Longhorn
Kiswahili Mufti
Mwongozo wa Mwalimu
Gredi ya 2
Wallah bin Wallah
Jacqueline M. Kinya
Kimechapishwa na:
Longhorn Publishers (Kenya) Ltd.,
Barabara ya Funzi, Eneo la Viwandani,
S.L.P. 18033–00500.
Nairobi, Kenya.
Longhorn Publishers (Rwanda) Ltd.,
Remera mkabala na Benki ya COGE,
S.L.P 5910,
Kigali, Rwanda.
Longhorn Publishers (Uganda) Ltd.,
Ploti 4, Eneo la Vubyabirenge, Ntinda,
S.L.P 24745,
Kampala, Uganda..
Longhorn Publishers (Tanzania) Ltd.
Barabara Mpya ya Bagamoyo/Garden,
Mikocheni B, Ploti Namba: MKC/MCB/81,
S.L.P 1237,
Dar es Salaam, Tanzania.
© Wallah bin Wallah, Jacqueline M.K. 2018
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kupigisha chapa,
kutafsiri au kukitoa kitabu hiki kwa jinsi yoyote ile bila idhini, kwa
maandishi ya Longhorn Publishers Ltd.
Chapa ya kwanza, 2018
ISBN 978 9966 64 006 2
Kimepigwa chapa na Autolitho Ltd.,
Barabara ya Enterprise, Eneo la Viwandani,
S.L.P 73476-00200, Nairobi, Kenya.
iii
Utangulizi ................................................................................................................ vi
Maazimio ya kazi ................................................................................................... viii
Mpangilio wa funzo ............................................................................................... ix
SURA YA 1 .................................................................................... 1
MADA KUU 1: SHULENI ............................................................. 1
Mada Ndogo 1: Sauti na majina ya herufi za Kiswahili ................................. 4
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Maamkizi ya nyakati za siku .... 13
Mada Ndogo 3: Msamiati ............................................................. ...................... 16
Mada Ndogo 4: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi .................................... 20
Mada Ndogo 5: Kusoma: Hadithi ..................................................................... 24
Mada Ndogo 6: Msamiati: Nambari 11-50 ........................................................ 28
Mada Ndogo 7: Sarufi: Matumizi ya -ako na -enu ............................................ 32
Majibu ..................................................................................................................... 35
SURA YA 2 ................................................................................... 36
MADA KUU 2: HAKI ZANGU ....................................................... 36
Mada Ndogo 1: Sauti na majina ya herufi za Kiswahili ................................. 38
Mada Ndogo 2: Msamiati .................................................................................. 47
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ................................. 50
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi ...................................................................... 54
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya vizuri na vibaya ..................................... 57
Majibu .................................................................................................................... 60
SURA YA 3 ................................................................................... 61
MADA KUU 3: USAFIRI ............................................................. 61
Mada Ndogo 1: Sauti na majina ya herufi za Kiswahili .................................... 64
Mada Ndogo 2: Msamiati - Usafiri ...................................................................... 71
iv
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ................................. 74
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi ...................................................................... 77
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya herufi kubwa ........................................... 80
Majibu ..................................................................................................................... 83
SURA YA 4 ..................................................................................... 84
MADA KUU 4: FAMILIA................................................................ 84
Mada Ndogo 1: Sauti za herufi mbili za Kiswahili ............................................. 87
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza:
Maneno ya heshima na adabu ................................................. 96
Mada Ndogo 3: Msamiati: Familia ....................................................................... 99
Mada Ndogo 4: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi .................................. 102
Mada Ndogo 5: Kusoma: Hadithi ....................................................................... 106
Mada Ndogo 6: Sarufi: Matumizi ya maneno yanayoashiria vitendo ............ 109
Majibu ..................................................................................................................... 112
SURA YA 5 .................................................................................... 113
MADA KUU 5: USALAMA WANGU ............................................... 113
Mada Ndogo 1: Sauti na herufi mbili za Kiswahili .......................................... 116
Mada Ndogo 2: Msamiati: Usalama wangu ..................................................... 122
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi .............. .................. 125
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi ........................................................................128
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya huyo na hao ............................................ 131
Majibu ..................................................................................................................... 134
SURA YA 6 .................................................................................... 135
MADA KUU 6: HALI YA ANGA ..................................................... 135
Mada Ndogo 1: Alfabeti za Kiswahili ................................................................. 138
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Msamiati ..................................... 141
v
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ....................................144
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi ....................................................................... 147
Mada Ndogo 5: Sarufi: Nafsi ya pili wakati uliopita .......................................... 150
Majibu ......................................................................................................................153
SURA YA 7.................................................................................... 154
MADA KUU 7: LISHE BORA ........................................................154
Mada Ndogo 1: Msamiati - Lishe bora .............................................................. 157
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ...................................160
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi ....................................................................... 163
Mada Ndogo 4: Sarufi: Matumizi ya
hiki
na
hivi
..................... ....................... 166
Majibu ......................................................................................................................169
SURA YA 8.....................................................................................170
MADA KUU 8: MNYAMA NIMPENDAYE..........................................170
Mada Ndogo 1: Msamiati ................................................................................... 172
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi ....................................176
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi ........................................................................ 180
Mada Ndogo 4: Sarufi: Matumizi ya
hili
na
haya
.................... ....................... 183
Majibu ......................................................................................................................186
vi
UTANGULIZI
Lugha ya Kiswahili imesambaa na kutambaa katika Afrika ya Mashariki, Kati
na Afrika nzima hadi duniani kote. Ni wajibu wa mwalimu kuwahamasisha
wanafunzi wake kuipenda lugha ya Kiswahili kwani kuna matumaini ya siku za
usoni. Mwalimu awahimize wanafunzi wake kuwa wanaweza kujiendeleza katika
somo la Kiswahili kupitia kwa: redio, runinga, magazeti, ualimu, tafsiri miongoni
mwa nyanja anuwai.
Jukumu la lugha ya taifa ni kuweza kutambulisha watu wa taifa moja na
kuwatia hisia kuwa wanaungana na kutambulika. Lugha ni kitambulisho muhimu
sana cha watu wa jamii fulani. Kutokana na kusambaa kwa lugha ya Kiswahili,
msamiati wake ulio mzuri, utafiti uliofanyiwa lugha hii na idadi kubwa ya watu
wanaoizungumza ni thibitisho tosha kuwa lugha hii inapaswa kupewa nafasi
mwafaka. Hii ni kwa sababu hii ndiyo lugha ya kutambulisha bara la Afrika katika
ramani ya dunia. Isitoshe, lugha ya Kiswahili ina wajibu wa kuleta mabadiliko ya
kijamii, kisiasa na kiuchumi katika bara la Afrika.
Malengo ya kufundisha Kiswahili katika shule za msingi
Malengo ya kufundisha Kiswahili katika shule za msingi kama
yanavyofafanuliwa na silabasi mpya ni kumwezesha mwanafunzi:
1. Kusikiliza na kuitikia vilivyo kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kuongea lugha ya Kiswahili kwa ufasaha.
3. Kusoma na kuelewa lugha ya Kiswahili.
4. Kujieleza kikamilifu kwa lugha ya Kiswahili kwa kuandika.
5. Kutunga kazi za kisanii kulingana na kiwango cha mwanafunzi.
6. Kuimarisha mazoea ya usomaji bora.
7. Kupenda na kujiendeleza katika somo la Kiswahili baada ya shule ya
msingi.
8. Kuionea fahari na kuikuza lugha ya Kiswahili katika mawasiliano.
9. Kutukuza na kuendeleza Kiswahili sanifu maishani.
10. Kutathmini, kufurahia na kujivunia Kiswahili kama lugha ya taifa na ya
kimataifa.
11. Kutambua na kushiriki katika kupata suluhisho la masuala ibuka
yanayohusu na kuathiri jamii kama vile: afya na UKIMWI, uadilifu, jinsia,
mazingira na teknolojia.
vii
Jukumu la mwalimu katika kutimiza malengo haya
Ili kutimiza malengo haya, mwalimu ana wajibu muhimu. Mwalimu azingatie
mazingira ya shule na kutoa mifano halisi ya vitu au watu wanaopatikana katika
mazingira ya shule. Kuna mazingira ya mjini na ya mashambani.
Mwalimu ana wajibu wa kujitayarisha mapema kabla ya somo kwa kuhakikisha
ana vifaa vya kutumia darasani ili kufanikisha somo. Vifaa hivi viwe vinapatikana
kwa urahisi au kwa bei rahisi iwapo ni vya kununuliwa.
