi
watunge sentensi nyepesi wakitumia maneno mapya watakayosikia katika hadithi.
69
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Sura ya
5
Simba na panya
(Kitabu cha mwanafunzi ukurasa 86–107)
Matokeo maalum yanayotarajiwa
Mada 1:
Kusikiliza
Mada 2.0:
Kuzungumza
Mada 3.0:
Kusoma
Mada 4.0:
Kuandika
Somo la 1.5:
Mawasiliano bora
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kusikiliza
kwa makini
na kushiriki
kikamilifu katika
mazungumzo
katika miktadha
mbalimbali.
b) kutambua na
kutumia msamiati
unaohusiana na
suala la Mimi,
Familia yangu,
Shule yangu na
Nyumbani kwetu.
c) kufurahia
kubadilishana
nafsi
wakishirikiana
na wenzao katika
mazungumzo.
Somo la 2.5:
Stadi ya kujieleza
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kutumia msamiati
mbalimbali ili
kujieleza ifaavyo.
b) kubadili sauti,
kutamka na
kuweka mkazo
ifaavyo ili
kujieleza ifaavyo.
c) kufurahia
matumizi
ya maneno
ya kiorodha
au kuvuka
kuunganisha.
Somo la 3.5:
Kusoma ufahamu
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kusoma jumbe
nyepesi kwa
ufasaha na
akielewa.
b) kusoma kwa
sauti jumbe na
hadithi fupi kwa
usahihi.
c) kusoma kwa
kasi inayostahili
ili kufurahi
kusoma.
d) kukuza ari
ya kusoma
hadithi fupi kwa
ufahamu.
Somo la 4.5:
Uandishi wa
kibunifu
Kukia mwisho wa
somo, mwanafunzi
aweze:
a) kupanga mawazo
yake.
b) kujifunza usemaji
na usomaji ili
kujihami kwa
maneno.
c) kutumia ujuzi
wa kuandika
kwa kuandika
kisa chenye
mshikamano.
d) kutumia ujuzi
wa kuandika
mazungumzo ili
kusaidia maana
na uwasilishaji.
70
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa
a) Ujasiri unaendelezwa katika wanafunzi wanapojieleza mbele ya wenzao.
b) Wanakuza ushirikiano na mawasiliano katika kushirikiana katika vikundi.
Aidha, wanakuza uwezo wao wa kujieleza ama kwa kuandika au kuzungumza.
c) Uwezo wa kukiri na kutatua matatizo unakuzwa kutokana na kubuni na
kujieleza na vilevile kupanga mawazo vizuri kwa uwasilishaji.
d) Uwezo wa kidijitali unahimizwa wanapotumia vifaa vya kidijitali kusikiliza
mazungumzo.
e) Umilisi wa kujifunza ujifunzaji unakuzwa kutokana na wanafunzi hawa
kufanya mazungumzo na wazazi au walezi wao.
f) Wanajifunza umilisi wa kusoma kwa kasi na mawasiliano bora ili wasisitesite
wakati wa kusoma.
Uhusiano na masuala mtambuko
a) Ujuzi wa kujua jinsi ya kuishi na watu wengine katika jamii unakuzwa kutokana
na kushirikiana vyema na wenzao katika makundi.
b) Stadi ya maisha inakuzwa ya kuweza kuwa raia mwema wa kushirikiana na
wengine.
Uhusiano na desturi na maadili ya jamii
a) Heshima itaendelezwa wakifanya kazi pamoja na wanafunzi wenzao.
b) Umoja utahimizwa kutokana na ushirikiano na wenzao au katika vikundi.
c) Wanajifunza kuwajibika wakitekeleza majukumu waliyopewa ya kusoma na
kutambua sentensi katika vikundi.
Shughuli za kijamii zinazopendekezwa kuchangia ujifunzaji
a) Wanafunzi wanawahusisha wazazi/walezi wao katika mazungumzo katika
mikutadha mbalimbali kama vile nyumbani, kanisani, msikitini nk.
b) Wanafunzi wanafanya mawasilisho katika sherehe na haa mbalimbali.
c) Wanafunzi wanawasomea wazazi/walezi wao kauli fupifupi nyumbani na
kujadiliana nao kuhusu maana.
d) Wanafunzi wanashiriki katika kusimulia hadithi za kubuni wakiwa na watoto
wengine katika jamii.
