Longhorn
Kiswahili Mufti
Mwongozo wa Mwalimu
Gredi ya 3
Wallah bin Wallah
Jacqueline M. Kinya
Kimechapishwa na:
Longhorn Publishers (Kenya) Ltd.,
Barabara ya Funzi, Eneo la Viwandani,
S.L.P. 18033–00500,
Nairobi, Kenya.
Longhorn Publishers (Uganda) Ltd.,
Ploti 4, Eneo la Vubyabirenge, Ntinda,
S.L.P 24745,
Kampala, Uganda.
Longhorn Publishers (Tanzania) Ltd.,
Barabara Mpya ya Bagamoyo/Garden,
Mikocheni B, Ploti Namba: MKC/MCB/81,
S.L.P 1237, Dar es Salaam, Tanzania.
Longhorn Publishers (Rwanda) Ltd.,
Remera mkabala na Benki ya COGE,
S.L.P 5910,
Kigali, Rwanda.
© Wallah bin Wallah, Jacqueline M.K. 2018
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kupigisha chapa,
kutafsiri au kukitoa kitabu hiki kwa jinsi yoyote ile bila idhini, kwa
maandishi ya Longhorn Publishers Ltd.
Chapa ya kwanza 2018
ISBN 978 9966 64 007 9
Kimepigwa chapa na Autolitho Ltd.,
Barabara ya Enterprise, Eneo la Viwandani,
S.L.P 73476-00200, Nairobi, Kenya.
Utangulizi ....................................................................................................................... vi
Maazimio ya kazi .......................................................................................................... viii
Mpangilio wa funzo ...................................................................................................... ix
SURA YA 1 .......................................................................................... 1
MADA KUU 1: SHAMBANI ................................................................ 1
Mada Ndogo 1: Sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja .................................... 4
Mada Ndogo 2: Msamiati wa shambani ................................................................... 13
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ......................................... 16
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi ............................................................................. 20
Mada Ndogo 5: Kuandika .......................................................................................... 25
Mada Ndogo 6: Sarufi: Nafsi ya tatu, wakati ujao (umoja na wingi) ................... 29
Majibu ........................................................................................................................... 32
SURA YA 2 .......................................................................................... 33
MADA KUU 2: UZALENDO ................................................................ 33
Mada Ndogo 1: Sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja ................................... 36
Mada Ndogo 2: Msamiati kuhusu uzalendo ............................................................ 45
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ......................................... 50
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi ............................................................................ 54
Mada Ndogo 5: Kuandika .......................................................................................... 58
Mada Ndogo 6: Sarufi: Matumizi ya -ake na -ako ................................................ 62
Majibu ............................................................................................................................ 65
SURA YA 3 .......................................................................................... 66
MADA KUU 3: MIEZI YA MWAKA .................................................... 66
Mada Ndogo 1: Sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja ................................... 69
Mada Ndogo 2: Msamiati: Majina ya miezi ............................................................. 78
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ......................................... 83
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi .............................................................................. 88
Mada Ndogo 5: Kuandika ............................................................................................ 91
Mada Ndogo 6: Msamiati: Tarakimu 51-100 ............................................................. 95
Mada Ndogo 7: Sarufi: Matumizi ya kikomo (.) ....................................................... 98
Majibu ............................................................................................................................ 101
SURA YA 4 ......................................................................................... 102
MADA KUU 4: KAZI MBALIMBALI .................................................... 102
Mada Ndogo 1: Sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja .................................. 105
Mada Ndogo 2: Msamiati wa kazi mbalimbali ..................................................... 112
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ...................................... 116
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi .......................................................................... 119
Mada Ndogo 5: Kuandika ....................................................................................... 123
Mada Ndogo 6: Sarufi: Ukanusho wa nyakati ............ ......................................... 126
Majibu ........................................................................................................................ 131
SURA YA 5 ........................................................................................ 132
MADA KUU 5: USALAMA ................................................................ 132
Mada Ndogo 1: Msamiati kuhusu usalama ........................................................... 135
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Maagano ......................................... 139
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ....................................... 142
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi ............................................................................. 148
Mada Ndogo 5: Kuandika ........................................................................................... 152
Mada Ndogo 6: Sarufi: Vinyume vya vitendo ......................................................... 155
Majibu ............................................................................................................................ 158
SURA YA 6 ........................................................................................ 159
MADA KUU 5: USAFI WA MAZINGIRA .............................................. 159
Mada Ndogo 1: Msamiati wa usafi wa mazingira ................................................ 162
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ...................................... 166
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi .......................................................................... 170
Mada Ndogo 4: Kuandika ....................................................................................... 175
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya haraka na polepole.................................. 179
Majibu ......................................................................................................................... 183
SURA YA 7 ........................................................................................ 184
MADA KUU 7: DUKANI ................................................................... 184
Mada Ndogo 1: Msamiati wa dukani ..................................................................... 187
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ...................................... ..191
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi ............................................................................ 195
Mada Ndogo 4: Kuandika .......................................................................................... 199
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya alama ya kuuliza (?) ..................................... 203
Majibu ........................................................................................................................... 206
SURA YA 8 ......................................................................................... 207
MADA KUU 8: NDEGE NIMPENDAYE ................................................ 207
Mada Ndogo 1: Msamiati wa ndege mbalimbali ................................................. 209
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ....................................... 214
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi ............................................................................ 218
Mada Ndogo 4: Kuandika ......................................................................................... 221
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya juu ya na chini ya ..................................... 225
Majibu .......................................................................................................................... 228
SURA YA 9 ......................................................................................... 230
MADA KUU 9: SOKONI .................................................................... 230
Mada Ndogo 1: Msamiati wa sokoni ...................................................................... 233
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ....................................... 238
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi ............................................................................. 241
Mada Ndogo 4: Kuandika .......................................................................................... 245
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya ndani ya na nje ya ..................................... 248
Majibu ............................................................................................................................. 252
vi
UTANGULIZI
Lugha ya Kiswahili imesambaa na kutambaa katika Afrika ya Mashariki, Kati
na Afrika nzima hadi duniani kote. Ni wajibu wa mwalimu kuwahamasisha
wanafunzi wake kuipenda lugha ya Kiswahili kwani kuna matumaini ya siku za
usoni. Mwalimu awahimize wanafunzi wake kuwa wanaweza kujiendeleza katika
somo la Kiswahili kupitia kwa: redio, runinga, magazeti, ualimu, tafsiri miongoni
mwa nyanja anuwai.
Jukumu la lugha ya taifa ni kuweza kutambulisha watu wa taifa moja na
kuwatia hisia kuwa wanaungana na kutambulika. Lugha ni kitambulisho muhimu
sana cha watu wa jamii fulani. Kutokana na kusambaa kwa lugha ya Kiswahili,
msamiati wake ulio mzuri, utafiti uliofanyiwa lugha hii na idadi kubwa ya watu
wanaoizungumza ni thibitisho tosha kuwa lugha hii inapaswa kupewa nafasi
mwafaka. Hii ni kwa sababu hii ndiyo lugha ya kutambulisha bara la Afrika katika
ramani ya dunia. Isitoshe, lugha ya Kiswahili ina wajibu wa kuleta mabadiliko ya
kijamii, kisiasa na kiuchumi katika bara la Afrika.
Malengo ya kufundisha Kiswahili katika shule za msingi
Malengo ya kufundisha Kiswahili katika shule za msingi kama
yanavyofafanuliwa na silabasi mpya ni kumwezesha mwanafunzi:
1. Kusikiliza na kuitikia vilivyo kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kuongea lugha ya Kiswahili kwa ufasaha.
3. Kusoma na kuelewa lugha ya Kiswahili.
4. Kujieleza kikamilifu kwa lugha ya Kiswahili kwa kuandika.
5. Kutunga kazi za kisanii kulingana na kiwango cha mwanafunzi.
6. Kuimarisha mazoea ya usomaji bora.
7. Kupenda na kujiendeleza katika somo la Kiswahili baada ya shule ya
msingi.
8. Kuionea fahari na kuikuza lugha ya Kiswahili katika mawasiliano.
9. Kutukuza na kuendeleza Kiswahili sanifu maishani.
10. Kutathmini, kufurahia na kujivunia Kiswahili kama lugha ya taifa na ya
kimataifa.
11. Kutambua na kushiriki katika kupata suluhisho la masuala ibuka
yanayohusu na kuathiri jamii kama vile: afya na UKIMWI, uadilifu, jinsia,
mazingira na teknolojia.
vii
Jukumu la mwalimu katika kutimiza malengo haya
Ili kutimiza malengo haya, mwalimu ana wajibu muhimu. Mwalimu azingatie
mazingira ya shule na kutoa mifano halisi ya vitu au watu wanaopatikana katika
mazingira ya shule. Kuna mazingira ya mjini na ya mashambani.
Mwalimu ana wajibu wa kujitayarisha mapema kabla ya somo kwa kuhakikisha
ana vifaa vya kutumia darasani ili kufanikisha somo. Vifaa hivi viwe vinapatikana
kwa urahisi au kwa bei rahisi iwapo ni vya kununuliwa.
Mwalimu anapaswa kutumia mwongozo huu na kitabu cha wanafunzi na
rasilimali nyingine yoyote itakayofanikisha kipindi chake. Mwalimu asitumie
mwongozo huu kisisisi bali awe mbunifu kulingana na uwezo wa wanafunzi wake
na vifaa vinavyopatikana.
Mwalimu aanze kwa kufundisha dhana sahili kabla ya kufundisha zile
changamano zaidi. Lazima azingatie uwezo wa wanafunzi wake.
Mwalimu anapaswa kuwashirikisha wanafunzi wake kadiri iwezekanavyo
katika somo la Kiswahili. Kwa kuwashirikisha, watakuza stadi zao za kusikiliza,
kuongea, kusoma na kuandika.
Mifano anayotoa darasani, iwe rahisi,sahihi, ya hali ya kila siku na inayoeleweka
kwa wanafunzi kuhusu mazingira yao na kuihusisha na masuala ibuka kama vile:
uadilifu, haki za watoto, Ukimwi, jinsia na teknolojia. Jukumu kubwa la mwalimu
ni kuwahamasisha wanafunzi kuongea, kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili
kwa ufasaha. Hili ni jukumu ambalo mwalimu yeyote wa Kiswahili hawezi
kuepuka.
Lazima mwalimu awe kielelezo kwa wanafunzi wake kwa sababu wanafunzi
hupenda sana kuiga. Awe ni mtu anayeipenda lugha ya Kiswahili na kuionea
fahari ili awatie ari wanafunzi wake kuipenda lugha ya Kiswahili.
Mwalimu mwema ni yule anayejaribu kuwa katika kiwango cha wanafunzi.
Kama ni kuimba, wote wanaimba, kama ni kuigiza naye anaigiza. Mwalimu
sharti awe mchangamfu ili awachangamshe wanafunzi wake. Asifunze mambo
au mada kidhahania tu. Ataje matukio halisi maishani mwa wanafunzi huku
akiwahusisha katika kila hatua darasani. Mwongozo huu ni kama dira kwa
mwalimu katika kutekeleza mambo haya.
Mwalimu ajaribu kutumia rekodi za redio pamoja na video ili kuwavutia
wanafunzi mbali na kuendeleza stadi za kusikiliza na matamshi bora. Mwalimu
awahusishe wanafunzi katika kuchora picha, kuigiza darasani, kuimba na
kuwahusisha katika mijadala ili somo la Kiswahili liwe hai. Mwalimu anaweza
kuwaalika shuleni watu waliobobea katika Kiswahili ili kuwahamasisha wanafunzi
kuipenda na kuionea fahari lugha ya Kiswahili.
viii
Mbinu za kufundisha Kiswahili
Kuna mbinu kadhaa zinazoweza kutumiwa kufundisha somola Kiswahili. Mwalimu
anashauriwa atumie mbinu kulingana na kiwango cha wanafunzi wake, uwezo
wao, mazingira, rasilimali na vifaa vinavyopatikana. Kuna mbinu kama kuigiza,
mijadala, kuwaalika watu wenye ujuzi wa lugha ya Kiswahili (kama waandishi wa
habari, wahadhiri, malenga, watangazaji) na kadhalika. Mbinu ya jadi ni maswali
na majibu lakini bado inatumiwa hasa kutathmini wanafunzi darasani. Michoro
au kuunda picha za vitu mbalimbali na kuwapanga wanafunzi katika vikundi ni
mbinu nyingine. Mwalimu akumbuke kuwa kila mbinu ina faida na upungufu
wake. Mwalimu atumie mbinu inayofaa zaidi na rahisi kwa wanafunzi ili kueleza
dhana inayohusika.
Kazi za wanafunzi
Sharti mwalimu awashirikishe wanafunzi katika somo la Kiswahili. Baadhi ya
shughuli za wanafunzi ni:
Kujibu na kuuliza maswali darasani.
Kusoma makala katika kitabu.
Kujadiliana darasani, kusimuliana hadithi na kukariri mashairi.
Kuchora vifaa mbalimbali.
Kuigiza vitendo mbalimbali.
Kusikiliza wenzao wakisoma, wakiongea au wataalamu walioalikwa.
Kuandika majibu ya maswali mbalimbali.
Vifaa vya kufundisha lugha ya Kiswahili
Mwalimu anaweza kutumia vifaa kama vile:
Kadi Mabango Vifaa halisi vinavyoweza kupatikana
kwa urahisi
Michoro Picha Tarakilishi
Redio Vitabu Simu za mkononi
Chati Video
Maazimio ya kazi
Kwa kawaida, mwalimu huandaa maazimio ya kazi baada ya kupokea silabasi
inayoeleza mada zinazotakiwa kufunzwa katika darasa fulani kwa mwaka mmoja.
Mwalimu sharti ajue sehemu mbalimbali za silabasi na malengo ya somo la
Kiswahili kwa ujumla. Kisha apange mada zake kwa mtiririko kutoka sahili hadi
changamano. Mwalimu apange na kutayarisha maazimio yake ya kazi mwanzo
wa muhula hasa wiki ya kwanza au hata wakati wa likizo.
ix
Maazimio ya kazi humwezesha mwalimu kuandaa vifaa vyake na kupanga
ufundishaji wake kimantiki. Isitoshe, maazimio ya kazi humwezesha mwalimu wa
Kiswahili kuhitimisha mada zilizopo katika silabasi kwa muda ziliotengewa.
Mfano wa maazimio ya kazi
Darasa Muhula Somo Mwaka Jina
Gredi ya
Tatu
Wa kwanza Kiswahili 2017 Ayubu Imani
Wiki Kipindi Mada
Malengo
Nyenzo Shughuli
za darasani
Tathmini Marejeleo Maoni
1 5 Msamiati
wa
shambani
Mwanafunzi
aweze:
a) Kutaja
vifaa vya
shambani.
b) Kutunga
sentensi
kwa
kutumia
majina ya
vifaa vya
shambani.
Michoro
Picha
Vifaa
halisi
Kutaja
vifaa vya
shambani.
Kutunga
sentensi
sahihi kwa
kutumia
majina ya
vifaa vya
shambani.
Kujibu
maswali.
Kutunga
sentensi
sahihi.
Kitabu cha
Mwanafunzi
ukurasa
10-14
Mpangilio wa funzo
Kwa kawaida, mpangilio wa funzo hutayarishwa kutoka kwenye maazimio ya
kazi. Huu ni uandalizi wa awali kabla ya kuingia darasani kufundisha. Mwalimu
anayeingia darasani kufundisha bila mpangilio wa funzo hawezi kutekeleza wajibu
wake ipasavyo kwani hajui aanzie wapi na amalizie wapi. Mpangilio wa funzo
ni dira inayomwongoza mwalimu darasani. Humwezesha mwalimu kukamilisha
mada yake kwa muda uliotengwa bila kwenda kombo. Pia, huchangia katika
kujiamini akiwa darasani. Aidha, humwezesha kutafuta vifaa na vielelezo vingine
atakavyotumia na kuhusisha somo na lile lililopita iwapo panahitajika.
Wakati wa utayarishaji wa mpangilio wa funzo, sharti mwalimu akumbuke
uwezo wa wanafunzi wake, vifaa vinavyopatikana na muda uliotengewa kipindi
fulani. Aidha, sharti awashirikishe wanafunzi katika shughuli mbalimbali huku
akionyesha kazi zake zitakazofanikisha kipindi. Kazi za mwalimu na wanafunzi
ziende sambamba. Kwa mfano, mwalimu akitaja mifano, nao wanafunzi
washirikishwe kutaja.
Mwalimu atumie ubao ipasavyo kwa kuelezea hoja muhimu katika somo.
Ufuatao ni mfano tu wa mpangilio wa funzo katika gredi ya tatu.
x
Mfano wa mpangilio wa funzo
TAREHE WAKATI GREDI SOMO IDADI YA
WANAFUNZI
12.10.17 8.00 - 8.30
3
KISWAHILI 30
Funzo: Msamiati
Mada: Vifaa vya shambani
Malengo: Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze:
(a) Kutambua vifaa vya shambani.
(b) Kutunga sentensi akitumia majina ya vifaa vya shambani.
Marejeleo: Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 10-14
Mwongozo wa Mwalimu, ukurasa 13-15.
Maendelezo ya funzo
- Mwalimu awaulize wanafunzi
majina ya vifaa vya shambani.
- Mwalimu awaambie wataje
vifaa wanavyoona kwenye
michoro waliyopewa.
- Mwalimu awape wanafunzi fursa
ya kutunga sentensi kuhusu vi
faa vya shambani.
- Mwalimu arejelee somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali.
- Awape mazoezi zaidi kuhusu
vifaa vya shambani.
Wanafunzi wataje vifaa vya
shambani wanavyoona, kwa
mfano: jembe, upanga n.k.
- Wanafunzi watunge sen
tensi sahihi wakitumia ma
jina ya vifaa vya shambani.
- Wanafunzi wajibu maswali.
- Wanakili mazoezi zaidi
katika madaftari yao.
Dakika 5Hitimisho
Kiini Dakika
20
Hatua Muda Kazi ya Mwalimu Kazi ya Mwanafunzi
Utangulizi Dakika 5
Ufundishaji wa mada mbalimbali
(i) Ufahamu
Kufunza somo la ufahamu barabara kama yalivyo masomo mengine kunahitaji
mwalimu afanye matayarisho ya kutosha kabla ya kipindi.
xi
Mwalimu anapaswa kufahamu barabara maana ya maneno au msamiati
unaotumiwa katika taarifa. Mwalimu anaweza kuanza kwa kuwauliza wanafunzi
maana ya baadhi ya maneno kabla ya kusoma makala yenyewe. Kisha anaweza
kuwaelezea maneno magumu watakayokumbana nayo katika kifungu. Wanafunzi
washirikishwe kutunga sentensi wakitumia maneno hayo. Mwalimu asahihishe
makosa pindi yanapotokea.
Mwalimu anaweza kuanza kusoma sentensi za kwanza mbili au tatu hivi.
Mwalimu daima akumbuke kuwa yeye ni kielelezo na hana budi kujizatiti katika
matamshi bora. Kisha awaongoze wanafunzi kuisoma taarifa, kwa makini huku
kila mwanafunzi akipata nafasi ya kuisoma. Mwalimu aandike maneno magumu
ubaoni huku akiwaongoza wanafunzi jinsi ya kuyatamka. Kisha awaeleze maana
na matumizi yake.
(ii) Sarufi
Sarufi kwa ujumla ni utaratibu, kanuni au sheria zinazotawala matumizi ya
maneno, maumbo ya maneno na miundo ya sentensi katika lugha fulani. Sarufi
ya Kiswahili ni pana na imetawaliwa na ngeli. Ngeli ni kundi moja la majina
yaliyo na upatanisho sawa wa kisarufi na viambishi sawa vya umoja na wingi.
Kwa mfano:
Umoja Wingi Ngeli
Mtu anakuja. Watu wanakuja.
A - WA
Mara nyingi, wanafunzi hawalichangamkii somo la sarufi, lakini likifunzwa
kwa kuhusishwa na masomo mengine na kutumia vifaa halisi na michoro, somo
litakuwa la kuvutia mno.
(iii) Msamiati
Msamiati ni jumla ya maneno yanayopatikana katika lugha fulani. Msamiati
unaweza kufunzwa kwa kuhusishwa na vipengele vingine kama vile sarufi au
ufahamu. Mwalimu anapofundisha msamiati sharti akumbuke kuwa neno moja
linaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa hivyo, ni vyema kuliweka neno
katika muktadha wa matumizi yake.
(iv) Kusoma na kuandika
Kusoma ni stadi moja ambayo inatiliwa mkazo mno katika silabasi mpya. Kusoma
kwa ufasaha ni tathmini ya kuonyesha kuwa mtu ameimudu lugha husika.
Mwalimu awaongoze wanafunzi kusoma makala ya kila aina kama ufahamu,
magazeti na mashairi.
xii
Mwalimu awaeleze wanafunzi maana ya ushairi. Anaweza kuanza kwa kuwauliza
wataje mifano ya wimbo au nyimbo wanazozifahamu. Kisha anaweza kuwaelezea
shairi kama utunzi au tungo ya kisanaa. Shairi ni wimbo wenye mpangilio maalum
wa lugha unaoelezea wazo fulani kuhusu maisha ya binadamu.
Tathmini
Kutathmini ni mfanyiko endelevu katika mfumo wa elimu. Kutathmini ni jambo
lisiloepukika katika elimu kwa sababu ufundishaji wa Kiswahili au somo jingine
hauwezi kuwa kamilifu bila kutathmini. Kupitia tathmini mwalimu anaweza
kuelewa udhaifu na uwezo wa wanafunzi wake. Kuna mbinu kadhaa za kutathmini
kama vile: kuuliza na kujibiwa maswali darasani, kufanya zoezi katika daftari na
kisha kulisahihisha, kusoma, kuandika na kusimulia hadithi. Katika kutathmini,
mwalimu atumie mbinu inayofaa wanafunzi wake ili kupima stadi husika kama
kusoma, kuandika, kusikiliza, ufahamu, sarufi na kuzungumza.
Mwongozo huu utakuwa dira mufti kwa mwalimu anapowaongoza wanafunzi
katika safari ya kuiendeleza na kuikuza lugha ya Kiswahili.
1
Matokeo maalum
yanayotarajiwa
Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kukia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutambua sauti mbili
zinazotamkwa pamoja ili
kuimarisha matamshi bora;
(b) Kutambua msamiati unaohusiana
na shughuli za shambani ili
kuimarisha mawasiliano;
(ch) Kusikiliza kwa makini masimulizi
kuhusu shambani katika kujenga
usikivu;
(d) Kutambua picha za vifaa
vinavyotumika shambani ili
kuimarisha ufahamu wa hadithi;
(e) Kuandika kisa kifupi kwa hati
nadhifu kulingana na mada ili
kujenga stadi ya uandishi;
(f) Kutambua maneno na viambishi
vinavyotumika kuonyesha nafsi ya
tatu, wakati ujao katika umoja na
wingi ili kuimarisha mawasiliano.
Mwanafunzi atambue sauti /bw/,
/fw/ na /kw/ katika maneno.
Mwanafunzi asome msamiati wa
shambani kama vile: jembe, shoka,
upanga, kifyekeo, plau, trekta, lima,
fyeka, panda na kwekwe katika kadi
na chati.
Mwanafunzi asimulie kuhusu
shambani.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi apewe hadithi yenye
mapengo ajaze kwa maneno
mwafaka.
Mwanafunzi atumie nafsi ya tatu,
wakati ujao hali ya umoja na wingi
katika mazungumzo.
Mada Kuu 1: SHAMBANI
Idadi ya vipindi: 17
Sura ya
1
2
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kazi ya vikundi.
Kushiriki katika vyama vya ushirika shuleni vinavyohusu ukulima.
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Mazingira
Nyenzo:
Michoro au picha za vifaa na shughuli za ukulima;
Vifaa halisi vya ukulima;
Kadi zenye sauti /bw/, /fw/ na /kw/;
Kadi zenye majina yenye sauti /bw/, /fw/ na /kw/;
Rekodi za hadithi na masimulizi bunifu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 1-23;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Mada hii inalenga kuwapa wanafunzi maarifa kuhusu majina ya vifaa mbalimbali
vya shambani, shughuli tofauti za ukulima pamoja na uwezo wa kutamka sauti
/bw/, /fw/ na /kw/ kwa usahihi na ufasaha. Pia, kipengele cha masimulizi na
hadithi bunifu zinazohusisha majina ya vifaa vya shambani pamoja na shughuli
za shambani kitafundishwa hapa. Kama tujuavyo, kilimo ni uti wa mgongo
wa nchi au jamii nyingi duniani. Hii ni kwa sababu kutokana na kilimo watu
hupata vyakula vya kula na vya kuuza ili kujipatia riziki. Chakula hudumisha na
kuendeleza uhai kwa binadamu. Hivyo, kilimo ni shughuli muhimu. Kila mtu,
tajiri au maskini hutia bidii kila siku ili kujipatia chakula. Vyakula hupatikana
shambani kupitia kwa kilimo.
Pia, mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kufahamu matumizi ya nafsi ya
tatu umoja na wingi katika wakati ujao pamoja na kutunga sentensi sahihi kwa
kutumia nafsi ya tatu, wakati ujao.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
Elimu ya maendeleo endelevu; athari za majanga kujua athari za vifaa
vya shambani,
3
Uraia mwema.
Utangamano wa kijamii: kushirikiana katika vikundi.
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watasoma katika mada hii
kuhusu vifaa vya kilimo pamoja na shughuli za shambani ni kama vile:
Msamiati Maana
1.
jembe
kifaa cha kulimia
2.
fyeka
kata nyasi na miti midogo midogo kwa ajili ya upanzi
3.
lima
tayarisha shamba kwa kutifua ardhi kwa jembe au plau
4.
palilia
ondoa magugu kwenye shamba la mazao kwa jembe au
mkono
5.
trekta
chombo chenye injini cha kukokotea plau ya kulima
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Katika ufundishaji wake, mwalimu ahakikishe kuwa ana vifaa maalum vya
kuwasaidia wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali ili kuweza
kuwashirikisha katika ujifundishaji wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa
kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu
anaweza kuwahusisha watafsiri wa lugha ya ishara.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kuona, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya breli pamoja na vifaa vya kunasia sauti. Haya yatawawezesha
wanafunzi hawa kusoma kama wanafunzi wenzao bila vikwazo vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya vipindi
Mada Ndogo 1: Sauti mbili tofauti zinazotamkwa
pamoja
4
Mada Ndogo 2: Msamiati
3
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 5: Kuandika
3
Mada Ndogo 6: Sarufi: Nafsi ya tatu wakati ujao,
umoja na wingi
2
JUMLA: 17
4
Mada Ndogo 1: Sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja
(Idadi ya vipindi: 4)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua sauti mbili zinazotamkwa pamoja ili kuimarisha matamshi bora;
b) Kutamka sauti lengwa ili kuimarisha matamshi bora;
ch) Kusoma silabi za sauti lengwa ili kuimarisha matamshi bora;
d) Kuandika silabi zinazotokana na sauti lengwa ili kuimarisha uandishi bora;
e) Kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa ili
kuimarisha usomaji;
f) Kuandika maneno kutokana na silabi zilizofunzwa ili kuimarisha uandishi
bora;
g) Kusoma hadithi zilizo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kumsaidia
mwanafunzi kutamka sauti husika ili kuimarisha matamshi na usomaji;
h) Kuchangamkia kutamka sauti lengwa ili kuimarisha mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atambue sauti /bw/, /fw/ na /kw/ katika maneno.
Mwanafunzi atamke silabi za sauti lengwa baada mwalimu, pamoja na
mwalimu, akiwa pekee yake, wawili na kama darasa. Mifano ya silabi hizi
ni: bwa, bwe, fya, fye, kwa, kwe, kwi n.k.
Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia (papaya) kutamkia sauti.
Mwanafunzi aweza kusikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi kwa mfano: bwana, mbwa,
fyata, afya, kwao, kwani na kwetu.
Mwanafunzi aandike herufi za sauti alizosoma hewani na vitabuni pamoja
na maneno yanayojumuisha sauti hizo.
Mwanafunzi asikilize imla ya maneno yaliyo na herufi za sauti lengwa na
kuyaandika kupitia kwa mwalimu au vifaa vya teknolojia.
5
III. Nyenzo:
Rekodi zenye sauti /bw/, /fw/ na /kw/;
Kadi zenye maneno yenye sauti /bw/, /fw/ na /kw/;
Kadi zenye sauti /bw/, /fw/ na /kw/;
Mgeni mwalikwa mwenye matamshi mazuri na sahihi;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 2;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Katika mada hii, mwalimu alenge kuwafundisha wanafunzi kuhusu sauti mbili
tofauti zinazotamkwa pamoja na majina ya herufi za Kiswahili kwa kurejelea
vifaa vya shambani na shughuli za kilimo. Sauti zitakazoangaziwa katika
funzo hili ni: /bw/, /fw/ na /kw/. Matamshi mazuri na sahihi ya wanafunzi
yatazingatiwa hapa na kukuzwa zaidi.
Mwalimu aandae mapema vifaa atakavyohitaji na kuvihifadhi kabla ya vipindi
hivi kama vilivyoorodheshwa hapo juu pamoja na vyombo vingine maalum vya
kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu na matatizo mbalimbali.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa alivyovileta darasani. Mwalimu akumbuke kuwa matumizi ya
michoro, picha na vifaa halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha
ufundishaji wa wanafunzi; hasa wale ambao wana ulemavu au matatizo
mbalimbali.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na mazoezi waliyopewa.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu aanze somo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichopita. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
6
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kuchunguza michoro iliyo katika
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 1. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa
kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na michoro hiyo. Baadhi ya maswali
ambayo mwalimu anaweza kuuliza ni kama vile: Mnaona nani kwenye michoro
hii? Mwalimu awaelekeze wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo. Wanafunzi
washirikishwe kwa ufupi kujadiliana kuhusu vifaa vya shambani pamoja na
shughuli mbalimbali za kilimo.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
(i) Sauti /bw/ (vipindi 2)
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 2.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Mnaona vifaa gani?
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu katika makundi yao.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti ya kwanza pekee ya majina hayo. Wanafunzi
watamke sauti /bw/ baada ya mwalimu katika darasa zima kisha wakiwa
wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi atamke sauti hii akiwa pekee yake.
Mwalimu awaombe wanafunzi waandike sauti /bw/ katika madaftari yao kwa
herufi kubwa na herufi ndogo. Yaani: bw na BW.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi bw, ambazo ni: bwa, bwe, bwi, bwo, bwu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi bw. Kwa mfano: bwana, bweka, bwia, bwaga, bweni, bwalo n.k. Mwalimu
awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye silabi za herufi bw
kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Wanafunzi wanalala kwenye bweni.
2. Hili ni bwalo letu.
3. Huyu ni bwana harusi.
7
4. Baba alibwaga chini mzigo.
5. Mbwa anabweka.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /bw/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) bwaga bwa ga
ii) bweni bwe ni
iii) bweka bwe ka
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi bw.
(ii) Sauti /fy/ (kipindi 1)
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 4.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti ya kwanza pekee ya majina hayo. Wanafunzi
watamke sauti /fy/ baada ya mwalimu katika darasa zima kisha wakiwa wawili
wawili na hatimaye kila mwanafunzi atamke sauti hii akiwa peke yake. Mwalimu
awaombe wanafunzi waandike sauti /fy/ katika madaftari yao kwa herufi
kubwa na herufi ndogo. Yaani: fy na FY.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi fy, ambazo ni: fya, fye, fyi, fyo, fyu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za herufi
fy. Kwa mfano: fyeka, fyatua, fyuka, fyonza, fyata n.k. Mwalimu awashirikishe
wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye silabi za herufi fy kwa usahihi.
Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
8
Kwa mfano:
1. Baba anafyeka nyasi.
2. Mbu anafyonza damu.
3. Askari alifyatua risasi.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /fy/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) fyata fya ta
ii) fyeka fye ka
iii) fyuka fyu ka
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi fy.
(iii) Sauti /kw/ (kipindi 1)
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 7.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyomo.
Maswali haya ni kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya
michoro hii. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti ya kwanza pekee ya majina hayo. Wanafunzi
watamke sauti /kw/ baada ya mwalimu katika darasa zima, kisha wakiwa
wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi atamke sauti hii akiwa peke yake.
Mwalimu awaombe wanafunzi waandike sauti /kw/ katika madaftari yao kwa
herufi kubwa na herufi ndogo, yaani: kw na KW.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi kw, ambazo ni: kwa, kwe, kwi, kwo, kwu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi kw. Kwa mfano: kwekwe, kwetu, kwatua, kwingi, kwao n.k. Mwalimu
awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye silabi za herufi
kw kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
9
Kwa mfano:
1. Mwalimu alikuja kwetu.
2. Nimetembea mahali kwingi.
3. Baba ataenda kwao.
4. Huku ni kwake.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /kw/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) kwangu kwa ngu
ii) kwetu kwe tu
iii) kwao kwa o
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi kw.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kusoma hadithi
waliyopewa katika vitabu vyao. Wanafunzi watambue sauti /bw/, /fw/ na
/kw/ katika maneno ya hadithi hiyo.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo hili kuhusu sauti /bw/, /fw/
na /kw/ kwa kuwauliza wanafunzi maswali tofauti kuhusu mambo muhimu
waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo uwezo wa wanafunzi wa kutamka
sauti /bw/, /fw/ na /kw/ kwa usahihi, kutambua na kutamka maneno yenye
sauti hizi kwa usahihi pamoja na kutunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno
yenye sauti hizi walizojifundisha. Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wanaweza kuandika sauti hizo kwa usahihi kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
VI. Majibu
Maswali ya utangulizi, ukurasa 1
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoyaona katika
michoro waliyopewa katika vitabu vyao.
10
Maswali ya makundi, ukurasa 2
(i) Sauti /bw/
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 4
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watambue maneno
yaliyotumia sauti /bw/, kwa mfano:
1. Mbwa anabweka.
2. Jembe hili ni kubwa.
3. Wanafunzi wanalala kwenye bweni.
4. Fisi alibwia chakula kingi.
5. Yule bwana ni afisa.
Zoezi, ukurasa 4
1. Jiwe kubwa.
2. Mbwa anabweka.
3. Hili ni bwawa la maji.
(ii) Sauti /fy/
Maswali ya makundi, ukurasa 5
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
6. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
11
Zoezi, ukurasa 6
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watambue maneno
yaliyotumia herufi fy.
Kwa mfano:
1. Mtoto huyu ana afya.
2. Mbu anafyonza damu.
3. Baba anafyeka nyasi.
4. Askari alifyatua risasi.
Zoezi, ukurasa 6-7
1. Mama ana afya.
2. Kaka anafyeka.
3. Mlevi anafyoa.
4. Simu inafyuka.
(iii) Sauti /kw/
Maswali ya makundi, ukurasa 7
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
6. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 8-9
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watambue maneno
yaliyotumia herufi kw.
Kwa mfano:
1. Gari letu limekwama.
12
2. Kwao kuna harusi.
3. Shamba lina kwekwe nyingi.
4. Chakula kimekwisha.
5. Kaka amekwea mti.
Zoezi, ukurasa 9
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Kwa mfano:
1. Juma ameenda kwao.
2. Paka alikwea mti.
3. Huku ni kwangu.
4. Nitaenda mahali kwingine.
Zoezi la makundi, ukurasa 9
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Kwa mfano:
1. Twende kwetu.
2. Ameenda kwake.
3. Ametembea kwingi.
4. Gari limekwama.
Zoezi la kusoma hadithi, ukurasa 9
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wanatambua sauti /bw/, /fy/ na /kw/
katika maneno ya hadithi waliyosoma.
Maswali ya hadithi, ukurasa 10
Mwalimu atathmini maneno yaliyotumia sauti /bw/, /fy/ na /kw/ katika
hadithi waliyosoma, kwa mfano: bwawa, Bwana, Kwame, anafyeka, afya,
bweni, kwetu, chafya, walibweka
13
Mada Ndogo 2: Msamiati wa shambani
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
(a) Kutambua msamiati unaohusiana na shughuli za shambani ili kuimarisha
mawasiliano;
(b) Kusoma maneno na sentensi kuhusu shambani ili kuimarisha usomaji;
(ch) Kutunga sentensi kwa kutumia msamiati wa shambani ili kuimarisha
mawasiliano;
(d) Kuandika maneno na sentensi zinazojumuisha msamiati wa shambani
katika kujenga uandishi bora;
(e) Kuthamini matumizi ya msamiati wa shambani katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome msamiati wa shambani kama vile: jembe, shoka, upanga,
kifyekeo, plau, trekta, lima, fyeka, panda na kwekwe katika kadi na chati.
Mwanafunzi ataje majina ya vifaa halisi, picha au michoro anavyoonyeshwa.
Mwanafunzi achore maumbo ya vifaa vinavyotumika shambani.
Wanafunzi waambatanishe kadi za maneno na vifaa halisi wakiwa katika
vikundi.
Wanafunzi washiriki katika nyimbo na mashairi kuhusu shambani.
Mwanafunzi aandike majina ya vifaa vinavyotumika shambani.
Mwanafunzi atunge na kusoma sentensi akitumia msamiati wa shambani.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za vifaa na shughuli za shambani;
Vifaa halisi vya shambani;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 10 -14;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
14
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu msamiati wa vifaa vya shambani pamoja na shughuli za
shambani. Mwalimu ahakikishe kuwa ametayarisha vifaa vinavyohitajika
kufundishia funzo hili ili kuwaelekeza wanafunzi ipasavyo. Anaweza kutumia
vifaa halisi vya shambani, michoro au picha za vifaa vyenyewe.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize funzo hili kwa kuwaamkua wanafunzi na kuwauliza maswali
mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi
wajibu maamkuzi ya mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa. Mwalimu
awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika kipindi
kilichotangulia. Wanafunzi wenye matatizo wasaidiwe.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kufahamu msamiati
wa vifaa vya shambani pamoja na shughuli mbalimbali za shambani. Mwalimu
awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha awaombe
watazame michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 10-11. Wanafunzi
wachunguze michoro hiyo na kuijadili. Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi
maswali ya kuwachangamsha kuhusiana na michoro hiyo. Maswali kama vile:
Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya vifaa mnavyoona. Watu hawa
wanafanya nini? n.k. Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu
maswali waliyoulizwa kwa kuwapa kitangulizi kama vile “Mimi ninaona...
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika majadiliano haya. Wanafunzi
wajibu maswali ya mwalimu kulingana na vifaa vya shambani wanavyoona
pamoja na shughuli za shambani wanazoona katika michoro waliyopewa. Kwa
mfano: Mimi ninaona jembe; Mimi ninaona shoka; Mimi ninaona watu wakilima
kwa plau n.k.
15
Baadaye mwalimu awaelekeze wanafunzi kujibu maswali waliyopewa katika
vitabu vyao. Wanafunzi wataje vifaa vya shambani wanavyojua au walivyo
navyo nyumbani kwao, kama vile: jembe, kifyekeo, upanga, reki, shoka, plau,
trekta, uma n.k.
Pia, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufahamu shughuli mbalimbali
za shambani kama vile: kulima, kufyeka, kupalilia, kunyunyizia mimea maji,
kupogoa, kuvuna, kupanda mbegu au miche n.k.
Baadaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi kutamka majina ya vifaa vya
shambani walivyopewa katika kadi mbalimbali na wachore majina ya vifaa vya
shambani.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kuimba wimbo wa shambani
ulio katika vitabu vyao. Mwalimu ahakikishe anamshirikisha kila mwanafunzi
katika shughuli hii. Baada ya kuimba wimbo huo, wanafunzi wajibu maswali ya
wimbo waliyopewa katika vitabu vyao.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika funzo hili.
Wanafunzi wanaopata matatizo katika ujifundishaji wao wasaidiwe.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali tofauti kwa kuchunguza
iwapo wanaweza kutambua na kutaja majina ya vifaa mbalimbali vya shambani.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamefahamu shughuli mbalimbali
za shambani. Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi yaliyo
katika vitabu vyao.
VI. Majibu
Zoezi la michoro, ukurasa 11
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanachoona
kwenye michoro waliyopewa.
2. (a) jembe (b) kifyekeo (ch) reki
(d) wakulima, ng’ombe na plau (e) upanga (f) shoka
3. Jembe au plau
16
4. Shoka au upanga
5. Kifyekeo
6. Watu hawa wanalima kwa kutumia plau.
7. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Zoezi la kulinganisha, ukurasa 12-13
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wanalinganisha kwa usahihi majina pamoja na
shughuli sahihi za shambani.
Maswali ya wimbo, ukurasa 14
1. Upanga, jembe, shoka, kifyekeo, plau, trekta
2. Shambani
3. Kufyeka nyasi
4. Kulima shamba
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kusikiliza kwa makini masimulizi kuhusu shambani katika kujenga usikivu;
b) Kutaja majina ya vifaa vinavyotumika shambani ili kuimarisha stadi ya
kuzungumza;
ch) Kuelezea vifaa vinavyotumika shambani ili kuimarisha stadi ya kuzungumza;
d) Kuelezea shughuli zinazofanyika shambani ili kuimarisha stadi ya
kuzungumza;
e) Kutambua matumizi ya vifaa vinavyotumika shambani ili kuimarisha stadi
ya kuzungumza;
f) Kuthamini umuhimu wa vifaa vinavyotumika shambani.
17
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu vifaa vinavyotumika shambani
kama vile: jembe, shoka, upanga, kifyekeo, plau, trekta, lima, fyeka na panda
akionyeshwa vifaa halisi, picha au michoro.
Mwanafunzi aeleze umuhimu wa vifaa vinavyotumika shambani.
Mwanafunzi aweza kushirikishwa katika nyimbo au mashairi kuhusu vifaa
vinavyotumika shambani.
Mwanafunzi aweza kutazama video inayoonyesha jinsi vifaa mbalimbali
vinavyotumika shambani.
Mwanafunzi anaweza kutumia tarakilishi kutambua vifaa mbalimbali kwa
majina yao.
III. Nyenzo:
Rekodi za masimulizi bunifu kuhusu vifaa na shughuli za shambani;
Michoro au picha za vifaa vya shambani;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Mgeni mwalikwa (mkulima);
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 15-16;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusikiliza masimulizi bunifu
yanayohusu vifaa mbalimbali vya shambani pamoja na shughuli mbalimbali
za shambani ili kujenga stadi yao ya kusikiliza na kuzungumza. Mwalimu
ahakikishe kwamba ametayarisha vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili
kufanikisha ufundishaji wake kama vilivyotajwa hapo juu. Mwalimu anaweza
kumwalika mgeni kama vile mkulima akaja kuzungumza kuhusu vifaa vya
shambani ambavyo yeye huvitumia pamoja na kueleza shughuli za shambani
ambazo yeye hujihusisha nazo shambani kwake.
18
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili wasaidiwe.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza masimulizi bunifu pamoja na stadi ya kuzungumza kupitia kwa
wao wenyewe kuwasimulia wenzao. Masimulizi haya yatahusu vifaa mbalimbali
vya shambani pamoja na shughuli mbalimbali za shambani.
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu
kisha awaombe watazame mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa
15. Wanafunzi katika makundi yao waeleze wanachoona katika mchoro huo
ambapo kuna baba na msichana mdogo wakiwa katika shughuli za shambani.
Baba analima kwa kutumia jembe ilhali msichana huyo anawalisha kuku punje za
mahindi.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
Wanafunzi wajibu maswali waliyopewa kwenye kitabu chao kuhusu mchoro
waliopewa.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi masimulizi bunifu
yafuatayo kuhusu mchoro waliopewa. Mwalimu ahakikishe wanafunzi wote
wanamsikiliza kwa makini. Pia, ahakikishe kuwa anasoma kwa ufasaha, kwa
matamshi sahihi na sauti ya kusikika na ya kuvutia. Iwapo mwalimu ana
matatizo ya kimatamshi, anaweza kumwalika msomaji stadi atakayewasomea
au kuwasimulia wanafunzi hadithi husika.
19
Mfano wa masimulizi
Shamba Letu
Mimi ninaitwa Mueni. Huyu ni baba yangu. Hili ni shamba letu. Sisi
tumepanda mahindi. Baba analima. Tutapanda mboga kwenye sehemu hiyo.
Baba anatumia jembe kulima. Yeye ana bidii sana. Baba amefuga ng’ombe, kuku,
kondoo na mbuzi. Mimi ninapenda kuwalisha kuku. Kuku wetu wanakula mahindi.
Mama yuko jikoni. Anatupikia chakula. Akimaliza atakuja shambani. Atamsaidia
baba kulima. Atakuja na jembe lake.
Baada ya kusomewa au kusimiliwa masimulizi haya, wanafunzi wajaribu katika
makundi yao kuelezana kuhusu masimulizi waliyosikia. Watoe muhtasari
wa masimulizi hayo katika makundi yao. Wanafunzi waelezane kuhusu vifaa
vya shambani pamoja na shughuli za shambani zilizotajwa katika masimulizi
waliyosomewa na mwalimu wao. Baadaye, mwalimu awashirikishe katika
kujibu maswali ya masimulizi waliyopewa. Mwalimu ahakikishe anawasaidia
wanafunzi wanaotatizika katika makundi yao.
Hatimaye, wanafunzi katika makundi yao wasimuliane kuhusu mashamba yao.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali ya kuchunguza iwapo
wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma masimulizi ya kubuni pamoja na
kufahamu vifaa na shughuli za shambani. Pia, mwalimu achunguze iwapo
wanafunzi wamepata maarifa ya kujibu kwa usahihi maswali ya masimulizi.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kufanya mazoezi yaliyo katika
vitabu vyao.
VI. Majibu
Maswali ya mchoro, ukurasa 15
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanachoona
kwenye mchoro husika.