Mwalimu anapaswa kutumia mwongozo huu na kitabu cha wanafunzi na
rasilimali nyingine yoyote itakayofanikisha kipindi chake. Mwalimu asitumie
mwongozo huu kisisisi bali awe mbunifu kulingana na uwezo wa wanafunzi wake
na vifaa vinavyopatikana.
Mwalimu aanze kwa kufundisha dhana sahili kabla ya kufundisha zile
changamano zaidi. Lazima azingatie uwezo wa wanafunzi wake.
Mwalimu anapaswa kuwashirikisha wanafunzi wake kadiri iwezekanavyo
katika somo la Kiswahili. Kwa kuwashirikisha, watakuza stadi zao za kusikiliza,
kuongea, kusoma na kuandika.
Mifano anayotoa darasani, iwe rahisi,sahihi, ya hali ya kila siku na inayoeleweka
kwa wanafunzi kuhusu mazingira yao na kuihusisha na masuala ibuka kama vile:
uadilifu, haki za watoto, Ukimwi, jinsia na teknolojia. Jukumu kubwa la mwalimu
ni kuwahamasisha wanafunzi kuongea, kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili
kwa ufasaha. Hili ni jukumu ambalo mwalimu yeyote wa Kiswahili hawezi
kuepuka.
Lazima mwalimu awe kielelezo kwa wanafunzi wake kwa sababu wanafunzi
hupenda sana kuiga. Awe ni mtu anayeipenda lugha ya Kiswahili na kuionea
fahari ili awatie ari wanafunzi wake kuipenda lugha ya Kiswahili.
Mwalimu mwema ni yule anayejaribu kuwa katika kiwango cha wanafunzi.
Kama ni kuimba, wote wanaimba, kama ni kuigiza naye anaigiza. Mwalimu
sharti awe mchangamfu ili awachangamshe wanafunzi wake. Asifunze mambo
au mada kidhahania tu. Ataje matukio halisi maishani mwa wanafunzi huku
akiwahusisha katika kila hatua darasani. Mwongozo huu ni kama dira kwa
mwalimu katika kutekeleza mambo haya.
Mwalimu ajaribu kutumia rekodi za redio pamoja na video ili kuwavutia
wanafunzi mbali na kuendeleza stadi za kusikiliza na matamshi bora. Mwalimu
awahusishe wanafunzi katika kuchora picha, kuigiza darasani, kuimba na
kuwahusisha katika mijadala ili somo la Kiswahili liwe hai. Mwalimu anaweza
kuwaalika shuleni watu waliobobea katika Kiswahili ili kuwahamasisha wanafunzi
kuipenda na kuionea fahari lugha ya Kiswahili.
viii
Mbinu za kufundisha Kiswahili
Kuna mbinu kadhaa zinazoweza kutumiwa kufundisha somo la Kiswahili. Mwalimu
anashauriwa atumie mbinu kulingana na kiwango cha wanafunzi wake, uwezo
wao, mazingira, rasilimali na vifaa vinavyopatikana. Kuna mbinu kama kuigiza,
mijadala, kuwaalika watu wenye ujuzi wa lugha ya Kiswahili (kama waandishi wa
habari, wahadhiri, malenga, watangazaji) na kadhalika. Mbinu ya jadi ni maswali
na majibu lakini bado inatumiwa hasa kutathmini wanafunzi darasani. Michoro
au kuunda picha za vitu mbalimbali na kuwapanga wanafunzi katika vikundi ni
mbinu nyingine. Mwalimu akumbuke kuwa kila mbinu ina faida na upungufu
wake. Mwalimu atumie mbinu inayofaa zaidi na rahisi kwa wanafunzi ili kueleza
dhana inayohusika.
Kazi za wanafunzi
Sharti mwalimu awashirikishe wanafunzi katika somo la Kiswahili. Baadhi ya
shughuli za wanafunzi ni:
Kujibu na kuuliza maswali darasani.
Kusoma makala katika kitabu.
Kujadiliana darasani, kusimuliana hadithi na kukariri mashairi.
Kuchora vifaa mbalimbali.
Kuigiza vitendo mbalimbali.
Kusikiliza wenzao wakisoma, wakiongea au wataalamu walioalikwa.
Kuandika majibu ya maswali mbalimbali.
Vifaa vya kufundisha lugha ya Kiswahili
Mwalimu anaweza kutumia vifaa kama vile:
Kadi Mabango Vifaa halisi vinavyoweza kupatikana
kwa urahisi
Michoro Picha Tarakilishi
Redio Vitabu Simu za mkononi
Chati Video n.k.
Maazimio ya kazi
Kwa kawaida, mwalimu huandaa maazimio ya kazi baada ya kupokea silabasi
inayoeleza mada zinazotakiwa kufunzwa katika darasa fulani kwa mwaka mmoja.
Mwalimu sharti ajue sehemu mbalimbali za silabasi na malengo ya somo la
Kiswahili kwa ujumla. Kisha apange mada zake kwa mtiririko kutoka sahili hadi
changamano. Mwalimu apange na kutayarisha maazimio yake ya kazi mwanzo
wa muhula hasa wiki ya kwanza au hata wakati wa likizo.
Maazimio ya kazi humwezesha mwalimu kuandaa vifaa vyake na kupanga
ufundishaji wake kimantiki bila kuhangaika. Isitoshe, maazimio ya kazi
ix
humwezesha mwalimu wa Kiswahili kuhitimisha mada zilizopo katika silabasi
kwa muda ziliotengewa.
Mfano wa maazimio ya kazi
Darasa:
Gredi ya
Pili
Somo:
Kiswahili
Jina: RITA
AMANI
Muhula:
wa kwanza
Mwaka:
2018
Wiki Kipindi Mada Malengo Nyenzo Shughuli
za darasani
Tathmini Marejeleo Maoni
1 3 Msamiati Mwanafunzi
aweze:
a) Kutaja
vifaa vya
darasani.
b) Kutunga
sentensi
kwa
kutumia
majina ya
vifaa vya
darasani.
Michoro
Vifaa
halisi
Kutaja vifaa
Kutunga
sentensi
Kujibu
maswali
Kutunga
sentensi
Kitabu cha
Mwanafunzi
ukurasa
11-15
Mpangilio wa funzo
Kwa kawaida, mpangilio wa funzo hutayarishwa kutoka kwenye maazimio ya
kazi. Huu ni uandalizi wa awali kabla ya kuingia darasani kufundisha. Mwalimu
anayeingia darasani kufundisha bila mpangilio wa funzo hawezi kutekeleza wajibu
wake ipasavyo kwani hajui aanzie wapi na amalizie wapi. Mpangilio wa funzo
ni dira inayomwongoza mwalimu darasani. Humwezesha mwalimu kukamilisha
mada yake kwa muda uliotengwa bila kwenda kombo. Pia, huchangia katika
kujiamini akiwa darasani. Aidha, humwezesha kutafuta vifaa na vielelezo vingine
atakavyotumia na kuhusisha somo na lile lililopita iwapo panahitajika.
Wakati wa utayarishaji wa mpangilio wa funzo, sharti mwalimu akumbuke
uwezo wa wanafunzi wake, vifaa vinavyopatikana na muda uliotengewa kipindi
fulani. Aidha, sharti awashirikishe wanafunzi katika shughuli mbalimbali huku
akionyesha kazi zake zitakazofanikisha kipindi. Kazi za mwalimu na wanafunzi
ziende sambamba. Kwa mfano, mwalimu akitaja mifano, nao wanafunzi
washirikishwe kutaja.
Mwalimu atumie ubao ipasavyo kwa kuelezea hoja muhimu katika somo.
Ufuatao ni mfano tu wa mpangilio wa funzo katika gredi ya pili.
x
Mfano wa mpangilio wa funzo
TAREHE WAKATI GREDI SOMO IDADI YA
WANAFUNZI
12.10.18 8.00 - 8.30
2
KISWAHILI 30
Funzo: Msamiati
Mada: Vifaa vya darasani
Malengo: Kufikia mwisho wa somo, mwanafunzi aweze:
(a) Kutambua vifaa vya darasani.
(b) Kutunga sentensi akitumia majina ya vifaa vya darasani.
Marejeleo: Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 11-15.
Mwongozo wa Mwalimu, ukurasa 10-14.