Shughuli nyingine zisizo rasmi zinazopendekezwa kuchangia ujifunzaji
a) Wanafunzi wanashiriki katika mazungumzo na wenzao kuhusu mada
mbalimbali.
b) Wanafunzi wanafanya mazoezi ya kuwasomea wenzao maandishi mepesi
mepesi.
c) Wanafunzi wanashiriki katika maongezi na mawasilisho ya kuongea.
71
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
d) Wanafunzi wanachangia makala kwa jarida la shule.
Tathmini zinazopendekezwa
a) Kusimulia hadithi (zingatia matumizi ya mianzo ya masimulizi)
b) Maswali na majibu, maigizo, usikilizaji wa kuigiza
c) Kusoma maneno na kauli fupi fupi
d) Wanafunzi wanajipanga kutoa hadithi mmoja na mwingine kusimulia hadithi
na kuandika maneno ya kufafanua picha.
Nyenzo za ujifunzaji zinazopendekezwa
Penseli, kadi za kusoma, picha, vipande vilivyokatwa vya magazeti, vitabu vya hadithi,
kanda za sauti, kanda za video kuhusu mazungumzo yanayohusiana na mada hii,
simu, nyenzo za kusoma, kadi za picha, chati, maktaba, rialia, mipangilio ya hadithi,
maneno funguzi katika hadithi nk.
Kuwashughulikia wanafunzi wenye mahitaji maalum
Usaidizi kwa wanafunzi wenye uwezo
mbalimbali
Usaidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji
maalum
· Himiza wanafunzi wenye uelewa wa
polepole kushiriki katika mazungumzo
kama maigizo na kusimulia hadithi.
· Wape wanafunzi wenye uelewa
wa haraka kazi nyingi ili kuepuka
kuwachosha na kuzubaa darasani.
· Wape wanafunzi wenye uelewa wa
polepole na haraka nafasi za kutosha
katika shughuli za darasani. Una jukumu
la kuhakikisha kwamba wanafurahiana
na kufurahia kukaa pamoja licha ya
tofauti zao.
· Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa
kuona, wape breli, picha za kugusa
na wale wasioweza kuona vizuri wape
maandishi makubwa.
· Kwa wanafunzi walio na shida ya
kusikia vizuri tumia lugha ishara au
kumleta mtaalamu wa lugha ishara
kufasiri.
· Wanafunzi ambao hawawezi kuona
mbali wakae mbele darasani na wenye
uwezo wa kuona mbali wakae nyuma.
· Wape wanafunzi wenye ulemavu
majukumu wanayoweza kutekeleza
kama vile kuigiza nafasi ya mwalimu
mkuu au balozi wa kijiji. Wape usaidizi
wa kutosha na kuhakikisha kwamba
wanafunzi wengine wanafanya
hivyo, kwa mfano, kuwasaidia katika
kusukuma kitimagurudumu cha kwa
mwanafunzi mlemavu.
72
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Wiki ya 10
Mpangilio wa vipindi
Kipindi cha 1: Kushiriki katika mazungumzo
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kusikiliza kwa makini na kushiriki
katika mazungumzo katika miktadha mbalimbali.
Habari za kimsingi
Wanafunzi watashiriki katika mazungumzo katika mikutadha mbalimbali.
Hakikisha kwamba wanafunzi wanashiriki katika kipindi hiki ili waelewe kipengele
cha mazungumzo na kanuni za kuzingatiwa katika mazungumzo. Utawashirikisha
wanafunzi kuhusu aina mbalimbali za mazungumzo kutegemea ufaafu wa umri.
Nyenzo zinazopendekezwa za ujifunzaji
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuwauliza wanafunzi kuzungumza kuhusu njia za kutunza
afya wanazozijua na walivyozijua au mahali walipozisikia. Wazungumzie usa wa
mwili na aina za vyakula vya kuimarisha afya wanavyokula.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waagize wanafunzi kusoma mazungumzo kati ya Yohana na Daktari katika
Kitabu cha Mwanafunzi wakiwa wawili wawili.