2. Baba analima shamba na Mueni anawalisha kuku mahindi.
20
3. Baba anatumia jembe.
4. Mahindi
5. Ng’ombe, mbuzi na kondoo
6. Wanafunzi wasikilize masimulizi watakayosomewa na mwalimu wao.
Maswali ya masimulizi, ukurasa 16
1. Mueni anawalisha kuku mahindi.
2. Jembe
3. Mahindi/Mihindi
4. Mahindi
5. Nyasi
Zoezi, ukurasa 16
1. Shambani ni mahali pa kulima.
2. Mtu hulima kwa kutumia jembe.
3. Mtu akiwa na mbegu atapanda.
4. Jembe la ng’ombe ni plau.
5. Tunafyeka nyasi ili kufukuza mbu.
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua picha za vifaa vinavyotumika shambani ili kuimarisha ufahamu
wa hadithi;
b) Kusoma hadithi za picha zinazohusu shamba ili kujenga usomaji bora;
ch) Kusikiliza hadithi zikisomwa na mwalimu kuhusu vifaa vinavyotumika
shambani ili kujenga usikivu;
21
d) Kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu shambani ili kupata
ujumbe;
e) Kuchangamkia kusoma hadithi za vifaa vinavyotumika shambani ili
kuendeleza stadi ya usomaji.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
Mwanafunzi asome na wengine darasani, wakiwa wawili wawili na baadaye
asome peke yake.
Wanafunzi waweza kusomeana hadithi wakiwa wawili wawili au katika
vikundi.
Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kwa kutumia vifaa vya teknolojia k.m.
tarakilishi na projekta.
Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kwa kutumia kitabu mbele ya darasa.
Wanafunzi wathibitishe utabiri wao baada ya kusoma hadithi.
Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma.
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kuhusu hadithi aliyosoma.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za vifaa na shughuli za shambani;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu shambani;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 17-20;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
22
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu inayohusu shambani kwa kutaja vifaa
vya shambani pamoja na shughuli mbalimbali za shambani ili kujenga stadi ya
wanafunzi ya kusikiliza na kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba ametayarisha
vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili kama vilivyoorodheshwa hapo
awali. Vifaa hivi vitamsaidia kufanikisha ufundishaji wake. Mwalimu anaweza
kurekodi hadithi kuhusu vifaa na shughuli za shambani ili wanafunzi waisikilize
darasani.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika lililotolewa kwenye vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wasahihishe zoezi walilopewa katika funzo
la hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao,
wasaidiwe.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao
ya kusikiliza pamoja na ya kusoma hadithi za kubuni hasa katika muktadha
wa shughuli za shambani pamoja na vifaa vya shambani. Mwalimu awagawe
wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha awaombe
watazame michoro waliyopewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 17.
Michoro hii ni ya mama na mvulana mdogo wakilima pamoja na watoto wawili
wanaonyunyizia mimea maji. Wanafunzi wachunguze michoro hiyo na kuijadili
katika makundi yao. Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote
katika shughuli hii ya kujadiliana kuhusu michoro iliyopo. Baada ya majadiliano,
wanafunzi waelekezwe kujibu maswali ya michoro waliyopewa katika vitabu
vyao.
23
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kutazama
michoro mingine waliyopewa katika vitabu vyao pamoja na kusoma vifungu
vifupi vifupi vinavyoambatana na michoro hiyo. Mwalimu anaweza kuwasomea
wanafunzi vifungu hivi kisha wao wakasoma baada yake wakiwa wawili na
hatimaye kila mmoja akasoma peke yake. Mwalimu ahakikishe anasahihisha
makosa ya kimatamshi pindi yanapotokea. Michoro iliyopo inaonyesha shughuli
mbalimbali za shambani kama vile: mjomba akilima, kaka akifyeka, dada na
kaka wakipanda mbegu shambani pamoja na mama na baba waking’oa magugu
shambani.
Baada ya wanafunzi kuchunguza michoro iliyopo na kusoma vifungu vifupi
vifupi vilivyoambatanishwa nayo, mwalimu anaweza kuwasomea wanafunzi
hadithi bunifu iliyo katika vitabu vya wanafunzi kuhusu shughuli za shambani.
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa makini. Pia, mwalimu
ahakikishe kuwa anasoma hadithi hiyo kwa matamshi sahihi, kwa ufasaha na
kwa sauti ya kusikika na kuvutia. Baada ya mwalimu kuwasomea wanafunzi
hadithi hiyo, wanafunzi wanaweza kuisoma hadithi hiyo wakiwa wawili wawili
na hatimaye kila mmoja akasoma akiwa peke yake.
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi walisikiliza hadithi ya mwalimu kwa makini,
mwalimu anaweza kuwauliza maswali kutokana na hadithi hiyo. Wanafunzi
wajibu maswali haya katika makundi yao. Mwalimu azunguke darasani ili
kuwasaidia wanafunzi wanaotatizika katika makundi yao. Baadaye, wanafunzi
washirikishwe kujibu maswali ya hadithi waliyopewa katika vitabu vyao.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi bunifu
kuhusiana na muktadha wa shambani. Pia, mwalimu achunguze iwapo
wanafunzi wamepata ufahamu wa msamiati wa shambani na shughuli
mbalimbali za shambani.
Mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wamepata maarifa ya kusoma hadithi
bunifu na kujibu kwa usahihi maswali ya hadithi hiyo.
24
VI. Majibu
Maswali ya utangulizi, ukurasa 17
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanachoona kwenye
michoro waliyopewa, kwa mfano:
1. Ninaona mama na mvulana mdogo wakilima shambani.
2. Watoto wawili wananyunyizia maji mimea yao.
3. Watu hawa wanajishughulisha na shughuli za shambani.
4. Wanalima shamba lao.
5. Watoto wananyunyizia maji mimea yao.
Maswali ya zoezi la kusoma, ukurasa 20
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano:
1. Mjomba analima shamba.
2. Kaka anafyeka nyasi shambani.
3. Dada anapanda mbegu shambani.
4. Mama anang’oa magugu shambani.
5. Baba anang’oa magugu shambani.
Maswali ya hadithi, ukurasa 20
1. Mjomba wangu ni mkulima.
2. Mjomba hulima shambani.
3. Mjomba hufyeka nyasi kwa kutumia kifyekeo.
4. Shamba kubwa hulimwa kwa kutumia trekta au plau.
5. Mjomba hupanda mbegu shambani.
25
Mada Ndogo 5: Kuandika
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi
ya uandishi;
b) Kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
Mwanafunzi aeleze yaliyo muhimu katika uandishi k.v. mwandiko nadhifu,
maudhui, mtiririko n.k.
Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwalimu au
wanafunzi wengine.
Wanafunzi wanaweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.
Mwanafunzi apewe fursa ya kuandika kisa kifupi kinachohusiana na mada.
Kisa hiki kifuate hatua tano za uandishi: maandalizi, nakala ya kwanza,
marejeleo, uhariri na uchapishaji. Vichwa vya visa vinaweza kutofautiana.
III. Nyenzo:
Hadithi bunifu zilizoandikwa kwenye chati kuhusu shughuli za shambani;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Rekodi za hadithi za kubuni kuhusu shughuli za shambani;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 21;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia na kadhalika).
IV. Maandalizi ya somo
Katika mada hii, mwalimu afahamu kuwa somo hili linahusu kukuza stadi ya
mwanafunzi ya kuandika kwa mwandiko nadhifu na kwa kufuata vipengele
26
vya uandishi bora. Katika mada hii, wanafunzi watapata maarifa ya kuandika
visa vifupi vifupi kwa kuzingatia mambo kadhaa kama vile: mwandiko nadhifu,
mtiririko, uhariri, marejeleo, maudhui na maandalizi kabambe. Shughuli hii
itawawezesha wanafunzi kufahamu jinsi ya kuandika visa bunifu kuhusu shughuli
za shambani kisha ujuzi huu utawawezesha kubuni na kuandika visa vifupi
mbalimbali vya miktadha mbalimbali. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta
vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili kama vilivyoorodheshwa hapo awali
ili kufanikisha ufundishaji wake pamoja na ujifundishaji wa wanafunzi hasa
walio na matatizo au ulemavu mbalimbali.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika lililotolewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
kusoma hadithi bunifu kuhusu shughuli za shambani. Wanafunzi wajibu salamu
za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi kusahihisha zoezi walilopewa katika funzo
la hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao,
wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kuandika na hata kubuni visa vifupi vifupi na kuviandika kwenye madaftari
yao kwa mwandiko nadhifu. Mwalimu anaweza kuwaomba wanafunzi kuandika
alfabeti zote za Kiswahili katika madaftari yao kwa herufi ndogo na herufi
kubwa. Alfabeti hapa inajumuisha irabu tano pamoja na konsonanti ishirini
na sita za Kiswahili ili kupata jumla ya herufi thelathini na moja (31) katika
Kiswahili. Shughuli hii ya kuandika alfabeti za Kiswahili itawasaidia wanafunzi
katika kuhakikisha kuwa wanaandika kwa mwandiko nadhifu kwa kuziandika
herufi mbalimbali kwa usahihi.
27
Baada ya shughuli hii ya kuandika alfabeti za Kiswahili, mwalimu awaelekeze
wanafunzi kuandika maneno waliyopewa kwenye kitabu chao kwa herufi kubwa
na herufi ndogo. Mwalimu awape wanafunzi mazoezi zaidi ya maneno na hata
sentensi ambazo wataziandika katika madaftari yao katika herufi ndogo na
herufi kubwa.
Baadaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi kubuni kisa kifupi na kukiandika katika
madaftari yao kwa hati nadhifu. Mwalimu ahakikishe wanafunzi wanazingatia
mambo muhimu ya uandishi bora katika shughuli hii. Wanafunzi wabuni kisa
kuhusu: Mimi na mama shambani
Wanafunzi wajibu maswali yafuatayo kwa ubunifu wao:
1. Ilikuwa siku ya _________.
2. Mimi na mama tulienda _________.
3. Mama alibeba _________.
4. Mimi nilibeba _________.
5. Nilifyeka nyasi kwa _________.
6. Mama alikata miti kwa _________.
7. Mimi nililima kwa _________.
8. Mama alichukua mbegu aka_________.
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wote wanashirikishwa katika zoezi hili. Kila
mwanafunzi abuni kisa chake tofauti kwa kuzingatia maswali waliyopewa katika
muktadha wa kwenda shambani. Mwalimu anaweza kuwaongoza wanafunzi
katika kuandaa nakala ya kwanza ya maelezo yao kisha waihariri nakala hii na
hatimaye kuandika nakala zao safi katika madaftari yao.
Baada ya kukamilisha zoezi hili, kila mwanafunzi apewe fursa ya kusimama mbele
ya wenzake na asome kisa alichobuni. Makosa ya kimatamshi yasahihishwe
pindi tu yanapotokea. Mwalimu ahakikishe amewasaidia wanafunzi kusahihisha
visa vyao iwapo hawakuzingatia mambo muhimu katika uandishi bora kama
vile: maudhui, mtiririko, uhariri na marejeleo.
28
Baada ya shughuli hii, mwalimu ahakikishe amesahihisha madaftari ya wanafunzi
ili kuondoa makosa yoyote ya kimaendelezo na hati isiyo nadhifu. Wanafunzi
walio na matatizo ya kuandika kwa hati isiyo nadhifu wapewe mazoezi zaidi ya
kuandika. Mwalimu awaelekeze zaidi.
Hatimaye, wanafunzi washirikishwe katika kufanya zoezi la kuchora lililo katika
vitabu vyao. Wanafunzi wahakikishe wanachora vifaa vya shambani walivyotaja
katika visa vyao walivyobuni pamoja na kuandika katika madaftari yao maelezo
kuhusu vifaa hivyo.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kubuni na kuandika visa vifupi vifupi
vya kubuni. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa
kuandika kwa mwandiko nadhifu na maendelezo sahihi pamoja na sarufi sahihi.
VI. Majibu
Zoezi la kuandika heru kubwa, ukurasa 21
1. JEMBE 2. UPANGA
3. SHOKA 4. KWEKWE
5. LIMA 6. BWEKA
Zoezi la kuandika, ukurasa 21
Mwalimu atathmini ubunifu na uandishi wa wanafunzi, kwa mfano:
1. Ilikuwa siku ya Jumamosi.
2. Mimi na mama tulienda shambani.
3. Mama alibeba jembe na shoka.
4. Mimi nilibeba kifyekeo na jembe.
5. Nilifyeka nyasi kwa kifyekeo.
6. Mama alikata miti kwa shoka.
7. Mimi nililima kwa jembe.
8. Mama alichukua mbegu akapanda.
29
Zoezi la kuchora, ukurasa 21
Mwalimu atathmini uchoraji wa wanafunzi pamoja na maelezo ya vifaa
walivyochora.
Mada Ndogo 6: Saru: Nafsi ya tatu, wakati ujao (umoja na
wingi) (Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua maneno na viambishi vinavyotumika kuonyesha nafsi ya tatu
na wakati ujao katika umoja na wingi ili kuimarisha mawasiliano;
b) Kutumia nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi katika sentensi
kwa usahihi ili kuimarisha mawasiliano;
ch) Kusoma vifungu vilivyo na nafsi ya tatu, wakati ujao kwa umoja na wingi
ili kujenga usomaji;
d) Kuandika vifungu vilivyo na nafsi ya tatu, wakati ujao kwa umoja na wingi
ili kujenga uandishi bora;
e) Kufurahia kutumia nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi katika
mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atumie nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi katika
mazungumzo.
Mwanafunzi atumie nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi katika
sentensi.
Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia nafsi ya tatu wakati ujao
hali ya umoja na wingi.
Wanafunzi wanaweza kupewa sentensi zinazojumuisha nafsi na nyakati
mbalimbali wazitambue katika vikundi;
Mwanafunzi aweza kupewa zoezi katika tarakilishi ili watumie mbinu ya
kuburuta na kutia kapuni.
30
Mwanafunzi aigize vitendo vya kuashiria nafsi ya kwanza, pili na ya tatu
huku akitunga sentensi.
Mwanafunzi aweza kupata ufafanuzi wa nafsi kwa kutumia vibonzo katika
tarakilishi.
III. Nyenzo:
Michoro ya watu wakitenda vitendo kwa kurejelea nafsi ya tatu;
Chati zenye sentensi katika umoja na wingi za nafsi ya tatu.
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 22-23;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Mwalimu anastahili kutilia maanani kuwa sarufi ni kipengele muhimu katika
ujifundishaji wa wanafunzi ili kuweza kuwahusisha wanafunzi kwa ukamilifu
katika somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla
ya vipindi hivi. Wanafunzi wenyewe watumiwe katika funzo hili kuonyesha
matumizi ya nafsi ya tatu, wakati ujao katika hali ya umoja na wingi.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa vyake kwa kukumbuka kuwa matumizi ya michoro, picha na vifaa
halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha ufundishaji wa wanafunzi.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo au ulemavu wa kutosikia au kutoona,
mwalimu ahakikishe ana vifaa au vyombo maalum vya kuwafundishia kama
vile watafsiri wa lugha ishara pamoja na breli.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa
katika vitabu vyao.
31
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu aanze funzo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu
awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika kipindi
kilichotangulia.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili
kisha awashirikishe katika kuchunguza sentensi walizopewa katika kitabu chao
kisha wazisome na kuzijibu. Sentensi hizi zinarejelea nafsi ya tatu katika wakati
ujao. Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
Wanafunzi waweze kubaini kiambishi kinachotumika kuashiria wakati ujao
katika sentensi ambacho ni -ta. Pia, wanafunzi wafahamu viashiria vya nafsi
ya tatu ambavyo ni neno yeye katika umoja na wao katika wingi. Wanafunzi
washirikishwe kutunga sentensi sahihi kwa kutumia nafsi ya tatu katika wakati
ujao hali ya umoja na wingi.
Kwa mfano:
Umoja Wingi
1. Yeye atalima shamba lake. Wao watalima mashamba yao.
2. Yeye atafyeka nyasi. Wao watafyeka nyasi.
3. Yeye atanunua jembe jipya. Wao watanunua majembe mapya.
Kutokana na shughuli hii ya kutunga sentensi, wanafunzi watapata fursa ya
kujifundisha matumizi ya yeye na wao, hali ya umoja na wingi kwa kurejelea
shughuli za shambani katika wakati ujao.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua kuwa yeye na wao ni maneno ya
kuonyesha au kuashiria mtu katika nafsi ya tatu, umoja na wingi. Kiambishi -ta-
hutumika kuonyesha wakati ujao.
Wanafunzi wafanye mazoezi zaidi ya kutunga sentensi sahihi kwa kutumia nafsi
ya tatu hali ya umoja na wingi katika wakati ujao.
32
(ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa kwa kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana
kwa kutumia nafsi ya tatu hali ya umoja na wingi katika wakati ujao.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza kutunga sentensi sahihi
katika umoja na wingi kwa kutumia nafsi ya tatu katika wakati ujao.
VI. Majibu
Maswali ya utangulizi, ukurasa 22
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na ubunifu wao na
muktadha wa swali husika, kwa mfano:
1. Mgeni ataenda kijijini kesho.
2. Walimu watafanya watafundisha darasani.
3. Yeye atasoma kitabu.
4. Msichana atalima shambani.
5. Wanafunzi watafyeka nyasi.
Zoezi, ukurasa 22
1. Wavulana watafyeka nyasi.
2. Wasichana watasoma kesho.
3. Mwalimu atakuja kwetu.
4. Mgeni atafika jioni.
5. Yeye atanisaidia.
Zoezi la kuigiza, ukurasa 22-23
Mwalimu atathmini usomaji wa wanafunzi.
Zoezi la kusoma, ukurasa 23
Mwalimu atathmini usomaji wa wanafunzi.
33
Matokeo maalum
yanayotarajiwa
Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kukia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutambua sauti mbili
zinazotamkwa pamoja ili
kuimarisha matamshi bora;
(b) Kutambua msamiati ambao
unahusiana na uzalendo ili
kuimarisha mawasiliano;
(ch) Kutambua maneno yanayoonyesha
uzalendo ili kuyatumia katika
mawasiliano;
(d) Kutambua rangi za bendera ili
kuimarisha uzalendo;
(e) Kuandika kisa kifupi kwa hati
nadhifu kulingana na mada ili
kujenga stadi ya uandishi;
(f) Kutambua matumizi ya –ake na –ao
ili kuimarisha mawasiliano.
Mwanafunzi atambue sauti /mw/,
/nd/ na /pw/ katika maneno.
Mwanafunzi asome maneno
yanayohusiana na uzalendo kama
vile: umoja, amani, upendo, bendera,
taifa, nchi, raia, gwaride, rangi
za bendera kwa kutumia kadi za
maneno.
Mwanafunzi aeleze baadhi ya
mambo yanayoweza kuimarisha
uzalendo katika nchi yake kwa
kutumia mgeni mwalikwa.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi apewe hadithi yenye
mapengo ajaze kwa maneno
mwafaka.
Mwanafunzi aonyeshe vitu vyake
na vya wengine darasani na
kuvirejelea akitumia –ake na –ao.
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kushiriki katika uskauti shuleni.
Kupandisha bendera shuleni.
Kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa.
Mada Kuu 2: UZALENDO
Idadi ya vipindi: 18
Sura ya
2
34
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Mazingira na somo la Sanaa.
Nyenzo:
Michoro au picha za vitendo vya kizalendo;
Kadi zenye sauti /mw/, /nd/ na /pw/;
Rekodi za sauti /mw/, /nd/ na /pw/;
Mtambaji au msimulizi mwalikwa;
Rekodi za masimulizi bunifu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 24-45;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Uzalendo ni muhimu sana kwa kila mwananchi kwa sababu huwawezesha watu
kuipenda nchi yao, kuithamini pamoja na kuitumikia. Kupitia kwa uzalendo wa
wananchi, taifa hunawiri, hasa uchumi wake pamoja na utangamano wa wananchi
kuboreshwa. Ni vyema kwa wanafunzi katika kiwango hiki kufundishwa kuhusu
uzalendo pamoja na vitendo vya kizalendo kwa kuwa watakua wakithamini nchi
yao na kuiboresha. Mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wote wanashirikishwa
kupata maarifa haya.
Pia, mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kujenga stadi yake ya kutamka
sauti za herufi mbili zinazoambatana ambazo ni: /mw/, /nd/ na /pw/,
kutamka maneno yenye sauti hizi pamoja na kutunga sentensi kwa kutumia
maneno yenye sauti hizi.
Mada hii itaangazia pia kukuza stadi ya wanafunzi ya kusoma na kusikiliza
kupitia kwa masimulizi na hadithi bunifu mbalimbali kuhusu uzalendo ambazo
wanafunzi watasomewa na nyingine watajisomea wenyewe wakiwa wawili
wawili na hatimaye mmoja mmoja.
Kipengele cha sarufi pia kitashughulikiwa katika mada hii ambapo wanafunzi
watafahamu matumizi ya -ake na -ao.
35
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
Uraia: uzalendo - kushiriki katika wimbo wa taifa;
Utangamano wa kijamii;
Amani na maadili.
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii ni kuhusu vitendo vya kizalendo kama vile:
Msamiati Maana
1. amani hali ya kutulia bila vita
2. bendera kitambaa maalum ambacho ni kitambulisho cha taifa
3. taifa nchi
4. wimbo wa taifa wimbo maalum ambao ni kitambulisho cha nchi
5. upendo hali ya kuwaenzi watu wengine
6. uzalendo hali ya kupenda nchi na kujitolea kuilinda
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Mwalimu ahakikishe anawashughulikia na kuwashirikisha wanafunzi walio na
ulemavu na matatizo mbalimbali, kwa kuwa na vifaa muhimu na maalum vya
kuwasaidia wanafunzi hawa katika ujifundishaji wao. Kwa wanafunzi wasio na
uwezo wa kuona, mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya breli pamoja na
vifaa vya kunasia sauti.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri
wa lugha ya ishara. Maandalizi haya yatawawezesha wanafunzi hawa kusoma
kama wanafunzi wenzao bila vikwazo vyovyote.
36
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya vipindi
Mada Ndogo 1: Sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja
5
Mada Ndogo 2: Msamiati
3
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 5: Kuandika
3
Mada Ndogo 6: Sarufi: Matumizi ya -ake na -ao
2
JUMLA: 18
Mada Ndogo 1: Sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja
(Idadi ya vipindi: 5)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
a) Kutambua sauti zinazotamkwa pamoja ili kuimarisha matamshi bora;
b) Kutamka sauti lengwa ili kuimarisha matamshi bora;
ch) Kusoma silabi za sauti lengwa ili kuimarisha usomaji;
d) Kuandika silabi zinazotokana na sauti lengwa ili kuimarisha uandishi bora;
e) Kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa ili
kuimarisha usomaji;
f) Kuandika maneno kutokana na silabi zilizofunzwa ili kuimarisha uandishi
bora;
g) Kusoma hadithi zilizo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kumsaidia
mwanafunzi kutamka sauti husika na kuimarisha matamshi na usomaji;
h) Kuchangamkia kutamka sauti lengwa ili kuimarisha mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atambue sauti /mw/, /nd/ na /pw/ katika maneno;
Mwanafunzi asikilize mwalimu akizitamka silabi zinazotokana na sauti
37
lengwa kisha atamke pamoja na mwalimu na baadaye atamke akiwa peke
yake, wakiwa wawili na wakiwa darasa zima k.m. mwa, mwe, mwi, mwo na
mwu.
Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia kama vile papaya, tarakilishi,
projekta na kipazasauti kumsaidia kuimarisha matamshi yake.
Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
Mwanafunzi atambue sauti alizosoma katika maneno kwa mfano: mwana,
mwananchi, ndoo, ndizi, uzalendo, pwani, pweza na pweke.
Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi na kugawa yaliyo marefu
zaidi katika sehemu ndogo ndogo.
Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa
darasani au wawili wawili;
Mwanafunzi anakili herufi na maneno yanayotokana na sauti alizofunzwa.
Mwanafunzi aandike maneno yanayojumuisha sauti lengwa.
Mwanafunzi asikilize imla ya maneno yaliyo na herufi za sauti lengwa na
kuyaandika.
III. Nyenzo:
Kadi za herufi mw, nd na pw;
Rekodi za sauti /mw/, /nd/ na /pw/;
Kadi zenye maneno yenye sauti /mw/, /nd/ na /pw/;
Mgeni mwalikwa mwenye matamshi mazuri na sahihi;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 25-33;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Mada hii inahusu kukuza stadi ya kutamka pamoja na kutumia sauti za herufi
mbili tofauti zinazotamkwa pamoja za Kiswahili kwa kurejelea vitendo vya
kizalendo. Herufi na sauti zitakazoangaziwa katika funzo hili ni: /mw/, /nd/
na /pw/,
38
Matamshi mazuri na sahihi ya wanafunzi yatazingatiwa hapa na kukuzwa zaidi.
Wanafunzi walio na matatizo ya matamshi wasaidiwe kukuza uwezo wao wa
kutamka kwa usahihi. Wanafunzi wa aina hii washirikishwe katika kufanya
mazoezi kadhaa ya utamkaji. Mwalimu awaongoze. Pia, wanafunzi wengine
wenye matamshi mazuri wanaweza kuwasaidia wanafunzi wanaolemewa.
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama
vilivyotajwa hapo awali. Vyombo maalum vya kuwasaidia wanafunzi wenye
ulemavu na matatizo mbalimbali pia viandaliwe mapema.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa alivyovileta darasani.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwenye vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize somo hili kwa kuwaamkua wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichopita. Wanafunzi wajibu
maamkuzi ya mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili
ili wachunguze mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 24. Mwalimu
awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na
mchoro huo. Baadhi ya maswali ambayo mwalimu anaweza kuuliza ni kama vile:
Mnaona nini kwenye mchoro huu? Watu hawa wako wapi? Mwalimu awaelekeze
wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo na kufahamu vitendo mbalimbali
vya kizalendo ambavyo ni pamoja na kupandisha bendera na kuimba wimbo
wa taifa.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Vipindi 2
i) Sauti /mw/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 25.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali kuhusiana na michoro iliyopo. Maswali
kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
39
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na michoro waliyopewa.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kama vile: mwalimu, mwezi na mwiko kisha watamke herufi mbili
za mwanzo pekee za majina hayo. Wanafunzi watamke herufi mw na hivyo sauti
/mw/ baada ya mwalimu katika darasa zima kisha wakiwa wawili wawili na
hatimaye kila mwanafunzi atamke sauti hii akiwa peke yake. Mwalimu awaombe
wanafunzi waandike herufi mw katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi
ndogo. Yaani: mw na MW.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o,
u kisha watambue silabi za herufi mw, ambazo ni: mwa, mwe, mwi, mwo, mwu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi mw. Kwa mfano: mwana, mwalimu, mwezi, mwema, mwovu, mwiko,
mwingi, mwuzaji, mwananchi n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika
kutamka maneno yenye silabi za herufi mw kwa usahihi. Hatimaye watunge
sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Mimi ni mwananchi mzalendo.
2. Huyu ni mwalimu wa Kiswahili.
3. Mama alitumia mwiko kupika ugali.
4. Mwana huyu ni mdogo.
5. Jirani yetu ni mwema.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutunga sentensi
sahihi kwa kutumia maneno yenye silabi za herufi mw.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /mw/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) mwana mwa na
ii) mwema mwe ma
iii) mwanafunzi mwa na fu nzi
40
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi mw.
Vipindi 2
ii) Sauti /nd/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 28.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Unaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti za herufi mbili za kwanza pekee za majina hayo.
Majina hayo ni: ndovu, ndama na ndizi. Wanafunzi watamke sauti /nd/ baada
ya mwalimu katika darasa zima kisha wakiwa wawili wawili na hatimaye kila
mwanafunzi atamke sauti hii akiwa peke yake. Mwalimu awaombe wanafunzi
waandike herufi nd katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
Yaani: nd na ND.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi nd, ambazo ni: nda, nde, ndi, ndo, ndu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi nd. Kwa mfano: ndani, ndege, ndizi, ndoo, ndugu, ndimu, ndengu n.k.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye silabi
za herufi nd kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Huyu ni ndugu yake.
2. Ndizi zote zimeiva vizuri.
3. Ndege amepaa angani.
4. Mama ameenda sokoni kununua ndimu.
5. Wageni wamekaa ndani ya nyumba.
41
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutunga sentensi
sahihi kwa kutumia silabi za herufi nd.
Baadaye, wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi
katika maneno yaliyo na sauti /nd/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) ndimu ndi mu
ii) ndani nda ni
iii) ndovu ndo vu
Mwisho, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi nd.
Kipindi 1
iii) Sauti /pw/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaombe wachunguze maneno waliyopewa kwenye kadi zilizo katika Kitabu
cha Mwanafunzi, ukurasa 31. Mwalimu awasomee wanafunzi maneno ya kadi
hizi kwa sauti ya kusikika na matamshi sahihi. Baadaye, awaelekeze wanafunzi
wasome baada yake wakiwa wawili na hatimaye kila mwanafunzi apewe fursa
ya kusoma maneno hayo akiwa peke yake. Mwalimu ahakikishe anakosoa
makosa ya kimatamshi ya wanafunzi pindi tu yanapotokea. Iwapo mwalimu
ana matatizo ya kimatamshi, anaweza kumwalika msomaji stadi akawasomea
wanafunzi maneno kwenye kadi walizopewa kwa ufasaha kisha wanafunzi
wakasoma baada yake. Maneno haya yanahusisha sauti /pw/.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua na kutamka sauti
za herufi mbili za kwanza pekee za maneno ya kadi walizopewa. Wanafunzi
watamke sauti /pw/ baada ya mwalimu katika darasa zima kisha wakiwa wawili
wawili na hatimaye kila mwanafunzi atamke sauti hii akiwa peke yake. Mwalimu
awaombe wanafunzi waandike herufi pw katika madaftari yao kwa herufi ndogo
na herufi kubwa, yaani: pw na PW.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi pw, ambazo ni: pwa, pwe, pwi, pwo, pwu.
42
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi
za herufi pw. Kwa mfano: pwani, pweke, mpwa, pweza, pwita n.k. Mwalimu
awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye silabi za herufi pw
kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Mpwa wangu atakuja kesho.
2. Bahari hii ina pweza wengi.
3. Ajuza yule yuko pweke sana.
4. Tutaenda pwani wakati wa likizo.
5. Huyu ni pwagu.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutunga sentensi
sahihi kwa kutumia silabi za herufi pw.
Baadaye, wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi
katika maneno yaliyo na sauti /pw/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) pwani pwa ni
ii) pweke pwe ke
iii) pwagu pwa gu
Mwisho, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi pw.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi kufanya zoezi la imla kwa kuwaomba
wasikilize maneno au sentensi zifuatazo ambazo atawasomea kwa matamshi
sahihi ili waziandike katika madaftari yao kwa mwandiko nadhifu na maendelezo
sahihi:
1. Mpwa wangu alimkamata pwagu.
2. Nguo yake inapwaya.
3. Ajuza mpweke amekuwa mgonjwa.
43
4. Pwani kuna watalii wengi.
5. Hawa pweza wamejaa pwani.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo hili kuhusu sauti /mw/, /nd/
na /pw/ kwa kuwauliza wanafunzi maswali tofauti kuhusu mambo muhimu
waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo uwezo wa wanafunzi wa kutamka
sauti /mw/, /nd/ na /pw/ kwa usahihi, kutambua na kutamka maneno yenye
sauti hizi kwa usahihi pamoja na kutunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno
yenye sauti hizi walizojifundisha.
Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza kuandika sauti hizo
kwa usahihi kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
VI. Majibu
Maswali ya utangulizi, ukurasa 24
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona kwenye
mchoro waliopewa, kwa mfano:
1. Ninaona wanafunzi na walimu wao wakiimba wimbo wa taifa.
2. Wanafunzi wako kwenye gwaride.
i) Sauti /mw/
Maswali ya michoro, ukurasa 26
1. Wanafunzi wataje majina ya michoro waliyopewa ambayo ni: mwalimu, mwezi,
mwiko.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 27-28
1. Huyu ni mwanafunzi.
2. Mzigo mwepesi umepotea.
44
3. Mwizi yule atakamatwa.
4. Mfuko wake umechomwa.
5. Mwaka huu ni mzuri.
Zoezi, ukurasa 28
1. mwe zi
2. mwa ga
3. mwa li mu
4. mwi ba
5. mwe u si
ii) Sauti /nd/
Maswali ya michoro, ukurasa 29
1. Wanafunzi wataje majina ya michoro waliyopewa ambayo ni: ndovu, ndama,
ndizi.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 30
1. Mtoto anakula ndizi.
2. Ndoo nyeupe ina unga.
3. Babu ana ndevu nyingi.
4. Niliota ndoto ya kutisha.
5. Nina ndugu watatu.
Zoezi, ukurasa 31
1. nda ma
2. ndo vu
3. ndu gu
45
4. nde vu
5. ndi zi
iii) Sauti /pw/
Maswali ya kadi za maneno, ukurasa 32
1. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 33
1. Pwagu amekamatwa na polisi.
2. Babu yuko pweke.
3. Mtoto hachapwi.
4. Pweza yuko ndani ya maji.
Zoezi, ukurasa 33
1. pwa ni
2. pwe za
3. pwa ya
4. cha pwa
Mada Ndogo 2: Msamiati kuhusu uzalendo
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati ambao unahusiana na uzalendo ili kuimarisha
mawasiliano;
b) Kusoma msamiati unaohusiana na uzalendo ili kujenga usomaji;
ch) Kueleza maana ya msamiati wa uzalendo ili kuimarisha mawasiliano;
46
d) Kutumia msamiati wa uzalendo katika sentensi sahihi ili kuimarisha
mawasiliano;
e) Kuandika maneno yanayohusiana na uzalendo ili kuimarisha uandishi
bora;
f) Kuthamini uzalendo ili kuwa mzalendo kwa nchi yake.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome maneno yanayohusiana na uzalendo kama vile: umoja,
amani, upendo, bendera, taifa, nchi, raia, gwaride, rangi za bendera kwa
kutumia kadi za maneno.
Mwanafunzi aeleze maana ya msamiati wa uzalendo.
Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu maana za maneno yanayohusiana
na uzalendo.
Mwanafunzi atunge sentensi sahihi kwa kutumia msamiati wa uzalendo.
Wanafunzi watazame video kuhusu vitendo vya kizalendo k.m. mashujaa
wa nchi.
Mwanafunzi atazame michoro na picha zinazolenga maana za maneno
kuhusu uzalendo.
Wanafunzi wajadiliane kuhusu umuhimu wa uzalendo wakiwa kwenye
vikundi.
III. Nyenzo:
Kadi zenye majina ya vitendo vya kizalendo;
Michoro au picha za vitendo vya kizalendo;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 34 - 36;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Msamiati wa vitendo mbalimbali vya kizalendo ni muhimu sana kwa
mwananchi kwani hukuza uzalendo wao kwa taifa lao. Mwalimu aandae vifaa
47
vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama vilivyotajwa hapo
juu pamoja na vyombo vingine muhimu na maalum vya kuwasaidia wanafunzi
wenye ulemavu na matatizo mbalimbali katika kufanikisha ujifundishaji wao.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kuona, mwalimu ahusishe matumizi
ya breli na vinasasauti. Pia, ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kusikia, mwalimu
anaweza kuhusisha matumizi ya lugha ishara katika kuwafundisha wanafunzi
wa aina hii. Vifaa hivi vitawawezesha wanafunzi hawa kujifundisha kama
wanafunzi wengine bila vikwazo vyovyote.
Ni vyema mwalimu ahakikishe kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi
ya wanafunzi wanaotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwa kila
shughuli ya wanafunzi katika vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu awaamkue wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na
msamiati wowote wanaofahamu kuhusiana na uzalendo ambao wamewahi
kuusikia au kuusoma. Wanafunzi wajibu maamkuzi ya mwalimu kisha wajibu
maswali waliyoulizwa.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awashirikishe katika kuchunguza mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi,
ukurasa 34. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali
mepesi kuhusiana na mchoro huo. Baadhi ya maswali ambayo mwalimu
anaweza kuuliza ni kama vile: Unaona nini kwenye mchoro huu? Taja jina la
mchoro huu. Unaona rangi gani kwenye mchoro huu? Mwalimu awaelekeze
wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo na kuelewa mchoro waliopewa
ambao ni wa bendera ya Kenya.
Mwalimu awaelekeze wanafunzi katika makundi yao wajadiliane kuhusu maswali
waliyopewa kuhusiana na mchoro waliopewa. Wanafunzi watambue rangi nne
za rangi ya bendera ambazo: rangi nyeusi, rangi nyeupe, rangi nyekundu na rangi
ya kijani.
48
Wanafunzi washirikishwe zaidi katika kujadiliana kuhusu ishara ya rangi za
bendera ya Kenya.
Kwa mfano:
Rangi ya bendera Maana/Ishara
Rangi nyeusi ishara ya rangi ya ngozi ya wananchi wa
Kenya/Uafrika
Rangi nyeupe ishara ya amani
Rangi nyekundu ishara ya damu iliyomwagika katika
upiganiaji wa uhuru
Rangi ya kijani ishara ya rutuba ya nchi
Wanafunzi katika kila kundi wapewe muda wa kusimuliana kuhusu bendera
ya Kenya na umuhimu wake kwa wananchi wa Kenya. Wanafunzi waelezane
iwapo wamewahi kuiona au hata kuigusa bendera ya nchi ya Kenya. Mwalimu
anaweza kuwatoa darasani na kuwapeleka wanafunzi katika eneo la gwaride
ambapo wanaweza kuiona na hata kuigusa bendera ya Kenya.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi waelekezwe kusoma msamiati wa uzalendo
ulio kwenye kadi mbalimbali zilizo kwenye vitabu vyao. Wanafunzi wasome
msamiati huu kwa matamshi sahihi kisha wajadiliane maana za msamiati huo
katika makundi yao.
Mwalimu anaweza kuwaonyesha wanafunzi picha au michoro ya vitendo
mbalimbali za kizalendo kama vile: kuimba wimbo wa taifa, kudumisha amani
n.k. Wanafunzi wajadiliane kuhusu vitendo hivyo vya kizalendo. Mwalimu
ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
Mwisho, mwalimu anaweza kuandaa video na kuirekodi kwenye tarakilishi
kuhusiana na vitendo vya kizalendo. Video inaweza kuhusu wananchi pamoja
na viongozi mbalimbali wakiadhimisha sherehe ya kitaifa kama vile: kuwatuza
mashujaa wa nchi au wafanyakazi mbalimbali. Mwalimu awashirikishe wanafunzi
wote katika shughuli hii. Mwalimu anaweza kutumia simu ya mkononi.
49
Ahakikishe video yake inaonekana vizuri na kila mwanafunzi. Anaweza kutumia
projekta. Baada ya kutazama video husika, wanafunzi waelekezwe kujibu
maswali waliyopewa katika vitabu vyao kuhusiana na zoezi hili la kutazama
video.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu msamiati wa kizalendo na maana zao kwa
kuzingatia vitendo mbalimbali vya kizalendo.
Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza kuandika kwa usahihi
msamiati wa uzalendo na kuufafanua.
VI. Majibu
Zoezi la mchoro wa bendera, ukurasa 34
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona kwenye
mchoro waliopewa, kwa mfano:
1. Ninaona bendera ya Kenya.
2. Ninaona rangi nyeupe, nyekundu, nyeusi na kijani.
3. Rangi za bendera zinamaanisha:
Rangi nyeusi ishara ya rangi ya wananchi/Uafrika
Rangi nyeupe ishara ya amani
Rangi nyekundu ishara ya damu iliyomwagika katika
upiganiaji wa uhuru
Rangi ya kijani ishara ya rutuba ya nchi
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Zoezi la kusoma, ukurasa 35
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano:
1. Maana za maneno:
a) umoja - hali ya kushirikiana pamoja
50
b) amani - hali ya kuwa bila fujo au vita
ch) upendo - hali ya kuwaenzi watu
d) taifa - nchi
e) nchi - taifa
f) bendera - kitambaa maalum ambacho ni utambulisho wa nchi
g) raia - wananchi wa nchi fulani
h) gwaride - eneo ambapo bendera hupandishwa
Zoezi, ukurasa 36
1. Uzalendo ni kuishi kwa umoja.
2. Bendera ya taifa ina rangi nne.
3. Wanafunzi hujipanga kwenye gwaride.
4. Tunasema umoja ni nguvu.
5. Tunapoimba wimbo wa taifa kila mtu anasimama.
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua maneno yanayoonyesha uzalendo ili kuyatumia katika
mawasiliano;
b) Kusimulia visa vinavyojumuisha mambo yanayoweza kuimarisha
uzalendo ili kujenga stadi ya kuzungumza;
ch) Kusikiliza masimulizi kuhusu uzalendo ili kuimarisha usikivu;
d) Kuthamini umuhimu wa uzalendo katika maisha ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aelezee baadhi ya mambo yanayoweza kuimarisha uzalendo
katika nchi yake kwa kutumia mgeni mwalikwa.
51
Mwanafunzi asimulie visa vinavyojumuisha mambo yanayoweza kuimarisha
uzalendo kama vile: amani, umoja, upendo na bendera ya Kenya.
Mwanafunzi asikilize kwa makini hadithi anazosimuliwa.
Mwanafunzi aweza kutazama video inayoonyesha vitendo vya kizalendo.
Wanafunzi wajadiliane kuhusu uzalendo katika makundi.
Wanafunzi waimbe wimbo wa taifa na kujadili maana ya baadhi ya maneno
ya kizalendo katika wimbo huo.
Mwanafunzi atunge sentensi kuhusu baadhi ya mambo yanayohusu
uzalendo.
Mwanafunzi ataje baadhi ta sifa za mzalendo kama vile: kupenda nchi yake,
amani na umoja.
III. Nyenzo:
Rekodi za masimulizi bunifu kuhusu uzalendo;
Michoro au picha za vitendo vya kizalendo;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 37-39;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusikiliza masimulizi
bunifu yanayohusu uzalendo ili kujenga stadi yao ya kusikiliza na kuzungumza.
Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo
hili kama vilivyotajwa hapo juu ili kufanikisha ufundishaji wake. Wanafunzi wenye
ulemavu mbalimbali washughulikiwe vilivyo kwa kuhusisha vifaa maalum kama
vile matumizi ya breli na lugha ishara.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika lililotolewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
52
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
msamiati wa uzalendo. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na
maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili wasaidiwe.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza masimulizi ya kubuni pamoja na stadi ya kuzungumza kupitia
kwa wao wenyewe na kuwasimulia wenzao. Masimulizi haya yatahusu uzalendo
vikiwemo vitendo mbalimbali vya kizalendo.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne wanne
kujadili kuhusu mchoro wa bendera ya Kenya waliopewa katika vitabu vyao.
Kila mwanafunzi apewe fursa ya kujibu maswali waliyoulizwa kuhusiana na
mchoro huo wa kalenda. Zoezi hili ni la kuwakumbusha wanafunzi kuhusu
waliyofundishwa katika somo la hapo awali kuhusiana na bendera ya Kenya,
rangi zake pamoja na maana ya rangi hizi.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasimulie wanafunzi masimulizi yafuatayo.
Ahakikishe kuwa anazungumza kwa sauti ya kusikika na kwa matamshi sahihi.
Iwapo mwalimu ana matatizo ya kimatamshi, anaweza kumwalika msimulizi
stadi akawasimulia wanafunzi masimulizi haya kwa sauti ya kusikika na matamshi
sahihi. Mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wanasikiliza kwa makini. Baada
ya wanafunzi kusomewa masimulizi haya, wapewe muda wajadiliane katika
makundi yao kuhusiana na ujumbe wa masimulizi hayo.
53
Mfano wa masimulizi
Mimi ninaitwa Rehema. Mimi ni mzalendo. Ninaipenda nchi yangu. Nchi yangu
inaitwa Kenya. Mji wake mkuu unaitwa Nairobi. Ninapenda amani. Ninapenda
kuwaona watu wakiishi kwa amani na upendo. Kama tunavyojua, umoja ndio
nguvu ya kuishi pamoja. Ni vizuri kila mwananchi kuwa mzalendo. Tuepuke
matendo yasiyo ya kizalendo kama vile: chuki, vita, ukabila, unyanyasaji na
ubaguzi. Kila mwananchi ampende mwenzake. Atangamane na wenzake kwa
amani kwa sababu sote tuna nchi moja tu ambayo ni Kenya.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika makundi yao waimbe wimbo
wa taifa waliopewa katika vitabu vyao. Mwalimu anaweza kuwaimbia ubeti
mmoja mmoja huku wanafunzi wakiimba baada yake kama darasa zima, katika
makundi yao na hatimaye kila mwanafunzi apewe fursa ya kuimba akiwa peke
yake. Mwalimu ahakikishe kwamba anaimba wimbo huo wa taifa kwa matamshi
sahihi na mahadhi ya kuvutia. Mwalimu anaweza kuwafundisha wanafunzi
mahadhi ya kuimba wimbo wa taifa la Kenya ili kuwachangamsha wanafunzi.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
Wanafunzi wajadiliane kuhusu ujumbe wa kila ubeti wa wimbo wa taifa
walioimba kisha wajibu maswali waliyopewa kwenye kitabu chao kuhusiana na
wimbo huo.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusimulia pamoja na
kufahamu shughuli mbalimbali za kizalendo. Pia, mwalimu achunguze iwapo
wanafunzi wameweza kupata ujasiri na maarifa ya kuimba wimbo wa taifa la
Kenya pamoja na kuelewa ujumbe wa kila ubeti wa wimbo huu.
54
VI. Majibu
Maswali ya mchoro wa bendera, ukurasa 37
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusiana na wanayoona
kwenye mchoro wa bendera waliopewa, kwa mfano:
1. Bendera ya Kenya
2. Rangi nne
3. Rangi yeusi, nyeupe, nyekundu na kijani.
4. Kila rangi inamaanisha:
Rangi nyeusi ishara ya rangi ya wananchi/Uafrika
Rangi nyeupe ishara ya amani
Rangi nyekundu ishara ya damu iliyomwagika katika
upiganiaji wa uhuru
Rangi ya kijani ishara ya rutuba ya nchi
Zoezi, ukurasa 39
1. Mzalendo ni mtu ambaye anapenda nchi yake.
2. Mzalendo anaishi kwa amani na umoja.
3. Kila mtu apende nchi yake.
4. Nchi yetu inaitwa Kenya.
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua rangi za bendera ili kuimarisha uzalendo;
b) Kutambua maneno yanayohusiana na uzalendo ili kuimarisha
mawasiliano;
ch) Kusoma hadithi za kizalendo ili kujenga usomaji;
55
d) Kusikiliza hadithi za mwalimu kuhusu uzalendo ili kuimarisha usikivu;
e) Kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu uzalendo ili kupata
ujumbe;
f) Kuthamini umuhimu wa uzalendo katika maisha ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi.
Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi
kama vile: amani, umoja, upendo, nchi, taifa, raia, bendera na wimbo wa
taifa.