Maendelezo ya funzo
- Mwalimu awaulize wanafunzi
majina ya vifaa darasani.
- Mwalimu awaambie wataje vifaa
wanavyoona kwenye mchoro.
Mwalimu awape wanafunzi fursa
ya kutunga sentensi kuhusu vifaa
vya darasani.
- Mwalimu arejelee somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali.
- Awape mazoezi zaidi kuhusu
vifaa vya darasani.
Wanafunzi wataje vifaa
wanavyoona darasani, kwa
mfano: rula, ubao n.k.
Wanafunzi watunge sentensi
sahihi wakitumia majina ya
vifaa vya darasani.
- Wanafunzi wajibu maswali.
- Wanakili mazoezi zaidi
katika madaftari yao.
Dakika 5Hitimisho
Kiini Dakika 20
Hatua Muda Kazi ya Mwalimu Kazi ya Mwanafunzi
Utangulizi Dakika 5
Ufundishaji wa mada mbalimbali
(i) Ufahamu
Kufunza somo la ufahamu barabara kama yalivyo masomo mengine kunahitaji
mwalimu afanye matayarisho ya kutosha kabla ya kipindi.
xi
Mwalimu anapaswa kufahamu barabara maana ya maneno au msamiati
unaotumiwa katika taarifa. Mwalimu anaweza kuanza kwa kuwauliza wanafunzi
maana ya baadhi ya maneno kabla ya kusoma makala yenyewe. Kisha anaweza
kuwaelezea maneno magumu watakayokumbana nayo katika kifungu. Wanafunzi
washirikishwe kutunga sentensi wakitumia maneno hayo. Mwalimu asahihishe
makosa pindi yanapotokea.
Mwalimu anaweza kuanza kusoma sentensi za kwanza mbili au tatu hivi.
Mwalimu daima akumbuke kuwa yeye ni kielelezo na hana budi kujizatiti katika
matamshi bora. Kisha awaongoze wanafunzi kuisoma taarifa, kwa makini huku
kila mwanafunzi akipata nafasi ya kuisoma. Mwalimu aandike maneno magumu
ubaoni huku akiwaongoza wanafunzi jinsi ya kuyatamka. Kisha awaeleze maana
na matumizi yake.
(ii) Sarufi
Sarufi kwa ujumla ni utaratibu, kanuni au sheria zinazotawala matumizi ya
maneno, maumbo ya maneno na miundo ya sentensi katika lugha fulani. Sarufi
ya Kiswahili ni pana na imetawaliwa na ngeli. Ngeli ni kundi moja la majina
yaliyo na upatanisho sawa wa kisarufi na viambishi sawa vya umoja na wingi.
Kwa mfano:
Umoja Wingi Ngeli
Mtu anakuja. Watu wanakuja.
A - WA
Mara nyingi, wanafunzi hawalichangamkii somo la sarufi, lakini likifunzwa
kwa kuhusishwa na masomo mengine na kutumia vifaa halisi na michoro, somo
litakuwa la kuvutia mno.
(iii) Msamiati
Msamiati ni jumla ya maneno yanayopatikana katika lugha fulani. Msamiati
unaweza kufunzwa kwa kuhusishwa na vipengele vingine kama vile sarufi au
ufahamu. Mwalimu anapofundisha msamiati sharti akumbuke kuwa neno moja
linaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa hivyo, ni vyema kuliweka neno
katika muktadha wa matumizi yake.
(iv) Kusoma na kuandika
Kusoma ni stadi moja ambayo inatiliwa mkazo mno katika silabasi mpya. Kusoma
kwa ufasaha ni tathmini ya kuonyesha kuwa mtu ameimudu lugha husika.
Mwalimu awaongoze wanafunzi kusoma makala ya kila aina kama ufahamu,
magazeti na mashairi.
xii
Mwalimu awaeleze wanafunzi maana ya ushairi. Anaweza kuanza kwa kuwauliza
wataje mifano ya wimbo au nyimbo wanazozifahamu. Kisha anaweza kuwaelezea
shairi kama utunzi au tungo ya kisanaa. Shairi ni wimbo wenye mpangilio maalum
wa lugha unaoelezea wazo fulani kuhusu maisha ya binadamu.
Tathmini
Kutathmini ni mfanyiko endelevu katika mfumo wa elimu. Kutathmini ni jambo
lisiloepukika katika elimu kwa sababu ufundishaji wa Kiswahili au somo jingine
hauwezi kuwa kamilifu bila kutathmini. Kupitia tathmini mwalimu anaweza
kuelewa udhaifu na uwezo wa wanafunzi wake. Kuna mbinu kadhaa za kutathmini
kama vile: kuuliza na kujibiwa maswali darasani, kufanya zoezi katika daftari na
kisha kulisahihisha, kusoma, kuandika na kusimulia hadithi. Katika kutathmini,
mwalimu atumie mbinu inayofaa wanafunzi wake ili kupima stadi husika kama
kusoma, kuandika, kusikiliza, ufahamu, sarufi na kuzungumza.
Mwongozo huu utakuwa dira mufti kwa mwalimu anapowaongoza wanafunzi
katika safari ya kuiendeleza na kuikuza lugha ya Kiswahili.
1
Matokeo maalum
yanayotarajiwa
Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kukia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutamka sauti nne za herufi moja
ili kuimarisha mazungumzo;
(b) Kutambua maneno yatumiwayo
katika maamkuzi ya nyakati za siku
shuleni kwa mawasiliano mwafaka;
(ch) Kutambua kwa kutaja msamiati wa
shuleni katika kuimarisha umilisi
wa lugha;
(d) Kutaja majina ya vitu
vinavyopatikana shuleni ili
kuimarisha stadi ya kuzungumza;
(e) Kutambua picha ya vitu
vinavyopatikana shuleni katika
kujenga stadi ya kuzungumza;
(f) Kutambua nambari 11-50
kwa maneno ili kuimarisha
mawasiliano;
(g) Kutambua matumizi yafaayo ya
ako na enu katika mawasiliano.
Mwanafuzi aweza kutambua
sauti /g/, /d/, /j/ na /r/ katika
maneno.
Mwanafunzi aigize maamkuzi
mbalimbali ya nyakati za siku, kwa
mfano: habari ya asubuhi, jioni,
mchana, umeamkaje na umeshindaje.
Mwanafunzi aonyeshwe vifaa
halisi, picha au michoro ya vitu
vinavyopatikana shuleni kama vile:
ofisi, maktaba, vyoo, darasa, bendera
na gwaride.
Mwanafunzi asimulie kisa kuhusu
shule.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi asome majina ya
nambari 11-50.
Mwanafunzi atunge sentensi zenye
matumizi ya ako na –enu.
Mada Kuu 1: Shuleni
Idadi ya vipindi: 22
Sura ya
1
2
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kazi ya vikundi.
Michezo.
Nyimbo na mashairi kuhusu usafi wa mwili.
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Kiingereza, lugha nyingine za kiasili pamoja na masuala ya
mazingira.
Nyenzo:
Rekodi za masimulizi mbalimbali;
Vifaa halisi vya darasani;
Kadi za tarakimu;
Michoro au picha za watu wakiamkuana;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 1;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia wanafunzi
wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Mada hii inashughulikia mazingira ya shuleni, vifaa halisi vya shuleni, maeneo
kadhaa ya shuleni kama vile: maktaba, ofisi, choo n.k, maamkuzi ya nyakati
mbalimbali za siku, kuhesabu tarakimu 11-50, masimulizi kuhusu mazingira ya
shuleni pamoja na kusoma hadithi kuhusiana na masuala ya elimu na maadili
ya wanafunzi. Pia, kipengele cha sarufi kuhusu matumizi ya –ako na –enu
yameangaziwa katika mada hii. Kama tujuavyo, maamkuzi ni kipengele muhimu
katika utamaduni wetu hivyo mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wanapata
maarifa haya.
Lengo kuu la mada hii ni kumsaidia mwanafunzi kujenga stadi yake ya kusikiliza,
kufahamu msamiati wa shuleni, kusimulia hadithi, kusoma hadithi, kuhesabu
tarakimu pamoja na kufahamu matumizi ya –ako na –enu katika sentensi na
mazungumzo kwa jumla.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
3
Uraia,
Utangamano wa kijamii, wanafunzi watangamane na kufanya kazi pamoja.