2. Mwagize mwanafunzi mmoja kusoma sehemu ya Yohana huku mwingine
akisoma sehemu ya Daktari. Waambie wanafunzi kubadilishana nafasi na
kusoma mazungumzo haya tena.
3. Wapange wanafunzi katika vikundi vidogo vidogo na kuwaagiza kujibu
maswali. Waulize wanafunzi kuandika majibu yao. Hili litaimarisha
stadi za mawasiliano na ushirikiano huku wanafunzi wakishiriki katika
mazungumzo kuhusu walivyokuwa hospitani au wakiwa na daktari.
4. Waagize wanafunzi kuelezana kuhusu marafiki wao wa dhati,
wanachokipenda kuwahusu na wanachokifanya kila mara wanapokuwa
pamoja. Shughuli hii itakuza stadi za maisha katika mwanafunzi, hasa
stadi za kujua na kuishi na wengine kupitia kwa mawasiliano mema.
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwaambia wanafunzi kuzingatia kanuni za mazungumzo kila
mara wakizungumza na kumsikiliza mtu mwingine. Waelekeze kusikiliza wakati mtu
akizungumza na kuzungumza tu wakati ambapo mtu huyo amekamilisha kauli yake.
Waelekeze kusikiliza kwa makini mtu anapokuwa akizungumza.
73
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Tathmini
Waagize wanafunzi kufanya kazi ya kufanyia nyumbani katika Kitabu cha
Mwanafunzi.
Kipindi cha 2: Shughuli zangu za kila siku
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kuwasiliana kwa toni, matamshi
mwafaka na kuzingatia mkazo unaofaa katika maneno ili ajieleze kwa ujasiri.
Habari za kimsingi
Wanafunzi watashiriki katika kuzungumzia ratiba zao za kila siku. Watafanya mazoezi
ya kubadili toni na kutumia matamshi stahifu katika kujieleza kwa ujasiri. Wahimize
wanafunzi wanaoelewa polepole kushirikia katika shughuli na kuwaeleza wenzao
darasani kuhusu mipango yao.
Nyenzo zinazopendekezwa za ujifunzaji
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuwauliza wanafunzi kuzungumza kuhusu shughuli zao za
kila siku ya wiki. Hili litawahimiza wanafunzi kupata ujasiri wa kuzungumza waziwazi
na wenzao katika kipindi kizima.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waagize wanafunzi kutazama picha katika Kitabu cha Mwanafunzi na
kusema wanachokiona mmoja baada ya mwingine.
2. Wakiwa wawili wawili, wanafunzi waelezane wanachokifanya asubuhi kila
siku ya wiki. Mawasiliano na ushirikiano vitakuzwa wanafunzi wakijieleza
kwa wenzao.
3. Shughuli hizi zitakuza uwezo wa mwanafunzi kujieleza huku wakipata ujasiri
wa kujieleza.
4. Katika kujifunza kuhusu jinsi ya kupanga wakati, wanafunzi watajifunza
uwajibikaji na jinsi ya kupanga wakati wao na kutekeleza mipango yao kwa
njia zifaazo.
5. Waruhusu wanafunzi kushiriki katika shughuli za kijamii au hata za shule.
Hili litaimarisha stadi za kujieleza katika wanafunzi na kuimarisha ujasiri
wao wa kusimama na kujieleza kwa watu.
Hitimisho
Katika kuhitimisha kipindi, waagize wanafunzi kuzungumziana katika mijadala
mbalimbali kuhusiana na masuala yanayowaathiri.
74
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Tathmini
Waagize wanafunzi kuandika vitu vitano watakavyofanya kesho na kubadilishana
sentensi hizo na maraki zao shuleni.
Kipindi cha 3: Kusoma kwa sauti
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kusoma kwa ufasaha maandishi
mafupi na kwa kuelewa.