Mwanafunzi ashiriki kusoma katika darasa, wakiwa wawili wawili, kwenye
vikundi au asome peke yake.
Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi husika ikisomwa kupitia kinasa sauti.
Mwanafunzi aweza kutazama video ya mtu au mtoto akisoma hadithi
husika kwa ufasaha kisha aige usomi ule.
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kutokana na hadithi aliyosoma au
kusomewa.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za vitendo vya kizalendo;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu uzalendo;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 39-41;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
56
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu inayohusu uzalendo kwa kutaja
msamiati wa kizalendo kama vile: amani, umoja, upendo, nchi, ushirikiano n.k. ili
kujenga stadi ya wanafunzi ya kusikiliza na kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba
ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili kama vilivyoorodheshwa
hapo juu. Hili litamsaidia kufanikisha ufundishaji wake. Mwalimu anaweza
kurekodi hadithi kuhusu uzalendo kwenye tarakilishi au simu ili wanafunzi
waisikilize darasani.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika lililotolewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
masimulizi ya kizalendo. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na
maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
funzo la hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji
wao wasaidiwe.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusoma pamoja na ya kusikiliza hadithi za kubuni. Mwalimu awagawe
wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha awaombe
watazame michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 39. Wanafunzi
wachunguze michoro hiyo na kuijadili katika makundi.
Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro
hiyo kama vile: Unaona nini kwenye michoro hii? Watu hawa wanafanya nini?
Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu maswali waliyoulizwa
kwa kurejelea michoro waliyopewa. Mwalimu ahakikishe amewashirikisha
57
wanafunzi wote katika majadiliano haya. Mchoro wa kwanza unaonyesha
wanafunzi kwenye gwaride wakiimba wimbo wa taifa huku bendera
iliyopandishwa kwenye mlingoti ikipepea. Hii ni ishara nzuri ya uzalendo wa
wanafunzi hawa kwa taifa lao. Mchoro wa pili unaonyesha rais wa nchi pamoja
na viongozi wengine na wananchi wakiadhimisha sherehe ya kitaifa. Hii pia
ni ishara ya uzalendo kwa taifa. Kisha, mwalimu awaelekeze wanafunzi kujibu
maswali kuhusu michoro waliyopewa katika vitabu vyao.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusoma hadithi
waliyopewa katika vitabu vyao kuhusu nchi ya Kenya. Mwalimu awasomee
wanafunzi hadithi hii kwa sauti ya kusikika na wanafunzi wote na kwa matamshi
sahihi. Wanafunzi wasome hadithi hiyo baada ya mwalimu wakiwa wawili
wawili na hatimaye kila mwanafunzi apewe fursa ya kuisoma akiwa peke yake.
Makosa ya kimatamshi yakosolewe pindi tu yanapotokea. Iwapo mwalimu
ana matatizo ya kimatamshi anaweza kumwalika msomaji stadi akawasomea
wanafunzi hadithi hiyo. Sharti, mwalikwa huyu awe na matamshi sahihi na sauti
ya kusikika na kuvutia.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kujibu maswali ya hadithi
waliyosoma kuhusu nchi ya Kenya. Wanafunzi wote washirikishwe katika
shughuli hii. Wanafunzi wajibu maswali waliyopewa kwa kurejelea hadithi
waliyosoma.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi bunifu.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa vitendo
mbalimbali vya kizalendo.
58
VI. Majibu
Zoezi, ukurasa 40
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona
kwenye michoro waliyopewa, kwa mfano:
1. Katika mchoro wa kwanza, ninaona wanafunzi kwenye gwaride na
katika mchoro wa pili ninaona rais wa nchi, viongozi pamoja na
wananchi wakiadhimisha sherehe ya kitaifa.
2. Watu hawa wanatenda vitendo vya kizalendo.
3. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali ya hadithi, ukurasa 41
1. Rangi za bendera ni: nyeusi, nyekundu, nyeupe na nyeusi.
2. Kuna ngao.
3. Sisi husimama wima tukiimba wimbo wa taifa.
4. Rangi nyekundu ni ishara ya damu iliyomwagika wakati wa
kupigania uhuru.
5. Rangi nyeupe ni ishara ya amani.
6. Rangi nyeusi ni ishara ya rangi ya wananchi wa Kenya; inaonyesha
Uafrika.
7. Rangi ya kijani ni ishara ya rutuba ya nchi.
Mada Ndogo 5: Kuandika
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi
ya uandishi;
b) Kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi.
59
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
Mwanafunzi aelezee yaliyo muhimu katika uandishi k.v. mwandiko nadhifu,
maudhui, mtiririko n.k.
Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwalimu.
Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.
Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa kama hiki
kifuate hatua tano za uandishi: maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo,
uhariri na uchapishaji. Vichwa vya visa vinaweza kutofautiana.
III. Nyenzo:
Hadithi bunifu zilizoandikwa kwenye chati kuhusu uzalendo;
Chati zilizoandikwa alfabeti za Kiswahili;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu uzalendo;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 42-43;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kukuza stadi ya mwanafunzi ya kuandika. Katika mada
hii, wanafunzi watapata maarifa ya kubuni na kuandika visa vifupi vifupi kwa
kuzingatia mambo kadhaa kama vile: mwandiko nadhifu, maudhui, mtiririko,
uhariri, marejeleo na maandalizi mengine kabambe. Shughuli hii itawawezesha
wanafunzi kufahamu jinsi ya kuandika visa vya kubuni katika muktadha
wowote. Muktadha wa uandishi katika mada hii ni kuhusu uzalendo. Mwalimu
ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili
kama vilivyoorodheshwa hapo juu ili kufanikisha ufundishaji wake pamoja na
ujifundishaji wa wanafunzi.
60
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika lililotolewa kwenye vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
kusoma hadithi za kubuni katika muktadha wa vitendo vya kizalendo. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi kusahihisha zoezi walilopewa katika funzo
la hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao,
wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kuandika kwa mwandiko nadhifu na hata kubuni hadithi na kuiandika
kwa hati nadhifu katika madaftari yao. Mwalimu awagawe wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha awaombe watazame alfabeti za
Kiswahili walizopewa katika vitabu vyao zilizo katika herufi kubwa na ndogo.
Wanafunzi wachunguze alfabeti hizi kisha mwalimu awaelekeze waandike
alfabeti zote za Kiswahili katika madaftari yao. Wanafunzi waandike alfabeti
hizi kwa mwandiko nadhifu. Shughuli hii ya kuandika alfabeti za Kiswahili ni
njia bora ya kuboresha mwandiko wa wanafunzi.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kuandika imla
ifuatayo ambayo mwalimu atawasomea. Mwalimu ahakikishe anasoma imla hii
kwa sauti ya kusikika na wanafunzi wote na kwa matamshi sahihi. Wanafunzi
wamsikilize mwalimu kwa makini na waandike imla ya mwalimu kwa mwandiko
nadhifu katika madaftari yao.
61
Mfano wa imla
Mimi ninaitwa Rehema. Mimi ni mzalendo. Ninaipenda nchi yangu. Ninapenda
amani. Natamani kuishi kwa amani na upendo. Umoja ndio nguvu ya kuishi bila
vita. Ni vizuri kila mwananchi kuwa mzalendo.
Baada ya wanafunzi kukamilisha kufanya zoezi la imla, mwalimu ahakikishe
kuwa atasahihisha madaftari ya wanafunzi ili kusahihisha makosa ya
kimaendelezo na kisarufi. Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika
kuchunguza hadithi waliyopewa katika vitabu vyao iliyo na mapengo. Hadithi
hii ina majibu kwenye mabano, hivyo mwanafunzi anastahili kuisoma, kuielewa
kisha kujaza mapengo yaliyomo kwa kuteua jibu mwafaka kutoka kwa yaliyo
kwenye mabano. Wanafunzi wafanye zoezi hili katika madaftari yao.
Mwalimu ahakikishe anasahihisha makosa yoyote ya kimaendelezo na mwandiko
usio nadhifu. Wanafunzi walio na matatizo ya kuandika kwa mwandiko nadhifu
wapewe mazoezi zaidi ya kuandika. Mwalimu awaelekeze zaidi.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kuandika maelezo kwa kuzingatia
mambo muhimu ya uandishi bora kama vile mwandiko nadhifu na mtiririko
unaofaa.
VI. Majibu
Maswali ya alfabeti, ukurasa 42
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na alfabeti walizopewa,
kwa mfano:
1. Ninaona baadhi ya alfabeti za Kiswahili.
2. Mwalimu atathmini maandishi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
62
Zoezi, ukurasa 43
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano:
Mzalendo hapendi vita wala fujo katika nchi yake. Mzalendo ana moyo safi
daima. Mzalendo anaiheshimu bendera ya nchi yake. Mzalendo anajua
kuuimba wimbo wa taifa. Mzalendo ni raia mwema wa nchi yake.
Mada Ndogo 6: Saru: Matumizi ya ‘–ake’ na ‘-ao’
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua matumizi ya –ake na –ao ili kuimarisha mawasiliano;
b) Kusoma vifungu vya maneno vinavyojumuisha –ake na –ao ili kujenga
usomaji;
ch) Kutunga sentensi akitumia –ake na –ao ili kuimarisha ubunifu;
d) Kuandika sentensi akitumia –ake na –ao ili kujenga uandishi bora;
e) Kuchangamkia kurejelea vitu vyake na vya wenzake kwa kutumia –ake
na –ao katika mawasiliano ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aonyeshe vitu vyake na vya wengine darasani na kuvirejelea
akitumia –ake na –ao.
Mwanafunzi asome vifungu vyenye matumizi ya –ake na –ao.
Mwanafunzi akamilishe vifungu kwa kutumia –ake na –ao k.m. Kalamu
________ (kalamu yake) Kalamu _____ (kalamu zao); Kitabu _____
(kitabu chako) Vitabu _____ (vitabu vyao).
Mwanafunzi atunge sentensi kwa kutumia –ake na –ao.
Mwanafunzi aweza kutumia tarakilishi kufanya zoezi.
III. Nyenzo:
Michoro ya watu wakiashiria vifaa mbalimbali;
63
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 43-45;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.)
IV. Maandalizi ya somo
Sarufi ni kipengele muhimu katika ujifundishaji wa wanafunzi. Mwalimu anastahili
kutilia maanani dhana hii ili kuweza kuwahusisha wanafunzi kwa ukamilifu
katika somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla
ya vipindi hivi. Vifaa hivi ni kama vile: michoro ya watu mbalimbali wakiashiria
vitu mbalimbali kuonyesha matumizi ya -ake na -ao. Wanafunzi watumiwe sana
katika funzo hili la kuonyesha matumizi ya -ake na -ao.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa vyake kwa kukumbuka kuwa matumizi ya michoro, picha, vifaa
halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha ufundishaji wa wanafunzi;
hasa wale ambao wana matatizo mbalimbali katika kuelewa na kufahamu
haraka yale wanayofundishwa darasani au wale walio na kiwango cha chini
katika ujifunzaji wao.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, mwalimu ahusihe matumizi ya breli na
vinasasauti ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha kama wanafunzi
wengine. Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, mwalimu anaweza
kuhusisha matumizi ya lugha ya ishara.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi
iliyopendekezwa katika Kitabu cha Mwanafunzi.
64
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu awasalimie wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia kuhusu uandishi bora. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awashirikishe wanafunzi wote katika kuchunguza michoro pamoja na sentensi
zinazoambatana na michoro hiyo iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa
43-44. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali mepesi
kuhusiana na michoro na sentensi hizo.
Katika hatua hii, wanafunzi watapata fursa ya kujifundisha kuhusu matumizi
ya -ake na -ao katika mawasiliano. Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika
makundi yao kuchukua mifuko ya wenzao na kuwauliza kila kifaa kilicho
mfukoni ni cha nani.
Kwa mfano:
Umoja Wingi
1. Kalamu hii ni yake. Kalamu hizi ni zao.
2. Kitabu hiki ni chake. Vitabu hivi ni vyao.
3. Raba hii ni yake. Raba hizi ni zao.
4. Mfuko huu ni wake. Mifuko hii ni yao.
Wanafunzi waelekezwe kutambua mabadiliko ya –ake katika umoja na kuwa
–ao katika wingi. Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika
shughuli hii katika makundi yao.
Mwalimu awaeleze wanafunzi kuwa:
Matumizi ya -ake na -ao ni katika kurejelea nafsi ya tatu umoja na wingi katika
Kiswahili. Mwalimu anaweza kuwagusia wanafunzi kidogo tu kuhusu nafsi ya
kwanza umoja na wingi ambayo ni: mimi sisi, -angu etu.
Kwa mfano: kiti changu viti vyetu.
65
(ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana kwa kutumia
-ake na -ao. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza kutunga
sentensi sahihi katika umoja na wingi kwa kutumia -ake na -ao.
VI. Majibu
Zoezi, ukurasa 45
1. Wasichana wamesuka nywele zao.
2. Dada ana kalamu yake.
3. Kichwa chake kinauma.
4. Wageni wameanza safari zao.
66
Matokeo maalum
yanayotarajiwa
Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutambua sauti mbili
zinazotamkwa pamoja ili
kuimarisha matamshi bora;
(b) Kutambua miezi ya mwaka
ili kuimarisha stadi ya
kuzungumza;
(ch) Kutambua majina ya miezi
ya mwaka kwa Kiswahili ili
kuimarisha mawasiliano;
(d) Kusikiliza hadithi ikisomwa na
mwalimu inayojumuisha miezi
ili kuimarisha stadi za kusikiliza
na kusoma;
(e) Kuandika kisa kifupi kwa hati
nadhifu kulingana na mada ili
kujenga stadi ya uandishi;
(f) Kutambua nambari 51-100 kwa
maneno ili kuimarisha stadi ya
kuzungumza;
(g) Kutambua matumizi ya
kikomo (.) katika kuimarisha
mawasiliano.
Mwanafunzi atambue sauti
/mb/ /nj/ na /ng/ katika
maneno.
Mwanafunzi asome majina ya
miezi ya mwaka ipasavyo kwa
kutumia kadi za maneno.
Mwanafunzi ataje miezi ya
mwaka.
Mwanafunzi asikilize mwalimu
akisoma hadithi.
Mwanafunzi apewe hadithi
yenye mapengo ajaze maneno
mwafaka.
Mwanafunzi asome majina ya
nambari 51-100.
Mwanafunzi asome sentensi
zenye kikomo (.) katika vikundi.
Mada Kuu 3: MIEZI YA MWAKA
Idadi ya vipindi: 19
Sura ya
3
67
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kushiriki katika vikundi vya ushirika vya wanafunzi.
Kazi ya vikundi.
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Hisabati na somo la Mazingira.
Nyenzo:
Kadi zenye herufi mb, nj na ng;
Kadi za majina yenye herufi mb, nj na ng;
Rekodi za sauti /mb/, /nj/ na /ng/;
Michoro au picha za kalenda;
Kadi za majina ya miezi ya mwaka;
Rekodi za masimulizi bunifu mbalimbali;
Rekodi za hadithi bunifu mbalimbali;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 46-67;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Mada hii inashughulikia utamkaji wa sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja
ambazo ni /mb/, /nj/ na /ng/, majina ya miezi mbalimbali ya mwaka pamoja
na masimulizi na hadithi kuhusu miezi ya mwaka katika kalenda. Pia, kipengele
cha sarufi kuhusu matumizi ya kikomo (.) kitaangaziwa katika mada hii.
Mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kujenga stadi yake ya kusikiliza,
kufahamu na kuweza kutaja majina mbalimbali ya miezi ya mwaka pamoja na
kusoma hadithi kwa ufasaha. Hadithi za kuvutia na zenye msamiati wa kiwango
cha wanafunzi wa gredi hii zibuniwe ili kuwafaa wanafunzi katika ujifundishaji
wao.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
68
Elimu ya kudumisha maendeleo: elimu ya masuala ya fedha: kujua kuratibu
shughuli za kila siku;
Utangamano wa kijamii;
Amani na maadili.
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii ni kuhusu miezi ya mwaka ni kama vile:
Msamiati Maana
1.
Januari
mwezi wa kwanza wa mwaka katika kalenda
2.
Februari
mwezi wa pili wa mwaka katika kalenda
3.
Septemba
mwezi wa tisa wa mwaka katika kalenda
4.
Disemba
mwezi wa kumi na mbili (mwisho) wa mwaka katika
kalenda
5.
Agosti
mwezi wa nane wa mwaka katika kalenda
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Ili kuweza kuwashirikisha wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali,
mwalimu awe na vifaa muhimu na maalum vya kuwasaidia wanafunzi hawa
katika ujifundishaji wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kuona, mwalimu
anaweza kuhusisha matumizi ya breli pamoja na vifaa vya kunasia sauti.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri
wa lugha ya ishara. Vifaa hivi vitawawezesha wanafunzi hawa kusoma kama
wanafunzi wenzao bila vikwazo vyovyote.
69
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya
vipindi
Mada Ndogo 1: Sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja
4
Mada Ndogo 2: Msamiati: Majina ya miezi
2
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 5: Kuandika
3
Mada Ndogo 6: Msamiati: Tarakimu 51-100
3
Mada Ndogo 7: Sarufi: Matumizi ya kikomo (.)
2
JUMLA: 19
Mada Ndogo 1: Sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja
(Idadi ya vipindi: 4)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua sauti mbili zinazotamkwa pamoja ili kuimarisha matamshi
bora;
b) Kutamka sauti lengwa ili kuimarisha matamshi bora;
ch) Kusoma silabi za sauti lengwa ili kuimarisha usomaji;
d) Kuandika silabi zinazotokana na sauti lengwa ili kuimarisha uandishi
bora;
e) Kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa ili
kuimarisha usomaji;
f) Kuandika maneno kutokana na silabi zilizofunzwa ili kuimarisha
uandishi bora;
g) Kusoma hadithi zilizo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kumsaidia
mwanafunzi kutamka sauti husika ili kuimarisha matamshi na
usomaji;
h) Kuchangamkia kutamka sauti lengwa ili kuimarisha mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atambue sauti /mb/, /nj/ na /ng/, katika maneno.
70
Mwanafunzi atamke silabi zinazotokana na sauti lengwa baada ya mwalimu,
kisha atamke pamoja na mwalimu na baadaye atamke akiwa peke yake,
wawili wawili na kama darasa zima k.m. mba, mbe, nje, nga, nge na ngi.
Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia kama vile papaya, tarakilishi,
projekta na kipazasauti katika kuimarisha matamshi yake.
Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
Mwanafunzi atambue sauti alizosoma katika maneno kwa mfano: mbuzi,
mboga, njugu, ngamia, njia na ngozi.
Mwanafunzi aandike maneno yanayojumuisha sauti lengwa.
Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi na kuchanganua yaliyo
marefu zaidi.
Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa
darasani au wawili wawili.
Mwanafunzi asikilize imla ya maneno yenye silabi za sauti lengwa na
kuyaandika.
III. Nyenzo:
Kadi zenye herufi mb, nj na ng,
Rekodi za sauti /mb/, /nj/ na /ng/,
Kadi zenye majina yenye sauti /mb/, /nj/ na /ng/,
Mgeni mwalikwa mwenye matamshi mazuri na sahihi;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 46;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Mada hii inahusu sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja na majina yenye sauti
hizo katika Kiswahili. Herufi na sauti zitakazoangaziwa katika funzo hili ni: sauti
/mb/, /nj/ na /ng/. Matamshi mazuri na sahihi ya wanafunzi yatazingatiwa
hapa na kukuzwa zaidi.
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi.
Vifaa hivi ni kama vile: rekodi za matamshi ya sauti lengwa, mgeni mwalikwa
mwenye matamshi mazuri na sahihi, kadi zenye herufi na sauti lengwa pamoja
71
na vyombo vingine maalum vya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu na
matatizo mbalimbali.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa alivyovileta darasani. Mwalimu akumbuke kuwa matumizi ya
michoro, picha na vifaa halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha
ufundishaji wa wanafunzi; hasa wale ambao wana matatizo mbalimbali katika
kuelewa na kufahamu haraka yale wanayofundishwa darasani au wale walio na
kiwango cha chini katika ujifundishaji wao.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, mwalimu ahakikishe
anahusisha matumizi ya lugha ya ishara. Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza
kuona, mwalimu ajitahidi kuhusisha matumizi ya breli pamoja na vyombo
vya kunasia sauti ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha kama
wanafunzi wengine.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa
katika vitabu vya wanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize somo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu utamkaji wa irabu pamoja na konsonanti za Kiswahili.
Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu kisha watamke irabu na konsonanti za
Kiswahili kama waliyoulizwa. Shughuli hii ya utamkaji wa irabu na konsonanti
(alfabeti) itakuwa njia bora ya kutanguliza funzo hili kuhusu utamkaji wa sauti
mbili tofauti zinazotamkwa pamoja katika Kiswahili.
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awashirikishe katika kuchunguza mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi,
ukurasa 46. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali
mepesi kuhusiana na mchoro huo. Baadhi ya maswali ambayo mwalimu
anaweza kuuliza ni kama vile: Unaona nini kwenye mchoro huu? Unaona siku zipi
kwenye mchoro huu? Unaona miezi ipi kwenye mchoro huu? Mwalimu awaelekeze
72
wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo na kuelewa mchoro waliopewa.
Mchoro uliopo unaonyesha kalenda ya mwaka 2017 iliyo na miezi ya mwaka
pamoja na siku za wiki. Baadaye wanafunzi wajibu maswali waliyopewa katika
vitabu vyao kuhusiana na mchoro uliopo.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Vipindi 2
i) Sauti /mb/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 47.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro
hii. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kwa kurejelea michoro waliyopewa
katika vitabu vyao.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa ambayo ni: mbuzi, mbao, mboga na mbu kisha watamke kwa pamoja
herufi mbili za kwanza za majina hayo pekee. Wanafunzi watamke sauti /mb/
baada ya mwalimu kisha wakiwa wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi
atamke sauti hii akiwa peke yake. Mwalimu awaombe wanafunzi waandike
herufi mb katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi ndogo. Yaani mb na
MB.
Wanafunzi washirikishwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o,
u kisha watambue silabi za herufi mb, ambazo ni: mba, mbe, mbi, mbo, mbu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi mb. Kwa mfano: mbuzi, mboga, mbuni, mbu, mbaya, mbegu, mbio n.k.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye silabi
za herufi mb kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Mkulima amepanda mboga shambani.
2. Huyu ni mbuzi wa nyanya.
3. Wanafunzi walikimbia mbio.
73
4. Mtoto aliumwa na mbu.
5. Ndege huyu anaitwa mbuni.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi mb.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /mb/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) mboga mbo ga
ii) mbio mbi o
iii) mbuzi mbu zi
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi mb’.
Kipindi 1
ii) Sauti /nj/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 50.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro
hii. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na wanayoona kwenye
michoro iliyopo.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya
michoro waliyopewa ambayo ni: njugu, manjano na injini. Kisha wanafunzi
watamke sauti /nj/ katika majina hayo. Wanafunzi watamke sauti /nj/ baada
ya mwalimu kisha wakiwa wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi atamke
sauti hii akiwa peke yake. Mwalimu awaombe wanafunzi waandike herufi nj
katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi ndogo. Yaani: nj na NJ.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi nj’, ambazo ni: nja, nje, nji, njo, nju.
74
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za herufi
nj. Kwa mfano: njugu, njia, njoo, njaa, nje, njumu n.k. Mwalimu awashirikishe
wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye silabi za herufi nj kwa usahihi.
Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Wanafunzi wanahisi njaa.
2. Mama amenunua njugu nyingi.
3. Wageni wamesimama nje ya mlango.
4. Dada amevaa rinda la manjano.
5. Njoo hapa!
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi nj.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /nj/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) njaa nja a
ii) njugu nju gu
iii) njoo njo o
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi nj.
Kipindi 1
iii) Sauti /ng/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 54.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro
hii. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na wanayoona katika
michoro iliyopo.
75
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti za kwanza za majina hayo pekee ambayo ni
sauti /ng/. Wanafunzi watamke sauti /ng/ baada ya mwalimu kisha wakiwa
wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi atamke sauti hii akiwa peke yake.
Mwalimu awaombe wanafunzi waandike herufi ng katika madaftari yao kwa
herufi kubwa na herufi ndogo. Yaani: ng na NG.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi ng, ambazo ni: nga, nge, ngi, ngo, ngu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ng. Kwa mfano: ngoma, ngamia, ngiri, ngumu, ngozi, ngazi, nguvu n.k.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye silabi
za herufi ng kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Waimbaji wana ngoma kubwa.
2. Ngozi ya mtoto ni nyororo.
3. Mwanafunzi anavua nguo.
4. Fundi anatumia ngazi kupanda jengo lile.
5. Kazi ya kubeba mawe ni ngumu.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ng.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /ng/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) ngumu ngu mu
ii) ngazi nga zi
iii) ngoma ngo ma
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi ng.
76
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo hili kuhusu sauti /mb/, /nj/ na
/ng/ kwa kuwauliza wanafunzi maswali tofauti kuhusu mambo muhimu
waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo uwezo wa wanafunzi wa kutamka
sauti/mb/, /nj/ na /ng/ kwa usahihi, kutambua na kutamka maneno yenye
sauti hizi kwa usahihi pamoja na kutunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno
yenye sauti hizi walizojifundisha. Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wanaweza kuandika sauti hizo kwa usahihi.
VI. Majibu
Maswali ya mchoro wa kalenda, ukurasa 46
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na mchoro wa kalenda
waliopewa, kwa mfano:
1. Ninaona kalenda.
2. Ninaona siku za: Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi, Ijumaa,
Jumamosi na Jumapili.
3. Kuna miezi ya: Januari, Februari, Machi, Aprili, Mei, Juni, Julai, Agosti,
Septemba, Oktoba, Novemba na Disemba.
4. Kalenda hii ni ya mwaka wa 2017.
i) Sauti /mb/
Maswali ya michoro, ukurasa 47
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona kwenye
michoro waliyopewa, kwa mfano:
1. Mbuzi, mbao, mboga na mbu.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
Zoezi, ukurasa 49
1. Mimi ninaishi mbali.
2. Tutakimbia mbio kesho.
77
3. Utakula mboga gani?.
4. Nilizaliwa mwezi Disemba.
5. Mbuni ni ndege mkubwa.
Zoezi, ukurasa 57-58
1. mbe gu
2. mba li
3. ki mbi a
4. mbu ni
ii) Sauti /nj/
Maswali ya michoro, ukurasa 54
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona kwenye
michoro waliyopewa, kwa mfano:
1. Njugu, manjano na injini.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
Zoezi, ukurasa 54
1. Nilitoka nje usiku.
2. Mtoto mjanja anasumbua.
3. Njiwa amepaa angani.
4. Njoo twende kanisani.
5. Nani amekula njugu?
Zoezi, ukurasa 57-58
1. nji wa
2. njo o
3. i nji ni
4. nja a
5. nji a
78
iii) Sauti /ng/
Maswali ya michoro, ukurasa 54
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona kwenye
michoro waliyopewa, kwa mfano:
1. Ngamia, ngazi, ngoma na ngiri.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
Zoezi, ukurasa 54
1. ngo ma
2. ngi ri
3. nga no
4. nga o
5. ngo zi
Zoezi, ukurasa 57-58
1. Tutapanda mbegu mwezi huu.
2. Njia nyingine njema ya kupitia ni nje.
3. Ngazi ngumu iko karibu na ngoma.
4. Kamba ya nguo haifungi ngozi ya ngiri.
5. Mbuga nyingi hazina njia nyembamba.
Mada Ndogo 2: Msamiati: Majina ya miezi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua miezi ya mwaka ili kuimarisha stadi ya kuzungumza;
b) Kusoma majina ya miezi ya mwaka ili kuimarisha usomaji bora;
79
ch) Kuandika majina ya miezi ya mwaka kwa mfuatano ili kujenga uandishi
bora;
d) Kutumia majina ya miezi katika sentensi ili kujenga ubunifu;
e) Kuchangamkia majina ya miezi katika mawasiliano ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome majina ya miezi ya mwaka ipasavyo kwa kutumia kadi
za maneno.
Wanafunzi wanaweza kukariri mashairi yanayohusu miezi ya mwaka.
Mwanafunzi anaweza kuimba nyimbo zinazohusu miezi ya mwaka.
Mwanafunzi aandike majina ya miezi ya mwaka.
Wanafunzi wanaweza kushirikishwa katika zoezi la kupanga upya majina
yaliyoparaganywa kuhusu miezi ya mwaka.
Mwanafunzi atunge sentensi akitumia majina ya miezi ya mwaka.
Mwanafunzi anaweza kuonyeshwa vibonzo kutaja majina ya miezi ya
mwaka na kuelezea matukio tofauti ya mwaka.
III. Nyenzo:
Kadi zenye majina ya miezi ya mwaka;
Chati zenye majina ya miezi ya mwaka;
Michoro au picha za kalenda;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 57-58;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Ni muhimu kwa kila mtu kufahamu kuhusu majina ya miezi ya mwaka pamoja
na siku za wiki. Hii ni kwa sababu shughuli zote za binadamu hutendeka katika
miezi ya mwaka na siku za wiki. Kalenda ya mwaka ina miezi kumi na miwili.
80
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama
vilivyotajwa hapo juu. Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue
wakati mwafaka wa kuweka hadharani vifaa alivyovileta darasani. Matumizi
ya michoro, picha, kadi na vifaa vingine ni mbinu bora ambayo hutumika
kufanikisha ufundishaji wa wanafunzi hasa walio na matatizo na ulemavu
mbalimbali au kiwango cha chini cha ujifundishaji.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, mwalimu ahusishe
matumizi ya lugha ishara. Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni vyema
mwalimu ajitahidi kuhusisha matumizi ya breli ili kuwawezesha wanafunzi wa
aina hii kujifundisha kama wanafunzi wengine.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba amewagawa wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwenye vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu awaamkue wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia kuhusu utamkaji wa sauti mbili
tofauti zinazotamkwa pamoja ambayo ni /ng/. Wanafunzi wajibu maamkuzi ya
mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusu
majina ya miezi ya mwaka ambayo wanafahamu. Wanafunzi wataje majina
ya miezi ya mwaka ambayo wanafahamu kama vile: Januari, Februari, Machi,
Aprili, Mei, Juni, Julai, Agosti, Septemba, Oktoba, Novemba na Disemba. Mwalimu
ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii. Hii itakuwa
namna nzuri ya kutanguliza funzo hili kuhusu msamiati wa majina ya miezi ya
mwaka.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu
kisha awaelekeze kusoma maneno yaliyo kwenye kadi mbalimbali walizopewa
81
katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 57. Mwalimu anaweza kuwasomea
wanafunzi maneno hayo ya kadi kisha wanafunzi wakasoma baada ya mwalimu
wakiwa watatu watatu na hatimaye kila mwanafunzi apewe fursa ya kusoma
akiwa peke yake. Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na
maneno ya kadi waliyosoma. Maswali kama vile: Haya ni majina ya nini? Majina
haya hupatikana wapi? Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na
maneno ya kadi waliyosoma kwa kusema: Majina haya ni ya miezi mbalimbali.
Majina haya hupatikana kwenye kalenda ya mwaka. Wanafunzi wapewe muda
katika makundi yao wa kujadiliana kuhusu majina ya miezi waliyosoma kisha
wajibu maswali waliyopewa kwenye vitabu vyao kuhusiana na maneno ya kadi
waliyosoma. Mwalimu ahakikishe anawasaidia wanafunzi wanaotatizika katika
makundi yao.
Kabla ya somo hili, mwalimu awe ametayarisha kadi mbalimbali za majina ya
miezi mbalimbali ambazo atawaonyesha wanafunzi nao watatamka kwa sauti
majina hayo. Shughuli hii itawasaidia wanafunzi kufahamu majina ya miezi yote
ya mwaka katika kalenda.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awaelekeze wanafunzi kufanya zoezi la
kupanga kadi za majina ya miezi mbalimbali ambazo zimeparaganywa au
zimechanganywa. Wanafunzi katika makundi yao wapange kadi za majina
hayo kuanzia mwezi wa kwanza hadi mwezi wa mwisho. Matokeo ya upangaji
yawape utaratibu ufuatao:
Mwezi Nambari
Januari wa kwanza
Februari wa pili
Machi wa tatu
Aprili wa nne
Mei wa tano
Juni wa sita
Julai wa saba
Agosti wa nane
82
Septemba wa tisa
Oktoba wa kumi
Novemba wa kumi na moja
Disemba wa kumi na mbili
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kuandika kwa maendelezo sahihi
majina ya miezi ya mwaka kuanzia mwezi wa kwanza hadi mwezi wa mwisho.
Mwalimu atathmini maandishi ya wanafunzi.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu majina ya miezi ya mwaka katika kalenda.
VI. Majibu
Maswali ya kadi za maneno, ukurasa 58
Mwalimu atathmini usomaji wa wanafunzi.
1. Mwezi wa kwanza ni Januari.
2. Mwezi wa pili ni Februari.
3. Mwezi wa nne ni Aprili.
4. Mwezi wa saba ni Julai.
5. Mwezi wa kumi na moja ni Novemba.
Zoezi la makundi, ukurasa 58
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi wapange kwa utaratibu
majina ya miezi kuanzia mwezi wa kwanza hadi mwezi wa mwisho, kwa
mfano:
Mwezi Nambari
Januari wa kwanza
Februari wa pili
Machi wa tatu
Aprili wa nne
83
Mei wa tano
Juni wa sita
Julai wa saba
Agosti wa nane
Septemba wa tisa
Oktoba wa kumi
Novemba wa kumi na moja
Disemba wa kumi na mbili
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kumtambua majina ya miezi ya mwaka kwa Kiswahili ili kuimarisha
mawasiliano;
b) Kutaja miezi ya mwaka kwa Kiswahili ili kuimarisha stadi ya kuzungumza;
ch) Kusikiliza masimulizi kuhusu miezi ya mwaka ili kujenga usikivu;
d) Kuthamini umuhimu wa miezi ya mwaka maishani.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ataje miezi ya mwaka.
Mwanafunzi aweza kueleza mambo yanayofanyika katika miezi fulani k.v.
kufungua shule - mwezi wa Januari, kufunga shule - mwezi wa Aprili n.k.
Mwanafunzi asimulie kuhusu matukio katika miezi mbalimbali k.v.
kuzaliwa, sherehe za kidini na kitaifa.
Mwanafunzi aweza kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu miezi ya
mwaka.
Mwanafunzi asome majina ya miezi ya mwaka kupitia kwa vifaa kama vile
kadi za majina.
84
Mwanafunzi aweza kutazama video kuhusu shughuli zinazofanyika katika
miezi tofauti.
Mwanafunzi asomee mwenzake au kikundi majina ya miezi ya mwaka.
Wanafunzi waweza kupewa kadi zilizo na matukio mbalimbali ya mwaka
waambatanishe na miezi yenyewe katika makundi.
Mwanafunzi aandike majina ya miezi ya mwaka.
Mwanafunzi aweza kupewa zoezi la kuambatanisha majina ya miezi kwa
Kiswahili.
III. Nyenzo:
Rekodi za masimulizi bunifu mbalimbali kuhusu miezi ya mwaka;
Michoro au picha za matukio katika miezi ya mwaka;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 59-61;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusikiliza masimulizi ya
kubuni yanayohusu majina ya miezi ya mwaka ili kujenga stadi yao ya kusikiliza
na kuzungumza. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika
kufundishia funzo hili kama vilivyotajwa hapo juu ili kufanikisha ufundishaji
wake. Wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali wasaidiwe vilivyo kwa kutumia
vifaa maalum kama vile matumizi ya breli na lugha ishara.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika lililotolewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
85
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
majina ya miezi ya mwaka. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na
maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili wasaidiwe.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza masimulizi bunifu pamoja na stadi ya kuzungumza kupitia kwa
wao wenyewe kuwasimulia wenzao. Masimulizi haya yatahusu majina ya miezi
ya mwaka pamoja na matukio mbalimbali katika miezi tofauti.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne wanne
kujadili kuhusu kalenda waliyopewa katika vitabu vyao. Kila mwanafunzi
apewe fursa ya kujibu maswali waliyoulizwa kuhusiana na kalenda hiyo. Zoezi
hili ni la kuwakumbusha wanafunzi kuhusu majina ya miezi ya mwaka na
yanavyopangwa kwenye kalenda ya mwaka.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika makundi yao
wakariri shairi walilopewa katika vitabu vyao kuhusu miezi mbalimbali katika
mwaka. Mwalimu anaweza kuwakariria wanafunzi shairi hilo kisha wanafunzi
wakakariri baada yake wakiwa wanne wanne, wawili wawili na hatimaye kila
mwanafunzi apewe fursa ya kulikariri shairi hilo akiwa peke yake. Mwalimu
ahakikishe anakariri shairi hilo kwa matamshi sahihi na mahadhi ya kuvutia.
Mwalimu anaweza kuwafundisha wanafunzi mahadhi mbalimbali ya kukariri
shairi ili kuwachangamsha.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
Wanafunzi wajadiliane kuhusu ujumbe wa shairi walilosoma kisha wajibu
maswali waliyopewa kwenye kitabu chao kuhusiana na shairi lililopo.
86
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kusimuliana kuhusu sherehe
ya Disemba. Kila mwanafunzi apewe fursa ya kuwasimulia wenzake kuhusu
sherehe ya Disemba kwa kusema:
1. Tarehe ya sherehe hiyo.
2. Siku ya sherehe hiyo.
3. Watu waliokuja kwenye sherehe hiyo.
4. Jina la sherehe hiyo.
5. Jinsi alivyosherehekea siku hiyo.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika shughuli hii. Wanafunzi
wanaweza kupewa muda zaidi wakasimuliana kuhusu sherehe na matukio
mbalimbali katika miezi tofauti ya mwaka kama vile:
Sherehe/Tukio Mwezi
Mwaka mpya Januari
Kufungua shule Januari
Kufunga shule Aprili
Siku ya wafanyakazi Mei
Krismasi Disemba
Shughuli hii ya wanafunzi kusimuliana kuhusu matukio na sherehe mbalimbali
za miezi ya mwaka itamwezesha kila mwanafunzi kukuza stadi yake ya kusikiliza
na kuzungumza kupitia kwa masimulizi. Pia, ujasiri wa kila mwanafunzi wa
kusimama na kuzungumza mbele ya wanafunzi utaboreshwa.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusimulia pamoja na
kufahamu matukio na sherehe mbalimbali katika miezi tofauti ya mwaka.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ujasiri na maarifa ya
kusimuliana kuhusiana na matukio ya miezi ya mwaka.
87
VI. Majibu
Maswali ya mchoro wa kalenda, ukurasa 59
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusiana na wanayoona kwenye
mchoro wa kalenda waliopewa, kwa mfano:
1. Ninaona kalenda ya mwaka yenye majina ya miezi mbalimbali na siku
za wiki.
2. Ninaona miezi ya: Januari, Februari, Machi, Aprili, Mei, Juni, Julai,
Agosti, Septemba, Oktoba, Novemba na Disemba.
3. Ninaona siku za: Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi, Ijumaa,
Jumamosi na Jumapili.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali ya shairi, ukurasa 60-61
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na shairi walilosoma.
1. Mwanzo wa mwaka shule hufunguliwa mwezi wa Januari.
2. Sikukuu ya Mashujaa nchini Kenya husherehekewa mwezi wa Oktoba.
3. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
5. Muhula wa pili shule hufungwa mwezi wa Agosti.
5. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali ya mchoro wa kalenda, ukurasa 61
Mwalimu atathmini masimulizi ya wanafunzi.
88
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kusikiliza hadithi ikisomwa na mwalimu inayojumuisha miezi ili
kuimarisha stadi ya kusikiliza na kusoma;
b) Kusoma hadithi zinazojumuisha miezi na nambari ili kuimarisha usomaji;
ch) Kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu miezi ya mwaka ili
kuelewa ujumbe;
d) Kuchangamkia kusoma hadithi katika maisha ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asikilize mwalimu akisoma hadithi.
Mwanafunzi asome hadithi peke yake.
Wanafunzi wasomeane hadithi wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
Mwanafunzi aweza kutazama video ambapo hadithi inasomwa.
Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kwa kutumia jitabu mbele ya darasa.
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kuhusu hadithi aliyosoma.
Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za hadithi bunifu kuhusu miezi ya mwaka;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 61-63;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
89
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu ili kujenga stadi ya wanafunzi ya
kusikiliza na kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika
kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake. Mwalimu anaweza
kubuni hadithi kadhaa kuhusu matukio ya miezi mbalimbali ya mwaka ambazo
atawasomea wanafunzi darasani na nyingine watajisomea wenyewe. Iwapo
mwalimu ana matatizo ya kimatamshi, anaweza kumwalika msomaji mashuhuri
akawasomea wanafunzi hadithi bunifu kisha wanafunzi wakasoma baada yake.
Mwalikwa huyu sharti awe na uwezo wa kusoma kwa sauti ya kusikika na kwa
matamshi sahihi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
masimulizi ya matukio na sherehe za miezi ya mwaka. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe
wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika funzo la hapo awali.
Wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao ya
kusikiliza pamoja na kusoma hadithi za kubuni. Mwalimu awagawe wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha awaombe watazame michoro
iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 62-63 pamoja na kusoma vifungu
vifupi vifupi vinavyoambatana na michoro hiyo. Wanafunzi wachunguze
michoro hiyo ya watu wanaojihusisha na matukio mbalimbali ya miezi ya
mwaka. Mwalimu awasomee wanafunzi vifungu walivyopewa kisha wasome
baada yake wakiwa wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi asome peke
yake.
90
Makosa ya matamshi yasahihishwe pindi tu yanapotokea. Wanafunzi wajadili
kuhusu ujumbe uliojitokeza katika vifungu walivyosoma.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu maswali
waliyoulizwa kuhusiana na vifungu walivyosoma. Mwalimu ahakikishe
amewashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii. Wanafunzi wajibu maswali
hayo kwa kurejelea vifungu walivyosoma.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kutazama video
aliyoandaa mapema kuhusu sherehe yoyote ya kitaifa. Inaweza kuwa video
kuhusu sherehe ya siku ya wafanyakazi ya mwezi wa Mei, sikukuu ya Madaraka
ya mwezi wa Juni, sikukuu ya Mashujaa ya mwezi wa Oktoba, sikukuu ya
Jamhuri ya mwezi wa Disemba n.k. Mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wote
wanaweza kuiona video hiyo vizuri. Anaweza kutumia tarakilishi au projekta.
Wanafunzi walio na ulemavu au matatizo mbalimbali katika ujifundishaji wao
washughulikiwe na mwalimu kwa kuhusisha matumizi ya vifaa maalum.
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi walitazama video husika kwa makini na
kuielewa, mwalimu awaulize maswali kadhaa kuhusiana na video hiyo, kwa
mfano:
1. Unaona nini katika video hii?
2. Watu hawa wako wapi?
3. Hii ni sherehe gani? Sherehe hii husherehekewa mwezi gani?
4. Nini kimekufurahisha katika video hii?
5. Umewahi kuhudhuria sherehe ya aina hii?
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kujibu maswali waliyoulizwa kwa
kurejelea video waliyoitazama. Mwalimu azunguke darasani ili kuwasaidia
wanafunzi wanaotatizika katika makundi yao.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi bunifu.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kusoma
hadithi au kutazama video na kuweza kujibu maswali ya hadithi hiyo kwa
usahihi kulingana na muktadha wa hadithi hiyo.
91
VI. Majibu
Maswali ya hadithi, ukurasa 72
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na waliyosoma katika
vifungu walivyopewa, kwa mfano:
1. Mwezi wa kwanza ni Januari.
2. Shule hufungwa mwezi wa Aprili.
3. Shamba la baba lililimwa mwezi wa Februari.
Zoezi, ukurasa 73
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na waliyoona katika
video waliyotazama.
Mada Ndogo 5: Kuandika
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi
ya uandishi;
b) Kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
Mwanafunzi aelezee yaliyo muhimu katika uandishi k.v. mwandiko nadhifu,
maudhui, mtiririko n.k.
Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwalimu.
Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.
92
Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa kama hiki
kifuate hatua tano za uandishi: maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo,
uhariri na uchapishaji. Vichwa vya visa vinaweza kutofautiana.
III. Nyenzo:
Hadithi bunifu zilizoandikwa kwenye chati kuhusu miezi ya mwaka;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu miezi ya mwaka;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 63-64;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kukuza stadi ya mwanafunzi ya kuandika. Katika mada
hii, wanafunzi watapata maarifa ya kubuni na kuandika visa vifupi vifupi kwa
kuzingatia mambo kadhaa kama vile: mwandiko nadhifu, maudhui, mtiririko,
uhariri, marejeleo na maandalizi mengine kabambe. Shughuli hii itawawezesha
wanafunzi kufahamu jinsi ya kuandika visa vya kubuni katika muktadha
wowote. Muktadha wa uandishi katika mada hii ni kuhusu matukio na sherehe
mbalimbali za miezi ya mwaka. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa
vinavyohitajika kufundishia funzo hili kama vilivyoorodheshwa hapo juu ili
kufanikisha ufundishaji wake pamoja na ujifundishaji wa wanafunzi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika lililotolewa kwenye vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
93
kusoma hadithi za kubuni katika muktadha wa matukio na sherehe mbalimbali
za miezi ya mwaka. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali
waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi kusahihisha zoezi walilopewa katika funzo
la hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga
stadi yao ya kuandika na hata kubuni hadithi na kuiandika kwa hati nadhifu
katika madaftari yao. Mwalimu awaelekeze na kuwashirikisha wanafunzi katika
kujadiliana kuhusu mambo muhimu yanayofaa kuzingatiwa katika uandishi
bora ambayo ni: maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo, uhariri, maudhui
na mtiririko. Wanafunzi wajadiliane mambo haya muhimu ya kuzingatia ili
kuboresha uandishi wao. Mwalimu awaombe wanafunzi katika makundi yao
(ya wanafunzi watatu watatu) wabuni kisa chochote kinachohusiana na miezi
ya mwaka kwa mfano sherehe na matukio katika miezi mbalimbali ya mwaka.
Wanafunzi wabuni kisa hiki na kukiandika kwa kuzingatia mambo muhimu
ya uandishi. Baada ya shughuli hii, kila kundi lipewe fursa ya kuwasilisha kisa
chao mbele ya darasa kwa kukiandika ubaoni. Makosa yoyote ya kimaendelezo
au kisarufi yasahihishwe. Mwalimu awasaidie wanafunzi wanaotatizika katika
makundi yao.