Msamiati maalum
Baadhi ya msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao
katika mada hii ni kama vile:
Msamiati Maana
1.
gwaride
mahali shuleni ambapo bendera hupandishwa
2.
maktaba
chumba cha kuhifadhia vitabu
3.
bendera
aina ya kitambaa maalum ambacho ni nembo ya taifa
4.
maamkuzi
maneno ya kumjulia mtu hali
5.
tarakimu
Nambari za kuhesabu
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Ili kuwashirikisha wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali, mwalimu
awe na vifaa maalum vya kuwasaidia wanafunzi wa aina hii katika ujifundishaji
wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri au
wajuzi wa lugha ya ishara.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kuona, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya breli pamoja na vifaa vya kunasia sauti. Haya yatawawezesha
wanafunzi hawa kusoma kama wanafunzi wenzao bila vikwazo vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya vipindi
Mada Ndogo 1: Sauti na majina ya herufi za Kiswahili
8
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza:
Maamkuzi ya nyakati na siku
2
Mada Ndogo 3: Msamiati: Shuleni
2
Mada Ndogo 4: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 5: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 6: Msamiati: Nambari 11-50
3
Mada Ndogo 7: Sarufi: Matumizi ya -ako na -enu
2
JUMLA: 22
4
Mada Ndogo 1: Sauti na majina ya heru za Kiswahili
(Idadi ya vipindi: 8)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutamka sauti nne za herufi moja ili kuimarisha mazungumzo;
b) Kutambua sauti za herufi moja zilizofunzwa katika kujenga stadi ya
kusikiliza;
ch) Kutambua majina ya herufi zinazowakilisha sauti lengwa katika kujenga
stadi ya kusikiliza;
d) Kusoma herufi za sauti moja katika kujenga stadi ya kusoma;
e) Kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa katika
kujenga stadi ya kusoma;
f) Kusoma vifungu vilivyo na maneno yaliyo na sauti lengwa katika kujenga
stadi ya kusoma;
g) Kuandika herufi zinazowakilishwa na sauti lengwa katika kujenga stadi
ya kuandika;
h) Kuchangamkia kutumia maneno yanayojumuisha sauti zilizofunzwa
katika mawasiliano ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
• Mwanafunzi aweza kutambua sauti /g/, /d/, /j/ na /r/ katika
maneno.
• Mwanafunzi asikilize mwalimu akitamka sauti lengwa, kisha atamke
pamoja na mwalimu na mwishowe atamke akiwa peke yake, wawili
wawili na kama darasa.
• Mwanafunzi atambue sauti alizosoma katika maneno.
• Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia (papaya) kusikiliza matamshi ya
sauti lengwa.
5
• Mwanafunzi atambue herufi zinazowakilisha sauti lengwa kwa kutumia
kadi za herufi.
• Mwanafunzi aambatanishe silabi katika kutambua sehemu mbalimbali
za maneno.
• Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
• Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi au kwa kuyagawa
maneno marefu katika sehemu fupi fupi.
• Mwanafunzi aandike herufi za sauti alizosoma hewani au vitabuni.
• Mwanafunzi aweza kufinyanga maumbo ya herufi.
• Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa
wakiwa wawili wawili.
• Mwanafunzi aweza kutumia vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi,
projekta na kipasa sauti kusikiliza na kusoma hadithi.
• Mwanafunzi anakili herufi na maneno yanayotokana na sauti
alizofunzwa.
• Mwanafunzi asikilize imla inayojumuisha maneno yaliyo na herufi za
sauti lengwa na kuyaandika.
III. Nyenzo:
ØKadi za herufi g, d, j na r;
ØRekodi za sauti /g/, /d/, /j/ na /r/;
ØMgeni mwalikwa mwenye matamshi sahihi;
ØWanafunzi wenyewe;
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 2;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
6
I V. Maandalizi ya somo
Mada hii inahusu sauti na majina ya herufi za Kiswahili. Herufi na sauti
zitakazoangaziwa katika funzo hili ni: /g/, /d/, /j/ na /r/. Matamshi mazuri
na sahihi ya wanafunzi yatazingatiwa hapa na kukuzwa zaidi.
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi. Vifaa
hivi ni kama vile: rekodi za matamshi ya sauti husika, mgeni mwalikwa mwenye
matamshi mazuri na sahihi, kadi zenye herufi na sauti husika pamoja na vyombo
vingine maalum vya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa alivyovileta darasani. Mwalimu akumbuke kuwa matumizi
ya michoro, picha, vifaa halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha
ufundishaji wa wanafunzi; hasa wale ambao wana matatizo mbalimbali katika
kuelewa na kufahamu haraka yale wanayofundishwa darasani au wale walio na
kiwango cha chini katika ujifunzaji wao.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia mwalimu awasaidie
kuvionyesha vifaa vilivyopo kwa wao kuvigusa huku wakiandika maelezo yake
ubaoni. Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi
kuandaa maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii
kujifundisha kama wanafunzi wengine.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa
katika Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize somo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu shule yao. Wanafunzi wajibu maamkuzi ya mwalimu
kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kuchunguza mchoro ulio katika
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 2. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa
7
kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na mchoro huo. Baadhi ya maswali
ambayo mwalimu anaweza kuuliza ni kama vile: Mnaona nini kwenye mchoro
huu? Mwalimu awaelekeze wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo na
kuelewa kinachoendelea katika mchoro uliopo.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
i) Sauti /g/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 3.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti za kwanza za majina hayo pekee. Wanafunzi
watamke sauti /g/ baada ya mwalimu kisha wakiwa wawili wawili na hatimaye
atamke sauti hii akiwa pekee yake. Mwalimu awaombe wanafunzi waandike
sauti /g/ katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi ‘g’, ambazo ni: ga, ge gi, go, gu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ‘g’. Kwa mfano: gani, gari, ganda, gereza, gereji, giza, gilasi, gorofa, godoro,
gurudumu, gundi, gunia n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika
kutamka maneno yenye silabi za herufi ‘g’ kwa usahihi. Hatimaye watunge
sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Gari limepita hapa.
2. Gereza hili ni safi.
3. Nyumba hii ina giza.
4. Baba alinunua godoro.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ‘g’.
8
ii) Sauti /d/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 6.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti za kwanza za majina hayo pekee. Wanafunzi
watamke sauti /d/ baada ya mwalimu kisha wakiwa wawili wawili na hatimaye
atamke sauti hii akiwa pekee yake. Mwalimu awaombe wanafunzi waandike
sauti /d/ katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi ‘d’, ambazo ni: da, de di, do, du.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi d. Kwa mfano: daka, dada, dakika, dereva, deski, dirisha, didimia, dondoka,
donda, doli, duka, dubu, duma n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote
katika kutamka maneno yenye silabi za herufi d kwa usahihi. Hatimaye watunge
sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Dada amefika.
2. Dereva anaendesha gari.
3. Dirisha hili limefungwa.
4. Mtoto anacheza na doli.
5. Duka hili lina mikate mingi.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi d ’.
iii) Sauti /j/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 9.
9
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti za kwanza za majina hayo pekee. Wanafunzi
watamke sauti /j/ baada ya mwalimu kisha wakiwa wawili wawili na hatimaye
atamke sauti hii akiwa pekee yake. Mwalimu awaombe wanafunzi waandike
sauti /j/ katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o,
u kisha watambue silabi za herufi j, ambazo ni: ja, je, ji, jo, ju.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi j. Kwa mfano: jagi, jamani, jaa, jembe, jenereta, jimbi, jirani, joto, joka,
jungu, juma, Jumatatu n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika
kutamka maneno yenye silabi za herufi j kwa usahihi. Hatimaye watunge
sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Jagi hili lina maji.
2. Mkulima anatumia jembe.
3. Huyu ni jirani yetu.
4. Mtoto ana joto jingi.
5. Leo ni siku ya Jumatatu.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ‘j’.
iv) Sauti /r/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 13.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
10
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti za kwanza za majina hayo pekee. Wanafunzi
watamke sauti /r/ baada ya mwalimu kisha wakiwa wawili wawili na hatimaye
atamke sauti hii akiwa pekee yake. Mwalimu awaombe wanafunzi waandike
sauti /r/ katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi ‘r’, ambazo ni: ra, re, ri, ro, ru.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ‘r’. Kwa mfano: raba, ramba, reki, reli, ringa, risiti, roga, robota, roketi,
rungu, ruka, rula n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka
maneno yenye silabi za herufi ‘r’ kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi
wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Raba hii ni ya Murkomen.