Habari za kimsingi
Wanafunzi watatangulizwa kwa kusoma ufahamu. Watakisia ujumbe wa hadithi kwa
kutazama picha kwenye hadithi kabla ya kusoma hadithi. Hili litakuza uwezo wa
kukiri wa wanafunzi. Hakikisha kwamba wanafunzi wanabadilishana makisio yao
na kusoma hadithi ili kuthibitisha makisio au utabiri wao.
Nyenzo zinazopendekezwa za ujifunzaji
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwauliza wanafunzi kueleza kipindi kisa walichowahi kusoma.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waagize wanafunzi kutazama picha katika hadithi wakiwa katika vikundi na
kusema wanavyoviona vikifanyika katika hadithi.
2. Wanafunzi wasome hadithi wakiwa katika vikundi vya wawili wawili na
kuthibitisha ikiwa makisio yao yalikuwa sahihi. Shughuli hii ya usomaji
itakuza stadi za mawasiliano na ushirikiano katika wanafunzi. Hadithi
itawafunza wanafunzi stadi ya heshima inavyoonyeshwa na simba, ambaye
mwanzoni alimdharau panya na hatimaye akasaidiwa na kuokolewa na huyo
huyo panya.
3. Waelekeze wanafunzi kujadili sababu za kukiri kwamba makisio yao ni
sahihi.
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwaagiza wanafunzi kueleza walichojifunza kutokana na
hadithi na jinsi wanavyoweza kukitumia maishani mwao.
Tathmini
1. Waulize wanafunzi kufanya zoezi la kufanyia nyumbani katika Kitabu cha
Mwanafunzi.
75
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 4: Kujibu maswali kutoka kwa hadithi
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kujibu maswali kutokana na
maandishi aliyosoma.
Habari za kimsingi
a) Waagize wanafunzi kusoma ufahamu na kujibu maswali kutoka kwenye
hadithi.
b) Waagize wanafunzi kusoma hadithi na kuielewa kabla ya kujibu maswali.
Nyenzo za ujifunzaji zinazopendekezwa
Vitabu Vitabu vya hadithi
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuwauliza wanafunzi kubadilishana vitabu na kusoma
majibu ya kila mmoja wao kutokana na kazi ya ziada waliyofanya.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waagize wanafunzi kusoma kisa cha Simba na panya kimya kimya.
2. Waagize wanafunzi kujibu maswali kutoka kwa kifungu.
3. Wanafunzi wajadiliane majibu kutoka kwa kifungu na kulinganisha majibu
yao. Hili litakuza stadi za maisha hasa stadi za kufahamu na kujua jinsi ya
kuishi na watu kupitia kwa mawasiliano bora.
4. Waagize wanafunzi kuandika maneno mapya ambayo wamejifunza katika
hadithi na kutafuta maana ya maneno hayo mapya kama yalivyotumiwa
katika kifungu.
5. Wanafunzi wajadiliane maana wanazopata za maneno mapya. Wasaidie
wanafunzi kupata maana ya maneno wanayoona magumu.
Hitimisho
Kamilisha kipindi kwa kuwaagiza wanafunzi kubadilishana maneno mapya
waliyoandika. Wahimize wanafunzi kujiandikia kamusi zao za maneno mapya
wanayokutana nayo na kupata maana ya maneno hayo.
Tathmini
Waagize wanafunzi kuandika sentensi zozote tano kutokana na hadithi kwa kutumia
maneno mapya waliyoandika.
76
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Kipindi cha 5: Kupimiana muda
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze kusoma katika muda ufaao kwa
kufurahia.
Habari za kimsingi
Wanafunzi watasoma na kupima kasi ya usomaji wao wakiwa wawili wawili. Wape
wanafunzi saa za kukadiria muda wakati wa kipindi hiki. Hakikisha kwamba
wanafunzi wanasoma kwa ufasaha na usahihi na kwamba wanaweza kuelewa ujumbe
wa hadithi huku wakiimarisha kasi yao ya kusoma.