Baada ya shughuli hii, mwalimu amwombe kila mwanafunzi anakili katika
daftari lake hadithi waliyopewa katika vitabu vyao iliyo na mapengo na kuyajaza
mapengo hayo kwa majibu mwafaka kutoka kwa yaliyo kwenye mabano. Kila
mwanafunzi ahakikishe ananakili hadithi hiyo kwa mwandiko nadhifu na kwa
maendelezo sahihi. Wanafunzi wajaze mapengo ya hadithi hiyo kwa majibu
mwafaka. Mwalimu ahakikishe atasahihisha madaftari ya wanafunzi baada ya
zoezi hili. Wanafunzi wote washirikishwe katika shughuli hii.
Hatimaye, mwalimu awasomee wanafunzi hadithi ifuatayo kuhusiana na miezi ya
mwaka. Kila mwanafunzi amsikilize mwalimu kwa makini. Mwalimu ahakikishe
anasoma hadithi hii kwa matamshi sahihi na kwa sauti ya kusikika na wanafunzi
94
wote. Iwapo mwalimu ana matatizo ya kimatamshi, basi anaweza kumwalika
msomaji stadi akawasomea wanafunzi hadithi hiyo. Baada ya kuwasomea
wanafunzi hadithi hii, mwalimu awaombe wanafunzi waelezane muhtasari wa
hadithi hiyo katika makundi yao.
Mfano wa hadithi
Mimi ninaitwa Chuchu. Ninasoma katika gredi ya tatu katika shule ya Bidii. Sisi
hufungua shule kila mwaka mwezi wa Januari. Mama hunipeleka shuleni asubuhi.
Mimi hukutana na wanafunzi wengine shuleni. Sisi husoma hadi mwezi wa Aprili
ambapo shule hufungwa. Likizo ya Aprili huwa nzuri kwangu kwa sababu mama
hunipeleka mjini Mombasa. Sisi huenda Mombasa kumtembelea shangazi yangu
anayeishi huko. Mimi hufurahia kuogelea baharini na kubarizi kwenye jua.
Shule hufunguliwa mwezi wa Mei kwa muhula wa pili. Katika mwezi huu
wafanyakazi wote dunia nzima husherehekea siku ya wafanyakazi. Likizo nyingine
huja mwezi wa Agosti. Mimi na wazazi wangu hutembelea mbuga ya wanyama
mjini Nairobi. Shule hufunguliwa kwa muhula wa mwisho mwezi wa Septemba.
Likizo ya mwisho wa mwaka huanza mwezi wa Novemba hadi Disemba ambapo
sherehe za Krismasi hufanyika. Sherehe hizi hufana sana. Mimi hufurahia sana
likizo zote katika mwaka wa kalenda. Je, wewe?
Mwalimu anaweza kuiandika hadithi hii ubaoni ili ionekane na wanafunzi wote.
Pia, anaweza kuwa tayari ameiandika hadithi hiyo kwenye chati ambazo anaweza
kuzionyesha kwa wanafunzi kisha wakanakili hadithi hiyo katika madaftari
yao. Baada ya shughuli hii, mwalimu ahakikishe amesahihisha madaftari ya
wanafunzi ili kukosoa makosa yoyote ya kimaendelezo na mwandiko usio
nadhifu. Wanafunzi walio na matatizo ya kuandika kwa mwandiko nadhifu
wapewe mazoezi zaidi ya kuandika. Mwalimu awaelekeze zaidi. Mwalimu
ahakikishe kuwa wanafunzi wote wanahusika katika shughuli hii ya kuandika
hadithi waliyosoma.
95
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kuandika maelezo kwa mwandiko
nadhifu na mtiririko unaofaa.
VI. Majibu
Zoezi la hadithi, ukurasa 63-64
Mwanzo wa mwaka shule ilipofunguliwa mzazi aliniambia nichukue mkoba
wangu wa vitabu. Ulikuwa mwezi wa kwanza. Mwezi huu huitwa Januari.
Tulipofika shuleni niliwaona wanafunzi wenzangu. Walinisalimia kwa
furaha. Tuliingia darasani tukaanza kusoma. Mwalimu wetu alifurahi kutuona.
Tulifunga shule mwezi wa Aprili. Huo ulikuwa mwisho wa muhula wa kwanza.
Mada Ndogo 6: Msamiati: Tarakimu 51-100
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua nambari 51-100 kwa maneno ili kuimarisha stadi ya
kuzungumza;
b) Kusoma nambari 51-100 kwa maneno ili kuimarisha usomaji bora;
ch) Kuandika nambari 51-100 kwa maneno ili kuimarisha uandishi bora;
d) Kuchangamkia kutumia nambari 51-100 kwa maneno katika
mazungumzo yake.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome majina ya nambari 51-100;
Wanafunzi waweza kupatiwa kadi za nambari 51-100 na majina yake ili
kuziambatanisha katika makundi;
Mwanafunzi aandike nambari 51-100;
96
Wanafunzi waweza kushirikishwa kupanga upya majina yaliyoparaganywa
ya nambari 51-100;
Mwanafunzi atunge sentensi akitumia majina ya nambari 51-100;
Mwanafunzi aweza kuonyeshwa vibonzo vikihesabu hadi 100 kwenye
tarakilishi .
III. Nyenzo:
Kadi za nambari 51-100;
Vifaa halisi vya kuhesabu darasani kama vile: peremende, kalamu, raba
n.k.,
Michoro au picha za vitu katika idadi za 51-100;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 64-66;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu msamiati wa kuhesabu nambari kutoka 51-100. Mwalimu
ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili
kuwaelekeza wanafunzi ipasavyo. Anaweza kutumia vifaa halisi vya wanafunzi
ambavyo wanaweza kuhesabu kama vile: kalamu, raba, rula, madaftari, vitabu,
michoro au picha ya vifaa katika idadi za 51-100 n.k. Mwalimu anaweza pia
kuleta vitu kama vile: peremende, mahindi, maharagwe n.k. ili wanafunzi
wahesabu darasani kwa kuzingatia idadi ya 51-100.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwaamkua wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia.
97
Wanafunzi wajibu maamkuzi ya mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wenye matatizo wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kufahamu jinsi ya
kuhesabu nambari 51-100 kwa nambari na kwa maneno. Mwalimu awagawe
wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha awaombe wasome
nambari zilizo katika kadi walizopewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi,
ukurasa 64. Wanafunzi wachunguze kadi hizo na kusoma nambari mbalimbali
zilizoandikwa kwenye kadi hizo za idadi 51-100. Wanafunzi wasome nambari
hizo katika makundi yao kisha kila mwanafunzi asome nambari hizo akiwa
peke yake.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika shughuli hii ya kuhesabu kisha
awaelekeze katika kuhesabu nambari zifuatazo. Anaweza kuzisoma nambari
hizi huku wanafunzi wakisoma baada yake wakiwa wawili na hatimaye kila
mwanafunzi apewe fursa ya kuzisoma akiwa peke yake.
51 hamsini na moja, 55 hamsini na tano, 58 hamsini na nane, 60 sitini,
63 sitini na tatu, 69 sitini na tisa, 70 sabini, 72 sabini na mbili, 77 sabini
na saba, 79 sabini na tisa, 80 themanini, 84 themanini na nne, 88 themanini
na nane, 90 tisini, 93 tisini na tatu, 96 tisini na sita, 99 tisini na tisa,
100 mia moja.
Mwalimu ahakikishe kuwa anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii
ya usomaji wa nambari hizo. Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi
zaidi ya usomaji wa nambari yaliyo katika vitabu vyao.
Baadaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika kufanya zoezi walilopewa
kwenye vitabu vyao kuhusu kuandika nambari mbalimbali walizopewa kwa
kutumia maneno. Mwalimu ahakikishe kila mwanafunzi anafanya zoezi hili
katika daftari lake. Awaelekeze wanafunzi wanaotatizika kufanya zoezi hili.
Mwalimu ahakikishe kuwa atasahihisha madaftari ya wanafunzi baada ya funzo
hili.
98
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika kutunga sentensi sahihi
wakitumia nambari walizofundishwa, kwa mfano:
1. Darasa letu lina wanafunzi hamsini na wawili.
2. Mimi nilipata alama themanini na nane katika mtihani wa Kiswahili.
3. Mama alinipatia shilingi mia moja nikanunue sukari kilo moja.
4. Wachezaji sitini walituzwa.
5. Walimu sabini na wawili wameajiriwa.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika funzo hili. Wanafunzi
wanaopata matatizo katika ujifundishaji wao wasaidiwe na mwalimu.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali tofauti kwa kuchunguza
iwapo wanaweza kuhesabu nambari 51-100 bila matatizo yoyote. Pia, mwalimu
achunguze iwapo wanafunzi wamefahamu kuandika nambari hizi kwa maneno
kwa usahihi. Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi yaliyo
katika vitabu vyao.
VI. Majibu
Zoezi la kuandika, ukurasa 65
1. Tisini na moja = 91
2. Tisini na mbili = 92
3. Tisini na tatu = 93
4. Tisini na nne = 94
5. Tisini na tano = 95
6. Tisini na sita = 96
7. Tisini na saba = 97
8. Tisini na nane = 98
9. Tisini na tisa = 99
10. Mia moja = 100
99
Mada Ndogo 7: Saru: Matumizi ya kikomo (.)
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua matumizi ya kikomo (.) katika kuimarisha mawasiliano;
b) Kuakifisha sentensi kwa kutumia kikomo (.) katika kuimarisha uandishi
bora;
ch) Kuzingatia kikomo (.) anaposoma kifungu na sentensi ili kuimarisha
usomaji bora;
d) Kuthamini matumizi ya kikomo (.) katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome sentensi zenye kikomo (.) katika vikundi.
Mwanafunzi aakifishe sentensi fupi kwa kutumia kikomo (.).
Mwanafunzi aandike sentensi akitumia kikomo (.).
III. Nyenzo:
Chati zenye sentensi zilizotumia kikomo (.);
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 66-67;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.)
IV. Maandalizi ya somo
Katika sehemu hii, mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla
ya vipindi hivi kama vilivyotajwa hapo juu. Wanafunzi wanaweza kutumiwa
katika funzo hili ili kuonyesha matumizi ya kikomo (.) kupitia kwa wao wenyewe
kutunga sentensi fupi na kuziandika ubaoni. Shughuli hii ya kutunga sentensi na
kuziandika ubaoni itawasaidia wanafunzi kubaini matumizi ya kikomo (.).
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
100
matumizi ya lugha ya ishara katika ufundishaji wake. Ikiwa kuna wanafunzi
wasioweza kuona, mwalimu ajitahidi kuandaa maelezo yake kwenye breli ili
kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha kama wanafunzi wengine.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi katika vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu aanze funzo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia kuhusiana na
msamiati wa kuhesabu nambari 51-100. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu
kisha wajibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika
kusahihisha zoezi walilopewa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wenye
matatizo wasaidiwe.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu
kisha awashirikishe katika kuchunguza na kusoma sentensi walizopewa katika
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 66. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa
kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na sentensi hizo kama vile: Alama gani
imetumika mwishoni mwa kila sentensi? Alama hii inamaanisha nini? Wanafunzi
wajibu maswali ya mwalimu kulingana na sentensi walizopewa katika vitabu
vyao. Wanafunzi waelekezwe kubaini kuwa alama iliyotumika mwishoni mwa
sentensi walizopewa ni alama ya kikomo (.). Alama ya kikomo hutumika
mwishoni mwa sentensi kuonyesha kuwa sentensi imekamilika.
Wanafunzi washirikishwe katika kutunga sentensi sahili na kuziandika katika
madaftari yao huku wakizingatia matumizi ya alama ya kikomo (.). Kwa mfano :
1. Mimi ninaitwa Karimi.
2. Shule yetu ina wanafunzi sitini.
3. Mwalimu wetu wa Kiswahili ni mzuri.
101
4. Mimi ninapenda kusoma hadithi za Kiswahili.
5. Tutafunga shule mwezi wa Aprili.
Kupitia kwa hatua hii ya utunzi wa sentensi na kuziandika, wanafunzi watapata
fursa ya kufahamu kuwa kila sentensi kamili huwekewa kikomo (.) mwishoni ili
kuashiria kuwa imekamilika. Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuandika alama
ya kuuliza kwa usahihi.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awaelekeze wanafunzi kufahamu kuwa alama
ya kikomo ni mojawapo ya alama za uakifishaji katika lugha.
Wanafunzi washirikishwe kufanya zoezi la kuandika sentensi walizopewa kwa
kutumia alama ya kikomo kwa usahihi.
Wanafunzi wafanye mazoezi kadhaa kuhusiana na matumizi ya alama ya
kikomo (.).
(ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa kwa kuchunguza ikiwa wamefahamu matumizi
sahihi ya alama ya kikomo (.). Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wanaweza kutunga sentensi sahihi na kuziandika kwa kutumia alama ya kikomo.
VI. Majibu
Zoezi, ukurasa 67
1. Mwalimu wetu ni mzuri.
2. Nilizaliwa mwezi Mei.
3. Dada yangu alizaliwa mwezi Agosti.
4. Tunaipenda nchi yetu.
5. Hiki ni kitabu changu.
102
Matokeo maalum
yanayotarajiwa
Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutambua sauti mbili
zinazotamkwa pamoja ili
kuimarisha matamshi bora;
(b) Kutambua msamiati wa kazi
mbalimbali ili kuimarisha
mawasiliano;
(ch) Kusikiliza kwa makini masimulizi
kuhusu kazi mbalimbali ili
kuimarisha usikivu;
(d) Kutambua picha za watu na
kazi mbalimbali ili kuimarisha
ufahamu wa hadithi;
(e) Kuandika kisa kifupi kwa hati
nadhifu kulingana na mada ili
kujenga stadi ya uandishi;
(f) Kutambua ukanusho wa -li-,
-na- na –ta- katika sentensi ili
kuimarisha mawasiliano.
Mwanafunzi atambue sauti /py/
na /vy/ katika maneno.
Mwanafunzi atazame picha na
michoro inayoonyesha watu
na kazi mbalimbali k.v. ualimu,
ukulima, udaktari, uyaya, unesi na
ubawabu ili azitambue peke yake
au katika vikundi.
Mwanafunzi asimulie kuhusu kazi
mbalimbali.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi apewe hadithi yenye
mapengo ajaze kwa maneno
mwafaka.
Wanafunzi watumie -li-,
-na- na -ta- kuelezea vitendo
walivyofanya katika wakati
uliopita (-li-), uliopo (-na-) na ujao
(-ta-) wakiwa katika vikundi au
wawili wawili.
Mada Kuu 4: KAZI MBALIMBALI
Idadi ya vipindi: 15
Sura ya
4
103
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji
Kazi ya vikundi.
Kushiriki katika kuigiza, kuimba nyimbo na kukariri mashairi katika tamasha
mbalimbali.
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Kiingereza na Somo la Mazingira.
Nyenzo:
Michoro na picha za watu katika kazi mbalimbali;
Kadi zenye sauti /py/ na /vy/;
Kadi zenye majina yenye sauti /py/ na /vy/;
Rekodi za hadithi na masimulizi bunifu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 68-83;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Kutokana na mada hii,wanafunzi wanafaa kupata maarifa kuhusu sauti /py/ na
/vy/, jinsi ya kuzitamka, maneno yenye sauti hizi pamoja na kutunga sentensi
kwa kutumia maneno yenye sauti hizi. Katika mada hii, wanafunzi watafundishwa
kazi mbalimbali za watu. Pia, kipengele cha masimulizi na hadithi za kubuni
zinazohusisha watu na kazi zao mbalimbali zitafundishwa hapa. Masimulizi na
hadithi za kuvutia na zenye msamiati wa kiwango cha wanafunzi wa gredi hii
zibuniwe ili kuwafaa wanafunzi katika ujifundishaji wao. Kama tujuavyo, kazi
ni muhimu kwa kila binadamu kwa sababu kutokana na kazi watu hupata riziki
yao ya kila siku. Kutokana na kazi binadamu hupata chakula, mavazi, matibabu,
karo na pesa za kujikimu kimaisha.
Pia, mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kufahamu matumizi ya wakati
uliopita, wakati uliopo na wakati ujao pamoja na ukanusho wa nyakati hizi.
104
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
Uraia,
Shughuli zinazomsaidia mwanafunzi: mwongozo wa ajira,
Utangamano wa kijamii,
Kuthamini kazi mbalimbali.
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na binadamu ni kama vile:
Msamiati Maana
1.
mwalimu
mtu ambaye huwafundisha wanafunzi
2.
daktari
mtu ambaye huwatibu wagonjwa
3.
bawabu
mtu anayelinda lango la kuingia mahali fulani kama vile:
shule
4.
kazi
shughuli ambayo mtu hufanya ili kupata riziki
5.
rubani
mtu ambaye huendesha ndege angani
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Katika ufundishaji wa mada hii, mwalimu ahakikishe kuwa ana vifaa muhimu na
maalum vya kuwasaidia wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali ili
kuweza kuwashirikisha katika ujifundishaji wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo
wa kuona, mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya breli pamoja na vifaa vya
kunasia sauti.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri
wa lugha ya ishara. Yote haya yatawawezesha wanafunzi hawa kusoma na
kujifundisha kama wanafunzi wenzao bila vikwazo vyovyote.
105
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya
vipindi
Mada Ndogo 1: Sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja
2
Mada Ndogo 2: Msamiati
3
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 5: Kuandika
3
Mada Ndogo 6: Sarufi: Ukanusho wa nyakati
2
JUMLA: 15
Mada Ndogo 1: Sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua sauti mbili zinazotamkwa pamoja ili kuimarisha matamshi
bora;
b) Kutamka sauti lengwa ili kuimarisha matamshi bora;
ch) Kusoma silabi za sauti lengwa ili kumarisha usomaji bora;
d) Kuandika silabi zinazotokana na sauti lengwa ili kuimarisha uandishi
bora;
e) Kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa ili
kuimarisha usomaji;
f) Kuandika maneno kutokana na silabi zilizofunzwa ili kuimarisha usomaji
bora;
g) Kusoma hadithi zilizo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kumsaidia
mwanafunzi kutamka sauti husika na kuimarisha matamshi na usomaji;
h) Kuchangamkia kutamka sauti lengwa ili kuimarisha mawasiliano.
106
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atambue sauti /py/ na /vy/ katika maneno.
Mwanafunzi atamke silabi zinazotokana na sauti lengwa baada ya mwalimu,
kisha atamke pamoja na mwalimu na baadaye atamke akiwa peke yake,
wawili na kama darasa zima k.m. pya, pye, vya na vye.
Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia kama vile papaya, tarakilishi projekta
na kipazasauti ili kuimarisha matamshi yake.
Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
Mwanafunzi atambue sauti alizosoma katika maneno.
Mwanafunzi aandike maneno yanayojumuisha sauti lengwa.
Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi na kuchanganua yaliyo
marefu zaidi.
Wanafunzi waweza kusoma hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti
lengwa darasani au wawili wawili.
Mwanafunzi asikilize imla ya maneno yaliyo na herufi za sauti lengwa na
kuyaandika.
III. Nyenzo:
Kadi zenye herufi py na vy;
Rekodi za sauti /py/ na /vy/;
Kadi zenye maneno yenye sauti /py/ na /vy/;
Mgeni mwalikwa mwenye matamshi mazuri na sahihi;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 69-74;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Mada hii inahusu sauti mbili za Kiswahili zinazotamkwa pamoja kwa kurejelea
watu na kazi zao mbalimbali. Herufi na sauti zitakazoangaziwa katika funzo
hili ni: /py/ na /vy/. Matamshi fasaha na sahihi ya wanafunzi yatazingatiwa
hapa na kukuzwa zaidi. Wanafunzi walio na matatizo ya utamkaji wa sauti hizi
wasaidiwe na mwalimu.
107
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi.
Vifaa hivi ni kama vile: kadi zenye herufi py na vy, rekodi za matamshi ya
sauti lengwa, mgeni mwalikwa mwenye matamshi mazuri na sahihi, kadi zenye
maneno yenye herufi na sauti lengwa pamoja na vyombo vingine maalum vya
kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo na ulemavu mbalimbali.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu akumbuke kuwa matumizi ya michoro,
picha, vifaa halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha ufundishaji wa
wanafunzi; hasa wale ambao wana matatizo au ulemavu mbalimbali katika
kuelewa na kufahamu haraka yale wanayofundishwa darasani.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa
katika Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize somo hili kwa kuwaamkua wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichopita. Wanafunzi wajibu
maamkuzi ya mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kuchunguza michoro iliyo katika
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 68. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa
kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na michoro hiyo. Baadhi ya maswali
ambayo mwalimu anaweza kuuliza ni kama vile: Mnaona nani kwenye mchoro
huu? Watu hawa wanafanya kazi gani? Mwalimu awaelekeze wanafunzi ili
waweze kujibu maswali hayo na kufahamu aina ya kazi zinazofanywa na watu
walio katika michoro waliyopewa.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
i) Sauti /py/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaelekeze kutazama mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 69.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na mchoro uliopo.
108
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye mchoro huu? Taja jina la mchoro huu.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua jina sahihi la mchoro
waliopewa ambalo ni kompyuta kisha watamke sauti /py/ kwa usahihi.
Wanafunzi watamke sauti /py/ baada ya mwalimu katika darasa zima kisha
wakiwa wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi atamke sauti hii akiwa peke
yake. Mwalimu awaombe wanafunzi waandike sauti /py/ katika madaftari yao
kwa herufi kubwa na herufi ndogo. Yaani: py na PY.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi py, ambazo ni: pya, pye, pyi, pyo, pyu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi py. Kwa mfano: kompyuta, kipya, upya n.k. Mwalimu awashirikishe
wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye silabi za herufi py kwa usahihi.
Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Hii ni kompyuta ya mwalimu.
2. Mama amevaa kiatu kipya.
3. Mavazi yake ni mapya.
4. Upya wa gari lake ulimfurahisha.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi py.
ii) Sauti /vy/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 71.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kutambua majina sahihi
ya michoro waliyopewa ambayo ni ya vyura, vyakula na vyoo, kisha watamke
109
sauti za kwanza za majina hayo pekee ambazo ni /vy/. Wanafunzi watamke
sauti /vy/ baada ya mwalimu katika darasa zima, kisha wakiwa wawili wawili
na hatimaye atamke sauti hii akiwa peke yake. Mwalimu awaombe wanafunzi
waandike sauti /vy/ katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
Yaani: vy na VY.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi vy, ambazo ni: vya, vye, vyi, vyo, vyu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi vy. Kwa mfano: vyura, vyoo, vyumba, vyangu, vyakula, vyombo, vyetu
n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye
silabi za herufi vy kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno
hayo.
Kwa mfano:
1. Vyakula hivi ni vitamu.
2. Hawa ni vyura wakubwa.
3. Fundi wanajenga vyumba vizuri.
4. Shule yetu ina vyoo vingi.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi vy.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo hili kuhusu sauti /py/ na /vy/ kwa
kuwauliza wanafunzi maswali tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali haya yatilie mkazo uwezo wa wanafunzi wa kutamka sauti /py/ na
/vy/ kwa usahihi, kutambua na kutamka maneno yenye sauti hizi kwa usahihi
pamoja na kutunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno yenye sauti hizi
walizojifundisha. Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza
kuandika herufi hizo kwa usahihi kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
110
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 68
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi waeleze kuwa wanaona
mwalimu, daktari na seremala katika michoro waliyopewa.
Maswali, ukurasa 69
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu chombo wanachoona
katika mchoro waliopewa ambacho ni kompyuta.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 70
Mwalimu atathmini maandishi ya wanafunzi.
Maswali, ukurasa 70
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watambue sauti /py/,
kwa mfano:
1. Kiatu cha mama ni kipya
2. Baba ananunua gari jipya.
3. Makoti haya ni mapya.
Zoezi, ukurasa 71
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi waonyeshe silabi katika
maneno waliyopewa, kwa mfano:
Neno Silabi
1. mapya ma pya
2. jipya ji pya
3. vipya vi pya
111
Maswali, ukurasa 72
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu wanachoona katika
michoro waliyopewa ambayo ni ya: vyura, vyakula na vyoo.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 72
Mwalimu atathmini maandishi ya wanafunzi ya herufi vy, kwa herufi ndogo
na herufi kubwa.
Maswali, ukurasa 74
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watambue sauti /vy/,
kwa mfano:
1. Vipande vyote vitatumiwa.
2. Vyombo vyenu vimeoshwa.
3. Vyakula vizuri ni hivi.
4. Vipindi vyote vimeanza.
5. Vyura wengi wamekufa.
Zoezi, ukurasa 74
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi waonyeshe silabi katika
maneno waliyopewa, kwa mfano:
Neno Silabi
1. vyao vya o
2. vyura vyu ra
3. vyuma vyu ma
112
Mada Ndogo 2: Msamiati wa kazi mbalimbali
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati wa kazi mbalimbali ili kuimarisha mawasiliano;
b) Kutunga sentensi akitumia msamiati wa kazi mbalimbali ili kujenga
ubunifu;
ch) Kusoma maneno na sentensi kuhusu kazi mbalimbali ili kuimarisha
usomaji;
d) Kuandika maneno na sentensi kuhusu kazi mbalimbali ili kuimarisha
uandishi bora;
e) Kuthamini kazi mbalimbali ili kutambua huduma zinazotolewa na watu
wanaofanya kazi mbalimbali.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atazame picha na michoro inayoonyesha watu na kazi
mbalimbali k.v. ualimu, ukulima, udaktari, uyaya, unesi na ubawabu ili
azitambue peke yake au katika vikundi.
Wanafunzi waweza kuambatanisha kadi za maneno na kazi mbalimbali
wakiwa katika makundi.
Mwanafunzi aeleze kazi mbalimbali.
Mwanafunzi aandike majina ya kazi mbalimbali.
Mwanafunzi asome msamiati wa kazi mbalimbali katika kadi, chati n.k.
Mwanafunzi aandike sentensi kuhusu kazi mbalimbali.
Mwanafunzi atunge na kusoma sentensi wakitumia msamiati wa kazi
mbalimbali.
III. Nyenzo:
Kadi zenye majina ya kazi mbalimbali;
Michoro au picha zinazoonyesha kazi mbalimbali;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 74-76;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
113
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Msemo kuwa kazi ni kazi hivyo ni muhimu kwa kila mtu kufahamu kuwa kazi
yoyote ni bora kuliko kukosa kazi kabisa kwa sababu angalau kutokana na kazi
yoyote mtu anaweza kujipatia riziki. Kuna kazi mbalimbali kama vile: udaktari,
unesi, uandishi, ualimu, upishi, ukulima, uhariri, udereva, urubani, ufugaji n.k.
Kazi mbalimbali zina manufaa kwa wanaozifanya na kwa wanaofanyiwa. Hivyo,
kazi ni muhimu kwa kila binadamu.
Mwalimu aandae funzo hili kwa namna ya kumwezesha kuwaelekeza wanafunzi
kufahamu kazi mbalimbali pamoja na majina ya watu ambao huzifanya kazi
hizo.
Vifaa vitakavyohitajika kama vile kadi zenye maneno mbalimbali ya kazi
mbalimbali pamoja na michoro au picha zinazoonyesha kazi mbalimbali
viandaliwe ili ujifunzaji wa funzo hili uwe rahisi na ufanikishwe. Vifaa hivyo
vionyeshwe hadharani kwa wakati unaofaa na ikiwa kuna wanafunzi wasioona
au wasiosikia, mwalimu awasaidie kwa kuwaomba kugusa vifaa au michoro
hiyo huku maelezo yake yakitamkwa kwa sauti na kuandikwa ubaoni au kwenye
breli.
Katika funzo hili, mwalimu ahakikishe kuwa amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa
kwa kila zoezi linalohusika.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize funzo lake kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu kipindi cha hapo awali kuhusu utamkaji wa sauti
mbili za Kiswahili zinazotamkwa pamoja ambazo ni /py/ na /vy/. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu na maswali waliyoulizwa kuhusu waliyofundishwa
katika kipindi kilichopita. Mwalimu awaongoze wanafunzi kwa kusahihisha kazi
iliyotolewa kama zoezi. Wanafunzi wasahihishe zoezi hilo na mwalimu awape
majibu kwa kutilia mkazo pale ambapo wanafunzi wanatatizika.
114
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne wanne na
awaombe watazame michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 74-
75. Wanafunzi wachunguze michoro hiyo. Mwalimu awachangamshe wanafunzi
kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusu michoro hiyo. Anaweza kuwauliza
maswali kama vile: Unaona nini kwenye michoro hii? Watu hawa wanafanya kazi
gani? n.k. Wanafunzi, kwa upande wao, wajibu maswali ya mwalimu wao kwa
kueleza kile wanachoona katika michoro hiyo. Kwa mfano: Ninaona nesi; Ninaona
bawabu; Ninaona dereva; Ninaona mekanika n.k. Baada ya mwalimu kuridhika
kuwa wanafunzi wamechunguza michoro hiyo na kuielewa, awashirikishe katika
kuigiza kazi mbalimbali ambazo hufanywa na watu katika michoro waliyopewa.
Mwalimu awaelekeze wanafunzi kufahamu watu na kazi zao mbalimbali, kwa
mfano:
1. daktari mtu ambaye huwatibu wagonjwa
2. nahodha mtu ambaye huendesha meli
3. mpishi mtu ambaye hupika vyakula mbalimbali
4. seremala - mtu ambaye hutengeneza fanicha kwa kutumia mbao
5. rais mtu ambaye ni kiongozi wa nchi au taifa
Katika makundi yao, wanafunzi waelekezwe kufanya zoezi la kulinganisha
majina ya kazi mbalimbali kwenye kadi walizopewa pamoja na maelezo sahihi
ya kazi hizo katika vitabu vyao. Mwalimu ahakikishe wanafunzi wanafanya
ulinganisho huu kwa usahihi.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu watu mbalimbali na kazi zao mbalimbali.
Wanafunzi waweze kutunga sentensi sahihi kwa kutumia majina ya kazi
mbalimbali. Wanafunzi wawaeleze wenzao kazi ambazo wangependa kuzifanya
baada ya wao kukamilisha masomo yao.
115
VI. Majibu
Maswali ya utangulizi, ukurasa 74-75
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona
kwenye michoro waliyopewa.
Kwa mfano:
1. Ninaona watu mbalimbali wa kazi mbalimbali.
2. Ninaona dereva, nesi, bawabu na mekanika.
3. Dereva huendesha gari, baiskeli, pikipiki n.k.; nesi huwahudumia
wagonjwa; mekanika hutengeneza magari yaliyoharibika na bawabu
hulinda lango la kuingia mahali fulani.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu kazi ambazo
wangependa kufanya baada ya wao kukamilisha masomo yao.
Zoezi la kusoma kadi, ukurasa 75-76
1. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi wanaposoma maneno
yaliyo kwenye kadi walizopewa.
2. Mwalimu atathmini ulinganisho wa wanafunzi wa majina
waliyopewa kwenye kadi na maelezo waliyopewa kwenye vitabu
vyao, kwa mfano:
1. Msichana anayelea watoto ni yaya.
2. Mlinzi wa lango ni bawabu.
3. Mtu anayewahudumia wagonjwa hospitalini ni muuguzi.
4. Mtu anayepanda mbegu na kuvuna mazao ni mkulima.
5. Mtu anayewafundisha wanafunzi ni mwalimu.
6. Mtu anayewatibu wagonjwa ni daktari.
7. Mtu anayepika vyakula ni mpishi.
8. Mtu anayeendesha ndege angani ni rubani.
116
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kusikiliza kwa makini masimulizi kuhusu kazi mbalimbali ili kuimarisha
usikivu;
b) Kueleza kuhusu kazi mbalimbali ili kumarisha stadi ya kuzungumza;
ch) Kutaja majina ya kazi mbalimbali na watu wanaozifanya ili kuimarisha
stadi ya kuzungumza;
d) Kutathmini kazi mbalimbali.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asimulie kuhusu kazi mbalimbali.
Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu kazi mbalimbali.
Mwanafunzi aelezee umuhimu wa kazi mbalimbali.
Mwanafunzi aweza kushiriki katika nyimbo au mashairi kuhusu kazi
mbalimbali.
Mwanafunzi ashiriki katika kuigiza kazi inayofanywa na watu mbalimbali.
Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa anapozungumza kuhusu
kazi mbalimbali.
Wanafunzi waweza kutazama picha au michoro inayoonyesha watu na kazi
mbalimbali wajadiliane katika vikundi.
III. Nyenzo:
Rekodi za masimulizi bunifu mbalimbali kuhusu kazi mbalimbali;
Michoro au picha za kazi mbalimbali;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Mgeni mwalikwa (karani, dereva, bawabu au mpishi);
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 77-78;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
117
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusikiliza masimulizi ya
kubuni yanayohusu watu na kazi mbalimbali wanazofanya ili kujenga stadi
yao ya kusikiliza na kuzungumza. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta
vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji na
uwasilishaji wake. Mwalimu anaweza kuwaalika wageni ambao ni watu wa kazi
mbalimbali kama vile: dereva, mpishi, bawabu, karani, mwalimu mwingine n.k.
watakaozungumza kuhusu kazi zao mbalimbali pamoja na umuhimu wa kazi
hizo kwa maisha yao na ya watu wengine. Mwalimu anaweza kuwapata wageni
hawa waalikwa kutoka shuleni kwao.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
msamiati wa kazi mbalimbali. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja
na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili wasaidiwe.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza masimulizi bunifu pamoja na stadi ya kuzungumza kupitia kwa
wao wenyewe kuwasimulia wenzao katika vikundi. Masimulizi haya yatahusu
kazi mbalimbali na watu wanaozifanya kazi hizo.
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne wanne kisha
awaombe waigize kazi zinazofuata:
118
1. Kazi ya udaktari
2. Kazi ya ualimu
3. Kazi ya udereva
4. Kazi ya upishi
5. Kazi ya ukulima
Baada ya shughuli hii ya uigizaji, mwalimu awasomee wanafunzi shairi walilopewa
katika vitabu vyao kuhusu watu na kazi zao mbalimbali. Mwalimu ahakikishe
wanafunzi wote wanamsikiliza kwa makini. Pia, mwalimu ahakikishe kuwa
anasoma shairi hilo kwa ufasaha, kwa matamshi sahihi na sauti ya kusikika na
ya kuvutia. Iwapo mwalimu ana matatizo ya kimatamshi, anaweza kumwalika
msomaji stadi atakayewasomea wanafunzi shairi hilo kuhusu watu na kazi zao
mbalimbali.
Baada ya kusomewa shairi hilo, wanafunzi wajaribu katika makundi yao (ya
wanafunzi wannewanne) kulisoma shairi hilo kwa ufasaha na matamshi sahihi.
Kisha, katika makundi yao walikariri shairi hilo kwa mahadhi mbalimbali wakiwa
wawili na hatimaye kila mwanafunzi alisome na kulikariri shairi hilo akiwa
peke yake. Mwalimu ahakikishe anasahihisha makosa ya kimatamshi pindi tu
yanapotokea. Baadaye, wanafunzi katika makundi yao waelezane kuhusu shairi
walilosoma linalohusu watu na kazi zao mbalimbali. Wanafunzi waelezane
kuhusu kazi mbalimbali zilizotajwa katika shairi walilosoma. Baadaye, mwalimu
awashirikishe katika kujibu maswali ya masimulizi waliyopewa. Mwalimu
ahakikishe anawasaidia wanafunzi wanaotatizika katika makundi yao.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao kusimuliana
kuhusu kazi ambazo wangependa kuzifanya baada ya wao kukamilisha
masomo yao. Kila mwanafunzi apewe muda wa kusimulia kuhusu kazi ambayo
angependa kuifanya baada ya masomo yake. Kila mwanafunzi aeleze sababu
za kuchagua kazi atakayoitaja. Wanafunzi wasimuliane umuhimu wa kazi kwa
maisha ya binadamu.
Wanafunzi wote washirikishwe katika masimulizi haya katika makundi yao.
Wanafunzi wanaopata matatizo katika makundi yao wasaidiwe.
119
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma kwa ufasaha
masimulizi bunifu pamoja na kuigiza kazi mbalimbali. Pia, mwalimu achunguze
iwapo wanafunzi wameweza kupata maarifa ya kujibu kwa usahihi maswali
ya shairi kulingana na muktadha husika. Wanafunzi pia watathminiwe zaidi ili
kubaini iwapo wamefahamu kazi mbalimbali pamoja na umuhimu wao kwa
binadamu.
VI. Majibu
Maswali ya shairi, ukurasa 78
1. Baba ni bawabu.
2. Mama ni daktari.
3. Kaka ni mwalimu.
4. Baba analinda kwa kutumia bunduki.
5. Mama anatibu kwa kutumia sindano.
6. Kaka anafundisha kwa kutumia chaki.
Zoezi la masimulizi, ukurasa 78
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi katika makundi yao kuhusu kazi
ambazo wangependa kufanya baada ya wao kukamilisha masomo yao.
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua picha za watu na kazi mbalimbali ili kuimarisha ufahamu wa
hadithi;
b) Kusikiliza hadithi ikisomwa na mwalimu kuhusu kazi mbalimbali ili
kuimarisha usomaji na usikivu;
120
ch) Kusoma hadithi kuhusu kazi mbalimbali ili kuimarisha stadi ya kusoma;
d) Kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu kazi mbalimbali ili
kuelewa ujumbe;
e) Kuchangamkia kusoma hadithi.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
Wanafunzi waweza kusoma katika darasa, wakiwa wawili na baadaye
mwanafunzi asome peke yake.
Mwanafunzi anaweza kusikiliza hadithi ikisomwa kupitia vifaa vya
kiteknolojia kama vile tarakilishi na projekta.
Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kwa kutumia kitabu mbele ya darasa.
Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi.
Mwanafunzi aweza kujibu na kuuliza maswali kuhusu hadithi aliyosoma.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za hadithi bunifu kuhusu kazi mbalimbali;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu kazi mbalimbali;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu, projekta;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 78-80;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu ili kujenga stadi ya wanafunzi ya
kusikiliza pamoja na ya kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa
vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake kama
vilivyotajwa hapo juu. Mwalimu anaweza kuwaonyesha wanafunzi michoro
121
au picha za hadithi bunifu hasa kuhusu kazi mbalimbali ambazo atawasomea
wanafunzi darasani na nyingine ambazo watajisomea wenyewe. Mwalimu
anaweza hata kumwalika mtambaji, msimulizi au msomaji mashuhuri
akawasomea wanafunzi hadithi hizo bunifu kisha wanafunzi wakasoma baada
yake kama darasa zima, wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi asome
akiwa peke yake. Msimulizi mwalikwa huyu sharti awe na uwezo wa kusoma
kwa sauti ya kusikika, ya kuvutia na asome kwa matamshi sahihi na kwa ufasaha.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
funzo la hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao
ya kusikiliza pamoja na kusoma hadithi bunifu. Mwalimu awagawe wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha wasome hadithi fupi
fupi walizopewa pamoja na kutazama michoro inayoambatana na hadithi
hizo. Wanafunzi wachunguze kila mchoro kwa kila hadithi waliyopewa na
kuichambua. Wanafunzi wasome hadithi hiyo katika makundi yao kisha wasome
wakiwa wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi apewe fursa ya kusoma
peke yake. Mwalimu ahakikishe anasahihisha makosa yoyote ya matamshi pindi
tu yanapotokea. Shughuli hii ya kila mwanafunzi kusoma peke yake itasaidia
katika kukuza uwezo na stadi ya kusoma ya kila mwanafunzi. Kupitia kwa zoezi
hili, ni rahisi kwa mwalimu kufahamu matatizo ya kila mwanafunzi kibinafsi.
Kila mwanafunzi ashughulikiwe kibinafsi. Baada ya shughuli hii, mwalimu
122
awaelekeze wanafunzi katika kuigiza baadhi ya vitendo vya usafi walivyopewa
katika vitabu vyao. Kila mwanafunzi ashirikishwe katika shughuli hii.
Hatimaye, mwalimu awasomee wanafunzi imla ifuatayo na wao waiandike
kwenye madaftari yao. Mwalimu ahakikishe anasoma kwa matamshi na sauti
ya kusikika.
Michoro iliyo katika vitabu vya wanafunzi inaonyesha kazi mbalimbali.
Wanafunzi wajadili hadithi walizosoma katika makundi yao.
Baada ya shughuli hii ya wanafunzi kusoma hadithi na kuchunguza michoro
waliyopewa, mwalimu awaelekeze kujibu maswali waliyoulizwa kutokana
na hadithi hizo. Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika
majadiliano haya. Azunguke darasani ili kuwasaidia wanafunzi wanaotatizika
katika makundi yao. Wanafunzi wajibu maswali hayo kwa kurejelea hadithi
walizosoma. Mwalimu anaweza kuzirekodi hadithi hizo kwenye tarakilishi
au simu ili wanafunzi wazisikilize tena na tena au hata kuziandika ubaoni ili
wanafunzi wajisomee wenyewe baada ya mwalimu kisha katika makundi yao na
hatimaye kila mmoja mmoja.
Wanafunzi wanaotatizika katika shughuli hii wasaidiwe.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi bunifu
pamoja na kufahamu kazi mbalimbali. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wamepata ufahamu wa kusoma hadithi na kuweza kujibu maswali ya hadithi
hiyo kwa usahihi kulingana na muktadha wa hadithi hiyo.
VI. Majibu
Maswali ya hadithi, ukurasa 80
1. Hadithi hii imetaja kazi ya mwalimu, daktari na mkulima.
2. Mwalimu huwafundisha wanafunzi.
3. Bwana Jembemali atapanda mahindi, viazi, mboga na matunda.
4. Daktari anatibu uso wa mgonjwa.
123
Mada Ndogo 5: Kuandika
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi
ya uandishi;
b) Kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
Mwanafunzi aelezee yaliyo muhimu katika uandishi k.v. mwandiko nadhifu,
maudhui, mtiririko.
Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwalimu.
Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.
Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa kama hiki
kifuate hatua tano za uandishi: maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo,
uhariri na uchapishaji. Vichwa vya visa vinaweza kutofautiana.
III. Nyenzo:
Hadithi bunifu zilizoandikwa kwenye chati;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu kazi mbalimbali;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 80-81;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kukuza stadi ya mwanafunzi ya kuandika. Katika mada hii,
wanafunzi watapata maarifa ya kuandika visa vifupi vifupi kwa kuzingatia mambo
kadhaa kama vile: mwandiko nadhifu, mtiririko, uhariri, marejeleo na maandalizi
124
kabambe. Shughuli hii itawawezesha wanafunzi kufahamu jinsi ya kuandika visa
bunifu. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia
funzo hili kama vilivyoorodheshwa hapo juu ili kufanikisha ufundishaji wake
pamoja na ujifundishaji wa wanafunzi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika lililotolewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
funzo la hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji
wao wasaidiwe.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga
stadi yao ya kuandika na hata kubuni hadithi na kuiandika madaftarini mwao.
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili
kisha awaombe wasome hadithi waliyopewa katika vitabu vyao. Wanafunzi
wasome hadithi hii katika makundi yao kisha kila mwanafunzi apewe fursa ya
kusoma peke yake. Baada ya shughuli hii ya kusoma, mwalimu amwombe kila
mwanafunzi aandike (anakili moja kwa moja) hadithi hiyo waliyosoma katika
madaftari yao. Mwalimu ahakikishe kuwa kila mwanafunzi anaandika hadithi
hiyo kwa hati nadhifu.
Mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wote wanahusika katika shughuli hii ya
kuandika hadithi waliyosoma. Mwalimu anaweza kuiandika hadithi hii ubaoni.
Pia, anaweza kuwa tayari ameiandika hadithi hiyo kwenye chati ambazo anaweza
kuzionyesha kwa wanafunzi kisha wakanakili hadithi hiyo katika madaftari yao.
Baada ya shughuli hii, mwalimu ahakikishe amesahihisha madaftari ya wanafunzi
ili kukosoa makosa yoyote ya kimaendelezo na mwandiko usio nadhifu.
125
Wanafunzi walio na matatizo ya kuandika kwa mwandiko nadhifu wapewe
mazoezi zaidi ya kuandika. Mwalimu awaelekeze zaidi.
Hatimaye, mwalimu amwombe kila mwanafunzi aandike maelezo mafupi
kuhusu kazi ambayo angependa kuifanya baada ya kuyakamilisha masomo yake.
Wanafunzi waelekezwe kuandika maelezo hayo mafupi kwa kujibu maswali haya:
1. Unapenda kazi gani?
2. Kazi hiyo inafanywa vipi?
3. Ni nani anafanya kazi hiyo?
4. Umewahi kuona mtu akifanya kazi hiyo?
5. Ukimaliza masomo unataka kufanya kazi gani? Kwa nini?
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wanaandika maelezo haya bunifu kuhusu kazi
wanazopenda kwa mwandiko nadhifu. Pia, wanafunzi wazingatie mtiririko
mwema pamoja na kuhariri kazi yao ili kupunguza makosa ya tahajia pamoja na
kisarufi. Mwalimu anaweza kuwaongoza wanafunzi katika kuandaa nakala ya
kwanza ya maelezo yao kisha waihariri nakala hii na hatimaye kuandika nakala
zao safi katika madaftari yao. Kila mwanafunzi apewe fursa ya kuwasomea
wanafunzi wenzake aliyoandika kuhusiana na kazi ambayo angependa kuifanya
baada ya masomo yao.
Mwalimu anaweza kumwomba kila mwanafunzi aandike nakala yake safi
ubaoni ili wanafunzi wenzake waisome na kuikosoa kwa kurejelea mwandiko,
makosa ya kimaendelezo pamoja na ya kisarufi. Pia, wanafunzi katika makundi
yao wanaweza kusahihisha nakala zao safi. Mwalimu azunguke darasani
kuhakikisha kila kundi linashughulika vyema bila matatizo. Wanafunzi walio na
matatizo wasaidiwe.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kubuni na kuandika maelezo bunifu. Pia,
mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kazi mbalimbali
ambazo wangependa kuzifanya baada ya masomo yao.
126
VI. Majibu
Zoezi la kuandika, ukurasa 80
Mwalimu atathmini maandishi ya wanafunzi. Wanafunzi wanakili kwa usahihi
katika madaftari yao hadithi waliyosoma kutoka kwenye vitabu vyao.