2. Garimoshi hupita mwenye reli.
3. Hili ni rinda zuri.
4. Hii ni roketi.
5. Rula yangu umevunjika.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ‘r’.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kufanya zoezi la imla.
Awasomee sentensi zifuatazo kisha wanafunzi waziandike kwenye madaftari
yao.
Zoezi la imla
1. Gunia lilikuwa na wadudu jana.
2. Dereva aliingia ndani ya duka akanunua kiberiti.
3. Rula yangu ni ndogo.
4. Dawa ya maji ina rangi ya kijani.
5. Shuleni kuna watoto werevu na wajanja.
11
Mwalimu ahakikishe anatamka maneno ya sentensi hizo kwa sauti na
matamshi sahihi. Baadaye, mwalimu asahihishe makosa ya maendelezo.
Mwalimu anaweza kuziandika sentensi za imla kwenye ubao na wanafunzi
waliokosea wakafanya masahihisho.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo hili kuhusu sauti /g/, /d/, /j/
na /r/ kwa kuwauliza wanafunzi maswali tofauti kuhusu mambo muhimu
waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo uwezo wa wanafunzi wa
kutamka sauti /g/, /d/, /j/ na /r/ kwa usahihi, kutambua na kutamka
maneno yenye sauti hizi kwa usahihi pamoja na kutunga sentensi sahihi
kwa kutumia maneno yenye sauti hizi walizojifundisha. Vilevile, mwalimu
achunguze iwapo wanafunzi wanaweza kuandika sauti hizo kwa usahihi.
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 2
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali, ukurasa 2
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
a) gunia b) gari ch) goti d) gitaa
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 3
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali, ukurasa 6
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
a) dawati b) debe ch) dirisha d) duka
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
12
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 8
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali, ukurasa 9 -10
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
a) jagi b) jembe ch) jiko d) jogoo
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 10
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali, ukurasa 13
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
a) raba b) redio ch) rinda d) rula
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 14
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Zoezi la imla, ukurasa 16
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wanaandika kwa usahihi sentensi
atakazowasomea.
13
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Maamkizi ya
nyakati za siku
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua maneno yatumiwayo katika maamkuzi ya nyakati za siku
shuleni kwa mawasiliano mwafaka;
b) Kuamkua na kuitikia maamkuzi ya nyakati za siku shuleni katika
kuimarisha mawasiliano;
ch) Kusoma maneno yanayotumiwa katika maamkuzi shuleni katika
kuimarisha stadi ya kusoma;
d) Kufafanua umuhimu wa salamu shuleni ili kuimarisha mawasiliano;
e) Kufurahia kuamkua wenzake, wafanyakazi na walimu shuleni katika
kujenga mshikamano wa jamii.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
• Mwanafunzi aigize maamkuzi mbalimbali ya nyakati za siku, kwa mfano:
habari ya asubuhi, jioni, mchana, umeamkaje na umeshindaje;
• Mwanafunzi aweza kuonyeshwa mchoro wa watu wawili wakisalimiana
halafu aongozwe katika kujadili picha;
• Wanafunzi wasalimiane na kisha washirikishwe katika mjadala kuhusu
maamkuzi;
• Wanafunzi waweza kuwekwa katika vikundi ili wajadili umuhimu wa
maamkuzi;
• Mwanafunzi aweza kutazama video inayoonyesha watu wakitumia
maamkuzi ya nyakati za siku;
• Mwanafunzi asome maamkuzi ya nyakati za siku katika kadi na chati.
14
III. Nyenzo:
ØMichoro ya watu wakisalimiana;
ØRekodi za maamkuzi ya nyakati za siku;
ØVideo ya maamkuzi;
ØWanafunzi wenyewe;
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 16;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Mwalimu aandae funzo hili kwa namna ya kumwezesha mwanafunzi kupata
ujuzi unaofaa kuhusu jinsi ya kuamkua na kuitikia salamu za nyakati mbalimbali
za siku. Ili kufanikisha lengo hili, mwalimu ahakikishe kuwa ameandaa vifaa vya
kutosha na vinavyofaa katika ufundishaji wa mada hii. Iwapo ataweza kuandaa
video ya jinsi ya kuamkua na kuitikia maamkuzi ya nyakati mbalimbali za siku,
afanye hivyo kabla ya kipindi hiki. Pia, michoro na picha za watu mbalimbali
wakisalimiana zinaweza kutayarishwa mapema.
Iwapo kuna wanafunzi wasioweza kuona au kusikia, ni lazima mwalimu atafute
namna ya kuwaelekeza kuelewa funzo hili aidha kwa kutumia lugha ya ishara
au breli huku maelezo mengine yakiandikwa ubaoni.
Ni vyema pia mwalimu ahakikishe kwamba wanafunzi wamejigawa katika
makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa
kwenye kitabu cha mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize funzo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mbalimbali kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia kuhusu sauti
na herufi za Kiswahili. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali
waliyoulizwa.
15
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awaombe wanafunzi wajigawe katika makundi ya wanafunzi watatu
watatu ili watazame michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa
17 na kujibu maswali waliyopewa. Kisha waigize maamkuzi wanayoyaona
kwenye michoro hiyo. Mwalimu azunguke darasani akiwaelekeza wanafunzi
wanaotatizika katika makundi yao. Baadaye, wanafunzi wanaweza kuigiza
maamkuzi hayo mbele ya wanafunzi wenzao. Shughuli hii itakuza ujasiri wa
wanafunzi wa kusimama na kuzungumza mbele ya watu. Mwalimu ahakikishe
kuwa anakosoa makosa ya wanafunzi ya kimatamshi pindi yanapotokea.
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, wanafunzi wafanye zoezi la
makundi lililo katika kitabu chao ambapo watahitajika kuigiza salamu za nyakati
mbalimbali za siku.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi kutazama michoro mbalimbali ya
watu wakisalimiana katika nyakati tofauti za siku. Baada ya haya, wanafunzi
wajibu maswali waliyopewa kuhusiana na michoro hiyo.
Katika majadiliano ya wanafunzi, mwalimu awashirikishe wanafunzi kueleza
umuhimu wa kusalimiana.
Baadhi ya majibu yao yanaweza kuwa:
1. Kusalimiana huwezesha kujuliana hali.
2. Kusalimiana huonyesha urafiki.
3. Salamu huonyesha upendo.
4. Salamu huleta amani na furaha.
5. Kusalimiana huwasaidia watu kujuana na kuelewana n.k
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wote wanashirikishwa katika majadiliano haya.
ch) Tathmini
Katika sehemu hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali tofauti kwa kurejelea
waliyojifundisha katika funzo hili. Wanafunzi wadhihirishe ujuzi wao wa kuamkua
na kuitikia salamu za nyakati mbalimbali za siku.
16
Mwalimu achunguze uwezo wa wanafunzi wa kuigiza maamkuzi mbalimbali
pamoja na kujadiliana kuhusu umuhimu wa maamkuzi kwa wanajamii.
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 17
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Zoezi la makundi, ukurasa 18
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Kwa mfano:
1. Habari ya asubuhi? / Umeamkaje?
2. Habari ya mchana? / Umeshindaje?
3. Habari ya jioni? / Umeshindaje?
4. Umeamkaje? / Habari ya asubuhi?
Maswali, ukurasa 21
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Mada Ndogo 3: Msamiati
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua kwa kutaja msamiati wa shuleni katika kuimarisha umilisi wa
lugha;
b) Kutumia msamiati wa shuleni katika mawasiliano ya kila siku;
ch) Kusoma maneno na sentensi zinazojumuisha msamiati wa shuleni katika
kuimarisha stadi ya kusoma;
17
d) Kuandika maneno ya sentensi fupi kuhusu shule ili kuimarisha stadi ya
kuandika;
e) Kufurahia kutumia msamiati wa shule katika mawasiliano ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
• Mwanafunzi aonyeshwe vifaa halisi, picha au michoro ya vitu
vinavyopatikana shuleni kama vile: ofisi, maktaba, vyoo, darasa,
bendera na gwaride;
• Mwanafunzi achore maumbo ya vifaa vinavyopatikana shuleni;
• Wanafunzi waambatanishe kadi za maneno na vifaa halisi wakiwa katika
vikundi;
• Wanafunzi waweza kushiriki katika nyimbo na mashairi kuhusu shule;
• Mwanafunzi aandike majina ya vitu vinavyopatikana shuleni;
• Mwanafunzi asome msamiati wa shuleni katika kadi au chati;
• Mwanafunzi atunge na asome sentensi akitumia msamiati wa shuleni.