Nyenzo zinazopendekezwa za ujifunzaji
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwaonesha wanafunzi jinsi ya kutayarisha saa zao za kukadiria
muda na jinsi ya kuzisimamisha mwenzao akikamilisha kusoma. Wanafunzi wafanye
mazoezi ya kutumia saa za kukadiria muda kabla ya kusoma hadithi.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waweke wanafunzi katika vikundi vya wawili wawili na uwaagize kutayarisha
saa zao za kukadiria muda.
2. Agiza mwanafunzi mmoja kusoma huku mwenzake akimpimia muda.
Waandike muda wanaotumia kukamilisha hadithi.
3. Mwagize manafunzi huyo mwingine kusoma huku mwenzake aliyesoma
mwanzo akisikiliza na kuandika muda uliotumiwa. Shughuli hizi zitakuza
mawasiliano na ushirikiano kwa kuwa wanafunzi watazifanya pamoja. Hili
litakuza umoja baina ya wanafunzi.
4. Waagize wanafunzi kulinganisha muda waliochukuwa kusoma hadithi baina
yao na kutaja aliyemaliza mbele baina ya jozi hiyo yao.
5. Waulize wanafunzi kutambua aliyechukua muda mfupi kabisa kusoma
hadithi na kuandika kwenye karatasi jina la mwanafunzi huyo na muda
aliotumia kisha wabandike ubaoni.
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwaambia wanafunzi kufanaya mazoezi ya kusoma kibinafsi
na kupima muda wenyewe ili kuimarisha kasi yao ya kusoma.
Tathmini
Waagize wanafunzi kufanya zoezi la kufanyia nyumbani katika Kitabu cha
Mwanafunzi.
77
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Wiki ya 11
Kipindi cha 1: Kuzungumza kujihusu
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa kipindi mwanafunzi aweze:
a) Kutumia msamiati mbalimbali katika kujieleza ifaavyo.
b) Kutambua na kutumia msamiati unaohusiana na mada Mimi, Familia yangu,
Shule yangu na Nyumbani kwetu.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza, hasa
zile zilizo chini ya Somo la 4.5. Jitahidi kuunganisha kusoma na kuandika katika
kipindi kwa kutumia mikutadha ya kufaa.
Nyenzo zinazopendekezwa za ujifunzaji
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwauliza wanafunzi kujaribu kufanya zoezi la kufanyia
nyumbani katika Kitabu cha Mwanafunzi.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kujaza zoezi la 1 katika Kitabu cha Mwanafunzi.
2. Waelekeze wanafunzi na kuwaagiza wajadili katika vikundi.
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Hili litakuza mawasiliano na ushirikiano miongoni mwa wanafunzi na hivyo
kutokeza maadili kama vile heshima na umoja huku wakiwasiliana baina yao katika
shughuli za darasani.
Kipindi cha 2: Kupangia siku yangu
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kubadilisha toni ifaavyo, matamashi
na msisitizo na kujieleza kwa ujasiri. Aidha, aweze kusikiliza na kujibu kwa makini
maagizo na maswali mepesi.
78
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza, hasa
zile zilizo chini ya Somo la 2.5. Jitahidi kuunganisha kusoma na kuandika katika
kipindi kwa kutumia mikutadha ya kufaa.
Nyenzo zinazopendekezwa za ujifunzaji
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwauliza wanafunzi kueleza jinsi walivyojipanga asubuhi hiyo.
Wape mfano wa jinsi ya kupanga siku yao.
Shughuli za ujifunzaji
1. Katika vikundi, wanafunzi wajadili kuhusu jinsi wanavyopanga siku yao.
2. Waweke wanafunzi katika vikundi na uwaelekeze kupanga matukio ya siku.
3. Waagize wanafunzi kubadilishana vitabu na kuelezana kuhusu mipango yao.
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Hili litakuza mawasiliano na ushirikiano miongoni mwa wanafunzi na hivyo kuzua
maadili kama vile heshima na umoja huku wakiwasiliana baina yao katika shughuli
za darasani.
Tathmini
Waambie wenzako au wazazi wakusikilize ukiimba wimbo mlioimba shuleni.
Kipindi cha 3: Kupanga mawazo
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo hili, mwanafunzi aweze kupanga mawazo yake vyema.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza, hasa
zile zilizo chini ya Somo la 4.5. Jitahidi kuunganisha kusoma na kuandika katika
kipindi kwa kutumia mikutadha ya kufaa.