Zoezi la kubuni na kuandika, ukurasa 80-81
Mwalimu atathmini ubunifu na uandishi wa wanafunzi wa kazi ambazo
wangependa kuzifanya baada ya kukamilisha masomo yao.
Mada Ndogo 6: Saru: Ukanusho wa nyakati
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua ukanusho wa -li-; -na- na –ta- katika sentensi ili kuimarisha
mawasiliano;
b) Kusoma ukanusho wa nyakati katika sentensi ili kuimarisha usomaji;
ch) Kuandika ukanusho wa nyakati katika sentensi ili kujenga ubunifu;
d) Kuchangamkia matumizi ya nyakati katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Wanafunzi watumie -li-, -na- na -ta- kuelezea vitendo walivyofanya katika
wakati uliopita (-li-), wakati uliopo (-na-) na wakati ujao (-ta-) wakiwa
katika vikundi au wawili wawili.
Mwanafunzi akamilishe vifungu kwa kutumia -li-, -na- na -ta- na ukanusho
wake.
Mwanafunzi asome vifungu vyenye matumizi -li-, -na- na -ta- na ukanusho
wake.
Mwanafunzi aweza kupewa zoezi la ukanusho wa nyakati akiwa peke yake,
wawili wawili au katika kikundi.
127
Mwanafunzi aweza kutazama jinsi nyakati zinavyokanushwa katika vifaa
vya teknolojia na kufanyia zoezi kwenye mtandao.
III. Nyenzo:
Chati zenye sentensi za kurejelea nyakati mbalimbali;
Chati zenye sentensi za kurejelea ukanusho wa nyakati mbalimbali;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 81-83;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Sarufi ni kipengele muhimu katika ujifundishaji wa wanafunzi. Mwalimu anastahili
kutilia maanani dhana hii ili kuweza kuwahusisha wanafunzi kwa ukamilifu katika
somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi
hivi. Vifaa hivi ni kama vile: chati zenye sentensi za kurejelea nyakati mbalimbali
pamoja na ukanusho wa nyakati hizo. Wanafunzi watumiwe sana katika funzo
kusimulia mambo waliyotenda wakati uliopita, watakayotenda wakati ujao
pamoja na matendo ya wakati wa sasa hivi.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa vyake kwa sababu matumizi ya vifaa halisi ni mbinu bora
ambayo hutumika kufanikisha ufundishaji wa wanafunzi.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, mwalimu anashauriwa kuandaa
maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha
kama wanafunzi wengine. Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia,
mwalimu anaweza kutumia lugha ya ishara.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa
katika Kitabu cha Mwanafunzi.
128
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu aanze funzo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe
wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika kipindi kilichotangulia.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu
kisha awaulize wasimuliane kuhusu matendo waliyotenda katika wakati uliopita.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu, kwa mfano:
1. Mimi nilikula jana.
2. Sisi tulicheza.
3. Mwalimu alitufundisha.
4. Baba alilima jana.
Mwalimu awaongoze wanafunzi kutambua kuwa kiambishi –li- hutumika
kurejelea wakati uliopita katika umoja na wingi. Baada ya shughuli hii, mwalimu
awaombe wanafunzi wakanushe sentensi walizotunga hapo juu katika wakati
uliopita, kwa mfano:
1. Mimi sikula jana.
2. Sisi hatukucheza.
3. Mwalimu hakutufundisha.
4. Baba hakulima jana.
Mwalimu awaongoze wanafunzi kutambua namna ya kukanusha sentensi katika
wakati uliopita kwa kutumia vikanushi si-, ha- na hu-.
Baada ya wanafunzi kuelewa matumizi ya wakati uliopita, awaongoze katika
makundi mapya ya wanafunzi watatu watatu kufahamu matumizi ya wakati uliopo.
Mwalimu awaambie wanafunzi wasimuliane kuhusu matendo waliyotenda sasa
hivi katika wakati uliopo. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kwa kutunga
sentensi za kueleza matendo yao ya sasa hivi, kwa mfano:
1. Mimi ninasoma.
2. Sisi tunaandika.
129
3. Mwalimu anatufundisha.
4. Baba analima shambani.
Mwalimu awaongoze wanafunzi kutambua kuwa kiambishi -na- hutumika
kurejelea wakati uliopo katika umoja na pia katika wingi. Baada ya shughuli hii,
mwalimu awaombe wanafunzi wakanushe sentensi walizotunga hapo juu katika
wakati uliopo, kwa mfano:
1. Mimi sisomi.
2. Sisi hatuchezi.
3. Mwalimu hatufundishi.
4. Baba halimi shambani.
Mwalimu awaongoze wanafunzi kutambua namna ya kukanusha sentensi katika
wakati uliopo kwa kutumia vikanushi si-, ha- na hu- pamoja na kiishio –i kwa
vitenzi vinavyoishia kwa kiishio -a.
Baada ya wanafunzi kuelewa matumizi ya wakati uliopo, mwalimu awaongoze
katika makundi yao kufahamu matumizi ya wakati ujao. Mwalimu awaambie
wanafunzi wasimuliane kuhusu matendo wanayopanga au wanayotarajia
kuyatenda katika wakati ujao. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kwa
kutunga sentensi za kueleza matendo yao ya wakati ujao, kwa mfano:
1. Mimi nitasoma.
2. Sisi tutaandika.
3. Mwalimu atatufundisha.
4. Baba atalima shambani.
Mwalimu awaongoze wanafunzi kutambua kuwa kiambsihi -ta- hutumika
kurejelea wakati ujao katika umoja na pia katika wingi. Baada ya shughuli hii,
mwalimu awaombe wanafunzi wakanushe sentensi walizotunga hapo juu katika
wakati ujao, kwa mfano:
1. Mimi sitasoma.
2. Sisi hatutacheza.
3. Mwalimu hatatufundisha.
4. Baba hatalima shambani.
130
Mwalimu awaongoze wanafunzi kutambua namna ya kukanusha sentensi katika
wakati ujao kwa kutumia vikanushi si-, ha- na hu-.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao kusoma
sentensi walizopewa katika vitabu vyao. Sentensi hizi zimeandikwa katika
wakati uliopita, wakati uliopo na wakati ujao katika umoja na wingi pamoja na
ukanusho wake katika umoja na wingi.
Katika hatua hii, wanafunzi watapata maarifa zaidi ya jinsi ya kukanusha
sentensi katika wakati uliopita, uliopo na ujao katika hali ya umoja na wingi
kwakutumia vikanushi mwafaka.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana kwa kutumia
wakati uliopita, wakati uliopo na wakati ujao katika umoja na wingi kupitia kwa
sentensi au maongezi ya jumla. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wanaweza kukanusha kwa usahihi sentensi zilizo katika wakati uliopita, wakati
uliopo na wakati ujao, hali ya umoja na wingi katika nafsi zote za Kiswahili.
131
VI. Majibu
Zoezi, ukurasa 82
1. Mtoto hakusoma.
2. Wewe hukusimama.
3. Mimi sikucheza.
4. Watoto hawakusoma.
5. Nyinyi hamkusimama.
Zoezi, ukurasa 82
1. Mtoto hasomi.
2. Watoto hawasomi.
3. Wewe husimami.
4. Nyinyi hamsimami.
5. Mimi sichezi.
Zoezi, ukurasa 83
1. Mtoto hatasoma.
2. Watoto hawatasoma.
3. Wewe hutasimama.
4. Nyinyi hamtasimama.
5. Mimi sitacheza.
132
Matokeo maalum
yanayotarajiwa
Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kukia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutambua msamiati ambao
hutumiwa katika usalama ili
kuimarisha mawasiliano;
(b) Kutambua maneno
yanayotumiwa katika maagano
ili kuwezesha mazungumzo;
(ch) Kutambua mambo yanayoathiri
usalama ili kujihakikishia
usalama;
(d) Kutambua picha zinazoonyesha
usalama katika mazingira
mbalimbali ili kurahisisha
ufahamu;
(e) Kutambua kisa chenye mantiki;
(f) Kutaja vinyume vya vitendo.
Mwanafunzi asome maneno
yanayohusiana na usalama kwa
kutumia kadi za maneno.
Mwanafunzi ashiriki katika
mjadala kuhusu matumizi ya
maagano kama vile: kwaheri,
siku njema, mchana mwema,
safari salama na usiku mwema.
Mwanafunzi asimulie baadhi ya
mambo yanayoweza kuhatarisha
usalama katika mazingira yake.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi aweza kupewa
hadithi yenye mapengo ajaze
kwa maneno mwafaka.
Mwanafunzi aweza kufafanuliwa
juu ya vinyume vya vitendo
kama vile: lala amka; keti
simama; cheka lia; enda rudi.
Mada Kuu 5: USALAMA
Idadi ya vipindi: 15
Sura ya
5
133
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kazi ya vikundi.
Kushiriki katika kuimba nyimbo na kukariri mashairi katika tamasha
mbalimbali kuhusu usalama.
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Mazingira.
Nyenzo:
Michoro au picha za vitendo vya usalama;
Kadi zenye maneno ya kuashiria usalama;
Rekodi za hadithi au masimulizi bunifu kuhusu usalama;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 84-93;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Mada hii itashughulikia kutambua msamiati kuhusiana na usalama, njia za
kujiepusha na hatari pamoja na madhara ya hatari mbalimbali. Kutokana na
mada hii, wanafunzi watafahamu umuhimu wa kuzingatia usalama katika
shughuli zao mbalimbali.
Pia, kipengele cha masimulizi na hadithi bunifu kuhusu usalama zitafundishwa
hapa. Masimulizi na hadithi za kuvutia na zenye msamiati wa kiwango cha
wanafunzi wa gredi hii zibuniwe ili kuwafaa wanafunzi katika ujifundishaji wao.
Kama tujuavyo, usalama ni muhimu kwa kila binadamu kwa sababu hatari
mbalimbali zina madhara mabaya kwa maisha ya binadamu. Heri kuwa salama
kuliko kujuta baadaye.
Pia, mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kufahamu vinyume vya vitendo
mbalimbali.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
Elimu ya kudumisha maendeleo: elimu ya usalama kupitia kwa kutambua
umuhimu wa mbinu za kidijitali na hali zinazohatarisha usalama.
Uzalendo: kushirikiana katika vikundi.
134
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii kuhusu usalama ni kama vile:
Msamiati Maana
1.
moto
joto kali lenye madhara liwakapo kwa wingi
2.
ajali
tendo ambalo hutokea bila kutarajiwa
3.
utekaji nyara
hali ya kumshika mtu na kumfungia kwa ajili ya
kupata faida
4.
hatari
hali yoyote ya kusababisha madhara
5.
kuvamiwa
kuingiliwa kwa nguvu bila matarajio
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Katika ufundishaji wa mada hii, mwalimu ahakikishe kuwa ana vifaa muhimu na
maalum vya kuwasaidia wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali
ili kuweza kuwashirikisha katika ujifundishaji wao. Kwa wanafunzi wasio na
uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya lugha ya ishara.
Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri wa lugha ya ishara.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kuona, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya breli pamoja na vifaa vya kunasia sauti.
Haya yatawawezesha wanafunzi hawa kusoma kama wanafunzi wenzao bila
vikwazo vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada
Idadi ya vipindi
Mada Ndogo 1: Msamiati
3
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Maagano
2
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 5: Kuandika
3
Mada Ndogo 6: Sarufi: Vinyume vya vitendo
2
JUMLA: 15
135
Mada Ndogo 1: Msamiati kuhusu usalama
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati ambao hutumiwa katika usalama ili kuimarisha
mawasiliano;
b) Kusoma msamiati unaohusiana na usalama ili kujenga usomaji bora;
ch) Kueleza maana ya msamiati wa usalama ili kuimarisha ufahamu;
d) Kutumia msamiati wa usalama katika sentensi ili kuimarisha ufahamu;
e) Kuandika maneno yanayohusiana na usalama ili kujenga uandishi bora;
f) Kuthamini usalama katika mazingira yake.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome maneno yanayohusiana na usalama kwa kutumia kadi
za maneno.
Mwanafunzi aelezee maana ya msamiati wa usalama. Akiwa peke yake au
katika vikundi.
Mwanafunzi atunge sentensi sahihi kwa kutumia msamiati wa usalama.
Mwanafunzi aweza kutazama video kuhusu usalama k.m. utekaji nyara.
Mwanafunzi atazame michoro na picha inayolenga maana za maneno
kuhusu usalama.
Wanafunzi wajadiliane kuhusu umuhimu wa usalama.
III. Nyenzo:
Kadi zenye maneno yanayohusu usalama;
Michoro au picha zenye kuonyesha vitendo vya usalama,
Video kuhusu usalama;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 84-86;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
136
IV. Maandalizi ya somo
Kila binadamu ana jukumu la kudumisha usalama wake binafsi kabla ya
kudumisha usalama wa wenzake. Kila mtu anashauriwa kuwa wakati wa
hatari ajikinge yeye kwanza kabla ya kufikiria kuwakinga wengine. Ni rahisi
kuwakinga wenzako ukiwa salama wewe binafsi. Usalama unapodumishwa kila
mahali hufanikisha shughuli za binadamu za kila siku. Kwa hivyo, funzo hili ni
muhimu sana kwa wanafunzi hata katika kiwango hiki kwa sababu litawasaidia
kujitahadharisha dhidi ya hatari zozote na kufahamu njia mbalimbali za
kudumisha usalama wao wenyewe wapatwapo na hatari. Mwalimu anastahili
kutilia maanani dhana hii wakati wa uandalizi wa funzo hili.
Mwalimu aandae mapema vifaa atakavyohitaji na kuvihifadhi kabla ya vipindi
hivi. Vifaa hivi ni kama vile: kadi zenye maneno yanayohusu usalama, michoro
au picha kuhusu usalama pamoja na vyombo vingine maalum vya kuwasaidia
wanafunzi wenye ulemavu na matatizo mbalimbali au kiwango cha chini katika
ujifundishaji wao.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa
kuweka hadharani vifaa alivyovileta darasani kwa kukumbuka kuwa matumizi
ya michoro, picha na hata kadi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha
ufundishaji wa wanafunzi.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, mwalimu ahusishe matumizi
ya lugha ya ishara au watafsiri wa lugha ya ishara. Ikiwa kuna wanafunzi
wasioweza kuona, mwalimu anashauriwa ajitahidi kuandaa maelezo yake
kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha bila matatizo
kama wanafunzi wengine.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwenye vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu awaamkue wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu maamkuzi ya
mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
137
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne wanne kisha
awaelekeze kutazama na kuchunguza mchoro waliopewa katika vitabu vyao
kuhusu mkasa wa moto. Mwalimu awaombe wanafunzi wajadiliane kuhusu
wanachoona katika mchoro huo (nyumba inayochomeka) kisha wajibu maswali
waliyopewa baada ya mchoro huo. Katika kuchunguza mchoro waliopewa,
wanafunzi waelekezwe kujibu maswali haya:
1. Unaona nini katika mchoro huu?
2. Moto unafanya nini?
3. Moto hutumika kufanya nini?
4. Moto huzimwa vipi?
5. Moto huweza kuhatarisha vipi maisha yako.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii. Hii
itakuwa namna nzuri ya kutanguliza funzo hili kuhusu usalama.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu aendeleze funzo hili kuhusu usalama kwa kuwaomba wanafunzi
wote kutazama video aliyoandaa na kuirekodi kwenye tarakilishi. Wanafunzi
waketi kwa namna ambayo itawawezesha kuiona video hiyo vizuri. Wanafunzi
wanaweza hata kuikaribia tarakilishi yenyewe ili kuona video vyema. Iwapo
mwalimu ataweza kupata projekta, basi itafaa zaidi katika kuifanya video hiyo
kuonekana vizuri zaidi na wanafunzi wote. Mwalimu ahakikishe ameiandaa
video husika mapema kabla ya kipindi hiki. Video hii inaweza kuhusu hatari
mbalimbali na usalama, kwa mfano: mtu akitekwa nyara, nyumba ikichomeka,
watu wakivuka barabara kwenye eneo lisilofaa na labda kupatwa na ajali, watu
waking’atwa na nyuki, mtu akiumwa na mbwa, mtu akianguka ndani ya shimo,
miongoni mwa visa vingine vingi kuhusu hatari mbalimbali na usalama.
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wote wanashiriki katika shughuli hii ya kutazama
video husika. Baada ya wanafunzi kutazama video hiyo na kuielewa, mwalimu
awaulize maswali mbalimbali kuhusiana na video hiyo kama vile:
a) Umeona nini kwenye video hii?
b) Watu/mtu anafanya nini katika video hii?
ch) Ni hatari gani uliyoiona katika video hii?
d) Je, unaweza kuepuka hatari uliyoona katika video kwa njia gani?
138
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kujadiliana kuhusu
hatari waliyoona katika video husika pamoja na hatari nyingine zinazoweza
kuwakumba binadamu. Wanafunzi waelekezwe kujadili njia mbalimbali za
kuepuka hatari tofauti tofauti.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu hatari mbalimbali, namna ya kuziepuka na
namna ya kuwasaidia watu wengine wanapopatwa na hatari tofauti tofauti.
Majibu
Maswali, ukurasa 84
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoyaona katika
mchoro waliopewa, kwa mfano:
1. Wanafunzi waeleze wanachoona katika michoro waliyopewa.
2. Wanafunzi waeleze athari za moto. Kama vile: kuharibu mali,
kusababisha maafa, kujeruhi watu n.k.
3. Wanafunzi waeleze kazi mbalimbali za moto kama vile: kupika chakula,
kutengeneza vifaa mbalimbali n.k.
4. Wanafunzi waeleze njia mbalimbali za kuzima moto kama vile kwa
kutumia maji, blanketi, mchanga, aina fulani za gesi n.k.
5. Wanafunzi waeleze namna moto unavyoweza kuhatarisha maisha yao,
kwa mfano kuwajeruhi, kuwasababishia maafa, kuwaharibia mali n.k.
139
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Maagano
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua maneno yanayotumiwa katika maagano ili kuwezesha
mazungumzo;
b) Kutumia maneno yanayotumiwa katika maagano kwenye mawasiliano;
ch) Kujibu maagano kwa njia ifaayo ili kudhihirisha ufahamu;
d) Kuthamini matumizi ya maagano katika mawasiliano ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu matumizi ya maagano kama
vile: kwaheri, siku njema, mchana mwema, safiri salama na usiku mwema.
Mwanafunzi atazame michoro inayoashiria vitendo vya kuagana.
Mwanafunzi ashiriki katika maigizo ya kuagana.
Mwanafunzi aweza kutazama vibonzo katika tarakilishi vikiigiza vitendo
na maneno mbalimbali ya kuagana.
Mwanafunzi aweza kutaja neno la kuagana linalofaa kutokana na maelezo
mbalimbali akiwa peke yake, wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za kuonyesha maagano;
Video ya kuonyesha maagano mbalimbali;
Kadi zenye maneno mbalimbali ya maagano;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 86-88;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Mada hii itashughulikia aina mbalimbali za maagano kati ya watu. Aghalabu
binadamu hufanya shughuli zao pamoja na hufikia wakati wa wao kuachana na
hivyo kuagana. Ni muhimu kwa binadamu kuagana kwa sababu huwa ni ishara
140
ya udugu, kuwatakia wengine mema na kuwaombea mema. Mara nyingine
watu huagana na kukosa kuonana tena kutokana na misiba mbalimbali ambayo
huweza kutokea bila kupangwa. Ni tabia njema kuwaaga wenzako na kuwatakia
mema kila mara mnapoachana kwani hakuna ajuaye linaloweza kutokea hapo
baadaye. Mwalimu atilie maanani dhana hii anapojiandaa kufundisha funzo hili
kuhusu maagano.
Mwalimu aandae funzo hili kwa namna ya kumwezesha kuwaelekeza wanafunzi
kufahamu namna mbalimbali za kuagana.
Vifaa vitakavyohitajika kama vile: michoro au picha za watu wakiagana, kadi
zenye maneno ya kuagana pamoja na vifaa vingine muhimu kwa ujifundishaji
wa wanafunzi walemavu viandaliwe ili ufundishaji wa funzo hili ufanikiwe.
Ili kufanikisha malengo ya ufundishaji wa funzo hili, mwalimu ahakikishe kuwa
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila zoezi linalohusika katika vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize funzo lake kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu kipindi cha hapo awali kuhusu usalama. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu na maswali waliyoulizwa. Mwalimu awaongoze
wanafunzi kwa kusahihisha zoezi lililotolewa katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi wasahihishe zoezi hilo na mwalimu awape majibu kwa kutilia mkazo
pale ambapo wanafunzi wanatatizika.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu na
awaombe watazame mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 86.
Wanafunzi wachunguze mchoro huo. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa
kuwauliza maswali mepesi kuhusu mchoro huo. Anaweza kuwauliza maswali
kama vile: Unaona nini kwenye mchoro huu? Watu hawa wanafanya nini?
Wanafunzi, kwa upande wao, wajibu maswali ya mwalimu wao kwa kueleza
kile wanachoona katika mchoro huo ambapo kuna watu wawili wanaoagana.
Watu hawa ni mgonjwa na muuguzi katika zahanati. Huenda muuguzi huyo
anamuaga mgonjwa huyo na kumtakia afueni ya haraka.
141
Baada ya shughuli hii, mwalimu awaonyeshe wanafunzi wote video aliyoandaa
kuhusu mtoto au mwanafunzi anayewaaga wazazi wake (mama na baba)
asubuhi akienda shuleni. Wazazi hawa pia waonekane katika video hiyo wakijibu
maagano ya mtoto wao. Mwalimu ahakikishe ameandaa video hii mapema
kabla ya kipindi hiki. Mbali na video hii, mwalimu anaweza kuandaa video
nyingine za ziada kuhusu njia mbalimbali za maagano ya nyakati mbalimbali.
Kwa mfano, maagano ya usiku, asubuhi, mchana, ya kusafiri n.k. Wanafunzi
wote washirikishwe katika shughuli hii ya ziada kisha baadaye waulizwe maswali
mbalimbali kuhusiana na video waliyotazama. Mwalimu awasaidie wanafunzi
wanaotatizika katika shughuli hii.
Baada ya mwalimu kuridhika kuwa wanafunzi wameweza kuielewa video
waliyotazama, awagawe katika makundi ya wawili wawili kisha waigize baadhi
ya maagano waliyoona kwenye video husika pamoja na yale waliyopewa katika
vitabu vyao. Mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wanashirikishwa viliyo
katika makundi yao. Uigizaji huu utaboresha stadi ya wanafunzi ya kusikiliza na
kuzungumza pamoja na kuwa na ujasiri wa kuzungumza mbele ya watu.
Hatimaye, wanafunzi washirikishwe katika kufanya zoezi walilopewa katika
vitabu vyao kuhusu kukamilisha sentensi kwa kutumia maneno mbalimbali ya
maagano waliyopewa.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu njia mbalimbali za maagano pamoja na
maneno mbalimbali ya maagano.
VI. Majibu
Majibu ya utangulizi, ukurasa 86
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona kwenye
mchoro waliopewa, kwa mfano: Ninaona watu wawili (mgonjwa na muuguzi)
wakiagana kwenye zahanati. Huenda muuguzi anamtakia mgonjwa afueni
ya haraka na mgonjwa naye anamshukuru muuguzi na kumuaga kuwa
wataonana siku nyingine.
142
Zoezi la kutazama video, ukurasa 87
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu walichoona kwenye video
husika.
Zoezi, ukurasa 87-88
1. Mtu anapoenda safari, unamwambia safiri salama.
2. Ulipotoka asubuhi kwenda shuleni ulimwambia mzazi mchana mwema.
3. Mtu anapoenda kukaa kazini siku nzima utamwambia siku njema.
4. Kwaheri.
5. Mimi huwaambia usiku mwema.
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua mambo yanayoathiri usalama ili kujihakikishia usalama;
b) Kutambua njia za kudumisha usalama katika mazingira yake ili
kujihakikishia usalama;
ch) Kusimulia kuhusu mambo yanayoweza kuhatarisha usalama katika
mazingira yake ili kuimarisha stadi ya kuzungumza;
d) Kusikiliza masimulizi kuhusu usalama ili kujenga stadi ya kusikiliza;
e) Kuthamini umuhimu wa usalama katika maisha ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asimulie baadhi ya mambo yanayoweza kuhatarisha usalama
katika mazingira yake.
Mwanafunzi aweza kutazama video inayoonyesha mambo yanayoathiri
usalama katika mazingira yake.
Wanafunzi wajadiliane namna ya kuepuka dhuluma k.m. kutozungumza na
watu wasiowajua, kupiga ukelele wanapokumbwa na hatari n.k.
143
Mwanafunzi aandike baadhi ya mambo yanayoathiri usalama katika
mazingira yake.
Mwanafunzi asimulie kisa alichokishuhudia kuhusu usalama.
III. Nyenzo:
Rekodi za masimulizi ya kubuni mbalimbali kuhusu usalama;
Michoro au picha za vitendo vya usalama;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 88-89;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusoma masimulizi
bunifu yanayohusu usalama, namna ya kuepuka dhuluma na njia mbalimbali
za kuepuka hatari mbalimbali ili kujenga stadi yao ya kusikiliza na kusoma.
Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo
hili ili kufanikisha ufundishaji wake. Mwalimu anaweza kumwalika mtambaji,
msimulizi au msomaji mashuhuri akawasomea wanafunzi masimulizi bunifu
au akawasimulia wanafunzi masimulizi bunifu kuhusu usalama. Wanafunzi
waelekezwe katika kusoma baada yake kama darasa zima, wawili wawili na
hatimaye mmoja mmoja. Mwalimu ahakikishe kuwa msimulizi au msomaji
huyu mwalikwa ana uwezo wa kusoma kwa sauti ya kusikika na kuvutia na kwa
matamshi sahihi.
Mwalimu anaweza kurekodi masimulizi bunifu kuhusu usalama kwenye
tarakilishi au simu kisha wanafunzi wakasikiliza darasani. Hii pia ni mbinu nzuri
ya ufundishaji kwa wanafunzi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
144
namna mbalimbali za maagano ya nyakati mbalimbali. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi kuhusu maagano
walilopewa katika kipindi cha hapo awali. Mwalimu ahakikishe anawasaidia
wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza pamoja na ya kusoma masimulizi bunifu. Mwalimu awagawe
wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha awaombe watazame
mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 88. Wanafunzi wachunguze
mchoro huo na kuujadili katika makundi yao wakielezana wanachokiona.
Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na mchoro
huo kama vile: Unaona nini kwenye mchoro huu? Watu hawa wanafanya nini?
Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu maswali waliyoulizwa.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na wanayoona katika mchoro
waliopewa. Wanafunzi wajaribu kutabiri matukio ya mchoro waliopewa, kwa
mfano, hawa ni wanafunzi waliovalia sare ya shule ambao wamekutana na mtu
wasiyemjua. Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kujadili mchoro huo
na kusimuliana kuhusu visa kadhaa vya watoto hasa wanafunzi kukutana na
mtu au watu wasiowajua njiani na madhara yake. Wapo watu ambao hutumia
vitu vya kuwavutia watoto kama vile: peremende, biskuti, keki n.k. ili kuweza
kuzungumza na hata kwenda na watoto hao. Mwalimu awaeleze wanafunzi
madhara ya kuzungumza na watu wasiowajua kama vile: wanaweza kuwaua,
kuwajeruhi, kuwauza, kuwanajisi, kuwafanyiza kazi ngumu kwa kuwafanya
watumwa n.k.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi masimulizi yafuatayo
kuhusu mchoro waliopewa. Ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa
makini. Pia, mwalimu ahakikishe kuwa anasoma kwa ufasaha, kwa matamshi
sahihi na sauti ya kusikika na ya kuvutia.
Mfano wa masimulizi
Jana ilikuwa siku ya Ijumaa. Mimi na rafiki zangu tulikuwa tunatoka shuleni
baada ya masomo ya siku hiyo kukamilika. Ilikuwa jioni. Tulitembea kwenye
njia inayopita karibu na msitu wa Nyakange. Tulizoea kupita kwenye njia hii.
Kila mara mama alinionya nisipite kwenye njia hiyo nikiwa peke yangu. Hivyo
nilizoea kuwangoja rafiki zangu kila wakati na kwenda nao shuleni na kurudi nao
145
nyumbani. Njia hii ilikuwa hatari. Ilikuwa na watu waliozoea kuwabembeleza
watoto kwa kutumia peremende, keki na biskuti ili kuwateka nyara.
Siku hii kama kawaida tulikuwa tunatoka shuleni. Mara alitokea mwanamume
mmoja mbele yetu. Alijaa tabasamu usoni. Sisi hatujawahi kumuona
mwanamume huyu. Alimsalimia Juma tuliyekuwa naye. Kisha akamtolea biskuti
na kutaka kumpa. Mimi nilipoona hivyo, nilimkataza Juma kupokea biskuti hizo.
Mwanamume huyo alimkonyezea Juma jicho na kumwomba akubali biskuti zake.
Mwanamume huyo alipozidi kutukaribia, tuliogopa. Nilitoa ishara ya kukimbia
kwa Juma na Petero tuliokuwa nao. Ghafla, tulitoka mbio. Mwanamume huyo
alijaribu kutukimbiza lakini alisita alipoona watu wanamwangalia. Tulikimbia
hadi nyumbani kwetu. Tuliepuka hatari ya kutekwa nyara na mwanamume huyo
ambaye hatukumjua.
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi walisikiliza masimulizi ya mwalimu kwa
makini, mwalimu awashirikishe katika kujibu maswali yafuatayo yanayohusu
masimulizi waliyosoma.
Maswali ya masimulizi
1. Masimulizi yanatokea siku gani?
2. Kwa nini wanafunzi hawa walizoea kwenda shuleni pamoja?
3. Kwa nini watu walizoea kwuwapa wanafunzi peremende, biskuti au keki?
4. Kwa nini njia hii ilikuwa hatari?
5. Kwa nini Juma alikataa kuchukua biskuti alizokuwa akipewa?
Mwalimu azunguke darasani ili kuwasaidia wanafunzi wanaotatizika katika
makundi yao kujibu maswali waliyopewa. Wanafunzi werejelee mchoro
waliopewa katika vitabu vyao pamoja na masimulizi waliyosomewa. Mwalimu
anaweza kuyaandika masimulizi haya ubaoni, kwenye chati au kuyarekodi
kwenye tarakilishi au simu ili wanafunzi wayasikilize kwa pamoja darasani.
Wanafunzi wanaweza kupewa fursa ya kuyasoma masimulizi hayo wakiwa
wawili wawili kisha mmoja mmoja. Mwalimu asahihishe makosa ya kimatamshi
pindi tu yanapotokea.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika makundi yao waelezane njia
salama ya kuvuka barabara kwa kujibu maswali waliyopewa katika vitabu vyao.
Kwa mfano, wanafunzi waelezane: mimi huvuka barabara palipo na kivukomilia;
mimi huangalia pande zote (kulia na kushoto) kabla ya kuvuka barabara; mimi
146
ninapoona gari likija barabarani, kwanza hungoja gari hilo lipite kabla ya kuvuka.
Mimi husaidiwa kuvuka barabara na rafiki zangu au watu wazima walio barabarani
n.k. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi katika makundi yao kuhusiana na
usalama wa kuvuka barabara.
Kila kundi lipewe muda wa kuwasilisha masimulizi yao mbele ya wanafunzi
wenzao. Shughuli hii itakuza ujasiri wa wanafunzi kusimama na kuzungumza
mbele ya watu. Pia, itakuza stadi ya wanafunzi ya kusikiliza na kuzungumza.
Hatimaye, mwalimu anaweza kuwaomba wanafunzi wasimuliane kuhusu kisa
chochote ambacho wamewahi kushuhudia kuhusu usalama wa barabara au
utekaji nyara.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma masimulizi bunifu.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kusoma
kwa ufasaha na kwa matamshi sahihi na iwapo wameweza kujibu maswali ya
masimulizi hayo kwa usahihi kulingana na muktadha wa masimulizi husika
ambao ni usalama.
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanachoona katika
mchoro waliopewa. Wanafunzi watabiri matukio katika mchoro huo. Kwa
mfano: mwanamume katika mchoro huu ana mpango wa kuwahadaa wanafunzi
hao na kuwateka nyara.
147
VI. Majibu
Maswali ya utangulizi, ukurasa 89
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanachoona katika
mchoro waliopewa. Wanafunzi watabiri matukio katika mchoro huo. Kwa
mfano: mwanamume katika mchoro huu ana mpango wa kuwahadaa wanafunzi
hao na kuwateka nyara.
Maswali ya masimulizi, ukurasa 89
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na masimulizi
waliyosomewa, kwa mfano:
1. Masimulizi yanatokea siku ya Ijumaa.
2. Kwa sababu njia hii ilikuwa hatari.
3. Ili kuwabembeleza kuzungumza nao na hata kwenda nao.
4. Ilikuwa na visa vingi vya utekaji nyara. Ilikuwa na watu wengi
waliokuwa wageni hapa.
5. Aliashiriwa na rafiki yake asichukue biskuti hizo. Hakumjua mtu huyo
aliyekuwa anampa biskuti hizo. Aliogopa.
Maswali ya hadithi, ukurasa 89
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu usalama wa barabarani,
kwa mfano:
1. Mimi huvuka barabara palipo na kivukomilia.
2. Mimi huangalia pande zote (kulia na kushoto) kabla ya kuvuka
barabara.
3. Mimi ninapoona gari linakuja barabarani hungoja kwanza gari hilo
lipite kabla ya kuvuka.
4. Mimi husaidiwa kuvuka barabara na rafiki zangu au watu wazima
walio barabarani.
.
148
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua picha zinazoonyesha usalama katika mazingira mbalimbali ili
kurahisisha ufahamu;
b) Kutambua maneno yanayohusiana na usalama ili kuyatumia katika
mawasiliano;
ch) Kusikiliza hadithi za mwalimu kuhusu usalama ili kuimarisha ufahamu;
d) Kusoma hadithi kuhusu usalama ili kujenga usikivu;
e) Kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu usalama ili kupata
ujumbe;
f) Kuthamini umuhimu wa usalama katika maisha ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
Mwanafunzi asome darasani, wakiwa wawili wawili na baadaye asome
peke yake.
Wanafunzi wasomeane hadithi wakiwa wawili au katika vikundi.
Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi husika ikisomwa kupitia kinasasauti.
Mwanafunzi aweza kutazama video ya mtu mzima au mtoto akisoma
hadithi husika kwa ufasaha kisha aige usomi huo.
Mwanafunzi athibitishe utabiri wao baada ya kusoma hadithi.
Mwanafunzi aweza kusimulia hadithi kutokana na picha alizopewa kuhusu
usalama.
Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kutokana na hadithi husika.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za vitendo vya usalama;
Rekodi za hadithi bunifu mbalimbali kuhusu usalama;
149
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu, projekta;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 89-91;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
III. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu kuhusu usalama ili kujenga stadi ya
wanafunzi ya kusoma pamoja na ya kusikiliza. Mwalimu ahakikishe kwamba
ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji
wake kama vilivyotajwa hapo juu. Mwalimu anaweza kumwalika mtambaji,
msimulizi au msomaji mashuhuri akawasomea wanafunzi hadithi za kubuni
kuhusu usalama kisha wanafunzi wakasoma baada yake katika darasa zima,
kisha wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi mmoja mmoja. Mwalimu
ahakikishe anakosoa makosa ya kimatamshi ya wanafunzi pindi tu yanapotokea.
Msimulizi mwalikwa sharti awe na uwezo wa kusoma kwa sauti ya kusikika, ya
kuvutia na kwa matamshi sahihi na kwa ufasaha.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
IV. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia
ambapo walisimuliwa kuhusu usalama. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu
pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
funzo la hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao ya
kusikiliza pamoja na ya kusoma hadithi bunifu. Hadithi hii bunifu ihusu usalama.
Mwalimu awaombe wanafunzi kama darasa zima watazame michoro iliyo katika
150
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 89-90. Wanafunzi wachunguze michoro hiyo
na kuijadili. Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali mepesi kuhusiana
na michoro hiyo kama vile: Unaona nini kwenye michoro hii? Wasichana hawa
wanafanya nini? Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu
maswali waliyoulizwa. Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote
katika majadiliano haya. Wanafunzi watabiri matukio katika michoro husika
kuhusu wasichana wawili wanaopatwa na hatari ya kung’atwa na nyuki wakienda
mtoni. Wanafunzi wajadili kisa hiki kisha wapewe fursa ya kuwasimulia wenzao
kuhusu aina yoyote ya hatari ambayo wamewahi kukumbana nayo. Wanafunzi
waeleze namna walivyojitoa kwenye hatari hiyo.
Baada ya majadiliano haya, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kujibu
maswali waliyopewa katika vitabu vyao kuhusiana na michoro waliyotazama.
Kila mwanafunzi ashirikishwe katika shughuli hii.
Baadaye, mwalimu awaongoze wanafunzi katika makundi yao kusoma
hadithi waliyopewa katika vitabu vyao kuhusu mkasa wa kung’atwa na nyuki
uliowapata Anita na Aneta. Wanafunzi wasome hadithi hii kama darasa zima,
kisha wasome wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi asome peke yake.
Mwalimu ahakikishe anakosoa makosa ya kimatamshi pindi tu yanapotokea.
Usomaji wa aina hii utakuza stadi ya mwanafunzi ya kusoma kwa ufasaha
pamoja na kukuza ujasiri wake wa kusimama na kuzungumza mbele ya watu.
Kupitia kwa usomaji wa aina hii, ni rahisi kwa mwalimu kufahamu matatizo ya
kila mwanafunzi kibinafsi. Kila mwanafunzi ashughulikiwe kibinafsi.
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi wamesoma hadithi hiyo kwa makini, mwalimu
awaelekeze wanafunzi wajibu maswali ya hadithi waliyopewa katika vitabu
vyao.
Maswali hayo yanahusu hadithi waliyoisoma darasani. Wanafunzi wanaotatizika
wasaidiwe.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusoma kwa ufasaha hadithi bunifu. Pia,
achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kusoma hadithi na kuweza
kujibu maswali ya hadithi hiyo kwa usahihi kulingana na muktadha wa hadithi
yenyewe.
151
VI. Majibu
Maswali ya michoro, ukurasa 90
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoyaona
kwenye michoro waliyopewa, kwa mfano: ninawaona wasichana wawili
wakienda mtoni na vibuyu vyao. Njiani, wanapatwa na mkasa wa
kung’atwa na nyuki wanapojaribu kuchuma maembe.
2. Wasichana hawa wanaenda mtoni kuchota maji. Wamebeba vibuyu.
3. Hatari ya wasichana hao kung’atwa na nyuki ambao ni wadudu hatari
sana.
4. Wasichana hao wanang’atwa na nyuki.
5. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu iwapo wamewahi
kung’atwa na mdudu yeyote hatari.
Maswali ya hadithi, ukurasa 91
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na hadithi waliyosoma.
1. Wasichana wawili: Anita na Aneta.
2. Mama yao.
3. Anita na Aneta waling’atwa na nyuki.
4. Nyuki walikuwa kwenye mwembe.
5. Anita na Aneta walipelekwa hospitalini.
6. Mama aliwahurumia na kuwapeleka hospitalini.
7. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu iwapo wamewahi
kuumwa na mdudu yeyote hatari.
8. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu wanayofanya
wanapopatwa na hatari yoyote.
152
Mada Ndogo 5: Kuandika
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua kisa chenye mantiki;
b) Kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada;
ch) Kufurahia uandishi wa visa tofauti.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aweza kupewa hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno
mwafaka.
Mwanafunzi aongozwe kujadili yaliyo muhimu katika uandishi k.v.
mwandiko nadhifu, maudhui, mtiririko n.k.
Mwanafunzi aweza kusoma kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwalimu
au wanafunzi wengine.
Wanafunzi waweza kuandika visa vifupi vifupi wakiwa wawili wawili.
Mwanafunzi apewe fursa ya kuandika kisa kifupi kinachohusiana na mada.
Kisa hiki kifuate hatua tano za uandishi: maandalizi, nakala ya kwanza,
marejeleo, uhariri na uchapishaji. Vichwa vya visa vinaweza kutofautiana.
III. Nyenzo:
Hadithi bunifu zilizoandikwa kwenye chati;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu usalama;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 91-92;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Katika mada hii, mwalimu afahamu kuwa somo hili linahusu kukuza stadi ya
mwanafunzi ya kuandika kwa mwandiko nadhifu na kwa kufuata vipengele
vya uandishi bora. Katika mada hii, wanafunzi watapata maarifa ya kuandika
153
visa vifupi vifupi kwa kuzingatia mambo kadhaa kama vile: mwandiko nadhifu,
mtiririko, uhariri, marejeleo na maandalizi kabambe. Shughuli hii itawawezesha
wanafunzi kufahamu jinsi ya kuandika visa bunifu kuhusu usalama kisha ujuzi huu
utawawezesha kubuni na kuandika visa vifupi mbalimbali vya mada mbalimbali.
Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo
hili kama vilivyoorodheshwa hapo awali ili kufanikisha ufundishaji wake pamoja
na ujifundishaji wa wanafunzi hasa walio na matatizo au ulemavu mbalimbali.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika lililotolewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
kusoma hadithi bunifu kuhusu usalama. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu
pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi kusahihisha zoezi walilopewa katika funzo
la hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
i) Sauti /py/
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kuandika na hata kubuni visa vifupi vifupi na kuviandika kwenye madaftari
yao. Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili
wawili kisha awaombe watazame baadhi ya herufi walizopewa katika vitabu
vyao kisha wazinakili katika madaftari yao. Baada ya shughuli hii, mwalimu
awaombe wanafunzi waandike alfabeti zote za Kiswahili katika madaftari yao
kwa herufi ndogo na herufi kubwa. Alfabeti hapa inajumuisha irabu tano za
Kiswahili pamoja na konsonanti ishirini na sita za Kiswahili ili kupata jumla ya
herufi thelathini na moja (31) katika Kiswahili. Shughuli hii ya kuandika alfabeti
154
za Kiswahili itawasaidia wanafunzi katika kuhakikisha kuwa wanaandika kwa
mwandiko nadhifu kwa kuziandika herufi mbalimbali kwa usahihi.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi ya
wanafunzi watatu watatu kusoma hadithi yenye mapengo waliyopewa katika
vitabu vyao kisha wajaze mapengo yaliyopo kwa kutumia majibu sahihi
kutoka kwa waliyopewa kwenye mabano. Mwalimu ahakikishe wanafunzi wote
wanashirikishwa katika zoezi hili. Baada ya kukamilisha zoezi hili, wanafunzi
wapewe fursa ya kusoma hadithi hiyo nzima na kusahihisha walipokosea.
Hatimaye, wanafunzi wainakili hadithi hii moja kwa moja katika madaftari yao
kwa mwandiko nadhifu. Mwalimu ahakikishe kuwa kila mwanafunzi anaandika
hadithi hiyo kwa mwandiko nadhifu.
Mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wote wanashiriki katika shughuli hii ya
kunakili hadithi waliyopewa. Mwalimu anaweza kuiandika hadithi hii ubaoni.
Baada ya shughuli hii, mwalimu ahakikishe amesahihisha madaftari ya
wanafunzi ili kusahihisha makosa yoyote ya kimaendelezo na mwandiko usio
nadhifu. Wanafunzi walio na matatizo ya kuandika kwa mwandiko nadhifu
wapewe mazoezi zaidi ya kuandika. Mwalimu awaelekeze zaidi.
Mwisho, mwalimu anaweza kuwapa wanafunzi zoezi la kubuni kisa kifupi
kuhusu usalama kisha wakiandike katika madaftari yao kwa mwandiko nadhifu,
kwa kuzingatia mtiririko mwafaka pamoja na kukihariri ili kupunguza makosa ya
kisarufi na kimaendelezo. Wanafunzi pia wabuni mada ya kisa chao. Mwalimu
anaweza kuwaongoza wanafunzi katika kuandaa nakala ya kwanza ya maelezo
yao kisha waihariri nakala hii na hatimaye kuandika nakala zao safi katika
madaftari yao. Kila mwanafunzi apewe fursa ya kuwasomea wanafunzi wenzake
aliyoandika kuhusiana na usalama. Mwalimu ahakikishe anasahihisha visa vya
kubuni vya wanafunzi ili kuwaelekeza ifuatavyo. Wanafunzi walio na matatizo
wasaidiwe.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kubuni na kuandika visa vifupi vifupi
vya kubuni.
155
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kuandika
kwa mwandiko nadhifu na maendelezo pamoja na sarufi sahihi.
VI. Majibu
Zoezi la makundi, ukurasa 92
Binadamu anaweza kuishi vizuri akiwa na usalama wa kutosha. Usicheze na
vitu hatari kama vile moto. Usimwamini kila mtu ambaye humjui. Ukiona hali
ya hatari, usinyamaze, piga kelele. Watu watakuja kukusaidia.
Mada Ndogo 6: Saru: Vinyume vya vitendo
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutaja vinyume vya vitendo;
b) Kusoma sentensi zilizo na vinyume vya vitendo;
ch) Kuandika vinyume vya vitendo;
d) Kuchangamkia kutumia vitendo na vinyume vyake katika mawasiliano ya
kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aweza kufafanuliwa juu ya vinyume vya vitendo kama vile:
lala amka; keti simama; cheka –lia; enda rudi.
Wanafunzi waweza kuigiza vinyume vya vitendo wakiwa wawili wawili.
Mwanafunzi aweza kushirikishwa kutunga na kusoma sentensi zilizo na
vinyume vya vitendo.
Mwanafunzi aweza kuelekezwa kuandika vinyume vya vitendo.
156
III. Nyenzo:
Michoro au picha za kuonyesha vinyume vya vitendo mbalimbali;
Chati zenye maneno ya vinyume vya vitendo mbalimbali;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 92-93;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.)