III. Nyenzo:
ØMichoro au picha za vifaa vya shuleni;
ØVifaa halisi vya shuleni,
ØWanafunzi wenyewe;
ØKadi zenye majina ya vifaa halisi vya shuleni;
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 21;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu msamiati wa vifaa vya shuleni. Mwalimu ahakikishe
kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kuwaelekeza
wanafunzi ipasavyo. Anaweza kutumia vifaa halisi vya shuleni, michoro au
18
picha za vifaa vyenyewe. Mwalimu anaweza kuwatoa wanafunzi nje ya darasa
na kuwaonyesha maktaba, vyoo, madarasa mengine, eneo la gwaride, bendera na
hata ofisi mbalimbali.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
maamkuzi ya nyakati za siku. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja
na maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha
zoezi walilopewa katika kipindi kilichotangulia na wanafunzi wenye matatizo
wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kufahamu msamiati wa vifaa vya
shuleni. Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu
watatu kisha awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi,
ukurasa 21. Wanafunzi wachunguze michoro hiyo ya vifaa mbalimbali vya
shuleni na kuijadili. Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali mepesi
kuhusiana na michoro hiyo kama vile: Taja majina ya vifaa mnavyoona. Mwalimu
awape wanafunzi mwongozo wa kujibu maswali hayo kwa kitangulizi kama vile
“Mimi ninaona…..
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika shughuli hii. Baadaye mwalimu
awaelekeze wanafunzi kujibu maswali waliyopewa vitabuni mwao. Wanafunzi
wataje vifa kama vile: maktaba, madarasa, vyoo, eneo la gwaride, bendera n.k.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika kusoma na kutunga sentensi
sahihi wakitumia majina ya vifaa vya shuleni.
Kwa mfano:
1. Hii ni ofisi ya mwalimu mkuu.
2. Darasa hili ni safi.
19
3. Maktaba yana vitabu vingi.
4. Bendera inapepea.
5. Wanafunzi wamesimama kwenye gwaride.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika kufahamu umuhimu
wa vifaa mbalimbali vya shuleni, kwa mfano: maktaba kuhifadhi vitabu vya
kusoma; gwaride mahali pa kupandisha bendera na kupewa matangazo na
viongozi wa shule, madarasa mahali pa wanafunzi kusomea n.k.
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wanaopata matatizo katika ujifundishaji wao
wanasaidiwa.
ch) Tathmini
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali kuhusiana na waliyofundishwa
katika funzo hili kwa lengo la kuchunguza iwapo wanaweza kutambua na
kutaja majina ya vifaa mbalimbali vya shuleni. Pia, mwalimu achunguze iwapo
wanafunzi wamefahamu matumizi ya vifaa mbalimbali vya shuleni.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi yaliyo katika vitabu
vyao.
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 21
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na michoro waliyopewa.
Zoezi la makundi, ukurasa 22-23
1. Hii ni bendera. 2. Huku ni shuleni. 3. Hili ni dawati.
4. Hizi ni chaki. 5. Hiki ni choo.
Maswali, ukurasa 23-24
1. Shulen i 2. Maktabani 3. Chooni/Msalani
4. Gwaride 5. Bendera 6. Ofisi
7. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
8. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
20
Mada Ndogo 4: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
a) Kutaja majina ya vitu vinavyopatikana shuleni ili kuimarisha stadi ya
kuzungumza;
b) Kuelezea vitu vinavyopatikana shuleni ili kuimarisha stadi ya kusikiliza;
ch) Kusikiliza kwa makini masimulizi ili kuimarisha stadi ya kusikiliza;
d) Kusimulia kuhusu vitu mbalimbali vinavyopatikana shuleni ili kuimarisha
stadi ya kusikiliza;
e) Kuthamini umuhimu wa vitu vinavyopatikana shuleni.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
• Mwanafunzi asimulie kisa kuhusu shule;
• Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu vifaa vinavyopatikana
shuleni;
• Mwanafunzi afafanue umuhimu wa vitu vinavyopatikana shuleni;
• Mwanafunzi aweza kushiriki katika nyimbo au mashairi kuhusu vifaa
vinavyopatikana shuleni;
• Mwanafunzi atazame picha pamoja na michoro inayoonyesha vifaa
vinavyopatikana shuleni kisha wajadiliane katika vikundi.
III. Nyenzo:
ØRekodi za hadithi bunifu mbalimbali;
ØMichoro au picha za hadithi bunifu mbalimbali;
ØVifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
ØWanafunzi wenyewe;
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 24-26;
21
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusoma masimulizi ya
kubuni ili kujenga stadi yao ya kusikiliza na kusoma. Mwalimu ahakikishe
kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha
ufundishaji wake. Mwalimu anaweza kuwaonyesha wanafunzi michoro au picha
za masimulizi bunifu ambazo atawasomea wanafunzi darasani na nyingine
watajisomea wenyewe. Mwalimu anaweza hata kumwalika mtambaji au
msomaji mashuhuri akawasomea wanafunzi masimulizi bunifu kisha wanafunzi
wakasoma baada yake. Mwalimu ahakikishe kuwa mwalikwa huyu ana uwezo
wa kusoma kwa sauti ya kusikika na kwa matamshi sahihi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwaamkua wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
vifaa mbalimbali vya shuleni. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja
na maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wasahihishe zoezi
walilopewa katika kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika
zoezi hili wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza pamoja na kusoma masimulizi bunifu. Mwalimu awagawe
wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha awaombe watazame
michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 24. Wanafunzi wachunguze
mchoro huo na kuujadili katika makundi yao. Mwalimu anaweza kuwauliza
22
wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na mchoro huo kama vile: Unaona nini
kwenye mchoro huu? Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu
maswali waliyoulizwa kwa kuwapa kitangulizi kama vile “Mimi ninaona…..
Mwalimu ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote katika majadiliano
haya. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na wanayoona katika
michoro waliyopewa.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi masimulizi yafuatayo.
Ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa makini. Pia, mwalimu ahakikishe
kuwa anasoma kwa matamshi sahihi na sauti ya kusikika.
Mfano wa hadithi
Siku ya kwanza nilipopelekwa shuleni, nilishangaa. Dada ndiye aliyenipeleka.
Alinipeleka kwenye ofisi ya mwalimu mkuu. Alitusalimia, “Habari ya asubuhi?”
Dada alijibu, “Njema. Nilishindwa kujibu.
Hapo shuleni niliona vitu vingi vya kunifurahisha. Niliona bendera ikipepea
hewani. Nilionyeshwa maktaba ya vitabu. Nilionyeshwa vyoo vya wanafunzi.
Hatimaye, nikapelekwa katika darasa. Nikaachwa ndani ya darasa ili niendelee
kusoma pamoja na wanafunzi wenzangu. Ninapenda masomo kweli.
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi walisikiliza masimulizi ya mwalimu kwa makini,
mwalimu awashirikishe katika kujibu maswali waliyopewa katika vitabu vyao.
Mwalimu azunguke darasani ili kuwasaidia wanafunzi wanaotatizika katika
makundi yao.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika kukariri shairi bunifu lililo
vitabuni mwao kuhusu Twende Shuleni’. Wanafunzi wakariri shairi hili kwa
mahadhi mbalimbali. Mwalimu awaelekeze katika kukariri huku kwa kuwapa
mahadhi mbalimbali. Wanafunzi wakariri shairi hilo katika makundi mawili
kisha wakariri wakiwa wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi apewe fursa
ya kukariri peke yake. Makosa ya matamshi yasahihishwe na mwalimu.
Baada ya kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi ameweza kukariri shairi husika kwa
usahihi, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao kujibu maswali
waliyopewa katika vitabu vyao pamoja na kubaini maana na matumizi ya
msamiati uliotumika katika shairi husika. Wanafunzi wanaotatizika wasaidiwe.
23
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma masimulizi bunifu.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kukariri
shairi kwa mahadhi mbalimbali na kuweza kujibu maswali ya shairi hilo kwa
usahihi kulingana na muktadha wa shairi husika.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi yaliyo katika vitabu
vyao.
VI. Majibu
Maswali ya masimulizi, ukurasa 25
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusiana na michoro waliyopewa
katika vitabu vyao.