Nyenzo zinazopendekezwa za ujifunzaji
Chati zilizo na maneno ya maagizo na maswali.
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwauliza wanafunzi kutazama picha zilizo katika Kitabu cha
Mwanafunzi.
79
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Tandaza chati zilizo na maneno ya maagizo na maswali.
Shughuli za ujifunzaji
a) Waelekeze wanafunzi kutazama picha zilizo katika Kitabu cha Mwanafunzi.
Katika vikundi, wanafunzi wajadiliane kuhusu wanachokiona.
b) Waweke wanafunzi katika vikundi na uwaelekeze kuandika kinachofanyika
katika picha.
c) Mwelekeze mwanafunzi kuelewa mfuatano wa matukio katika hadithi.
d) Wasaidie wanafunzi kupanga sentensi hizi katika njia sahihi.
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Hili litakuza mawasiliano na ushirikiano miongoni mwa wanafunzi na hivyo
kutokeza maadili kama vile heshima na umoja huku wakiwasiliana baina yao katika
shughuli za darasani.
Tathmini
Kazi ya kufanyia nyumbani
1. Muombe mzazi au mlezi wako kukupa vipande vya magazeti vilivyo na picha.
2. Mwambie mlezi au mzazi wako kinachofanyika katika picha.
Kipindi cha 4: Kusoma
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kujibu maswali na maagizo mepesi kwa
ujasiri kutoka kwa kifaa kingine cha kidijitali.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza, hasa
zile zilizo chini ya Somo la 3.4. Jitahidi kuunganisha kusoma na kuandika katika
kipindi kwa kutumia mikutadha ya kufaa.
Nyenzo zinazopendekezwa za ujifunzaji
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi hiki kwa kuimba wimbo katika Kitabu cha Mwanafunzi ukurasa wa
99.
80
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Shughuli za ujifunzaji
1. Waweke wanafunzi katika vikundi vidogo vidogo.
2. Mpe kila mwanafunzi fursa ya kusoma shairi hili la Siku ya Ardhi’.
3. Wasaidie wanafunzi kujibu maswali.
4. Wahimize wanafunzi kujibu maswali ikihitajika.
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Kipindi hiki kitakuza stadi ya maisha katika kujua na kuishi na wanafunzi wengine
kutokana na mawasiliano mema. Hivyo basi, hakikisha kwamba kila mwanafunzi
anashiriki katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha mawasiliano, ushirikiano na umoja.
Tathmini
Zoezi la kufanyia nyumbani
Kwa usaidizi wa mlezi au mzazi, tumia maneno uliyoandika katika zoezi la 1 kutunga
sentensi.
Kipindi cha 5: Maneno ya kuunganisha
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kufurahia kutumia maneno ya mvuko/
kuunganisha katika kupanga au kufuatanisha matukio.
Habari za kimsingi
Kipindi hiki kitawasaidia wanafunzi kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza, hasa
zile zilizo chini ya Somo la 2.5. Jitahidi kuunganisha kusoma na kuandika katika
kipindi kwa kutumia mikutadha ya kufaa.
Nyenzo zinazopendekezwa za ujifunzaji
Kitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwaweka wanafunzi katika vikundi vya wawili wawili na
kuwaelekeza kusoma ufahamu.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waelekeze wanafunzi kusoma kifungu katika vikundi vidogo vidogo kisha
wakiwa wawili wawili.
2. Waelekeze wanafunzi kujibu maswali kuhusu shughuli hii.
81
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
3. Waagize wanafunzi kubadilishana vitabu.
4. Wahimize wanafunzi kuuliza maswali ikihitajika.
Hitimisho
Wahimize wanafunzi kuuliza maswali inapohitajika.
Kipindi hiki kitakuza stadi ya maisha katika kujua na kuishi na wanafunzi wengine
kutokana na mawasiliano mema. Hivyo basi, hakikisha kwamba kila mwanafunzi
anashiriki katika kazi hii ya darasa ili kuimarisha mawasiliano, ushirikiano na umoja.