IV. Maandalizi ya somo
Katika sehemu hii, mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya
vipindi hivi kama vilivyotajwa hapo juu. Wanafunzi wanaweza kutumiwa katika
funzo hili la kuonyesha vinyume vya vitendo mbalimbali ambapo mwanafunzi
mmoja anaweza kutenda kitendo kimoja kisha mwanafunzi mwingine akatenda
kinyume cha kitendo hicho. Hii itakuwa njia nzuri na mwafaka sana katika
ufundishaji wa mada hii.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa vyake kwa kukumbuka kuwa matumizi ya michoro, picha na
chati ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha ufundishaji wa wanafunzi
hasa walio na matatizo au ulemavu au hata kiwango cha chini cha uelewa.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia au kuona, mwalimu
anashauriwa kuhusisha matumizi ya lugha ya ishara au breli ili kuwawezesha
wanafunzi hawa kujifundisha kama wanafunzi wengine.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa
katika Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu aanze funzo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia kuhusu kuandika
visa bunifu mbalimbali kwa mwandiko nadhifu. Wanafunzi wajibu salamu za
157
mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi
katika kusahihisha zoezi walilopewa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi
wenye matatizo wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili
kisha awashirikishe katika kuchunguza michoro waliyopewa katika Kitabu cha
Mwanafunzi, ukurasa 92-93. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza
wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro hiyo kama vile: Mnaona nini
kwenye michoro hii? Watu hawa wanafanya vitendo gani? Wanafunzi wajibu
maswali ya mwalimu kulingana na wanayoona kwenye michoro waliyopewa
vitabuni mwao. Kisha, wanafunzi wajadiliane kuhusu vitendo vinavyotendwa
katika michoro hiyo na waeleze ugunduzi wao. Wanafunzi waeleze kuwa katika
michoro hiyo kuna vitendo vya kulala kuamka na kuketi kusimama.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya zoezi
la maigizo walilopewa katika vitabu vyao katika makundi yao ya wanafunzi
wawili wawili mbele ya darasa. Wanafunzi waigize kuketi na kusimama, kulala
na kuamka, kwenda na kurudi, kuvaa viatu na kuvua viatu. Kando na vitendo
walivyopewa katika vitabu vyao, mwalimu anaweza kuwapendekezea vitendo
zaidi vya kuigiza ili kuzidisha maarifa yao kuhusiana na vinyume vya vitendo.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
Katika hatua hii, wanafunzi watapata fursa ya kujifundisha kuhusu vinyume vya
vitendo mbalimbali.
Kwa mfano:
Kitendo Kinyume
1. lia - cheka
2. vaa - vua
3. fuma - fumua
4. safisha - chafua
158
Mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua jinsi ya kuitunga sentensi katika
umoja na wingi kwa kutumia vinyume vya vitendo, kwa mfano :
1. Mwanafunzi anavaa nguo.
Mwanafunzi anavua nguo.
2. Kaka anasafisha sare yake.
Kaka anachafua sare yake.
3. Fundi anafuma sweta ya mtoto.
Fundi anafumua sweta ya mtoto.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa katika kuchunguza ikiwa wamefahamu vinyume
vya vitendo mbalimbali. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza
kutunga sentensi sahihi kwa kutumia vinyume vya vitendo mbalimbali.
VI. Majibu
Zoezi la ufunguzi, ukurasa 92-93
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na michoro wanayoiona,
kwa mfano:
1. Mwanafunzi aeleze anachokiona katika michoro iliyopo.
2. Mwanafunzi aeleze vitendo anavyoviona kama vile: kulala, kuamka,
kuketi na kusimama.
3. Mwanafunzi aeleze ugunduzi wake ambao ni: vitendo hivi ni vinyume
vya vitendo vilivyopo.
Zoezi, ukurasa 93
1. rudi
2. inuka
3. fungua
159
Matokeo maalum
yanayotarajiwa
Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutambua msamiati wa usafi wa
mazingira;
(b) Kutofautisha mazingira safi na
yasiyo safi;
(ch) Kutambua msamiati uliotumiwa
katika hadithi;
(d) Kuandika kisa kifupi kwa hati
nadhifu kulingana na mada ili
kujenga stadi ya uandishi;
(e) Kutambua matumizi ya haraka
na polepole ili kuimarisha
mawasiliano.
Mwanafunzi aweza kuelekezwa
kusoma maneno yanayohusiana
na usafi wa mazingira kwa
kutumia kadi za maneno.
Mwanafunzi aweza kufahamu
maana ya usafi wa mazingira.
Mwanafunzi aweza kujadili
kuhusu picha zilizojumuishwa
kwenye hadithi.
Mwanafunzi apewe hadithi
yenye mapengo ajaze kwa
maneno mwafaka.
Mwanafunzi aweza kujaza
mapengo kwa kutumia haraka
na polepole.
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kuimba nyimbo na kukariri mashairi katika tamasha mbalimbali ili
kuhamasisha kuhusu usafi wa mazingira.
Kazi ya vikundi.
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Mazingira.
Mada Kuu 6: USAFI WA MAZINGIRA
Idadi ya vipindi: 13
Sura ya
6
160
Nyenzo:
Rekodi za masimulizi ya kubuni mbalimbali kuhusu usafi wa mazingira;
Vifaa halisi vya kufanyia usafi kama vile: ufagio, jaa la takataka n.k.;
Michoro au picha za watu wakifanya usafi wa mazingira;
Michoro au picha za mazingira safi na machafu;
Rekodi za hadithi bunifu mbalimbali kuhusu usafi wa mazingira;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 94-104;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Mada hii inashughulikia usafi wa mazingira pamoja na masimulizi na hadithi
bunifu kuhusu usafi wa mazingira. Pia, vipengele vya kuandika visa vifupi
kuhusiana na usafi wa mazingira pamoja na sarufi kuhusu matumizi ya
haraka na polepole vitaangaziwa katika mada hii.
Mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kujenga stadi yake ya kusikiliza,
kufahamu njia mbalimbali za kudumisha usafi wa mazingira, umuhimu wa
kudumisha usafi wa mazingira, vifaa ambavyo huhitajika katika shughuli za
kusafisha mazingira pamoja na kusoma kwa ufasaha hadithi za kubuni kuhusu
usafi wa mazingira. Hadithi za kuvutia na zenye msamiati wa kiwango cha
wanafunzi wa gredi hii zibuniwe ili kuwafaa wanafunzi katika ujifundishaji wao.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
Elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya mazingira kupitia kwa kutambua
umuhimu wa kudumisha usafi katika mazingira yake,
Utangamano wa kijamii,
Amani na maadili.
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii ni kuhusu usafi wa mazingira ni kama vile:
161
Msamiati Maana
1.
ufagio
kifaa cha kukusanyia takataka kwa kufagia
2.
safisha
ondoa uchafu kwa kuosha kwa maji na sabuni
3.
uchafu
vitu visivyo safi ambavyo aghalabu hunuka na
huweza kuleta magonjwa
4.
jaa
chombo ambamo takataka hutupwa
5.
majitaka
maji ambayo ni machafu kwa kuchanganyikana na
takataka
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Ili kuweza kuwashirikisha wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali,
mwalimu awe na vifaa maalum vya kuwasaidia wanafunzi hawa katika ujifundishaji
wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kuona, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya breli pamoja na vifaa vya kunasia sauti.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri wa
lugha ya ishara. Haya yatawawezesha wanafunzi hawa kusoma kama wanafunzi
wenzao bila vikwazo vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya
vipindi
Mada Ndogo 1: Msamiati
3
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 4: Kuandika
3
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya haraka na polepole
2
JUMLA: 13
162
Mada Ndogo 1: Msamiati wa usa wa mazingira
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati wa usafi wa mazingira;
b) Kutumia msamiati wa usafi wa mazingira katika sentensi;
ch) Kubainisha mazingira safi na yale machafu;
d) Kuthamini mazingira safi.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aweza kuelekezwa kusoma maneno yanayohusiana na usafi
wa mazingira kwa kutumia kadi za maneno.
Mwanafunzi aweza kuelekezwa kutoa maana ya msamiati unaohusiana na
usafi wa mazingira.
Wanafunzi waweza kujadiliana kuhusu maana za maneno yanayohusiana
na usafi wa mazingira.
Mwanafunzi aweza kutunga sentensi sahihi kwa kutumia msamiati
unaohusiana na usafi wa mazingira.
Mwanafunzi aweza kutazama video kuhusu usafi wa mazingira k.m. kuokota
na kuchoma takataka, kufyeka nyasi n.k.
Mwanafunzi aweza kutazama michoro na picha zinazolenga maana za
maneno kuhusu usafi wa mazingira.
Wanafunzi waweza kujadiliana kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira
wakiwa kwenye vikundi.
III. Nyenzo:
Kadi zenye maneno yanayohusu usafi wa mazingira;
Michoro au picha za watu wakidumisha usafi wa mazingira;
Michoro au picha za mazingira safi na machafu;
Vifaa halisi vya kudumisha usafi wa mazingira;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 95-97;
163
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Ni muhimu kwa kila mtu kufahamu kuhusu usafi wa mazingira, njia za kudumisha
usafi wa mazingira pamoja na umuhimu wa kuwa na mazingira yaliyo safi.
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi
kama vilivyotajwa hapo juu. Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu
atambue wakati mwafaka wa kuweka hadharani vifaa alivyovileta darasani kwa
kukumbuka kuwa matumizi ya michoro, picha, kadi, vifaa halisi ni mbinu bora
ambayo hutumika kufanikisha ufundishaji wa wanafunzi hasa walio na ulemavu,
matatizo mbalimbali au kiwango cha chini cha uelewa.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, wavionyeshe vifaa vilivyopo
kwa kuvigusa huku wakiandika maelezo yake ubaoni. Mwalimu anaweza
kuhusisha matumizi ya lugha ishara. Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona,
mwalimu ahusishe matumizi ya breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii
kujifundisha kama wanafunzi wengine bila vikwazo vyovyote.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwenye vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu awaamkue wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia kuhusu vinyume vya vitendo.
Wanafunzi wajibu maamkuzi ya mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusu
usafi wa darasa lao na shule yao kwa ujumla. Maswali kama vile: Nani
husafisha darasa lenu? Wao hutumia vifaa gani? Nani hufagia eneo la gwaride?
Nani huokota takataka uwanjani? n.k. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu
kulingana na wanaosafisha darasa na shule yao kwa ujumla pamoja na kueleza
164
vifaa mbalimbali ambavyo hutumika katika shughuli hii. Mwalimu ahakikishe
anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii. Hii itakuwa namna nzuri ya
kutanguliza funzo hili kuhusu usafi wa mazingira.
Kabla ya somo hili, mwalimu awe ametayarisha kadi za maneno kuhusu usafi wa
mazingira ambazo atawaonyesha wanafunzi nao watatamka kwa sauti maneno
hayo. Shughuli hii itawasaidia wanafunzi kufahamu maneno kadhaa ambayo
hutumiwa kurejelea usafi wa mazingira.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne wanne kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 94.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Unaona nini? Watu hawa wanafanya nini? Wanafunzi wajibu
maswali ya mwalimu kulingana na wanayoyaona kwenye michoro waliyopewa.
Wanafunzi wapewe muda katika makundi yao wa kujadiliana kuhusu michoro
waliyopewa. Wanafunzi waeleze kuwa wanawaona wanafunzi wakisafisha
mazingira yao, kuna msichana anayefagia pamoja na mvulana aliyekusanya
takataka na kuzichoma.
Baada ya shughuli hii, (iwapo inawezekana) mwalimu awe ameandaa mapema
video kwenye tarakilishi au kwenye projekta kuhusu vitendo mbalimbali vya
kudumisha usafi wa mazingira ambayo anaweza kuwaonyesha wanafunzi
darasani. Wanafunzi wachangamke na kutazama video hiyo kwa makini ili
kupata ujumbe uliokusudiwa.
Baada ya kutazama video husika, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika
makundi yao kujadili kuhusu njia za kudumisha usafi wa mazingira yao kama
vile: kufagia, kufyeka nyasi, kuosha vyumba, kusafisha madirisha, kusafisha vyoo,
kuokota takataka n.k. Wanafunzi waeleze shughuli mbalimbali za kudumisha
mazingira safi ambazo wao hutekeleza.
Wanafunzi pia waelekezwe katika makundi yao kutaja vifaa mbalimbali
ambavyo wao hutumia kudumisha usafi wa mazingira kama vile: ufagio, reki,
jaa la takataka, kifyekeo, brashi n.k.
165
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusoma maneno yaliyo
kwenye kadi zilizo kwenye vitabu vyao yanayohusu usafi wa mazingira.
Mwalimu anaweza kuandaa kadi hizi halisi na kuwaonyesha wanafunzi darasani.
Wanafunzi wasome maneno kwenye kadi hizo kwa sauti wakiwa wawili wawili
kisha mmoja mmoja. Baada ya shughuli hii, wanafunzi watazame na kuchunguza
michoro waliyopewa katika vitabu vyao na waelezane kuhusu wanayoyaona
kuhusiana na usafi wa mazingira.
Baadaye, wanafunzi waigize vitendo mbalimbali kuhusu njia za kudumisha usafi
wa mazingira walivyopewa kama zoezi katika vitabu vyao. Mwalimu anaweza
kuwaruhusu wanafunzi kutoka nje ya darasa ili kutazama mazingira yao na
kubaini iwapo ni safi au ni machafu.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu njia mbalimbali za kudumisha usafi wa
mazingira pamoja na umuhimu wa mazingira safi kwa binadamu.
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 94
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na michoro waliyopewa,
kwa mfano:
1. Wanafunzi waeleze wanachoona katika michoro waliyopewa, kwa
mfano: wanafunzi wanasafisha mazingira yao, msichana anafagia na
mvulana anachoma takataka.
2. Watu hawa wanasafisha mazingira yao kwa kufagia na kuchoma
takataka.
3. Wanafunzi waeleze mahali wao hutupa takataka, kwa mfano:
kwenye jaa la takataka.
4. Wanafunzi waeleze wao hufagia nyumba kwa kutumia vifaa gani,
kwa mfano: ufagio.
5. Wanafunzi waeleze mtu hufyeka nyasi akitumia kifaa gani, kwa
mfano: kifyekeo.
166
Maswali, ukurasa 96
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Kwa mfano:
1. Wanafunzi waeleze wanachoona katika michoro waliyopewa: msichana
anafagia, mvulana anafyeka nyasi na mvulana anatupa takataka kwenye
jaa la takataka.
2. Watu hawa wanasafisha mazingira kwa kufagia, kutupa takataka na
kufyeka nyasi.
3. Takataka zinatupwa kwenye jaa la takataka.
4. Wanafunzi waeleze iwapo wao hufagia nyumba zao. Mwalimu
atathmini majibu ya wanafunzi.
5. Wanafunzi waeleze mahali wao hutupa takataka. Mwalimu atathmini
majibu ya wanafunzi.
6. Wanafunzi waeleze umuhimu wa kudumisha usafi wa mazingira.
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutofautisha mazingira safi na yasiyo safi;
b) Kutambua umuhimu wa mazingira safi;
ch) Kusikiliza masimulizi kuhusu usafi wa mazingira;
d) Kueleza kuhusu usafi wa mazingira;
e) Kueleza jinsi ya kutunza mazingira yake;
f) Kufurahia mazingira safi maishani mwake.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aweza kufahamu maana ya usafi wa mazingira.
Wanafunzi waongozwe katika vikundi kusimulia visa vinavyohusiana na
167
usafi wa mazingira k.v. umuhimu wa kutunza mazingira.
Mwanafunzi aweza kuigiza jinsi ya kudumisha usafi wa mazingira yake.
Wanafunzi waweza kutazama video inayohusu mazingira safi na machafu
kisha wabainishe mazingira wanayofurahia.
Mwanafunzi anaweza kuchora vifaa vinavyotumiwa kusafisha mazingira.
Wanafunzi waweza kujadiliana kuhusu jinsi wanavyoweza kuchangia
katika usafi wa mazingira.
Mgeni aweza kualikwa ili kusimulia kuhusu mazingira huku wanafunzi
wakiandika yaliyo muhimu na kuuliza na kujibu maswali.
III. Nyenzo:
Rekodi za masimulizi bunifu mbalimbali kuhusu usafi wa mazingira;
Michoro au picha za vifaa vya kudumisha usafi wa mazingira;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Mgeni mwalikwa (afisa wa mazingira);
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 97-98;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusikiliza masimulizi bunifu
yanayohusu njia za kudumisha usafi wa mazingira, vifaa vya kudumisha usafi
wa mazingira pamoja na umuhimu wa usafi wa mazingira ili kujenga stadi
yao ya kusikiliza na kuzungumza. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa
vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake kama
vilivyotajwa hapo juu. Mwalimu anaweza kumwalika mgeni kama vile afisa
wa mazingira au mtunzi wa mazingira akawaeleza wanafunzi kuhusu njia
mbalimbali za kudumisha usafi wa mazingira pamoja na umuhimu wa kuwa na
mazingira safi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
168
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
msamiati wa usafi wa mazingira. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja
na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili wasaidiwe
na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza masimulizi bunifu pamoja na stadi ya kuzungumza kupitia
kwa wao wenyewe kuwasimulia wenzao. Masimulizi haya yatahusu usafi wa
mazingira.
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne wanne kisha
watazame na kuchunguza michoro waliyopewa katika vitabu vyao. Mwalimu
awashirikishe wanafunzi katika kujibu maswali waliyopewa kuhusu michoro
iliyopo. Wanafunzi waeleze vifaa walivyopewa katika michoro husika hutumika
kufanya kazi gani na iwapo wao wamewahi kutumia vifaa hivyo.
Kila kundi lipewe muda wa kujadiliana kuhusu michoro hiyo na maswali
waliyopewa. Mwalimu azunguke darasani akiwasaidia wanafunzi wanaopata
matatizo katika makundi yao.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao
ya wanafunzi wanne wanne kuigiza vitendo kadhaa vya kudumisha usafi wa
mazingira kama vilivyotajwa katika vitabu vyao. Wanafunzi wote washirikishwe
katika shughuli hii ya uigizaji.
Baadaye, mwalimu awasimulie wanafunzi masimulizi bunifu kuhusu usafi wa
mazingira. Mwalimu ana uhuru wa kubuni masimulizi yoyote kuhusiana na
usafi wa mazingira. Anaweza kuwasomea wanafunzi masimulizi hayo au hata
169
akayarekodi kwenye tarakilishi na wanafunzi wakayasikiliza darasani. Mwalimu
ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa makini. Pia, mwalimu ahakikishe
kuwa anasoma masimulizi hayo kwa ufasaha, kwa matamshi sahihi na sauti
ya kusikika na ya kuvutia. Iwapo mwalimu ana matatizo ya kimatamshi,
anaweza kumwalika msomaji stadi atakayewasomea au kuwasimulia wanafunzi
masimulizi hayo kuhusu usafi wa mazingira.
Baada ya kusomewa masimulizi kuhusu usafi wa mazingira, wanafunzi wajaribu
katika makundi yao kujadili masimulizi hayo. Wanafunzi watoe muhtasari wa
masimulizi hayo katika makundi yao.
Hatimaye, kila mwanafunzi apewe fursa ya kusimama mbele ya darasa na
kusimulia kuhusu usafi wa mazingira kwa kujibu maswali ya zoezi la masimulizi
waliyopewa kwenye vitabu vyao. Mwalimu ahakikishe anasahihisha makosa ya
kimatamshi ya wanafunzi pindi tu yanapotokea. Wanafunzi wote wapewe fursa
ya kusimulia kuhusu njia mbalimbali za kudumisha usafi wa mazingira pamoja
na umuhimu wa usafi wa mazingira.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali mbalimbali
ya kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma masimulizi
bunifu pamoja na kufahamu njia mbalimbali za kudumisha usafi wa mazingira
na umuhimu wa usafi wa mazingira. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wamepata maarifa ya kujibu kwa usahihi maswali ya masimulizi
170
VI. Majibu
Maswali ya michoro, ukurasa 98
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano:
1. Wanafunzi waeleze wanachokiona katika michoro waliyopewa.
2. Jaa la takataka, kifyekeo na ufagio.
3. Jaa la takataka ni mahali pa kutupa takataka, kifyekeo ni cha kukata
nyasi na ufagio hutumika kukusanya takataka kutoka eneo fulani.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Zoezi la masimulizi, ukurasa 98
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
(a) Kutambua msamiati uliotumiwa katika hadithi;
(b) Kusikiliza mwalimu kwa makini anaposoma hadithi kuhusu usafi wa
mazingira;
(ch) Kusoma hadithi kuhusu mazingira safi;
(d) Kufahamu hadithi aliyosoma na aliyosomewa kuhusu usafi wa mazingira;
(e) Kuthamini mazingira safi.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aweza kujadili kuhusu picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi aweza kutabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
171
Mwanafunzi aweza kuthibitisha utabiri wake baada ya kusoma hadithi.
Mwanafunzi aweza kufahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye
hadithi.
Wanafunzi waweza kusoma kama darasa zima, wakiwa wawili wawili na
baadaye kila mwanafunzi asome peke yake.
Mwanafunzi aweza kutoa muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.
Mwanafunzi aweza kutabiri kitakachotokea katika hadithi katika kundi la
wawili wawili au darasa zima.
Wanafunzi waweza kusomeana hadithi wakiwa wawili wawili.
Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kupitia kwa kinasasauti.
Mwanafunzi aweza kutazama video ya mtu au mtoto akisoma hadithi
husika kwa ufasaha kisha aige usomi ule.
Wanafunzi waweza kusomeana hadithi katika vikundi.
Mwanafunzi aweza kusimulia hadithi kutokana na picha alizopewa kuhusu
usafi wa mazingira.
Mwanafunzi aweza kuuliza na kujibu maswali kudhihirisha ufahamu.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za hadithi bunifu mbalimbali kuhusu usafi wa mazingira;
Vifaa halisi vya kudumisha usafi wa mazingira;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 99-100;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu ili kujenga stadi ya wanafunzi ya
kusikiliza na kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika
kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake. Mwalimu anaweza kutumia
michoro au picha za hadithi za kubuni kuhusu usafi wa mazingira ambazo
172
atawasomea wanafunzi darasani na nyingine watajisomea wenyewe. Mwalimu
anaweza hata kumwalika mtambaji au msomaji mashuhuri akawasomea
wanafunzi hadithi bunifu kuhusu usafi wa mazingira kisha wanafunzi wakasoma
baada yake, wakiwa wawili wawili kisha mmoja mmoja. Sharti, mwalikwa huyu
awe na uwezo wa kusoma kwa sauti ya kusikika na kwa matamshi sahihi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
masimulizi yanayohusu usafi wa mazingira. Wanafunzi wajibu salamu za
mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi
katika kusahihisha zoezi walilopewa katika funzo la hapo awali. Wanafunzi
wenye matatizo katika ujifundishaji wao wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao
ya kusoma hadithi bunifu pamoja na kusikiliza. Mwalimu awagawe wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi wanne wanne kisha awaombe watazame mchoro
ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 99. Wanafunzi wachunguze
mchoro huo wa binti anayesafisha mazingira kwa kufagia na kuujadili katika
makundi yao. Mazingira yanayoonekana katika mchoro uliopo ni safi sana
na ya kupendeza. Wanafunzi watabiri matukio ya mchoro uliopo. Wanaweza
kusimuliana kuhusu usafi wa mazingira yao wanakoishi wao wenyewe na jinsi
wao husaidia katika kuyasafisha na kuyafanya yapendeze. Mwalimu awaelekeze
wanafunzi katika kujibu maswali ya mchoro husika waliyopewa katika vitabu
vyao katika makundi yao. Mwalimu azunguke darasani akiwasaidia wanafunzi
wanaotatizika katika makundi yao.
173
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi hadithi bunifu ifuatayo
kuhusu usafi wa mazingira. Mwalimu ahakikishe anasoma hadithi hii kwa
sauti ya kusikika na ya kuvutia na kwa matamshi sahihi. Wanafunzi wote
wamsikilize mwalimu kwa makini anaposoma hadithi hii. Mwalimu anaweza
kuirekodi hadithi hii kwenye tarakilishi kisha wanafunzi wakaisikiliza darasani.
Baada ya wanafunzi kusikiliza hadithi hii, mwalimu awaelekeze katika makundi
yao ya wanafunzi watatu watatu kusimuliana kuhusu hadithi waliyosomewa
au waliyosikiliza. Mwalimu anaweza kuiandika hadithi hii kwenye chati na
wanafunzi wakapewa fursa ya kuisoma katika makundi yao kisha mmoja mmoja.
Mfano wa hadithi
Mimi ninaitwa Sara. Mimi ninapenda usafi. Ninapenda mazingira safi. Mama
yangu amenifundisha njia mbalimbali za kudumisha usafi. Usafi wa mwili
wangu pamoja na usafi wa mazingira yangu. Nyumba yetu ni safi. Mazingira
ya nyumba yetu yanapendeza sana. Mimi hufagia takataka zote na kusafisha
nyumba yetu. Mimi hutumia maji na sabuni kusafisha nyumba yetu. Madirisha
yetu ni safi. Kuta za nyumba yetu zimepakwa rangi nzuri na uchafu wowote
kwenye ukuta husafishwa kwa kitambaa. Ufagio ambao mama alinunua
hutumiwa kufagia nyumba yetu. Tumefyeka nyasi zilizo karibu na nyumba yetu.
Nyasi hizi zilifyekwa na kaka yangu kwa kutumia kifyekeo. Shule yetu pia ni
safi. Sisi huokota takataka zote na kuziweka kwenye pipa. Tumefyeka nyasi zote
zilizo karibu na shule yetu. Tumeokota karatasi na takataka zote na kuzichoma.
Sisi sote tunapenda usafi. Tunapenda usafi wa mazingira. Uchafu una madhara
mengi. Husababisha magonjwa kama vile kipindupindu. Wadudu hatari kama
vile mbu na nzi huletwa na uchafu. Mazingira safi ni afya kwa binadamu wote.
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi walisikiliza hadithi ya mwalimu kwa makini,
mwalimu awaulize maswali mbalimbali kwa kurejelea hadithi hiyo, kwa mfano:
1. Sara anapenda nini?
2. Sara hufanya nini kusafisha mazingira yao?
3. Sara hutumia nini kusafisha mazingira yao?
4. Kwa nini mazingira safi ni muhimu kwa binadamu?
174
5. Taja wadudu ambao huletwa na uchafu.
6. Taja ugonjwa ambao husababishwa na uchafu.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika makundi yao (ya
wanafunzi wawili wawili) kusoma hadithi kuhusu aina ya mazingira anayopenda
Kasidi iliyo katika vitabu vyao. Wanafunzi wasome hadithi hii kwa sauti wakiwa
wawili kisha kila mmoja asome peke yake. Makosa ya kimatamshi yakosolewe
pindi tu yanapotokea. Mwalimu anaweza kumwomba kila mwanafunzi kusoma
hadithi hii mbele ya darasa zima. Shughuli hii itakuza ujasiri wa wanafunzi wa
kusimama na kuzungumza mbele ya watu. Stadi yao ya kusoma pia itaboreshwa
zaidi.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kujibu maswali
ya hadithi waliyosoma. Wanafunzi wajibu maswali hayo kwa kurejelea
hadithi waliyosoma kuhusu mazingira ambayo Kasidi anapenda. Wanafunzi
wanaotatizika wasaidiwe na mwalimu.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi za kubuni.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kusoma
hadithi na kuweza kujibu maswali ya hadithi hiyo kwa usahihi kulingana na
muktadha wa hadithi hiyo. Wanafunzi waeleze iwapo wamefahamu umuhimu
wa kuwa na mazingira safi.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kufanya mazoezi yaliyo katika
vitabu vyao.
175
VI. Majibu
Maswali ya mchoro, ukurasa 99
1. Wanafunzi waeleze wanachoona katika mchoro waliopewa, kwa
mfano: mimi ninaona binti anayefagia mazingira yao.
2. Wanafunzi wataje vitu wanavyoona katika mchoro waliopewa, kwa
mfano: mimi ninaona ufagio, mazingira safi n.k.
3. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu wanachopenda katika
mchoro waliopewa.
Maswali ya hadithi, ukurasa 100
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na hadithi waliyosoma
kuhusu Kasidi, kwa mfano:
1. Kasidi anapenda mazingira safi.
2. Kasidi anaondoa uchafu wote kutoka kwenye mazingira yao.
3. Kwa sababu yeye huondoa uchafu wote na kuutupa kwenye jaa.
4. Kasidi anatupa takataka kwenye jaa.
5. Uchafu unaleta nzi, mbu na mende.
6. Wadudu wanaleta magonjwa.
Mada Ndogo 4: Kuandika
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi
ya uandishi;
b) Kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi.
bora;
176
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
Mwanafunzi aeleze yaliyo muhimu katika uandishi k.v. mwandiko nadhifu,
maudhui, mtiririko.
Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwalimu.
Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.
Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa kama hiki
kifuate hatua tano za uandishi: maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo,
uhariri na uchapishaji. Vichwa vya visa vinaweza kutofautiana.
III. Nyenzo:
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Hadithi za kubuni zilizoandikwa kwenye chati;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu usafi wa mazingira;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 101-102;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Lengo kuu la somo hili ni kukuza stadi ya mwanafunzi ya kuandika. Katika
somo hili, wanafunzi watapata maarifa ya kuandika visa vifupi vifupi kwa
kuzingatia mambo kadhaa kama vile: mwandiko nadhifu, mtiririko, uhariri,
marejeleo, nakala safi na maandalizi mengine. Shughuli hii itawawezesha
wanafunzi kufahamu jinsi ya kuandika visa mbalimbali bunifu. Mwalimu
ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili kama
vilivyoorodheshwa hapo juu. Hili litamsaidia kufanikisha ufundishaji wake
pamoja na ujifundishaji wa wanafunzi.
Katika kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila
zoezi husika lililotolewa kwenye vitabu vyao.
177
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
kusoma hadithi za kubuni kuhusu usafi wa mazingira. Wanafunzi wajibu salamu
za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wasahihishe zoezi walilopewa katika kipindi
cha hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kuandika na hata kubuni hadithi kwa kuandika nakala ya kwanza, kisha
kuihariri na hatimaye kuandika nakala safi katika madaftari yao. Nakala safi
itazingatia mwandiko nadhifu, mtiririko mwafaka pamoja na kuhaririwa ili
kuondoa makosa ya kimaendelezo na kisarufi. Mwalimu awagawe wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha awaombe watazame
michoro miwili waliyopewa katika vitabu vyao. Michoro hii miwili ni ya shule
ya Bwiza iliyo na mazingira safi na mchoro wa pili ni wa shule ya Kimira iliyo
na mazingira machafu. Mwalimu awaelekeze wanafunzi katika makundi yao
kujadiliana kuhusu michoro hiyo miwili kisha waandike katika madaftari yao
tofauti zilizopo kati ya michoro hiyo. Wanafunzi wahakikishe wanaandika kwa
mwandiko nadhifu na wanaepuka makosa ya kimaendelezo na kisarufi.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awaelekeze wanafunzi kufanya zoezi la kujaza
mapengo ya hadithi kuhusu usafi wa mazingira waliyopewa katika kitabu
chao. Wanafunzi wayajaze mapengo hayo kwa majibu mwafaka kutoka kwa
waliyopewa kwenye mabano. Wanakili hadithi hii kwa mwandiko nadhifu katika
madaftari yao.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya zoezi la kuandika
katika madaftari yao kuhusu namna wanavyosafisha darasa lao. Wanafunzi
waandike maelezo yao kwa mwandiko nadhifu. Mwalimu ahakikishe kuwa kila
mwanafunzi anaandika maelezo hayo kwa hati nadhifu. Mwalimu awahusishe
178
wanafunzi wote katika shughuli hii ya kuandika maelezo kuhusu namna ya
kusafisha darasa lao.
Baada ya shughuli hii, mwalimu ahakikishe kuwa amesahihisha madaftari ya
wanafunzi ili kusahihisha makosa yoyote ya kimaendelezo na mwandiko usio
nadhifu. Wanafunzi walio na matatizo ya kuandika kwa mwandiko nadhifu
wapewe mazoezi zaidi ya kuandika. Mwalimu awaelekeze zaidi.
Mwalimu anaweza kumwomba kila mwanafunzi aandike nakala yake safi ubaoni
(kuhusu namna ya kusafisha darasa lao) ili wanafunzi wenzake waisome na
kuisahihisha kwa kurejelea mwandiko nadhifu, makosa ya kimaendelezo pamoja
na ya kisarufi. Pia, wanafunzi katika makundi yao wanaweza kusahihisha nakala
zao safi. Wanafunzi walio na matatizo wasaidiwe.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali mbalimbali
ya kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kubuni na kuandika maelezo bunifu.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata uelewa wa umuhimu wa
usafi wa mazingira pamoja na njia mbalimbali za kudumisha usafi wa mazingira.
VI. Majibu
Zoezi la kuandika, ukurasa 101
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na michoro waliyopewa,
kwa mfano:
1. Ninaona shule mbili: shule ya Bwiza na shule ya Kimira.
2. Ninaona mazingira machafu.
3. Ninaona mazingira safi.
4. Shule ya Bwiza ina mazingira safi nayo shule ya Kimira ina
mazingira machafu.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu shule yao
inavyoonekana.
179
Mada Ndogo 5: Saru: Matumizi ya ‘haraka’ na ‘polepole’
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua matumizi ya haraka na polepole ili kuimarisha mawasiliano
mwafaka;
b) Kutumia haraka na polepole katika kutunga sentensi ili kuimarisha
mawasiliano mwafaka;
ch) Kusoma sentensi zilizo na matumizi ya haraka na polepole ili kujenga
usomaji bora;
d) Kuandika sentensi sahihi zilizotumia haraka na polepole ili kuimarisha
uandishi bora;
e) Kuchangamkia matumizi ya haraka na polepole katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia haraka na polepole.
Mwanafunzi aweza kubainisha matumizi ya vielezi vya jinsi vinavyofunzwa
kwa kutumia vifaa vya teknolojia.
Zoezi, ukurasa 102
Mama yangu hapendi uchafu karibu na nyumba yetu. Akiona takataka
zozote anaziokota. Anazitupa katika jaa. Pia, mama anachoma takataka
kwa moto. Mimi pia nimeiga tabia ya mama. Sipendi uchafu. Kila siku
ninataka mazingira yetu yawe safi.
Zoezi la kubuni na kuandika, ukurasa 102
Mwalimu atathmini ubunifu na uandishi wa wanafunzi kuhusu namna
wanavyosafisha darasa lao.
180
Mwanafunzi atazame vitu mbalimbali na avirejelee kwa kutumia zilizo na
matumizi ya haraka na polepole k.m. Mtoto anatembea polepole.
Wanafunzi washiriki katika maigizo wakitumia haraka na polepole wakiwa
darasani.
Mwanafunzi aandike maneno na sentensi kwa kutumia haraka na
polepole.
III. Nyenzo:
Chati zenye sentensi zilizojumuisha matumizi ya haraka na polepole;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 103-104;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Kama tunavyofahamu, sarufi ni kipengele muhimu katika ujifundishaji wa
wanafunzi. Mwalimu anastahili kutilia maanani dhana hii ili kuweza kuwahusisha
wanafunzi kwa ukamilifu katika somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema
kama vilivyoorodheshwa hapo juu na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi.
Mwalimu aandae funzo hili kwa namna ya kumwezesha kuwaelekeza wanafunzi
kufahamu kazi mbalimbali pamoja na majina ya watu ambao huzifanya kazi
hizo mbalimbali.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa
maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha
kama wanafunzi wengine. Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia,
mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya lugha ya ishara. Mwalimu anaweza
pia kumshirikisha mtaalamu wa lugha ya ishara katika kuwasaidia wanafunzi
hawa.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu anashauriwa kuwagawa
wanafunzi katika makundi yanayotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa
kwa kila shughuli ya wanafunzi katika vitabu vya wanafunzi.
181
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu awasalimie wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu salamu za
mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi
katika kusahihisha zoezi walilopewa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi
waliopata matatizo katika kufanya zoezi hilo wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne wanne
kisha awashirikishe katika kutazama michoro waliyopewa katika kitabu chao.
Wanafunzi wajadili michoro hiyo kwa kurejelea matumizi ya haraka na
polepole. Wanafunzi waelezane kuhusu watu au wanyama wanaoenda polepole
na wanaoenda kwa haraka. Mwalimu atathmini majadiliano ya wanafunzi katika
makundi yao kwa kurejelea michoro waliyopewa. Shughuli hii itawawezesha
wanafunzi kufahamu matumizi ya haraka na polepole.
Baada ya wanafunzi kujadili kuhusu michoro husika, mwalimu awashirikishe
katika kujibu maswali waliyopewa yanayohusu michoro iliyopo. Wanafunzi
wajibu maswali haya katika makundi yao. Waeleze watu au wanyama katika
michoro iliyopo wanaoenda kwa haraka na wanaoenda polepole pamoja na
kutoa sababu za majibu yao. Katika hatua hii ya wanafunzi kujadiliana kuhusu
matumizi ya haraka na polepole, wanafunzi watapata fursa ya kufahamu tofauti
za vielezi hivi vya jinsi.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kuigiza vitendo
walivyopewa katika vitabu vyao ambavyo ni:
1. Kutembea haraka.
2. Kula polepole.
3. Kuandika haraka.
4. Kusoma polepole.
5. Kusimama haraka.
182
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika maigizo haya.
Wanafunzi waigize jinsi ya kutenda vitendo haraka haraka na jinsi ya kutenda
vitendo polepole.
Mwalimu awaelekeze wanafunzi kutunga sentensi sahihi kwa kutumia haraka
na polepole, kwa mfano:
1. Mtoto anakula polepole.
2. Sungura anakimbia haraka.
3. Kobe anatembea polepole.
4. Mama mjamzito anaongea polepole.
5. Mwalimu anaandika polepole.
Wanafunzi waelekezwe kutambua kuwa haraka na polepole ni vielezi vya
jinsi au namna. Mwalimu ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote katika
shughuli hii ya kutunga sentensi sahihi kwa kutumia haraka na polepole.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi waliyopewa
katika vitabu vyao kuhusu matumizi ya haraka na polepole. Mwalimu awasaidie
wanafunzi wanaotatizika katika kufanya mazoezi haya.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa kwa kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana
kwa kutumia haraka na polepole. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wanaweza kutunga sentensi sahihi katika kwa kutumia vielezi vya jinsi ambavyo
ni: haraka na polepole.
183
VI. Majibu
Maswali ya michoro, ukurasa 104
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano:
1. Ninaona kobe, sungura, mama mja mzito, kipofu na bikizee.
2. Kobe
3. Sungura
4. Mjamzito, kipofu na bikizee. Kwa sababu mjamzito amechoka
sana, kipofu haoni hivyo hawezi kutembea haraka na bikizee
amezeeka.
5. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Zoezi la maigizo, ukurasa 104
Mwalimu atathmini maigizo ya wanafunzi.
Zoezi, ukurasa 104
1. Kinyonga anatembea polepole.
2. Meli husafiri baharini haraka.
3. Sungura alikimbia haraka akampita kobe.
4. Usiimbe haraka, imba polepole.
5. Mgonjwa alitembea polepole mpaka hospitalini.
184
Matokeo maalum
yanayotarajiwa
Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutambua msamiati wa dukani
ili kuutumia katika mawasiliano;
(b) Kutambua maneno
yanayotumiwa katika muktadha
wa dukani ili kuimarisha
mawasiliano;
(ch) Kutambua msamiati uliotumiwa
katika hadithi ili kurahisisha
ufahamu;
(d) Kuandika kisa kifupi kwa hati
nadhifu kulingana na mada ili
kujenga stadi ya uandishi;
(e) Kutambua matumizi ya alama
ya kuuliza (?) katika kuimarisha
mawasiliano.
Mwanafunzi asome maneno
yanayohusiana na shughuli
za dukani kwa kutumia kadi
za maneno kama vile: nunua,
uza, bei, kilo, mnunuzi, mwuzaji,
hasara, faida, pesa, baki, sarafu na
noti.
Mwanafunzi asimulie kuhusu
shughuli za dukani kwa kutumia
mgeni mwalikwa.
Mwanafunzi asikilize mwalimu
akisoma hadithi na baadaye
kuuliza na kujibu maswali.
Mwanafunzi apewe hadithi yenye
mapengo ajaze kwa maneno
mwafaka.
Mwanafunzi aandike alama ya
kuuliza (?).
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kazi ya vikundi.
Kushiriki katika maigizo ya shughuli za dukani.
Mada Kuu 7: DUKANI
Idadi ya vipindi: 13
Sura ya
7
185
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Hisabati na somo la Kiingereza
Nyenzo:
Kadi zenye msamiati wa dukani;
Bidhaa halisi za dukani;
Rekodi za masimulizi na hadithi bunifu kuhusu shughuli za dukani;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 105-115;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Mada hii inashughulikia kuwapa wanafunzi maarifa au ujuzi kuhusiana na
shughuli za dukani, msamiati wa dukani pamoja na kutunga sentensi kwa
kutumia msamiati wa dukani, kusimulia masimulizi yanayohusisha shughuli
za dukani pamoja na kusoma hadithi zinazohusisha shughuli za dukani. Kama
tujuavyo, watu wengi hununua bidhaa nyingi kutoka dukani ili kuweza kujikimu
kimaisha. Shughuli za dukani ni muhimu kwa binadamu kwa sababu wauzaji
hujipatia riziki kutokana na biashara hii na wanunuzi hupata bidhaa mbalimbali
za kuwafaa maishani.
Mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kujenga stadi yake ya kufahamu
msamiati wa shughuli za dukani pamoja na kusoma hadithi za kubuni kuhusu
shughuli za dukani kwa ufasaha. Mwalimu ahakikishe hadithi za kuvutia na
zenye msamiati wa kiwango cha wanafunzi wa gredi hii zimebuniwa ili kuwafaa
wanafunzi katika ujifundishaji wao.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
Elimu ya maendeleo endelevu; elimu ya masuala ya kifedha katika ujuzi
wa kutumia pesa vizuri.
Utangamano wa kijamii.
Amani na maadili.
186
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii kuhusu shughuli za dukani ni kama vile:
Msamiati Maana
1.
uza
tendo la kumpa mtu kitu kwa bei fulani
2.
nunua
tendo la kupewa kitu kwa bei fulani na kulipa kwa pesa
3.
mteja
mtu anayenunua bidhaa au huduma
4.
mwuzaji
mtu anayeuza bidhaa au huduma
5.
baki
pesa zinazobaki baada ya mnunuzi kulipia bidhaa
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Ili kuwahusisha wanafunzi wenye ulemavu na matatizo mbalimbali katika
ujifundishaji wa mada hii, mwalimu ahakikishe kuwa ana vifaa muhimu na
maalum vya kuwasaidia wanafunzi hawa. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa
kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu
anaweza kuwahusisha watafsiri wa lugha ya ishara.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kuona, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya breli pamoja na vifaa vya kunasia sauti. Haya yatawawezesha
wanafunzi hawa kusoma kama wanafunzi wenzao bila vizuizi vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya
vipindi
Mada Ndogo 1: Msamiati
3
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 4: Kuandika
3
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya alama ya kuuliza (?)
2
JUMLA: 13
187
Mada Ndogo 1: Msamiati wa dukani
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati wa dukani ili kuutumia katika mawasiliano;
b) Kusoma maneno yanayohusiana na shughuli za dukani ili kujenga
usomaji bora;
ch) Kueleza maana ya msamiati wa dukani ili kuimarisha stadi ya
kuzungumza;
d) Kutumia msamiati wa dukani katika sentensi sahihi ili kuimarisha stadi
ya kuzungumza;
e) Kuandika maneno yanayohusiana na uuzaji na ununuzi ili kuimarisha
stadi ya kusoma;
f) Kuthamini shughuli za biashara.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome maneno yanayohusiana na shughuli za dukani kwa
kutumia kadi za maneno kama vile: nunua, uza, bei, kilo, mnunuzi, mwuzaji,
hasara, faida, pesa, baki, sarafu na noti.
Mwanafunzi ashiriki katika majadiliano kuhusu maana za maneno
yanayohusiana na shughuli za dukani kwa kutumia picha au michoro.
Mwanafunzi atunge sentensi sahihi kwa kutumia msamiati wa dukani.
Mwanafunzi aweza kutazama video kuhusu uuzaji na ununuzi.
Mwanafunzi ashiriki katika majadiliano kuhusu umuhimu wa kufanya
biashara wakiwa kwenye makundi.
III. Nyenzo:
ØKadi zenye msamiati wa shughuli za dukani;
ØBidhaa halisi za dukani;
ØWanafunzi wenyewe;
188
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 106-108;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Ununuzi na uuzaji wa bidhaa mbalimbali ni shughuli muhimu sana katika maisha
ya binadamu ya kila siku. Wanunuzi pamoja na wauzaji hujipatia riziki kutokana
na shughuli ya ununuzi wa bidhaa mbalimbali. Kila mwanafunzi hutumia bidhaa
mbalimbali zilizonunuliwa kutoka kwa duka fulani, kwa mfano kalamu, chakula,
peremende n.k.
Mwalimu aandae funzo hili kwa namna ya kumwezesha kuwaelekeza wanafunzi
kufahamu msamiati wa shughuli za dukani. Vifaa vitakavyohitajika kama vile
bidhaa halisi za dukani, kadi zenye msamiati wa dukani pamoja na michoro au
picha za bidhaa mbalimbali na shughuli za dukani viandaliwe ili ufundishaji wa
somo hili uwe rahisi. Vifaa hivyo vionyeshwe hadharani kwa wakati unaofaa.
Mwalimu atilie maanani wanafunzi wenye ulemavu na matatizo mbalimbali
wakati wa kuandaa vifaa vya kutumia katika ufundishaji wake ili kuwahusisha
wanafunzi wote katika somo hili.
Katika funzo hili, mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wamejigawa katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa
kwa kila zoezi linalohusika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulie funzo lake kwa kuwaamkia wanafunzi na kuwauliza maswali
mbalimbali kuhusu kipindi cha hapo awali. Wanafunzi nao wajibu maamkuzi
ya mwalimu na maswali waliyoulizwa kuhusu waliyofundishwa katika kipindi
kilichopita. Mwalimu awaongoze wanafunzi kusahihisha kazi iliyotolewa
kama zoezi katika kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wasahihishe zoezi hilo
na mwalimu atoe maelezo yake kwa kutilia mkazo pale ambapo wanafunzi
wanatatizika.
189
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu na
awaombe watazame mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 105.