Maswali ya hadithi, ukurasa 25
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano:
1. shuleni
2. dada yangu
3. ofisi
4. bendera
5. darasa
Maswali ya shairi, ukurasa 26
1. Wanafunzi wawili wawili wakariri shairi walilopewa.
2. Mwanafunzi mmoja mmoja akariri shairi walilopewa.
3. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano: shairi linahusu
kwenda shuleni ili kujionea vifaa mbalimbali ambavyo hupatikana shuleni.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano: maktaba, bendera,
ofisi, gwaride, vyoo n.k.
24
Mada Ndogo 5: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua picha za vitu vinavyopatikana shuleni katika kujenga stadi ya
kusoma;
b) Kuelezea picha katika hadithi ili kuimarisha stadi ya kuzungumza;
ch) Kusikiliza hadithi zikisomwa na mwalimu kuhusu vitu vinavyopatikana
shuleni ili kuimarisha umakinifu;
d) Kusoma hadithi kuhusu shule ili kuimarisha stadi ya kusoma;
e) Kufahamu hadithi aliyoisoma katika kupata mafunzo ya hadithi;
f) Kuchangamkia kusoma hadithi kuhusu shule.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
• Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi;
• Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi;
• Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi;
• Mwanafunzi asikize mwalimu anaposoma hadithi kisha asome pamoja
na mwalimu na baadaye asome peke yake kwa sauti;
• Wanafunzi wasomeane hadithi wakiwa wawili wawili au katika vikundi;
• Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kwenye vifaa vya
teknolojia k.v. tarakilishi na kinasasauti na kufuatilia yanayosomwa
kwenye projekta;
• Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kutoka kwa kitabu mbele ya darasa;
• Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi;
• Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali yanayotokana na hadithi
aliyosoma na kusomewa;
• Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.
25
III. Nyenzo:
ØMichoro au picha za hadithi bunifu mbalimbali;
ØVifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu, projekta;
ØWanafunzi wenyewe;
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 27-28;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu ili kujenga stadi ya wanafunzi
ya kusikiliza na kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa
vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake. Mwalimu
anaweza kuwaonyesha wanafunzi michoro au picha za hadithi bunifu ambazo
atawasomea wanafunzi darasani na nyingine ambazo watajisomea wenyewe.
Mwalimu anaweza hata kumwalika mtambaji au msomaji mashuhuri
akawasomea wanafunzi hadithi bunifu kisha wanafunzi wakasoma baada yake
katika makundi makubwa hadi kusoma mwanafunzi mmoja mmoja. Mwalikwa
huyu sharti awe na uwezo wa kusoma kwa sauti ya kusikika na kwa matamshi
sahihi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwaamkua wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi wajibu maamkuzi ya mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
funzo la hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe.
26
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao
ya kusikiliza pamoja na kusoma hadithi bunifu. Mwalimu awagawe wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha awaombe watazame michoro
iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 27. Wanafunzi wachunguze michoro
hiyo na kuijadili katika makundi yao. Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi
maswali mepesi kuhusiana na michoro hiyo kama vile: Unaona nini kwenye
michoro hii? Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu maswali
waliyoulizwa kwa kuwapa kitangulizi kama vile “Mimi ninaona….. Mwalimu
ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote katika majadiliano haya.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi hadithi ifuatayo.
Ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa makini. Pia, mwalimu ahakikishe
kuwa anasoma hadithi hiyo kwa matamshi sahihi na sauti ya kusikika.
Mfano wa hadithi
Mtoto mzuri shuleni
Mtoto mzuri huenda shuleni kusoma. Mtoto mzuri ana heshima na adabu njema.
Mtoto mzuri anasimama kwa heshima kwenye gwaride. Hapa ni penye gwaride.
Mtoto mzuri ananyamaza wakati bendera inapopeperushwa mlingotini. Mtoto
mzuri akiwa ndani ya darasa hunyamaza na kumsikiliza mwalimu. Akienda
kwenye maktaba husoma kimya kimya. Akienda msalani au chooni, hachafui
choo.
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi walisikiliza hadithi ya mwalimu kwa makini,
mwalimu awashirikishe katika kujibu maswali waliyopewa katika vitabu vyao.
Mwalimu azunguke darasani ili kuwasaidia wanafunzi wanaotatizika katika
makundi yao.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika kusoma hadithi bunifu
iliyo vitabuni mwao kuhusu mtoto mzuri. Wanafunzi wasome hadithi hiyo
katika makundi mawili kisha wasome wakiwa wawili wawili na hatimaye kila
mwanafunzi apewe fursa ya kusoma pekee yake. Mwalimu ahakikishe anakosoa
makosa yoyote ya matamshi pindi tu yanapotokea.
Baada ya kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi amesoma hadithi hiyo kwa
27
usahihi, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao kujibu maswali
waliyopewa katika vitabu vyao. Maswali hayo yanahusu hadithi waliyoisoma
darasani. Wanafunzi wanaotatizika wasaidiwe.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya kuchunguza
iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi za kubuni. Pia, mwalimu
achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kusoma hadithi na kuweza
kujibu maswali ya hadithi hiyo kwa usahihi kulingana na muktadha wa hadithi
hiyo.
VI. Majibu
Maswali ya hadithi, ukurasa 27
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano: mtoto mzuri huenda
shuleni, huwa na heshima na adabu n.k.
3. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano: mtoto mzuri
husimama kwa heshima.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano: mtoto mzuri
hunyamaza bendera inapopeperushwa mlingotini.
5. Wanafunzi wasikilize hadithi ya mwalimu.
Maswali ya hadithi, ukurasa 28
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano: mtoto mzuri
hatukani wenzake, haogopi mwalimu, hapigani na wanafunzi wengine n.k.
2. Mtoto mzuri anapendwa na mama, baba, watoto wengine, msimulizi,
Mungu n.k.
3. Ofisi ya mwalimu.
4. Mzuri.
5. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
6. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
28
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua nambari 11-50 kwa maneno ili kuimarisha mawasiliano;
b) Kusoma nambari 11-50 kwa maneno ili kujenga stadi ya kusoma;
ch) Kuandika nambari 11-50 kwa maneno ili kujenga stadi ya kuandika;
d) Kuchangamkia kutumia nambari 11-50 kwa maneno katika mazungumzo
yake.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
• Mwanafunzi asome majina ya nambari 11-50;
• Wanafunzi wasome kadi za nambari 11-50 na majina yake ili
kuziambatanisha katika vikundi;
• Mwanafunzi aandike nambari 11-50;
• Wanafunzi waweza kupanga upya majina yaliyoparaganywa ya nambari
11-50 wakiwa wawili wawili au katika vikundi;
• Mwanafunzi atunge sentensi akitumia majina ya nambari 11-50;
• Mwanafunzi aweza kutazama vibonzo vikitaja nambari 11 hadi 50
kwenye tarakilishi.
III. Nyenzo:
ØKadi za nambari 11-50;
ØVifaa halisi vya kuhesabu darasani kama vile: peremende, kalamu, raba
n.k.,
ØMichoro au picha za vitu katika idadi mbalimbali;
ØWanafunzi wenyewe;
Mada Ndogo 6: Msamiati: Nambari 11-50
(Idadi ya vipindi: 3)
29
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 29-31;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu msamiati wa kuhesabu nambari kutoka 11-50. Mwalimu
ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili
kuwaelekeza wanafunzi ipasavyo. Anaweza kutumia vifaa halisi vya wanafunzi
ambavyo wanaweza kuhesabu kama vile: kalamu, raba, rula, madaftari, vitabu,
michoro au picha ya vifaa katika idadi mbalimbali n.k. Mwalimu anaweza
pia kuleta vitu kama vile: peremende, mahindi, maharagwe n.k. ili wanafunzi
wahesabu darasani.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwaamkua wanafunzi kisha awaulize
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi
wajibu maamkuzi ya mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wenye matatizo wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kufahamu jinsi ya
kuhesabu nambari 11-50 kwa nambari na kwa maneno. Mwalimu awagawe
wanafunzi katika makundi ya wawili wawili kisha awaombe wahesabu nambari
zilizo katika kadi walizopewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 30.
Wanafunzi wachunguze kadi hizo na kuhesabu nambari mbalimbali zilizoandikwa
kwenye kadi hizo. Wanafunzi wasome nambari hizo katika makundi yao kisha
kila mwanafunzi ahesabu nambari hizo akiwa pekee yake.
30
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika shughuli hii ya kuhesabu.