Tathmini
Zoezi la kufanyia nyumbani
1. Hakikisha wanafunzi wamekamilisha zoezi hili. Sahihisha ipasavyo.
Wiki ya 12
Kipindi cha 1: Kuzungumza na maraki
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kusikiliza kwa makini na kuhusika
katika mazungumzo ya miktadha mbalimbali.
Habari za kimsingi
Wanafunzi watashiriki katika mazungumzo ya pamoja ya maudhui mbalimbali.
Zingatia ufasaha, usahihi wa maneno na matamshi na stadi ya kubadilishana nafasi.
Hili litahakikisha kuwa kila mwanafunzi amehusika katika shughuli hii ili kuakia
malengo ya kipindi.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwauliza wanafunzi wataje sheria wanazojua zinazodhibiti
mazungumzo. Baadhi ya wanafunzi wajitokeze kujibu swali hili.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waambie wanafunzi wasome mazungumzo kati ya Joyce na Ken kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi wakiwa wawili wawili. Shughuli hii itakuza stadi ya
mawasiliano na ushirikiano.
2. Mwanafunzi mmoja asome sehemu ya Joyce na mwingine sehemu ya Ken.
3. Waambie wanafunzi wabadilishane majukumu.
82
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
4. Waweke katika makundi madogo madogo kisha uwambie waigize
mazungumzo kati ya Ken na Joyce. Hii itasaidia kuleta ujasiri wanapojieleza.
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwaambia wanafunzi wawili warudie somo kwa wenzao.
Tathmini
1. Waambie wanafunzi wasikilize taarifa za habari za jioni baada ya kutoka
shuleni.
2. Waambie wanafunzi waeleze taarifa za habari zilihusu nini wakiwa shuleni
siku itakayofuata.
Kipindi cha 2: Kurekodi mawasiliano
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kurekodi mawasiliano na kuyasikiliza
ili ayatumie katika mawasiliano.
Habari za kimsingi
Wanafunzi watarekodi mazungumzo na kuyacheza. Andaa kifaa cha kurekodi na
uhakikishe kuwa kila mwanafunzi anakikia.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu Vifaa vya kurekodi
Utangulizi
Tanguliza kipindi kwa kuwauliza wanafunzi ikiwa wamewahi kutumia kifa cha
kurekodi au kifaa chochote cha elektroniki. Waambie wanafunzi wawaeleze wenzao
mahali na mbona walitumia kifaa cha elektroniki.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waambie wanafunzi watazame video kwa makini na kujadiliana kuhusu
video wakiwa katika makundi.
2. Warekodi wanafunzi wanapojadiliana kuhusu video. Hii itawakuza katika
ujuzi wa kidijitali. Kujadiliana huku kutainua stadi ya mwanafunzi ya
kuwasiliana na kushikirikiana.
3. Waambie wanafunzi wajadiliane ikiwa wamewahi kuhusika katika video
yoyote na jinsi walivyohusika.
4. Cheza video upya.
Hitimisho
83
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Waambie wanafunzi waseme waliyojifunza kutokana na kipindi hiki. Angalau kila
mwanafunzi apate nafasi ya kutoa hoja moja moja.
Tathmini
Waambie wanafunzi wawambie wazazi au walezi wao waliyojifunza shuleni leo.
Kipindi cha 3: Kuandika sentensi
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kuandika sentensi.
Habari za kimsingi
Waongoze wanafunzi kuandaa hadithi kwa kufuatisha vyema sentensi zilizopangwa
visivyo.Wahimize wanafunzi watumie sentensi hizo kuandika vifungu na aya.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu Kadi
Utangulizi
Tanguliza somo kwa kuwaambia wanafunzi wasome maneno machache kutoka
kwenye kamusi zao kwa wanafunzi wengine.
Shughuli za ujifunzaji
1. Andika maneno kwenye ubao kisha uwateue wanafunzi watatu kuandika
sentensi wakitumia maneno hayo.Wanafunzi wakihusika katika kuandika
sentensi, wataimarisha uwezo wa mawasiliano na ushirikiano. Mfano: Mimi
ninapenda kandanda. Ninapenda kulala.