Wanafunzi wachunguze mchoro huo. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa
kuwauliza maswali mepesi kuhusu mchoro huo. Anaweza kuwauliza maswali
kama vile: Unaona nini kwenye mchoro huu? Watu hawa wanafanya nini? Watu
hawa wako wapi? n.k. Wanafunzi, kwa upande wao, wajibu maswali ya mwalimu
wao kwa kueleza kile wanachoona katika mchoro huo. Kwa mfano: Ninawaona
muuzaji na mnunuzi wakiwa dukani; Ninaona bidhaa mbalimbali dukani. Baada ya
mwalimu kuridhika kuwa wanafunzi wamechunguza mchoro huo na kuuelewa,
awashirikishe katika kujibu maswali waliyopewa katika vitabu vyao kuhusiana
na mchoro huo.
Katika makundi yao, wanafunzi waelekezwe kusoma msamiati wa shughuli
za dukani ulio katika kadi ambazo mwalimu atakuwa ameziandaa mapema
kabla ya somo hili. Wanafunzi wasome msamiati huo wakiwa wawili wawili
kisha kila mmoja asome peke yake. Makosa ya kimatamshi yakosolewe pindi
tu yanapojitokeza. Baada ya shughuli hii, wanafunzi waelekezwe kusimuliana
katika makundi yao kuhusu duka la kwao pamoja na shughuli za duka hilo na
bidhaa zake. Kila mwanafunzi ashiriki katika masimulizi haya.
Hatimaye, wanafunzi katika makundi yao waelekezwe kutazama michoro ya bidhaa
mbalimbali za dukani iliyo katika vitabu vyao na kutaja majina yazo. Wanafunzi
washirikishwe katika kutaja bidhaa mbalimbali za dukani wanazofahamu pamoja
na bei zao na umuhimu wao.
Kwa mfano:
Bidhaa Bei Umuhimu/Matumizi
mkate shilingi hamsini chakula
sabuni shilingi mia moja kuogea
pakiti (unga wa ugali) mia moja chakula
kalamu shilingi ishirini kuandika
190
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wote wamepata ufahamu wa msamiati wa
shughuli za dukani.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
ufahamu wa wanafunzi wa bidhaa mbalimbali za dukani pamoja na shughuli
kadhaa za dukani.
VI. Majibu
Maswali ya utangulizi, ukurasa 105
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona kwenye
mchoro waliopewa, kwa mfano:
1. Ninaona mazingira ya dukani.
2. Ninaona mwuzaji na mnunuzi.
3. Mahali hapa ni dukani.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi
5. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi
Zoezi la kusoma kadi, ukurasa 106
Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi. Makosa ya kimatamshi
yasahihishwe.
Zoezi la masimulizi, ukurasa 107
Mwalimu atathmini masimulizi ya wanafunzi katika makundi yao kuhusu
duka la kwao.
191
Maswali ya michoro, ukurasa 108
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanachoona katika
michoro waliyopewa, kwa mfano:
1. Ninaona bidhaa mbalimbali za dukani.
2. Unga wa ngano, mafuta ya kupikia chakula, sukari na mkate.
3. Mtu anaweza kununua vitu hivi dukani.
Zoezi, ukurasa 108
1. Mtu anayeuza vitu dukani anaitwa mwuzaji.
2. Mtu anayenunua vitu dukani anaitwa mnunuzi.
3. Pesa zikibaki baada ya kununua vitu zinaitwa baki.
4. Pesa za karatasi zinaitwa noti.
5. Mwuzaji anapima uzito wa sukari kwa kilo.
6. Mnunuzi akitaka kununua kitu kwanza anauliza bei.
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua maneno yanayotumiwa katika muktadha wa dukani ili
kuimarisha ufahamu;
b) Kueleza shughuli za dukani ili kuimarisha stadi ya kuzungumza;
ch) Kusikiliza masimulizi kuhusu uuzaji na ununuzi ili kujenga usikivu;
d) Kuthamini biashara katika maisha ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asimulie kuhusu shughuli za dukani kwa kutumia mgeni
mwalikwa;
192
Mwanafunzi atambue maneno yanayotumiwa katika muktadha wa dukani
kama vile: uuzaji, bei, kilo, ununuzi, hasara, faida, pesa na baki;
Mwanafunzi asikilize kwa makini hadithi zinazosimuliwa kuhusu muktadha
wa dukani;
Mwanafunzi aweza kutazama video inayoonyesha mambo yanayohusiana
na ununuzi na uuzaji dukani;
Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu shughuli za dukani katika
vikundi;
Mwanafunzi atunge sentensi kuhusu shughuli za dukani;
Mwanafunzi aweza kuigiza kununua na kuuza katika duka darasani.
III. Nyenzo
Rekodi za masimulizi bunifu mbalimbali kuhusu shughuli za dukani;
Michoro au picha za masimulizi bunifu mbalimbali kuhusu shughuli za
dukani;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 109-110;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusoma masimulizi bunifu
yanayohusu shughuli za dukani ili kujenga stadi yao ya kusikiliza na kusoma.
Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo
hili kama vilivyotajwa hapo juu ili kufanikisha ufundishaji wake. Mwalimu
anaweza kuwaonyesha wanafunzi michoro au picha za masimulizi bunifu
ambayo atawasomea wanafunzi darasani na mengine watajisomea wenyewe
katika makundi kisha kila mmoja mmoja asome peke yake. Mwalimu anaweza
hata kumwalika mtambaji, msimulizi au msomaji mashuhuri akawasomea
wanafunzi masimulizi ya kubuni kuhusu shughuli za dukani kisha wanafunzi
wakasoma baada yake wakiwa wawili wawili na hatimaye kila mmoja akasoma
peke yake. Mwalimu ahakikishe kuwa msimulizi huyu mwalikwa ana uwezo wa
kusoma kwa sauti ya kusikika na kuvutia na kwa matamshi sahihi.
193
Mada hii itashughulikia aina mbalimbali za vyakula vya kiasili pamoja na majina
yao na hata umuhimu wao katika miili ya binadamu.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
lililotolewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
msamiati wa shughuli za dukani. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja
na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali kuhusu kujaza sentensi walizopewa kwa jibu mwafaka
kati ya majibu waliyopewa. Wanafunzi waliopata matatizo katika zoezi hili
wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga
stadi yao ya kusikiliza pamoja na ya kusoma masimulizi ya kubuni. Mwalimu
awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaombe watazame mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa
109. Wanafunzi wachunguze mchoro huo na kuujadili katika makundi yao
wakielezana wanachokiona. Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali
mepesi kuhusiana na mchoro huo kama vile: Unaona nini kwenye mchoro huu?
Mahali hapa ni wapi? Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu
maswali waliyoulizwa. Mwalimu ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote
katika majadiliano haya. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na
wanayoona katika mchoro waliopewa. Mchoro huu ni wa mazingira ya dukani.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika makundi yao
kusimuliana kuhusu siku ambayo kila mwanafunzi aliwahi kutumwa dukani
kununua bidhaa. Kila mwanafunzi ashirikishwe kusimulia kuhusu siku hiyo kwa
wenzake.
194
Kila manafunzi aongozwe na maswali waliyopewa katika vitabu vyao wakati wa
kusimuliana kuhusu siku aliyotumwa dukani.
Baada ya masimulizi haya, kila mwanafunzi anaweza kupewa fursa ya kusimulia
kuhusu siku aliyotumwa dukani mbele ya darasa zima. Mwalimu ahakikishe
anakosoa makosa ya kimatamshi pindi tu yanapotokea. Shughuli ya wanafunzi
ya kutoa masimulizi mbele ya wenzao ni muhimu kwa sababu itakuza stadi yao
ya kuzungumza na kusikiliza pamoja na kukuza ujasiri wao wa kusimama na
kuzungumza mbele ya watu.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao kuigiza shughuli
mbalimbali za dukani kama walivyoelekezwa katika vitabu vyao. Wanafunzi
wanaotatizika wasaidiwe na mwalimu. Makosa ya kimatamshi yasahihishwe
pindi tu yanapotokea ili kukuza lugha sanifu na sahihi ya wanafunzi.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya kuchunguza
iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza masimulizi na kuzungumza kwa ufasaha.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu na ujasiri wa
kutoa masimulizi mbele ya wanafunzi wenzao hasa kwa kurejelea muktadha wa
shughuli za dukani.
VI. Majibu
Maswali ya mchoro, ukurasa 109
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanachoona katika
mchoro waliopewa, kwa mfano:
1. Ninaona muuzaji na mnunuzi katika mazingira ya dukani.
2. Hapa ni dukani.
Zoezi la masimulizi, ukurasa 109
Mwalimu atathmini masimulizi ya kila mwanafunzi kuhusu siku aliyowahi
kutumwa dukani.
Zoezi la maigizo, ukurasa 110
Mwalimu atathmini maigizo ya wanafunzi katika makundi yao kuhusiana
na shughuli mbalimbali za dukani za kununua na kuuza bidhaa.
195
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati uliotumiwa katika hadithi ili kiuwezesha ufahamu;
b) Kusikiliza hadithi ikisomwa na mwalimu kuhusu shughuli za dukani ili
kuimarisha stadi ya kusikiliza;
ch) Kusoma hadithi kuhusu dukani kwa ufasaha ili kujenga usomaji bora;
d) Kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu shughuli za dukani
ili kupata ujumbe;
e) Kuthamini biashara kama njia ya kujitegemea maishani.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asikilize mwalimu akisoma hadithi na baadaye kuuliza na
kujibu maswali.
Mwanafunzi asome pamoja na wengine darasani kisha wasome wawili
wawili na baadaye asome peke yake.
Mwanafunzi jadili picha.
Mwanafunzi atabiri kuhusu kitakachotokea katika hadithi wakiwa wawili
wawili.
Mwanafunzi ashirikiane na wengine kujadili msamiati uliotumika katika
hadithi.
Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi husika ikisomwa kupitia kwa
kinasasauti na kisha kuijadili.
Mwanafunzi aweza kutazama video ya mtu mzima au mtoto akisoma
hadithi husika kwa ufasaha kisha aige usomaji huo.
Wanafunzi waweza kusomeana hadithi katika vikundi.
Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma.
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali.
196
Mwanfunzi ashiriki katika kujadili baadhi ya maswali darasani, katika
vikundi au wakiwa wawili wawili.
III. Nyenzo
ØMichoro au picha za hadithi bunifu mbalimbali kuhusu shughuli za
dukani;
ØRekodi za hadithi bunifu mbalimbali kuhusu shughuli za dukani;
ØVifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu, projekta;
ØWanafunzi wenyewe;
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 110-111;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Katika somo hili, wanafunzi watasoma hadithi bunifu ili kujenga stadi yao ya
kusikiliza pamoja na ya kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa
vinavyohitajika kufundishia funzo hili kama vilivyoorodheshwa hapo awali ili
kufanikisha ufundishaji wake na ujifundishaji wa wanafunzi. Mwalimu anaweza
kuwaonyesha wanafunzi michoro au picha za hadithi bunifu kuhusu shughuli
za dukani ambazo atawasomea wanafunzi darasani na nyingine ambazo
watajisomea wenyewe katika vikundi, wakiwa wawili wawili na hatimaye kila
mmoja mmoja. Mwalimu anaweza hata kumwalika mtambaji, msimulizi au
msomaji mashuhuri akawasomea wanafunzi hadithi bunifu kuhusu shughuli za
dukani kisha wanafunzi wakasoma baada yake katika makundi hadi kusoma kwa
mwanafunzi mmoja mmoja. Msimulizi mwalikwa huyu sharti awe na uwezo wa
kusoma kwa sauti ya kusikika, ya kuvutia na kwa matamshi sahihi na ufasaha.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
197
maswali mbalimbali kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
funzo la hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao
ya kusikiliza pamoja na kusoma hadithi bunifu katika muktadha wa shughuli
za dukani. Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili
wawili kisha awaombe watazame mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi,
ukurasa 110. Wanafunzi wachunguze mchoro huo na kuujadili katika makundi
yao. Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na
mchoro huo kama vile: Unaona nini kwenye mchoro huu? Hapa ni wapi? Mwalimu
awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu
ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote katika majadiliano haya.
Baada ya shughuli hii ya kuchunguza mchoro uliopo na kujibu maswali husika,
mwalimu awasomee wanafunzi hadithi waliyopewa katika vitabu vyao kuhusu
Katuni. Wanafunzi wamsikilize mwalimu kwa makini. Mwalimu ahakikishe kuwa
anasoma hadithi hiyo kwa matamshi sahihi, kwa ufasaha na kwa sauti ya kusikika
na kuvutia. Baada ya mwalimu kuisoma hadithi hiyo, wanafunzi wapewe fursa
ya kuisoma wakiwa wawili wawili kisha mmoja mmoja. Mwalimu ahakikishe
anakosoa makosa yoyote ya kimatamshi pindi tu yanapotokea. Usomaji wa kila
mwanafunzi peke yake utakuza stadi ya kusoma kwa kila mwanafunzi pamoja
na kuwapa ujasiri wa kuzungumza mbele ya watu. Kupitia kwa zoezi hili, ni
rahisi kwa mwalimu kufahamu matatizo ya kila mwanafunzi kibinafsi. Kila
mwanafunzi asaidiwe kibinafsi.
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi walielewa hadithi waliyosoma, mwalimu
awashirikishe katika makundi yao kujibu maswali waliyopewa katika vitabu
vyao. Mwalimu azunguke darasani ili kuwasaidia wanafunzi wanaotatizika
katika makundi yao. Maswali hayo yanahusu hadithi waliyoisoma darasani.
Wanafunzi wanaotatizika wasaidiwe na mwalimu.
198
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi bunifu
hasa katika muktadha wa shughuli za dukani. Pia, mwalimu achunguze iwapo
wanafunzi wamepata ufahamu wa kusoma hadithi na kuweza kujibu maswali ya
hadithi hiyo kwa usahihi kulingana na muktadha wa hadithi hiyo.
VI. Majibu
Maswali ya mchoro, ukurasa 111
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanachoona kwenye
mchoro waliopewa, kwa mfano:
1. Ninaona muuzaji akiwa dukani.
2. Muuzaji anapanga bidhaa za kuuza katika duka lake.
3. Hapa ni dukani.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali ya hadithi, ukurasa 111
1. Mama yake.
2. Katuni alitumwa sukari kilo moja na mkate mmoja.
3. Katuni alitumwa dukani.
4. Bidhaa zilikuwa za shilingi mia moja na hamsini.
5. Katuni alisahau pesa nyumbani.
6. Katuni aliogopa mama angekasirika kwa kusahau pesa nyumbani
hivyo angerudi nyumbani bila bidhaa alizokuwa ametumwa. Huenda
mama angemwadhibu.
199
Mada Ndogo 4: Kuandika
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi
ya uandishi;
b) Kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
Mwanafunzi aeleze yaliyo muhimu katika uandishi k.v. mwandiko nadhifu,
maudhui, mtiririko n.k.
Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwalimu.
Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.
Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa kama hiki
kifuate hatua tano za uandishi: maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo,
uhariri na uchapishaji. Vichwa vya visa vinaweza kutofautiana.
III. Nyenzo:
Hadithi bunifu zilizoandikwa kwenye chati kuhusu shughuli za dukani;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Rekodi za hadithi za kubuni kuhusu shughuli za dukani;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 112-113;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kukuza stadi ya mwanafunzi ya kuandika. Katika mada
hii, wanafunzi watapata maarifa ya kubuni na kuandika visa vifupi vifupi kwa
200
kuzingatia mambo kadhaa kama vile: mwandiko nadhifu, maudhui, mtiririko,
uhariri, marejeleo na maandalizi mengine kabambe. Shughuli hii itawawezesha
wanafunzi kufahamu jinsi ya kuandika visa bunifu katika muktadha wowote.
Muktadha wa uandishi katika mada hii ni kuhusu shughuli za dukani. Mwalimu
ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili
kama vilivyoorodheshwa hapo juu ili kufanikisha ufundishaji wake pamoja na
ujifundishaji wa wanafunzi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika lililotolewa kwenye vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
kusoma hadithi bunifu katika muktadha wa shughuli za dukani. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi kusahihisha zoezi walilopewa katika funzo
la hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kuandika na hata kubuni hadithi na kuiandika kwa hati nadhifu katika
madaftari yao. Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi
watatu watatu kisha awaombe watazame michoro ya pesa za kiwango tofauti
tofauti waliyopewa katika vitabu vyao. Wanafunzi katika makundi yao watazame
michoro hiyo na kuijadili. Kila mwanafunzi apewe fursa ya kutambua idadi ya
pesa katika michoro husika. Mwalimu anaweza kuwachangamsha wanafunzi
kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na michoro husika kama vile: Unaona
nini katika michoro hii? Hizi ni pesa ngapi? Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu
kulingana na wanachoona katika michoro husika. Wanafunzi waelezane iwapo
wamewahi kuziona pesa za Kenya kwa macho yao na iwapo wamewahi
201
kuzigusa. Pia, wanafunzi waelezane kiasi cha pesa ambacho wamewahi kuona,
kugusa na hata kutumia.
Baada ya shughuli hii ya kujadili michoro husika, mwalimu awaelekeze wanafunzi
katika makundi yao kujibu maswali waliyopewa katika vitabu vyao kuhusiana
na michoro waliyoitazama. Wanafunzi wafanye zoezi hili katika madaftari
yao. Mwalimu azunguke darasani akiwasaidia wanafunzi wanaotatizika katika
makundi yao.
Wanafunzi wakikamilisha majadiliano yao katika makundi pamoja na kufanya
zoezi walilopewa katika vitabu vyao, mwalimu awashirikishe kuchunguza hadithi
waliyopewa yenye mapengo. Hadithi hii ina majibu kwenye mabano, hivyo
mwanafunzi anastahili kuisoma, kuielewa kisha kujaza mapengo yaliyopo kwa
kuteua jibu mwafaka kutoka kwa yaliyo kwenye mabano. Wanafunzi wafanye
zoezi hili katika madaftari yao.
Hatimaye, mwalimu awasomee wanafunzi hadithi iliyo katika vitabu vyao
kumhusu Sabina. Wanafunzi wamsikilize mwalimu wao kwa makini sana. Iwapo
mwalimu ana matatizo ya kimatamshi, basi anaweza kumwalika msomaji stadi
akawasomea wanafunzi hadithi hiyo. Baada ya kuwasomea wanafunzi hadithi
hiyo, mwalimu awaombe wanafunzi waisome hadithi yenyewe wakiwa wawili
wawili kisha kila mwanafunzi atapewa fursa ya kusimama mbele ya wanafunzi
wenzake darasani na kuisoma peke yake. Mwalimu ahakikishe anasahihisha
makosa ya kimatamshi pindi tu yanapotokea. Shughuli hii ya kila mwanafunzi
kusoma peke yake ni njia mwafaka ya kuukuza ujasiri wa wanafunzi kusimama
na kuzungumza mbele ya watu. Pia, ni mbinu nzuri ya kukuza stadi ya kusoma
kwa kila mwanafunzi.
Baada ya kila mwanafunzi kusoma hadithi iliyopo, mwalimu amwombe kila
mwanafunzi aandike (anakili moja kwa moja) hadithi hiyo waliyosoma katika
madaftari yao. Mwalimu ahakikishe kuwa kila mwanafunzi anaandika kwa hati
nadhifu.
Mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wote wanahusika katika shughuli hii ya
kuandika hadithi waliyosoma. Mwalimu anaweza kuiandika hadithi yenyewe
ubaoni ili ionekane na wanafunzi wote. Pia, anaweza kuwa tayari ameiandika
202
hadithi hiyo kwenye chati ambazo anaweza kuzionyesha kwa wanafunzi kisha
wakanakili hadithi hiyo katika madaftari yao. Baada ya shughuli hii, mwalimu
ahakikishe amesahihisha madaftari ya wanafunzi ili kukosoa makosa yoyote
ya kimaendelezo na mwandiko usio nadhifu. Wanafunzi walio na matatizo ya
kuandika kwa mwandiko nadhifu wapewe mazoezi zaidi ya kuandika. Mwalimu
awaelekeze zaidi.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kuandika maelezo kwa hati nadhifu na
mtiririko unaofaa.
VI. Majibu
Maswali ya michoro, ukurasa 112
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanachoona kwenye
michoro waliyopewa, kwa mfano:
1. Ninaona pesa: sarafu na noti.
2. Ninaona shilingi tano, kumi, ishirini, hamsini, mia moja, mia mbili na
mia tano.
3. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
4. Baki yangu ni shilingi thelathini (30).
5. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Zoezi, ukurasa 112
Mama alinituma dukani kununua sukari kilo mbili. Nilimuuliza muuzaji bei
naye akasema ni shilingi hamsini pesa za Kenya. Nilimpa noti ya shilingi mia
moja, akanirudishia baki ya shilingi hamsini.
Zoezi la kusoma na kuandika, ukurasa 113
Mwalimu atathmini usomaji na uandishi wa wanafunzi wa hadithi waliyopewa
katika vitabu vyao.
203
Mada Ndogo 5: Saru: Matumizi ya alama ya kuuliza (?)
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua matumizi ya alama ya kuuliza (?) katika kuimarisha
mawasiliano;
b) Kusoma sentensi zilizo na matumizi ya alama ya kuuliza (?) katika
kuimarisha stadi ya kusoma;
ch) Kuandika sentensi akitumia alama ya kuuliza (?) katika kuimarisha stadi
ya kuandika;
d) Kuthamini matumizi ya alama ya kuuliza (?) katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aandike alama ya kuuliza (?).
Mwanafunzi afafanue matumizi ya alama ya kuuliza (?).
Mwanafunzi atunge sentensi akitumia alama ya kuuliza (?).
Mwanafunzi asome sentensi zilizo na alama ya kuuliza (?).
Wanafunzi waweza kushirikishwa kusoma sentensi zinazotumia alama ya
kuuliza (?) wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
Mwanafunzi aandike sentensi akitumia alama ya kuuliza (?).
III. Nyenzo:
Chati zenye sentensi zilizotumia alama ya kuuliza (?);
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 113-115;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
204
IV. Maandalizi ya somo
Katika sehemu hii, mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla
ya vipindi hivi kama vilivyotajwa hapo awali. Wanafunzi wanaweza kutumiwa
katika funzo hili ili kuonyesha matumizi ya alama ya kuuliza kupitia kwa wao
wenyewe kuulizana maswali na kuyajibu au kupitia kwa mwalimu kuwauliza
maswali nao kuyajibu. Shughuli hii ya kuulizana maswali na kuyajibu itawasaidia
wanafunzi kubaini matumizi ya alama ya kuuliza.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara katika ufundishaji wake. Ikiwa kuna wanafunzi
wasioweza kuona, mwalimu ajitahidi kuandaa maelezo yake kwenye breli ili
kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha kama wanafunzi wengine.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi katika vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu aanze funzo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia kuhusiana na
shughuli za dukani. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu kisha wajibu maswali
waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi
walilopewa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wenye matatizo wasaidiwe.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili
kisha awashirikishe katika kuchunguza na kusoma mazungumzo yaliyo katika
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 113-114 kati ya Feni na Rubi. Mwalimu
awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali kuhusiana na mazungumzo
hayo kama vile: Feni anasema nini katika mazungumzo haya? Rubi anasema nini
katika mazungumzo haya? Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na
mazungumzo waliyosoma katika vitabu vyao. Wanafunzi waelekezwe kusoma
sentensi zifuatazo na kuzitofautisha kwa kurejelea kiimbo chake:
205
Unaitwa nani.
Unaitwa nani?
Katika hatua hii, wanafunzi watapata fursa ya kufahamu kuwa kila swali ambalo
mtu huuliza hutumia alama ya kuuliza mwishoni mwake. Mwalimu awaelekeze
wanafunzi kuandika alama ya kuuliza kwa usahihi. Wanafunzi waandike alama
hii katika makundi yao kisha kila mmoja aiandike ubaoni huku wanafunzi
wengine wakikosoa palipo na kosa.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awaelekeze wanafunzi kufahamu matumizi
ya alama ya kuuliza katika mawasiliano. Wanafunzi wafahamu kuwa alama ya
kuuliza huwekwa mwishoni mwa sentensi ili kuuliza swali. Alama ya kuuliza ni
mojawapo ya alama za uakifishaji katika lugha.
Wanafunzi washirikishwe kufanya zoezi la kusoma sentensi ambazo ni maswali
kisha watoe majibu ya maswali hayo. Kila mwanafunzi ashirikishwe katika zoezi
hili. Wanafunzi wanaweza kuelekezwa kubuni maswali yao wenyewe na kuulizana
katika makundi yao. Wanafunzi waandike maswali haya katika madaftari yao ili
alama ya kuuliza ijitokeze vyema. Mifano ya maswali wanayoweza kuulizana ni
kama vile:
1. Unapenda kula nini?
2. Kwa nini unapenda kusoma?
3. Wewe hulala saa ngapi?
4. Unaishi wapi?
5. Ulikula nini leo asubuhi?
Wanafunzi wafanye mazoezi kadhaa kuhusiana na matumizi ya alama ya
kuuliza. Wanafunzi waulizane maswali na kuyajibu pamoja na kuyaandika katika
madaftari yao. Pia, mwanafunzi mmoja anaweza kusimama mbele ya darasa na
kuwauliza wanafunzi wenzake maswali mbalimbali kwa kuyaandika ubaoni nao
wakayajibu.
Hatimaye, wanafunzi washirikishwe kufanya zoezi lililo katika vitabu vyao.
206
(ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa katika kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana
kwa kutumia alama ya kuuliza swali. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wanaweza kutunga sentensi sahihi na kuziandika kwa kutumia alama ya kuuliza
swali.
VI. Majibu
Zoezi la kusoma, ukurasa 113-114
Mwalimu atathmini usomaji wa wanafunzi ili kubaini matumizi ya alama ya
kuuliza. Kiimbo cha kuuliza maswali kizingatiwe.
Zoezi, ukurasa 115
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
207
Matokeo maalum
yanayotarajiwa
Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kukia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutaja majina ya ndege
mbalimbali ili kuimarisha stadi
ya kuzungumza;
(b) Kutaja aina za ndege wa
nyumbani anaowajua ili kujenga
stadi ya kuzungumza;
(ch) Kutambua msamiati uliotumiwa
katika hadithi aliyosoma au
kusomewa ili kuimarisha
ufahamu;
(d) Kuandika kisa kifupi kwa hati
nadhifu kulingana na mada ili
kujenga stadi ya uandishi;
(e) Kutambua matumizi ya juu
ya na chini ya ili kuimarisha
mawasiliano.
Mwanafunzi atazame picha
za kuwatambua ndege tofauti
tofauti.
Mwanafunzi ataje aina za ndege
anaowajua.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi apewe hadithi
yenye mapengo ajaze kwa
maneno mwafaka.
Mwanafunzi asome sentensi
zinazodhihirisha matumizi ya
juu ya na chini ya.
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kazi ya vikundi.
Kushiriki katika vyama vya ushirika.
Mada Kuu 8: NDEGE NIMPENDAYE
(Idadi ya vipindi: 13)
Sura ya
8
208
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Mazingira na somo la Kiingereza.
Nyenzo:
Picha au michoro ya aina mbalimbali za ndege;
Kadi zenye majina ya aina mbalimbali za ndege;
Ndege halisi kama vile: kuku;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 116-127;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Katika mada hii, wanafunzi wataweza kupata ufahamu wa aina mbalimbali za
ndege pamoja na majina yao na tabia zao, kusimulia masimulizi yanayohusisha
aina mbalimbali za ndege, kusoma hadithi kuhusu aina mbalimbali za ndege
pamoja na kubuni visa vifupi vifupi vinavyohusu aina mbalimbali za ndege. Kila
mwanafunzi atapata fursa ya kueleza kuhusu ndege anayempenda kwa kutoa
sababu za uteuzi wa ndege huyo.
Pia, mada hii inalenga kumhami mwanafunzi na maarifa ya kipengele cha sarufi
kuhusu matumizi ya juu ya na chini ya katika kuimarisha mawasiliano.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
Elimu ya maendeleo endelevu; maslahi ya wanyama, kujali na kutunza
ndege,
Utangamano wa kijamii,
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii kuhusu aina mbalimbali za ndege ni kama vile:
Msamiati Maana
1.
kuku
ndege wa nyumbani anayetaga mayai na kuangua
vifaranga
2.
bata
ndege wa nyumbani au majini anayeangua viyoyo
209
3.
tausi
ndege aliye mrembo na mwenye maringo kuliko
ndege wote
4.
kiyoyo
mtoto wa bata
5.
kifaranga
mtoto wa kuku
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Mwalimu ahakikishe kuwa ana vifaa muhimu na maalum vya kuwasaidia
wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali ili kuweza kuwashirikisha
katika ujifundishaji wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu
anaweza kuhusisha matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza
kuwahusisha watafsiri wa lugha ya ishara.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kuona, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya breli pamoja na vifaa vya kunasia sauti.
Haya yatawawezesha wanafunzi hawa kusoma kama wanafunzi wenzao bila
vizuizi vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada
Idadi ya vipindi
Mada Ndogo 1: Msamiati
3
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 4: Kuandika
3
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya juu ya na chini ya
2
JUMLA: 13
Mada Ndogo 1: Msamiati wa ndege mbalimbali
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutaja majina ya ndege mbalimbali ili kuimarisha stadi ya kuzungumza;
b) Kutambua msamiati unaotumiwa katika kutunza ndege ili kuimarisha
mawasiliano;
210
ch) Kutumia majina ya ndege katika sentensi sahihi ili kuwezesha
mazungumzo;
d) Kutumia msamiati wa kutunza ndege katika sentensi ili kuwezesha
mazungumzo;
e) Kusoma maneno na sentensi kuhusu ndege ampendaye ili kujenga
usomaji bora;
f) Kuandika maneno na sentensi kuhusu ndege ampendaye ili kujenga
uandishi bora;
g) Kuthamini utunzaji wa ndege ampendaye.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atazame picha za kuwatambua ndege tofauti tofauti.
Mwanafunzi atunge sentensi sahihi kwa kutumia msamiati kuhusu ndege.
Mwanafunzi atoe maana ya msamiati unaotumiwa katika kutunza ndege.
Mwanafunzi achore baadhi ya ndege.
Mwanafunzi aweza kutazama video ya utunzaji wa ndege.
Mwanafunzi atazame michoro na picha za ndege wa nyumbani
wakitunzwa.
Mwanafunzi asome maneno na sentensi katika kadi na chati kuhusu
ndege.
Mwanafunzi aandike majina na sentensi kuhusu ndege.
III. Nyenzo:
Michoro na picha za aina mbalimbali za ndege;
Kadi zenye majina ya aina mbalimbali za ndege;
Ndege halisi kama vile: kuku;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 118-119;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Mwalimu ajiandae kufundisha somo hili kwa njia ambayo itawawezesha
wanafunzi kufahamu kuwa ndege ni viumbe wenye uhai ambao wana mbawa na
211
uwezo wa kupaa angani na hutaga mayai. Kuna ndege wanaofugwa nyumbani
na ndege wanaoishi porini.
Mwalimu aandae funzo hili kwa namna ya kumwezesha kuwaelekeza wanafunzi
katika kutambua majina ya aina mbalimbali za ndege wa nyumbani na wa
porini. Vifaa vitakavyohitajika kama vile: michoro au picha za aina mbalimbali
za ndege, kadi zenye majina ya ndege mbalimbali pamoja na ndege halisi
kama vile kuku viandaliwe ili ufundishaji wa somo hili uwe rahisi. Vifaa hivyo
vionyeshwe hadharani kwa wakati unaofaa na ikiwa kuna wanafunzi wasioona
au wasiosikia, mwalimu awasaidie kwa kuhusisha matumizi ya breli na lugha
ishara.
Katika funzo hili, mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wamejigawa katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa
kwa kila zoezi linalohusika.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize funzo hili kwa kuwaamkia wanafunzi na kuwauliza maswali
mbalimbali kuhusu kipindi cha hapo awali kuhusu matumizi ya alama ya kuuliza.
Wanafunzi nao wajibu maamkuzi ya mwalimu na maswali waliyoulizwa kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichopita. Mwalimu awaongoze wanafunzi
kwa kusahihisha kazi iliyotolewa kama zoezi katika kipindi cha hapo awali.
Wanafunzi wasahihishe zoezi hilo na mwalimu atoe majibu sahihi kwa kutilia
mkazo pale ambapo wanafunzi wanatatizika.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne wanne na
awaombe watazame michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 116.
Wanafunzi wachunguze michoro hiyo ya aina mbalimbali za ndege. Mwalimu
awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na
michoro hiyo. Anaweza kuwauliza maswali kama vile: Unaona nini kwenye
michoro hii? Taja majina ya ndege unaowaona katika michoro hii n.k. Wanafunzi,
kwa upande wao, wajibu maswali ya mwalimu wao kwa kueleza aina za ndege
wanaowaona katika michoro waliyopewa. Kwa mfano: Ninawaona tausi; Ninaona
njiwa; Ninaona kuku; Ninaona bata; Ninaona kanga. Baada ya mwalimu kuridhika
kuwa wanafunzi wamechunguza michoro hiyo na kuifahamu, awashirikishe
katika kutaja aina nyingine za ndege; wa nyumbani na wa porini.
212
Baadaye, wanafunzi wote washirikishwe kujibu maswali waliyopewa katika vitabu
vyao kuhusiana michoro ya ndege waliyopewa.
Katika makundi yao, wanafunzi waelekezwe kusoma majina ya ndege mbalimbali
yaliyo kwenye kadi walizopewa kwenye vitabu vyao. Wanafunzi wasome majina
hayo kwa sauti na matamshi sahihi. Mwalimu ahakikishe anasahihisha makosa
ya kimatamshi pindi tu yanapotokea.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao
kutazama michoro mingine ya ndege iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa
118. Wanafunzi wachunguze michoro hii na kuitaja kwa majina yao sahihi. Kwa
mfano, mimi ninaona kasuku; mimi ninaona batamzinga; mimi ninaona kunguru;
mimi ninaona bundi. Mwalimu azunguke darasani kuhakikisha kuwa wanafunzi
wanataja majina sahihi ya ndege waliopewa katika michoro iliyopo. Baada ya
wanafunzi wote kufahamu majina ya ndege walio kwenye michoro iliyopo,
wajibu maswali waliyopewa kuhusiana na michoro husika.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao kujadiliana
kuhusu ndege mbalimbali wa nyumbani pamoja na wa porini. Wanafunzi
waeleze sifa za ndege hawa pamoja na faida zao kwa binadamu. Kwa mfano:
Ndege Faida
Kuku hutupatia mayai, nyama na manyoya
Bata hutupatia mayai, nyama na manyoya
Tausi hutupatia mayai, manyoya na kuvutia watalii
Mwisho, kila mwanafunzi apewe fursa ya kueleza kuhusu ndege anayempenda,
sifa na tabia za ndege huyo, faida za ndege huyo pamoja na anavyoonekana
ndege huyo na makao yake. Ikiwezekana kila mwanafunzi amchore ndege
anayempenda katika daftari lake. Mwalimu asahihishe kazi za wanafunzi.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kutaja aina mbalimbali za ndege (wa nyumbani na wa
porini) pamoja na kueleza sifa zao, tabia zao, maumbile yao na faida zao. Kando
na kujua aina mbalimbali za ndege, kila mwanafunzi aweze kueleza na kuchora
ndege anayempenda.
213
Majibu
Maswali ya utangulizi, ukurasa 116-117
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na ndege
wanaowaona kwenye michoro waliyopewa.
2. Tausi, njiwa kuku, bata na kanga.
3. Njiwa, kuku, bata na kanga.
4. Bata.
5. Tausi, njiwa na kanga.
Zoezi, ukurasa 118
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi katika makundi yao.
Maswali ya michoro, ukurasa 119
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na ndege
wanaowaona kwenye michoro waliyopewa.
2. Kunguru, bundi, kasuku na batamzinga.
3. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Zoezi la makundi, ukurasa 119
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano:
1. Ndege wa nyumbani ni kama vile: kuku, bata, njiwa, batamzinga n.k.
2. Ndege wa porini ni kama vile: kunguru, kasuku, tausi, bundi n.k.
3. Ndege wa majini ni kama vile: bata, heroe n.k.
214
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutaja aina za ndege wa nyumbani anaowajua ili kujenga stadi ya
kuzungumza;
b) Kumtambua ndege ampendaye ili kujenga stadi ya kuzungumza;
ch) Kusimulia kuhusu ndege ampendaye ili kujenga stadi ya kuzungumza;
d) Kusimulia kuhusu jinsi anavyomtunza ndege ampendaye ili kujenga stadi
ya kuzungumza;
e) Kusikiliza kwa makini masimulizi kuhusu utunzaji wa ndege wa nyumbani
ili kujenga usikivu;
f) Kuthamini ndege wa nyumbani.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ataje aina za ndege anaowajua.
Mwanafunzi atambue ndege ampendaye.
Mwanafunzi asimulie kuhusu ndege ampendaye katika darasa zima,
wakiwa wawili wawili na katika vikundi.
Mwanafunzi atazame picha za ndege mbalimbali wa nyumbani ili
awatambue.
Mwanafunzi aweza kutazama video na picha zinazoashiria utunzaji wa
ndege mbalimbali.
Mwanafunzi asimulie jinsi ya kutunza ndege kupitia kwa mgeni mwalikwa.
Wanafunzi washiriki katika mjadala kuhusu jinsi wanavyowatunza ndege
wawapendao.
Wanafunzi waweza kushirikishwa katika kuimba nyimbo na kukariri mashairi
kuhusu ndege wawapendao.
III. Nyenzo:
Rekodi za masimulizi bunifu kuhusu aina mbalimbali za ndege;
Michoro au picha za masimulizi bunifu kuhusu aina mbalimbali za ndege;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Wanafunzi wenyewe;
215
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 119-121;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusoma masimulizi bunifu
yanayohusu aina mbalimbali za ndege pamoja na kusimuliana kuhusu ndege
mbalimbali katika makundi ili kujenga stadi yao ya kusikiliza na kuzungumza.
Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo
hili kama vilivyotajwa hapo juu ili kufanikisha ufundishaji wake na ujifundishaji
wa wanafunzi. Mwalimu anaweza kutayarisha masimulizi bunifu kuhusu aina
mbalimbali za ndege ambayo atawasomea wanafunzi darasani na mengine
watajisomea wenyewe katika makundi kisha kila mmoja mmoja. Mwalimu
anaweza kumwalika mtambaji, au msimulizi akawasomea wanafunzi masimulizi
bunifu kisha wanafunzi wakasoma baada yake katika makundi na hatimaye kila
mmoja mmoja. Mwalimu ahakikishe kuwa msimulizi mwalikwa ana uwezo wa
kusoma kwa sauti ya kusikika na kuvutia na kwa matamshi sahihi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika kama lilivyotolewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
msamiati wa aina mbalimbali za ndege. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu
pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili wasaidiwe
na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza masimulizi bunifu pamoja na ya kuzungumza. Mwalimu
awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha awaombe
watazame mchoro ulio kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 119. Wanafunzi
216
wachunguze mchoro huo na kuujadili katika makundi yao wakielezana
wanachokiona. Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali mepesi
kuhusiana na mchoro huo kama vile: Unaona nini kwenye mchoro huu? Unaona
ndege yupi? Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu maswali
waliyoulizwa. Wanafunzi wanaweza kutoa majibu kama vile: Mimi ninaona
kuku waliofugwa. Mimi ninaona mayai. Mwalimu ahakikishe amewashirikisha
wanafunzi wote katika majadilianohaya. Wanafunzi wajibu maswali waliyoulizwa
kulingana na wanayoona katika mchoro waliopewa. Mwalimu awaelekeze
wanafunzi kufahamu kuwa kuku wakitunzwa vizuri huweza kumpatia binadamu
faida nyingi za kupata mayai mengi, makubwa na mazuri, nyama nzuri na
vifaranga wengi wenye afya. Mwalimu awashirikishe wanafunzi kujadiliana
kuhusu njia mbalimbali za kuwatunza kuku. Kila mwanafunzi apewe fursa ya
kusimulia katika makundi yao na hata mbele ya darasa zima.
Baada ya shughuli hii, mwalimu anaweza kuwasomea wanafunzi masimulizi
yoyote bunifu (aliyoandaa mapema) kuhusiana na utunzaji wa kuku nyumbani.
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa makini. Pia, mwalimu
ahakikishe kuwa anasoma kwa ufasaha, kwa matamshi sahihi na sauti ya
kusikika na ya kuvutia.
Ili kukuza zaidi stadi ya wanafunzi ya kusikiliza na kuzungumza, mwalimu
awashirikishe wanafunzi katika makundi yao kutazama mchoro wa bata
na viyoyo wake ulio katika vitabu vyao na kuwaomba kuujadili. Wanafunzi
wasimuliane kuhusu wanayoyafahamu kumhusu bata, sifa zake, tabia zake,
makao yake, maumbile yake pamoja na faida zake kwa binadamu. Wanafunzi
washirikishwe kuyajibu maswali waliyopewa katika vitabu vyao kuhusiana ma
mchoro huo wa bata.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika kuwasimulia wenzake kuhusu
ndege wanaowapenda. Kila mwanafunzi apewe fursa ya kusimama mbele ya
darasa zima na kusimulia kuhusu ndege anayempenda kwa kujibu maswali
haya:
1. Ndege unayempenda ni yupi?
2. Ndege huyo ana rangi gani?
3. Ndege huyo hula nini?
4. Kwa nini unampenda ndege huyo?
5. Ndege huyo anakupa faida gani?
217
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii ya
masimulizi kuhusu ndege wanaowapenda. Shughuli hii ya wanafunzi kusimama
na kuzungumza mbele ya wanafunzi wengine ni mbinu bora ya kukuza ujasiri
wa wanafunzi wa kuzungumza mbele ya watu pamoja na kukuza stadi yao ya
kusikiliza na kuzungumza. Mwalimu ahakikishe anakosoa makosa ya kimatamshi
pindi tu yanapotokea. Wanafunzi wanaotatizika wasaidiwe na mwalimu.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya kuchunguza
iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusimulia masimulizi bunifu hasa kuhusu
muktadha wa aina mbalimbali za ndege wanaowapenda. Pia, mwalimu achunguze
iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa utunzaji wa aina mbalimbali za ndege
pamoja na faida za ndege hao kwa binadamu.
VI. Majibu
Majibu ya utangulizi, ukurasa 120
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoyaona katika
mchoro waliopewa, kwa mfano:
1. Ninaona kuku waliofugwa.
2. Kuku
3. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu jinsi wanavyotunza
ndege wawapendao.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
218
Zoezi la makundi, ukurasa 120
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoyaona
katika mchoro waliopewa, kwa mfano: ninaona bata na viyoyo wake.
2. Mayai, nyama, manyoya n.k.
3. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano: nafaka.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Zoezi, ukurasa 120-121
Mwalimu atathmini masimulizi ya wanafunzi katika makundi yao.
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati uliotumiwa katika hadithi aliyosoma au kusomewa ili
kuimarisha ufahamu;
b) Kusoma hadithi zinazohusu ndege wa nyumbani ili kujenga usomaji bora;
ch) Kusikiliza hadithi zikisomwa na mwalimu zinazohusu ndege wa nyumbani
ili kujenga usikivu;
d) Kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu ndege wanaofugwa
ili kupata ujumbe;
e) Kuchangamkia kusoma hadithi ili kuendeleza ari ya kusoma zaidi.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi.
219
Mwanafunzi ashiriki katika kusoma darasani, wakiwa wawili na baadaye
asome peke yake.
Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ya mwalimu au hadithi iliyorekodiwa.
Wanafunzi waweza kusomeana hadithi wakiwa wawili wawili au katika
vikundi.
Wanafunzi waweza kusoma hadithi kwa kutumia vifaa vya teknolojia k.v.
tarakilishi na projekta.
Mwanafunzi atunge sentensi akitumia msamiati uliotumiwa katika hadithi.
Mwanafunzi anakili majina na sentensi zinazojumuisha majina ya ndege.
Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kwa kutumia jitabu mbele ya darasa.
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kutokana na hadithi.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za hadithi bunifu kuhusu aina mbalimbali za ndege;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu aina mbalimbali za ndege;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu, projekta;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 121-123;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu katika muktadha wa aina mbalimbali za
ndege ili kujenga stadi ya wanafunzi ya kusikiliza pamoja na ya kusoma. Mwalimu
ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili kama
vilivyoorodheshwa hapo juu ili kufanikisha ufundishaji wake. Mwalimu anaweza
kuandaa mapema hadithi za kubuni kuhusu aina mbalimbali za ndege ambazo
atawasomea wanafunzi darasani na nyingine ambazo watajisomea wenyewe.
Mwalimu anaweza kumhusisha mtambaji, msimulizi au msomaji mashuhuri
akawasomea wanafunzi hadithi bunifu hizo kisha wanafunzi wakasoma baada
yake wakiwa wawili wawili hadi mmoja mmoja. Sharti msimulizi mwalikwa awe
na uwezo wa kusoma kwa sauti ya kusikika, ya kuvutia na kwa matamshi sahihi
na kwa ufasaha. Mwalimu anaweza kuzirekodi hadithi za kubuni kuhusu aina
mbalimbali za ndege kwenye tarakilishi au projekta na wanafunzi wakazisoma
wenyewe katika makundi kisha mmoja mmoja.
220
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia
kuhusu masimulizi yanayohusu aina mbalimbali za ndege. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
funzo la hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao
ya kusikiliza pamoja na ya kusoma hadithi bunifu hasa katika muktadha wa
aina mbalimbali za ndege. Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi
ya wanafunzi watatu watatu kisha awaombe watazame michoro waliyopewa
kwenye vitabu vyao pamoja na kusoma vifungu vifupi vifupi vinavyoambatana
na michoro hiyo. Michoro hii ni ya aina mbalimbali za ndege mbalimbali.
Wanafunzi wachunguze michoro hiyo na kuijadili katika makundi yao pamoja
na kusoma vifungu walivyopewa baada ya kila mchoro. Mwalimu anaweza
kuwasomea wanafunzi vifungu hivyo kisha wakasoma baada yake. Mwalimu
ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii ya kusoma
vifungu husika. Wanafunzi wasome vifungu hivyo wakiwa watatu watatu, wawili
wawili na hatimaye mmoja mmoja. Makosa ya kimatamshi yakosolewe pindi tu
yanapotokea.
Baada ya shughuli hii ya kuchunguza michoro iliyopo na kusoma vifungu
vilivyoambatanishwa nayo, mwalimu anaweza kuwasomea wanafunzi hadithi
yoyote bunifu katika muktadha wa aina mbalimbali za ndege. Mwalimu
ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa makini. Pia, mwalimu ahakikishe
kuwa anasoma hadithi hiyo kwa matamshi sahihi, kwa ufasaha na kwa sauti ya
kusikika na kuvutia.