2. Waambie wanafunzi waandike sentensi vitabuni mwao.
3. Waambie wanafunzi wapange vyema sentensi zilizo kwenye Kitabu cha
Mwanafunzi.
4. Waambie wanafunzi walinganishe sentensi zao na kuwathibitishia majibu
yao.
Majibu sahihi
1. Ninasoma kitabu
i. Anwani ya kitabu ni Simba na Panya.
ii. Kitabu ni cha simba na panya.
iii. Ni kitabu kizuri sana.
5. Waambie wanafunzi waandike sentensi kujihusu, kuhusu familia, nyumbani
kwao na maraki.
84
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
6. Waambie wanafunzi wabadilishane vitabu na kusoma sentensi za wenzao.
Hili litasaidia kukuza umoja.
Hitimisho
Hitimisha kipindi kwa kuwaambia wanafunzi kuelezana waliyojifunza wakati wa
kipindi.
Tathmini
Waambie wanafunzi waandike sentensi tano kuhusu familia zao.
Kipindi cha 4: Jinsi ya kujipanga
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kutumia ujuzi wa kupanga mambo
kuandika hadithi inayotiririka vyema.
Habari za kimsingi
Wanafunzi watatumia hatua za mipango kuandika sentensi na aya. Mwongoze
mwanafunzi jinsi ya kutumia hatua za mipango kupanga shughuli za siku au wiki.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu Penseli
Utangulizi
Tanguliza somo kwa kuwauliza wanafunzi jinsi wao hupanga shughuli za siku.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waambie wanafunzi wasome shughuli katika Kitabu cha Mwanafunzi kisha
waseme wanayoyaona wakiwa katika makundi.
2. Waambie wanafunzi waandike sentensi moja moja kwa kila shughuli ambayo
Jane atafanya.
3. Waambie wanafunzi wabadilishane vitabu na kusoma sentensi za wenzao.
Hili litahimiza shughuli za mawasiliano na ushirikiano.
4. Waambie wanafunzi wachore hatua zao za mipango na waandike
watakayofanya shuleni leo.
Hitimisho
Kamilisha kipindi kwa kuwaambia wanafunzi wawambie wenzao waliyojifunza
wakati wa kipindi.
85
Kimeidhinishwa na KICD-Toleo la 2018
Tathmini
Waambie wanafunzi wachore hatua za mpangilio wa yale watakayofanya baada ya
kutoka shuleni.
Kipindi cha 5: Kusoma sentensi
Matokeo maalum ya ujifunzaji
Kukia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze kusoma vifungu vifupi na hadithi kwa
sauti na usahihi.
Habari za kimsingi
Wanafunzi watasoma sentensi na vifungu kwa sauti. Hili litapima usahihi na
matamshi wakati wa kusoma. Hakikisha kuwa wanafunzi wanashiriki katika shughuli
za kipindi hiki.
Nyenzo za ujifunzaji
Vitabu
Utangulizi
Tanguliza somo kwa kuandika sentensi zifuatazo ubaoni na kuwaambia wanafunzi
wazisome kwa pamoja:
i. Maria alipiga mpira.
ii. Yohana anaenda shuleni.
iii. Tunakunywa maji.
iv. Ninapenda kula.
Shughuli za ujifunzaji
1. Waambie wanafunzi wasome sentensi katika Kitabu cha Mwanafunzi
wakiwa katika makundi. Hili litakuza uwezo wa wanafunzi kuwasiliana na
kushirikiana wanapofanya shughuli hii.
2. Waambie wanafunzi waandike sentensi nne kama za Alex na kuwasomea
wenzao sentensi hizo.
3. Waambie wanafunzi wasome sentensi za wenzao kwa sauti.
Hitimisho
Kamilisha kipindi kwa kuwaambia wanafunzi wazoee kusoma ili wakuze ufasaha,
usahihi na uelewa pamoja na kukuza msamiati wao.
Tathmini
Waambie wanafunzi wakamilishe zoezi la kufanyia nyumbani katika Kitabu cha
Mwanafunzi.