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi walisikiliza hadithi ya mwalimu kwa makini,
mwalimu anaweza kuwauliza maswali kutokana na hadithi hiyo. Wanafunzi
221
wajibu maswali haya katika makundi yao. Mwalimu azunguke darasani ili
kuwasaidia wanafunzi wanaotatizika katika makundi yao.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi za
kubuni. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa
kusoma au kusikiliza hadithi na kuweza kujibu maswali ya hadithi hiyo kwa
usahihi kulingana na muktadha wa hadithi hiyo. Wanafunzi pia wawe wamepata
ufahamu wa tabia na sifa za aina mbalimbali za ndege.
VI. Majibu
Maswali ya michoro, ukurasa 123
1. Mtoto wa kuku ni kifaranga.
2. Mtoto wa bata ni kiyoyo.
3. Ndege maridadi sana ni tausi.
4. Ndege anayependa kucheza kwenye matope ni bata.
5. Ndege wa majini ni bata.
Mada Ndogo 4: Kuandika
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
a) Kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi
ya uandishi;
b) Kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
Mwanafunzi aelezee yaliyo muhimu katika uandishi k.v. mwandiko nadhifu,
maudhui, mtiririko n.k.
Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwalimu.
Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.
222
Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa kama hiki
kifuate hatua tano za uandishi: maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo,
uhariri na uchapishaji. Vichwa vya visa vinaweza kutofautiana.
III. Nyenzo:
Hadithi bunifu kuhusu aina za ndege zilizoandikwa kwenye chati;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu aina za ndege mbalimbali;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 123-125;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
III. Maandalizi ya somo
Lengo kuu la somo hili ni kukuza stadi ya mwanafunzi ya kuandika kwa
mwandiko nadhifu. Katika somo hili, wanafunzi watapata maarifa ya kubuni na
kuandika visa vifupi vifupi kwa kuzingatia mambo kadhaa kama vile: hati nadhifu,
mtiririko, uhariri, marejeleo, nakala safi na maandalizi mengine. Shughuli hii
itawawezesha wanafunzi kufahamu jinsi ya kuandika visa mbalimbali bunifu.
Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo
hili kama vilivyoorodheshwa hapo juu. Hili litamsaidia kufanikisha ufundishaji
wake pamoja na ujifundishaji wa wanafunzi.
Katika kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila
zoezi husika lililotolewa kwenye vitabu vyao.
IV. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
kusoma hadithi bunifu zinazohusu aina mbalimbali za ndege. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wasahihishe zoezi walilopewa katika kipindi
cha hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji
wao, wasaidiwe na mwalimu.
223
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kubuni hadithi na kuandika nakala ya kwanza, kisha kuihariri na hatimaye
kuandika nakala safi katika madaftari yao. Nakala safi itazingatia mwandiko
nadhifu, mtiririko mwafaka pamoja na kuhaririwa ili kuondoa makosa ya
kimaendelezo na kisarufi. Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya
wanafunzi wawili wawili kisha awaombe watazame michoro miwili waliyopewa
katika vitabu vyao. Mchoro wa kwanza ni wa kitoweo cha kuku na mchoro
wa pili ni wa kuku aliyeatamia mayai. Mwalimu awaelekeze wanafunzi katika
makundi yao kujadiliana kuhusu michoro hiyo miwili kisha waandike katika
madaftari yao wanayoyaona. Wanafunzi waandike jinsi ya kuandaa kitoweo
cha kuku. Pia, wanafunzi katika makundi yao waandike kuhusu mchakato wa
jinsi kuku anavyotaga mayai, anayaatamia na hatimaye kuangua vifaranga.
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wote wanashirikishwa katika shughuli hii na
kuwa wanaandika maelezo yao kwa hati nadhifu na wanaepuka makosa ya
kimaendelezo na kisarufi.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awaelekeze wanafunzi kusoma hadithi
waliyopewa katika vitabu vyao inayohusu ndege wa nyumbani. Wanafunzi
wasome hadithi hii wakiwa wawili wawili na hatimaye kila mmoja mmoja. Baada
ya kusoma kwa usahihi, kila mwanafunzi anakili hadithi hii katika daftari lake. Kila
mwanafunzi ahakikishe ananakili hadithi hii kwa hati nadhifu. Mwalimu anaweza
kuiandika hadithi hii kwenye chati ambazo wanafunzi wanaweza kuzitazama
na kunakili hadithi kwenye madaftari yao. Kila mwanafunzi anaweza kupewa
fursa ya kuandika hadithi hii katika ubao ili kusaidia katika kusahihisha makosa
yoyote ya kimaendelezo na kisarufi. Mwalimu asahihishe kazi za wanafunzi.
Hatimaye, wanafunzi waelekezwe katika makundi yao kufanya zoezi la kujaza
mapengo ya hadithi kuhusu ndege waliyopewa katika kitabu chao. Wanafunzi
wanakili hadithi hiyo katika madaftari yao kwa hati nadhifu kisha wayajaze
mapengo hayo kwa majibu mwafaka kutoka kwa waliyopewa kwenye mabano.
Wanafunzi wote washirikishwe katika shughuli hii.
Mwisho, wanafunzi wakiwa wawili wawili, wabuni kisa kuhusu ndege wawapendao
na kukiandika katika madaftari yao kwa hati nadhifu. Mwalimu ahakikishe kuwa
kila mwanafunzi anabuni kisa kuhusu ndege ampendaye na kukiandika kwa
mhati nadhifu kwenye madaftari yao. Mwalimu awahusishe wanafunzi wote
katika shughuli hii ya kubuni kisa kuhusu ndege ampendaye.
224
Baada ya shughuli hii, mwalimu ahakikishe amesahihisha madaftari ya
wanafunzi ili kukosoa makosa yoyote ya kimaendelezo na mwandiko usio
nadhifu. Wanafunzi walio na matatizo ya kuandika kwa mwandiko nadhifu
wapewe mazoezi zaidi ya kuandika. Mwalimu awaelekeze zaidi.
Mwalimu anaweza kumwomba kila mwanafunzi aandike nakala yake safi ubaoni
(kuhusu ndege ampendaye) ili wanafunzi wenzake waisome na kuikosoa kwa
kurejelea mwandiko nadhifu, makosa ya kimaendelezo pamoja na ya kisarufi.
Pia, wanafunzi katika makundi yao wanaweza kusahihisha nakala zao safi.
Wanafunzi walio na matatizo wasaidiwe na mwalimu.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kubuni kisa katika muktadha wa ndege
ampendaye na kukiandika kwa mwandiko nadhifu. Pia, mwalimu achunguze
iwapo wanafunzi wamepata uelewa wa mambo muhimu ya kuzingatia katika
uandishi kama vile: mwandiko nadhifu, mtiririko, maudhui, nakala safi na uhariri.
VI. Majibu
Maswali ya michoro, ukurasa 123
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu wanachoona katika
michoro waliyopewa, kwa mfano: ninaona kitoweo cha kuku; ninaona
kuku akiatamia mayai.
2. Kuku
3. Kitoweo cha kuku na mayai
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu iwapo wamewahi
kula kitoweo cha kuku au mayai.
Zoezi, ukurasa 124
Ndege ni viumbe wenye mbawa. Mbawa hizi zinawasaidia kuruka angani.
Ndege wengine huishi porini. Wengine huishi nyumbani. Kila ndege ana
miguu miwili. Mdomo wa ndege unaitwa kidona. Ndege hutaga mayai. Watoto
wa ndege wakiwa wengi wanaitwa makinda. Watoto wa kuku wanaitwa
vifaranga. Ndege anayependa kula vifaranga wa kuku huitwa mwewe.
225
Zoezi la kubuni na kuandika, ukurasa 125
Mwalimu atathmini ubunifu na uandishi wa kila mwanafunzi kuhusu namna
ndege ampendaye.
Mada Ndogo 5: Saru: Matumizi ya ‘juu ya’ na ‘chini ya’
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua matumizi ya juu ya na chini ya ili kuimarisha mawasiliano;
b) Kutumia juu ya na chini ya katika sentensi kwa usahihi ili kuimarisha
mawasiliano;
ch) Kusoma sentensi zinazodhihirisha matumizi ya juu ya na chini ya ili
kuimarisha usomaji bora;
d) Kuandika sentensi zinazodhihirisha matumizi ya juu ya na chini ya ili
kuimarisha uandishi bora;
e) Kuchangamkia matumizi ya juu ya na chini ya katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome sentensi zinazodhihirisha matumizi ya juu ya na chini
ya.
Mwanafunzi atunge sentensi zinazorejelea vitu halisi darasani k.m. kitabu
kipo juu ya meza katika vikundi.
Mwanafunzi ashiriki katika kuigiza vitendo vinavyoonyesha juu ya na
chini ya.
Mwanafunzi aweza kukamilisha sentensi zinazodhihirisha matumizi ya juu
ya na chini ya kwa kurejelea michoro tofauti tofauti akiwa peke yake au
katika vikundi.
Mwanafunzi aweza kutumia tarakilishi kufanyia mazoezi ya matumizi ya
juu ya na chini ya.
226
III. Nyenzo:
Chati zenye sentensi zilizojumuisha matumizi ya juu ya na chini ya;
Michoro au picha zinazoonyesha matumizi ya juu ya na chini ya;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 125-127;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Kama tunavyofahamu, sarufi ni kipengele muhimu katika ujifundishaji wa
wanafunzi. Mwalimu anastahili kutilia maanani dhana hii ili kuweza kuwahusisha
wanafunzi kwa ukamilifu katika somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema
kama vilivyoorodheshwa hapo juu na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, mwalimu ajitahidi kuhusisha matumizi
ya breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha kama wanafunzi
wengine. Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia mwalimu anaweza
kuhusisha matumizi ya lugha ya ishara. Mwalimu anaweza pia kumshirikisha
mtaalamu wa lugha ya ishara katika kuwasaidia wanafunzi hawa.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu anashauriwa kuwagawa
wanafunzi katika makundi yanayotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa
kwa kila shughuli ya wanafunzi katika Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu awasalimie wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia kuhusu kubuni kisa (kuhusu
ndege wawapendao) na kukiandika kwa mwandiko nadhifu. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe
wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi waliopata matatizo katika kufanya zoezi hilo wasaidiwe na mwalimu.
227
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili
kisha awashirikishe katika kutazama michoro waliyopewa katika kitabu chao.
Wanafunzi wajadili michoro hiyo kwa kurejelea matumizi ya juu ya na chini
ya. Wanafunzi waelezane kuhusu vitu wanavyoona kwenye michoro iliyopo
na waeleze mahali vitu hivyo vilivyo. Wanafunzi wanaweza kutumia sentensi
walizopewa katika vitabu vyao ambazo ni:
1. Mpira uko juu ya meza.
2. Kiatu kiko chini ya meza.
3. Mwanafunzi yuko chini ya mti.
4. Ndege yuko juu ya mti.
5. Kofia iko juu ya meza.
6. Paka yuko chini ya kiti.
Mwalimu atathmini majadiliano ya wanafunzi katika makundi yao kwa
kurejelea michoro waliyopewa na matumizi ya juu ya na chini ya. Shughuli hii
itawawezesha wanafunzi kufahamu matumizi kamili ya juu ya na chini ya.
Baada ya wanafunzi kujadili kuhusu michoro waliyopewa pamoja na sentensi
zao sahihi, mwalimu awashirikishe katika majadiliano zaidi kuhusiana na
matumizi ya juu ya na chini ya.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao
waigize vitendo walivyopewa katika vitabu vyao ambavyo ni:
1. Weka chaki juu ya meza.
2. Weka kalamu chini ya dawati.
3. Weka mkoba juu ya kiti.
4. Mtoe paka chini ya kabati.
5. Tazama juu ya mti.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika maigizo haya.
Wanafunzi waigize jinsi ya kutenda vitendo walivyoelekezwa kutenda ili
kuimarisha ufahamu wao wa matumizi ya juu ya na chini ya.
228
Mwalimu awaelekeze wanafunzi katika kutunga sentensi sahihi kwa kutumia
juu ya na chini ya, kwa mfano:
1. Mpira uko juu ya dawati.
2. Wanafunzi wameketi chini ya mti.
3. Ndege anapaa juu ya nyumba yetu.
4. Kiatu kiko chini ya kitanda.
5. Kitabu kimewekwa juu ya meza ya mwalimu.
Wanafunzi waelekezwe kutambua kuwa juu ya na chini ya ni vihusishi yaani
ni maneno yanayoonyesha uhusiano wa vitu (nomino) zaidi ya kimoja, kwa
mfano: kitabu kiko juu ya meza; juu ya inaonyesha uhusiano wa kitabu na
meza’. Mwalimu ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote katika shughuli
hii ya kutunga sentensi sahihi kwa kutumia juu ya na chini ya.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kufanya mazoezi
waliyopewa katika vitabu vyao kuhusu matumizi ya juu ya na chini ya. Mwalimu
awasaidie wanafunzi wanaotatizika katika kufanya mazoezi haya.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa katika kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana
kwa kutumia juu ya na chini ya. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wanaweza kutunga sentensi sahihi katika kwa kutumia vihusishi ambavyo ni:
juu ya na chini ya.
VI. Majibu
Zoezi la maigizo, ukurasa 126
Mwalimu atathmini maigizo ya wanafunzi.
229
Zoezi, ukurasa 127
1. Toa kalamu chini ya meza uiweke juu ya meza.
2. Tunda limetoka juu ya mti likaanguka chini ya mti.
3. Kikombe cha chai kiko juu ya meza si chini ya meza.
4. Kitabu kilichokuwa juu ya kitanda kimeanguka chini ya kitanda.
230
Matokeo maalum
yanayotarajiwa
Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutambua msamiati
unaohusiana na shughuli
za sokoni ili kuimarisha
mawasiliano;
(b) Kutaja vitu vinavyopatikana
sokoni katika kuendeleza
mazungumzo;
(ch) Kutambua msamiati uliotumiwa
katika hadithi ili kuwezesha
ufahamu;
(d) Kuandika kisa kifupi kwa hati
nadhifu kulingana na mada ili
kujenga stadi ya uandishi;
(e) Kutambua matumizi ya ndani
ya na nje ya ili kuimarisha
mawasiliano.
Mwanafunzi asome maneno
kuhusu soko kwenye kadi na
chati.
Mwanafunzi ataje vitu
vipatikanavyo sokoni k.v.
mkokoteni, vibanda, risiti, bidhaa
na ratili.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi apewe hadithi
yenye mapengo ajaze kwa
maneno mwafaka.
Mwanafunzi asome sentensi
zinazodhihirisha matumizi ya
ndani ya na nje ya.
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kazi ya vikundi.
Kushiriki katika kuigiza shughuli za sokoni.
Mada Kuu 9: SOKONI
Idadi ya vipindi: 13
Sura ya
9
231
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Hisabati, somo la Kiingereza, somo la Mazingira pamoja na somo
kuhusu lugha za kiasili.
Nyenzo:
Michoro au picha zinazoonyesha mazingira ya sokoni;
Kadi zenye msamiati wa sokoni;
Chati zenye msamiati na sentensi kuhusu msamiati wa sokoni;
Rekodi za hadithi au masimulizi bunifu kuhusu sokoni;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 128-137;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Mada hii itashughulikia msamiati wa sokoni pamoja na matumizi yake
katika sentensi na mawasiliano kwa jumla. Kutokana na mada hii, wanafunzi
watafahamu msamiati mbalimbali wa sokoni ambao wanaweza kuutumia
katika mawasiliano yao. Wanafunzi watafahamu shughuli mbalimbali za sokoni
pamoja na umuhimu wa shughuli hizi kwa binadamu.
Pia, kipengele cha masimulizi na hadithi bunifu zinazohusisha msamiati wa
sokoni na shughuli mbalimbali za sokoni zitafundishwa hapa. Masimulizi na
hadithi za kuvutia na zenye msamiati wa kiwango cha wanafunzi wa gredi hii
zibuniwe ili kuwafaa wanafunzi katika ujifundishaji wao.
Pia, mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kufahamu sarufi ya matumizi ya
ndani ya na nje ya katika sentensi na mawasiliano kwa jumla.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
Elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya masuala ya kifedha kujadili
umuhimu wa sokoni.
Uraia - kushirikiana katika vikundi.
Utangamano wa kijamii.
232
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii kuhusu msamiati wa sokoni na shughuli za sokoni ni kama vile:
Msamiati Maana
1.
mkokoteni
kijigari cha kubururwa cha kubebea mizigo
2.
risiti
kijikaratasi maalum cha kuonyesha malipo ya bidhaa
au huduma
3.
bidhaa
vitu vinavyouzwa
4.
mnunuzi
mtu ambaye ananunua bidhaa
5.
mwuzaji
mtu ambaye anauza bidhaa
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Katika ufundishaji wa mada hii, mwalimu ahakikishe kuwa ana vifaa muhimu na
maalum vya kuwasaidia wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali ili
kuweza kuwashirikisha katika ujifundishaji wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo
wa kuona, mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya breli pamoja na vifaa vya
kunasia sauti.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri
wa lugha ya ishara.
Vifaa hivi vitawawezesha wanafunzi wa aina hii kusoma kama wanafunzi wenzao
bila vikwazo vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada
Idadi ya
vipindi
Mada Ndogo 1: Msamiati
3
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 4: Kuandika
3
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya ndani ya na nje ya
2
JUMLA: 13
233
Mada Ndogo 1: Msamiati wa sokoni
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati unaohusiana na shughuli za sokoni ili kuimarisha
mawasiliano;
b) Kusoma msamiati wa sokoni ili kujenga usomaji bora;
ch) Kufahamu maana ya msamiati unaotumiwa sokoni ili kuwezesha
mawasiliano;
d) Kutunga sentensi akitumia msamiati wa sokoni ili kuimarisha
mawasiliano;
e) Kuandika maneno na sentensi akitumia msamiati wa sokoni ili
kuimarisha stadi ya kuandika;
f) Kuthamini shughuli za sokoni.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome maneno kuhusu soko kwenye kadi na chati.
Mwanafunzi afafanue maana ya msamiati wa sokoni k.v. mkokoteni,
vibanda, risiti, dalali, mnunuzi, mwuzaji, mchuuzi n.k.
Mwanafunzi achore vitu vipatikanavyo sokoni.
Mwanafunzi anaweza kutazama picha au video za vitu vya sokoni
zikiambatanishwa na sauti na maneno.
Mwanafunzi aambatanishe majina na vitu vipatikanavyo sokoni.
Mwanafunzi anaweza kujaza nafasi wazi katika sentensi kwa maneno
yanayotumiwa sokoni.
Mwanafunzi anakili msamiati kuhusu shughuli za sokoni.
Mwanafunzi atunge sentensi akitumia msamiati kuhusu shughuli za sokoni.
III. Nyenzo:
Kadi zenye msamiati wa sokoni;
Chati zenye msamiati wa sokoni;
234
Bidhaa halisi za sokoni;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 129-131;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Mada hii inahusu msamiati wa sokoni kwa kurejelea shughuli mbalimbali za
sokoni. Shughuli za sokoni kama vile kununua na kuuza bidhaa mbalimbali ni
muhimu kwa binadamu. Hii ni kwa sababu kupitia kwa shughuli hizi, mnunuzi
huweza kupata chakula na bidhaa nyingine za matumizi yake na vilevile mwuzaji
huweza kujipatia riziki kwa kupata pesa za kukidhi mahitaji yake. Shughuli
za sokoni pia huimarisha utangamano wa wanajamii hivyo kuleta amani na
mahusiano katika jamii na taifa kwa jumla.
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama
vilivyotajwa hapo juu bila kusahau vyombo vingine maalum vya kuwasaidia
wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali kama vile breli, vinasasauti na mtafsiri
wa lugha ya ishara. Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati
mwafaka wa kuweka hadharani vifaa alivyovileta darasani. Mwalimu akumbuke
kuwa matumizi ya michoro, picha na vifaa halisi ni mbinu bora ambayo hutumika
kufanikisha ufundishaji wa wanafunzi.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi katika
vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize somo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichopita kuhusiana
na kipengele cha sarufi cha matumizi ya juu ya na chini ya. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
235
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne wanne kisha
awashirikishe katika kuchunguza mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi,
ukurasa 128. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali
mepesi kuhusiana na mchoro huo. Baadhi ya maswali ambayo mwalimu anaweza
kuuliza ni kama vile: Mnaona nani kwenye mchoro huu? Watu hawa wanaenda
wapi? Mwalimu awaelekeze wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo na
kufahamu kinachoendelea katika mchoro uliopo. Mchoro huu unaonyesha watu
wa rika mbalimbali wakienda sokoni pamoja na bidhaa mbalimbali za sokoni.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika shughuli hii ili waweze kutambua
mazingira ya sokoni.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika kuendeleza funzo hili kuhusu msamiati wa sokoni na shughuli za sokoni,
mwalimu awaelekeze wanafunzi katika makundi yao kutazama michoro iliyo
katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 129. Wanafunzi wajadili kuhusu michoro
hii katika makundi yao. Waelezane wanayoyaona. Mwalimu anaweza kuwauliza
wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro hiyo. Maswali kama vile:
Mnaona nini kwenye michoro hii? Watu hawa wanafanya nini? Wanafunzi wajibu
maswali ya mwalimu kwa kurejelea michoro waliyopewa. Michoro hii inaonyesha
mnunuzi na mwuzaji wakiwa sokoni pamoja na hamali wanaosukuma mkokoteni
uliobeba bidhaa. Baada ya mwalimu kuhakikisha kuwa wanafunzi wameielewa
michoro waliyopewa, awaelekeze kujibu maswali waliyopewa katika vitabu
vyao kuhusiana na michoro hiyo.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusoma kadi zenye
msamiati mbalimbali wa sokoni zilizo katika vitabu vyao. Wanafunzi wasome
msamiati huu wakiwa wawili wawili kisha kila mwanafunzi apewe fursa ya
kuusoma peke yake. Mwalimu ahakikishe anasahihisha makosa ya kimatamshi
pindi yanapotokea. Msamiati wa sokoni ni kama vile: mnunuzi, mwuzaji, risiti,
ratili, nunua, uza, mkokoteni, mteja, bidhaa, kilo, ratili n.k. Mwalimu ahakikishe
wanafunzi wanafahamu maana ya msamiati huu na hata kuweza kuutungia
sentensi sahihi.
236
Kwa mfano:
1. Mnunuzi amenunua bidhaa nyingi.
2. Mwuzaji atapata faida nyingi leo.
3. Mama alinituma sokoni nikanunue sukari kilo tatu.
4. Dada alipewa risiti baada ya kununua bidhaa alizotumwa.
5. Mwuzaji alitumia ratili kunipimia mchele kilo nne.
Hatimaye wanafunzi wote washirikishwe katika makundi yao kujadiliana na
kusimuliana kuhusu soko lao na iwapo wamewahi kutumwa sokoni. Wanafunzi
wajibu maswali ya mwalimu kwa kujibu maswali haya:
1. Umewahi kwenda sokoni?
2. Uliona nini sokoni?
3. Ulinunua nini sokoni?
4. Ulinunua bidhaa zako kwa pesa ngapi?
Mwalimu ahakikishe wanafunzi katika makundi yao wamepata ufahamu wa
msamiati wa sokoni pamoja na shughuli mbalimbali za sokoni. Wanafunzi
wanaotatizika katika makundi yao wasaidiwe na mwalimu.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo hili kuhusu msamiati wa sokoni na
shughuli za sokoni kwa kuwauliza wanafunzi maswali tofauti kuhusu mambo
muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo uwezo wa wanafunzi
wa kutaja msamiati wa sokoni, kutambua maana ya msamiati huu pamoja
na kutunga sentensi sahihi kwa kutumia msamiati huu wa sokoni. Vilevile,
mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza kueleza umuhimu wa shughuli
za sokoni kwa binadamu.
237
VI. Majibu
Maswali ya utangulizi, ukurasa 128
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona kwenye
mchoro waliopewa, kwa mfano:
1. Ninaona mazingira ya sokoni.
2. Hapa ni sokoni.
3. Kuna watu wananunua na wengine wanauza. Wengine wamebeba
mizigo ya bidhaa mbalimbali.
Maswali ya michoro, ukurasa 129
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona kwenye
michoro waliyopewa, kwa mfano:
1. Ninaona mnunuzi na muuzaji sokoni; hamali akisukuma mokoteni.
2. Mnunuzi, mwuzaji na hamali.
3. Ndizi, mboga, nyanya, vitunguu n.k.
4. Mahali hapa ni sokoni.
Zoezi, ukurasa 131
1. Gari linalosukumwa au kukokotwa la kubeba mizigo sokoni linaitwa
mkokoteni.
2. Mtu anayeuza bidhaa sokoni ni mwuzaji.
3. Mtu anayenunua bidhaa sokoni ni mnunuzi.
4. Mnunuzi anayenunua bidhaa kwa pesa.
238
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutaja vitu vinavyopatikana sokoni katika kuendeleza mazungumzo;
b) Kutaja watu wanaopatikana sokoni katika kuendeleza mazungumzo;
ch) Kusikiliza maelezo kuhusu sokoni ili kujenga usikivu;
d) Kueleza shughuli zinazoendeshwa sokoni ili kuimarisha stadi ya
kuzungumza;
e) Kueleza umuhimu wa soko ili kujenga stadi ya kuzungumza;
f) Kuthamini shughuli za sokoni kama njia moja ya kujipatia riziki.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ataje vitu vinavyopatikana sokoni k.v. mkokoteni, vibanda,
ratili, bidhaa na risiti.
Mwanafunzi ataje watu wanaopatikana sokoni kama vile: dalali, mnunuzi,
mwuzaji na mchuuzi.
Mwanafunzi anaweza kushiriki katika kuigiza michezo kuhusu shughuli
zinazoendeshwa sokoni.
Mwanafunzi ashiriki katika kujadili kuhusu shughuli za sokoni.
Mwanafunzi ajadili michoro, chati na picha kuhusu sokoni.
Mwanafunzi atoe maelezo kuhusu umuhimu wa soko.
Mwanafunzi aweza kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu shughuli
za sokoni.
Mwanafunzi aweza kutazama video na picha kuhusu shughuli za sokoni.
Mwanafunzi asimulie kisa chochote alichoshuhudia kuhusu sokoni peke
yake, akiwa katika kikundi au wakiwa wawili wawili.
III. Nyenzo:
Masimulizi bunifu kuhusu shughuli za sokoni;
Kadi zenye msamiati wa sokoni;
239
Rekodi au video za vitendo vinavyodhihirisha shughuli za sokoni,
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 131-132;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Mwalimu aandae mapema vifaa atakavyohitaji katika kufundisha funzo hili na
kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama vilivyotajwa hapo awali bila kusahau
vyombo vingine maalum vya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali.
Mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri wa lugha ishara iwapo kuna wanafunzi
walio na matatizo ya kusikia ili kufanikisha ujifundishaji wao. Ikiwa kuna
wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa maelezo
yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha kama
wanafunzi wengine.
Ni vyema mwalimu ahakikishe kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi
ya wanafunzi wanaotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwa kila
shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa katika Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu awasalimie wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia kuhusu msamiati wa sokoni.
Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awashirikishe katika kuchunguza mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi,
ukurasa 131. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali
kuhusiana na mchoro huo. Baadhi ya maswali ambayo mwalimu anaweza
kuuliza ni kama vile: Watu hawa wanafanya nini? Wanafunzi waelekezwe na
mwalimu kujibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi
wawili wawili wasome mazungumzo kati ya Suka na Fasia yanayoambatana na
240
mchoro waliopewa. Mchoro waliopewa unaonyesha vijana wawili wakisalimiana
na kuzungumza. Vijana hawa ambao ni Suka na Fasia wanazungumza kwa
kusimuliana kuhusu Fasia kwenda sokoni na aliyoyaona kule. Wanafunzi
washirikishwe katika kuigiza mazungumzo haya katika makundi yao na mbele
ya darasa.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi wawili wawili kuigiza mbele
ya darasa nafasi ya mnunuzi na mwuzaji. Mwanafunzi mmoja aigize kama
mnunuzi na mwanafunzi wa pili aigize kama mwuzaji. Wanafunzi hawa waigize
katika muktadha wa sokoni. Kila kundi lipewe muda wa kuigiza. Makosa ya
kimatamshi yasahihishwe pindi tu yanapotokea. Wanafunzi wahimizwe kuwa
jasiri wanapozungumza na kuigiza mbele ya wenzao. Mwalimu afahamu kuwa
shughuli hii ya maigizo ni njia bora ya kuimarisha na kukuza ujasiri wa wanafunzi
wa kusimama na kuzungumza mbele ya wanafunzi. Stadi ya kusikiliza na
kuzungumza itaimarishwa kupitia kwa shughuli hii ya maigizo.
Hatimaye, wanafunzi katika darasa zima washirikishwe katika kuimba wimbo
wa sokoni ulio katika vitabu vyao. Mwalimu anaweza kuimba wimbo huo
kisha wanafunzi wakaimba baada yake. Mwalimu awaruhusu wanafunzi
kuimba peke yao kwa sauti na matamshi sahihi. Baada ya kuimba, wanafunzi
wajadiliane kuhusu ujumbe wa wimbo huo. Wimbo huo unahusu shughuli za
sokoni. Wanafunzi washirikishwe katika kujibu maswali ya wimbo waliyopewa
katika vitabu vyao. Kila mwanafunzi ashirikishwe katika shughuli hii. Mwalimu
ahakikishe anawasaidia wanafunzi wanaotatizika katika ujifundishaji wao.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kusikiliza na kuzungumza kwa kurejelea muktadha
wa shughuli za sokoni. Wanafunzi wawe wamepata uwezo wa kusimuliana
masimulizi mbalimbali hasa kuhusu muktadha wa shughuli za sokoni.
241
VI. Majibu
Zoezi la maigizo, ukurasa 132
Mwalimu atathmini maigizo ya wanafunzi.
Maswali ya wimbo, ukurasa 132
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wimbo walioimba,
kwa mfano:
1. Tunaenda sokoni.
2. Sokoni kuna wauzaji na wanunuzi.
3. Sokoni kuna bidhaa mbalimbali kama vile: ndizi, maembe, viatu n.k.
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati uliotumiwa katika hadithi ili kuwezesha ufahamu;
b) Kusikiliza hadithi zikisomwa na mwalimu kuhusu sokoni ili kujenga
usikivu;
ch) Kusoma hadithi kuhusu sokoni ili kuimarisha stadi ya kusoma;
d) Kufahamu hadithi aliyoisoma au kusomewa kuhusu sokoni ili kupata
ujumbe;
e) Kuchangamkia kusoma hadithi ili kujenga ari ya kuendeleza ujifunzaji.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi.
Mwanafunzi ashiriki kusoma darasani, wakiwa wawili wawili na baadaye
asome peke yake.
242
Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
Mwanafunzi asikilize mwalimu akisoma hadithi.
Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kupitia kwa vifaa vya
teknolojia huku mwanafunzi akikumbushwa kusikiliza kwa makini.
Wanafunzi waweza kusomeana hadithi wakiwa wawili wawili au katika
vikundi.
Wanafunzi waweza kushirikishwa kupanga upya aya ambapo sentensi
zimeparaganywa kuhusu sokoni katika vikundi.
Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kwa kutumia jitabu mbele ya darasa.
Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyoisoma.
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kutokana na hadithi.
III. Nyenzo:
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu shughuli za sokoni;
Michoro au picha za hadithi bunifu kuhusu shughuli za sokoni;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu, projekta;
Msomaji mwalikwa;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 133-135;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu ili kujenga stadi ya wanafunzi ya
kusikiliza na kusoma. Muktadha wa hadithi katika somo hili ni kuhusu shughuli za
sokoni. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia
funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake kama vilivyotajwa hapo juu. Mwalimu
anaweza kumwalika msomaji mashuhuri akawasomea wanafunzi hadithi bunifu
kuhusu shughuli za sokoni kisha wanafunzi wakasoma baada yake katika
makundi na hatimaye kila mwanafunzi asome peke yake. Msomaji mwalikwa
sharti awe na uwezo wa kusoma kwa sauti ya kusikika na kwa matamshi sahihi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi.
243
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwaamkua wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia
kuhusu masimulizi ya shughuli za sokoni. Wanafunzi wajibu maamkuzi ya
mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi
katika kusahihisha zoezi walilopewa katika funzo la hapo awali. Wanafunzi
wenye matatizo katika ujifundishaji wao wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao ya
kusoma pamoja na kusikiliza hadithi za kubuni. Mwalimu awagawe wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha awaombe watazame mchoro
ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 133. Wanafunzi wachunguze mchoro
huo na kuujadili katika makundi yao. Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi
maswali mepesi kuhusiana na mchoro huo kama vile: Unaona nini kwenye mchoro
huu? Wasichana hawa wanaenda wapi? Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu
namna ya kujibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu ahakikishe amewashirikisha
wanafunzi wote katika majadiliano haya. Mchoro uliopo unaonyesha wasichana
wawili waliobeba vikapu wakielekea sokoni. Huenda wametumwa kununua
bidhaa kadhaa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi kujibu maswali waliyopewa
kuhusiana na mchoro husika.Wanafunzi wanaotatizika wasaidiwe na mwalimu.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi hadithi iliyo katika
vitabu vyao kuhusu wasichana wawili wanaoitwa Rosana na Kachupa. Hadithi
hii inarejelea mchoro walioujadili hapo mwanzoni kuhusu wasichana wawili
wanaoenda sokoni. Mwalimu ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa
makini anaposoma hadithi hii. Pia, mwalimu ahakikishe anasoma hadithi hii
kwa matamshi sahihi. Baadaye, wanafunzi wasome hadithi hiyo wakiwa wawili
wawili na hatimaye kila mwanafunzi asome akiwa peke yake. Shughuli hii ya kila
mwanafunzi kusoma akiwa peke yake itamsaidia mwalimu kutambua udhaifu
wa kila mwanafunzi katika usomaji na hivyo kuweza kumsaidia. Makosa ya
kimatamshi yakosolewe pindi tu yanapotokea.
244
Baada ya kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi amesoma hadithi hiyo kwa
usahihi, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao kujibu maswali
waliyopewa katika vitabu vyao. Maswali hayo yanahusu hadithi waliyoisoma
darasani kuwahusu Rosana na Kachupa. Wanafunzi wanaotatizika wasaidiwe
na mwalimu.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya kuchunguza
iwapo wamepata ujuzi wa kusoma pamoja na kusikiliza hadithi bunifu. Pia,
mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kusoma hadithi
na kuweza kujibu maswali ya hadithi hiyo kwa usahihi kulingana na muktadha
wa hadithi hiyo. Muktadha wa hadithi hapa ni shughuli za sokoni.
VI. Majibu
Maswali ya mchoro, ukurasa 133
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona kwenye
mchoro waliopewa, kwa mfano:
1. Ninawaona wasichana wawili wakiwa wamebeba vikapu.
2. Wasichana hawa wanaenda sokoni.
Maswali ya hadithi, ukurasa 134
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na hadithi
waliyosoma,kwa mfano:
1. Rosana alienda sokoni na Kachupa.
2. Mama alimtuma Rosana mboga, nyanya na vitunguu.
3. Kachupa alinunua ndizi nne.
4. Baki ya Kachupa ilikuwa shilingi kumi.
5. Rosana hakupewa baki kwa sababu bidhaa alizonunua zilikuwa
za shilingi mia mbili na alimpa mwuzaji shilingi mia mbili, hivyo
hakukuwa na baki yoyote.
245
Mada Ndogo 4: Kuandika
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi
ya uandishi;
b) Kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
Mwanafunzi aeleze yaliyo muhimu katika uandishi k.v. mwandiko nadhifu,
maudhui, mtiririko.
Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwalimu.
Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.
Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa kama hiki
kifuate hatua tano za uandishi: maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo,
uhariri na uchapishaji. Vichwa vya visa vinaweza kutofautiana.
III. Nyenzo:
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Hadithi bunifu zilizoandikwa kwenye chati;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu shughuli za sokoni;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 135;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Lengo kuu la somo hili ni kukuza stadi ya mwanafunzi ya kuandika. Katika somo
hili, wanafunzi watapata maarifa ya kuandika visa vifupi vifupi kwa kuzingatia
mambo kadhaa kama vile: hati nadhifu, mtiririko, uhariri, marejeleo, nakala
246
safi na maandalizi mengine. Shughuli hii itawawezesha wanafunzi kufahamu
jinsi ya kuandika visa mbalimbali vya kubuni katika miktadha mbalimbali.
Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo
hili kama vilivyoorodheshwa hapo juu. Hili litamsaidia kufanikisha ufundishaji
wake pamoja na ujifundishaji wa wanafunzi. Muktadha unaorejelewa hapa ni
shughuli za sokoni.
Katika kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila
zoezi husika lililotolewa kwenye vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
kusoma hadithi bunifu kuhusu shughuli za sokoni. Wanafunzi wajibu salamu za
mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wasahihishe zoezi walilopewa katika kipindi
cha hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kuandika na hata kubuni hadithi kwa kurejelea muktadha wa shughuli
za sokoni kwa kuandika nakala ya kwanza kisha kuihariri na hatimaye kuandika
nakala safi katika madaftari yao. Nakala safi izingatie mwandiko nadhifu, mtiririko
mwafaka pamoja na kuhaririwa ili kuondoa makosa yoyote ya kimaendelezo na
kisarufi.
Mwalimu awasomee wanafunzi hadithi waliyopewa katika vitabu vyao kuhusu
dada na kaka kwenda sokoni. Wanafunzi wamsikilize mwalimu kwa makini.
Wanafunzi wasome hadithi hiyo baada ya mwalimu wakiwa wawili wawili
kisha kila mwanafunzi asome akiwa peke yake. Makosa yoyote ya kimatamshi
yasahihishwe pindi tu yanapotokea. Baada ya shughuli hii ya usomaji, wanafunzi
wanakili hadithi waliyosoma katika madaftari yao kwa mwandiko nadhifu.
247
Mwalimu asahihishe makosa ya kimaendelezo.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi kufanya zoezi la kujaza mapengo ya
hadithi waliyopewa katika vitabu vyao. Wanafunzi wanakili hadithi hiyo katika
madaftari yao. Baada ya zoezi hili, mwalimu ahakikishe amesahihisha madaftari
ya wanafunzi.
Mwisho, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kubuni kisa kifupi kuhusiana
na shughuli za sokoni na kila mwanafunzi aandike kisa chake katika daftari lake.
Makosa ya kimaendelezo yasahihishwe. Mwalimu ahakikishe kila mwanafunzi
anaandika kisa chake kwa mtiririko mwema na maudhui yahusiane na shughuli
za sokoni. Wanafunzi wanaweza kuandika nakala ya kwanza, wakaihariri ili
kuondoa makosa ya kimaendelezo na kisarufi na hatimaye waandike nakala
safi. Wanafunzi walio na matatizo ya kuandika kwa mwandiko nadhifu wapewe
mazoezi zaidi ya kuandika. Mwalimu awaelekeze zaidi.
Mwalimu anaweza kumwomba kila mwanafunzi aandike nakala yake safi
ubaoni (kuhusiana na shughuli za sokoni) ili wanafunzi wenzake waisome na
kuikosoa kwa kurejelea hati nadhifu, makosa ya kimaendelezo pamoja na ya
kisarufi. Pia, wanafunzi katika makundi yao wanaweza kusahihisha nakala zao
safi. Wanafunzi walio na matatizo wasaidiwe.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kubuni na kuandika maelezo au visa
bunifu kwa mwandiko nadhifu, mtiririko na kwa kuzingatia maudhui lengwa.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata uelewa wa shughuli za
sokoni pamoja na msamiati wa sokoni.
248
VI. Majibu
Zoezi la kuandika, ukurasa 135
Bwana Nafu ni muuzaji wa bidhaa sokoni. Anauza katika kibanda chake.
Kibanda chake kina ratili ya kupima uzito wa bidhaa. Bwana Nafu
huwaandikia wanunuzi wake risiti.
Mada Ndogo 5: Saru: Matumizi ya ‘ndani ya’ na ‘nje ya’
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua matumizi ya ndani ya na nje ya ili kuimarisha mawasiliano;
b) Kutumia ndani ya na nje ya katika sentensi kwa usahihi ili kuimarisha
mawasiliano;
ch) Kusoma sentensi zinazodhihirisha matumizi ya ndani ya na nje ya ili
kuimarisha stadi ya kusoma;
d) Kuandika sentensi zinazodhihirisha matumizi ya ndani ya na nje ya ili
kuimarisha stadi ya kuandika;
e) Kuchangamkia matumizi ya ndani ya na nje ya katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome sentensi zinazodhihirisha matumizi ya ndani ya na
nje ya.
Mwanafunzi atunge sentensi zinazorejelea vitu halisi darasani k.m. Kitabu
kimo ndani ya kabati; Mwanafunzi yupo nje ya darasa; katika vikundi.
Mwanafunzi ashiriki katika kuigiza vitendo vinavyoonyesha ndani ya na
nje ya.
Mwanafunzi aweza kukamilisha sentensi zinazodhihirisha matumizi ya
ndani ya na nje ya kwa kurejelea michoro tofauti tofauti akiwa peke yake
au katika vikundi.
249
Mwanafunzi aweza kufanya mazoezi ya kutumia ndani ya na nje ya kwa
kutumia vifaa vya kiteknolojia.
III. Nyenzo:
Chati zenye sentensi zilizojumuisha matumizi ya ndani ya na nje;
Michoro au picha zinazoonyesha matumizi ya ndani ya na nje;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 136-137;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Kama tunavyofahamu, sarufi ni kipengele muhimu katika ujifundishaji wa
wanafunzi. Mwalimu anastahili kutilia maanani dhana hii ili kuweza kuwahusisha
wanafunzi kwa ukamilifu katika somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema
kama vilivyoorodheshwa hapo juu na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, mwalimu ajitahidi kuhusisha matumizi
ya breli au vinasasauti ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha
kama wanafunzi wengine. Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia
mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya lugha ya ishara. Mwalimu anaweza
pia kumshirikisha mtaalamu au mtafsiri wa lugha ya ishara katika kuwasaidia
wanafunzi hawa.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu anashauriwa kuwagawa
wanafunzi katika makundi yanayotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa
kwa kila shughuli ya wanafunzi katika Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
(a) Utangulizi
Mwalimu awasalimie wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia kuhusu kubuni kisa (kuhusu
shughuli za sokoni) na kukiandika kwa mwandiko nadhifu. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
250
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi kilichotangulia. Wanafunzi waliopata matatizo katika kufanya zoezi hilo
wasaidiwe na mwalimu.
(b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili
kisha awashirikishe katika kutazama michoro waliyopewa katika kitabu chao.
Wanafunzi wajadili michoro hiyo kwa kurejelea matumizi ya ndani ya na nje
ya. Wanafunzi waelezane kuhusu vitu wanavyoona kwenye michoro iliyopo
na waeleze mahali vitu hivyo vilivyo. Wanafunzi wanaweza kutumia sentensi
walizopewa katika vitabu vyao ambazo ni:
1. Kitabu kimewekwa ndani ya mkoba.
2. Mti umemea nje ya nyumba.
3. Maembe yako ndani ya kikapu.
4. Maua yamemea nje ya dirisha.
5. Joni ameweka mikono ndani ya mifuko.
Mwalimu atathmini majadiliano ya wanafunzi katika makundi yao kwa kurejelea
michoro waliyopewa na matumizi ya ndani ya na nje ya. Shughuli hii itawawezesha
wanafunzi kufahamu matumizi kamili ya ndani ya na nje ya.
Baada ya wanafunzi kujadili kuhusu michoro waliyopewa pamoja na sentensi
zilizopo, mwalimu awashirikishe katika majadiliano zaidi kuhusiana na matumizi
ya ndani ya na nje ya.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao
ili waigize vitendo mbalimbali vinavyodhihirisha matumizi ya ndani ya na nje
ya. Kwa mfano:
1. Mwanafunzi kusimama nje ya darasa.
2. Wanafunzi kuingia ndani ya darasa.
3. Mwanafunzi kuweziweka chaki za mwalimu ndani ya kabati.
4. Wanafunzi kuweka vitabu vyao ndani ya mikoba yao.
5. Mwanafunzi kuweka kalamu yake ndani ya mfuko wake.
6. Mwanafunzi kuweka dawati lake nje ya darasa lao.
251
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika maigizo haya.
Wanafunzi waigize jinsi ya kutenda vitendo walivyoelekezwa kutenda ili
kuimarisha ufahamu wao wa matumizi ya ndani ya na nje ya.
Mwalimu awaelekeze wanafunzi katika kutunga sentensi sahihi kwa kutumia
ndani ya na nje ya, kwa mfano:
1. Machungwa yako ndani ya kikapu.
2. Wanafunzi wameketi nje ya darasa lao.
3. Wageni wameketi ndani ya nyumba.
4. Mbwa amelala nje ya lango letu.
5. Kitabu kimewekwa ndani ya kabati.
Wanafunzi waelekezwe kutambua kuwa ndani ya na nje ya ni vihusishi yaani
ni maneno yanayoonyesha uhusiano wa vitu (nomino) zaidi ya kimoja, kwa
mfano: wageni wameketi ndani ya nyumba; ndani ya inaonyesha uhusiano wa
‘wageni’ na ‘nyumba’. Mwalimu ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote
katika shughuli hii ya kutunga sentensi sahihi kwa kutumia ndani ya na nje ya.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi waliyopewa
katika vitabu vyao kuhusu matumizi ya ndani ya na nje ya. Mwalimu awasaidie
wanafunzi wanaotatizika katika kufanya mazoezi haya.
(ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa katika kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana
kwa kutumia ndani ya na nje ya. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wanaweza kutunga sentensi sahihi katika kwa kutumia vihusishi ambavyo ni:
ndani ya na nje ya.
252
VI. Majibu
Zoezi la kusoma, ukurasa 137
Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
Zoezi, ukurasa 137
1. Weka pesa ndani ya mfuko.
2. Samaki hawezi kuishi nje ya maji.
3. Wanafunzi husomea ndani ya darasa.
4. Usichezee ndani ya chumba chezea nje.
5. Muuzaji aliweka vitunguu nje ya gunia ili mnunuzi avione.