Wanafunzi wahesabu:
11 kumi na moja, 12 kumi na mbili, 13 kumi na tatu, 14 kumi na nne, 15 -
kumi na tano, 16 kumi na sita, 17 kumi na saba, 18 kumi na nane, 19 kumi
na tisa, 20 ishirini, 21 ishirini na moja, 22 ishirini na mbili, 23 ishirini na
tatu, 24 ishirini na nne, 25 ishirini na tano, 26 ishirini na sita, 27 ishirini na
saba, 28 ishirini na nane, 29 ishirini na tisa, 30 thelathini.
Baadaye mwalimu awaelekeze wanafunzi kufanya zoezi walilopewa katika
vitabu vyao kuhusu kulinganisha nambari na maneno kwa usahihi.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wawili wawili katika kuhesabu nambari 41-
50 kwa nambari na maneno, yaani:
41 arubaini na moja, 42 arubaini na mbili, 43 arubaini na tatu, 44 arubaini
na nne, 45 - arubaini na tano, 46 arubaini na sita, 47 arubaini na saba, 48
arubaini na nane, 49 arubaini na tisa, 50 hamsini.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi wote katika kutunga sentensi sahihi
wakitumia nambari walizofundishwa, kwa mfano:
1. Mimi nina miaka kumi na mitatu.
2. Baba amenipa shilingi hamsini.
3. Tulikimbia kwa dakika ishirini.
4. Mtihani huu ni wa dakika thelathini.
5. Kitabu hiki kina kurasa arubaini na nne.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika funzo hili. Wanafunzi
wanaopata matatizo katika ujifundishaji wao wasaidiwe.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali tofauti kwa kuchunguza
iwapo wanaweza kuhesabu nambari 11-50 bila matatizo yoyote. Pia, mwalimu
achunguze iwapo wanafunzi wamefahamu kuandika nambari hizi kwa maneno
kwa usahihi. Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi yaliyo
katika vitabu vyao.
31
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 29
1. Mwalimu atathmini kuhesabu kwa wanafunzi, yaani:
11 kumi na moja, 12 kumi na mbili, 13 kumi na tatu, 14 kumi na nne,
15 - kumi na tano, 16 kumi na sita, 17 kumi na saba, 18 kumi na nane,
19 kumi na tisa, 20 ishirini, 21 ishirini na moja, 22 ishirini na mbili, 23
ishirini na tatu, 24 ishirini na nne, 25 ishirini na tano, 26 ishirini na sita,
27 ishirini na saba, 28 ishirini na nane, 29 ishirini na tisa, 30 thelathini.
2. Mwalimu atathmini kuhesabu kwa kila mwanafunzi mmoja mmoja.
3. 11 kumi na moja
4. 30 thelathini
5. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
6. 20 (ishirini) na 30 (thelathini)
Zoezi la kulinganisha nambari kwa maneno sahihi, ukurasa 30
Nambari Maneno
31 - Thelathini na moja
32 - Thelathini na mbili
33 - Thelathini na tatu
34 - Thelathini na nne
35 - Thelathini na tano
36 - Thelathini na sita
37 - Thelathini na saba
38 - Thelathini na nane
39 - Thelathini na tisa
40 - Arubaini
Zoezi la kuhesabu, ukurasa 30
Mwalimu atathmini kuhesabu kwa wanafunzi, yaani:
32
41 arubaini na moja, 42 arubaini na mbili, 43 arubaini na tatu, 44
arubaini na nne, 45 - arubaini na tano, 46 arubaini na sita, 47 arubaini na
saba, 48 arubaini na nane, 49 arubaini na tisa, 50 hamsini.
Maswali, ukurasa
1. Mwalimu atathmini kuhesabu kwa wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini kuhesabu kwa kila mwanafunzi.
3. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
4. 50 - hamsini
5. 41 arubaini na moja
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua matumizi yafaayo ya –ako na –enu katika mawasiliano;
b) Kusoma sentensi zinazojumuisha –ako na –enu katika kujenga stadi ya
kusoma;
ch) Kutumia –ako na –enu katika sentensi katika kuimarisha mawasiliano;
d) Kuandika sentensi zinazohusisha –ako na –enu katika kuimarisha stadi
ya kuandika;
e) Kuthamini matumizi ya –ako na –enu katika mawasiliano ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
• Mwanafunzi atunge sentensi zenye matumizi ya –ako na –enu.
• Mwanafunzi aandike sentensi zinazohusisha –ako na –enu.
• Mwanafunzi asome sentensi zenye kutumia maneno –ako na –enu.
• Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia –ako na –enu.
Mada Ndogo 7: Saru: Matumizi ya ‘-ako’ na ‘-enu’
(Idadi ya vipindi: 2)
33
• Mwanafunzi aweza kupewa zoezi la kujaza mapengo kwa tarakilishi
(mchezo wa kuvuta na kutia kapuni.
III. Nyenzo:
ØMichoro ya watu wakiashiria vifaa mbalimbali;
ØWanafunzi wenyewe;
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 31-33;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Sarufi ni kipengele muhimu katika ujifundishaji wa wanafunzi. Mwalimu anastahili
kutilia maanani dhana hii ili kuweza kuwahusisha wanafunzi kwa ukamilifu
katika somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla
ya vipindi hivi. Vifaa hivi ni kama vile: michoro ya watu mbalimbali wakiashiria
vitu mbalimbali kuonyesha kuwa ni ‘chako’ na ni ‘vyenu’. Wanafunzi watumiwe
sana katika funzo hili la kuonyesha -ako na -enu.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa
kuweka hadharani vifaa vyake kwa kukumbuka kuwa matumizi ya michoro,
picha na vifaa halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha ufundishaji
wa wanafunzi; hasa wale ambao wana matatizo mbalimbali katika kuelewa na
kufahamu haraka yale wanayofundishwa darasani au wale walio na kiwango
cha chini katika ujifunzaji wao.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa
maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha
kama wanafunzi wengine. Mwalimu atawaomba wanafunzi wa aina hii kuvigusa
vifaa vilivyopo wakivitolea maelezo. Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo
ya kusikia, wavionyeshe vifaa vilivyopo kwa kuvigusa huku wakiandika maelezo
yake ubaoni.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
34
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa
katika Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu awasalimie wanafunzi na kuwauliza maswali kuhusu waliyofundishwa
katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu kisha
wajibu maswali waliyoulizwa.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wane wanne kisha
awashirikishe wanafunzi wote katika kuchunguza michoro iliyo katika Kitabu
cha Mwanafunzi, ukurasa 31-32. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa
kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na michoro hiyo.
Katika hatua hii, wanafunzi watapata fursa ya kujifundisha kuhusu matumizi
ya ako na –enu katika mawasiliano. Mwalimu awagawe wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi wanne wanne kisha awaombe kuchukua mifuko ya
wenzao na kuwauliza kila kifaa kilicho mfukoni ni cha nani.
Kwa mfano:
Umoja Wingi
1. Kalamu hii ni yako. Kalamu hizi ni zenu.
2. Kitabu hiki ni chako. Vitabu hivi ni vyenu.
3. Raba hii ni yako. Raba hizi ni zenu.
4. Mfuko huu ni wako. Mifuko hii ni yenu.
Wanafunzi waelekezwe kutambua mabadiliko ya –ako katika umoja na kuwa
–enu katika wingi. Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika
shughuli hii katika makundi yao. Mwalimu awaeleze wanafunzi kuwa:
Matumizi ya –ako na –enu ni katika kurejelea nafsi ya pili umoja na wingi katika
Kiswahili. Mwalimu anaweza kuwagusia wanafunzi kidogo tu kuhusu nafsi ya
kwanza umoja na wingi ambayo ni mimi sisi, -angu etu.
Kwa mfano: kiti changu viti vyetu
35
ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa kwa kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana
kwa kutumia –ako na –enu. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wanaweza kutunga sentensi sahihi katika umoja na wingi kwa kutumia –ako
na –enu.
VI. Majibu
Zoezi, ukurasa 33
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Umoja Wingi
1. Hii ni rula yako. Hizi ni rula zenu.
2. Hili ni darasa lako. Haya ni madarasa yenu.
3. Hii ni ofisi yako. Hizi ni ofisi zenu.
4. Huyu ni mwalimu wako. Hawa ni walimu wenu.
5. Huu ni mkoba wako. Hii ni mikoba yenu.
36
Matokeo maalum yanayotarajiwa Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kukia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutamka sauti tatu za herufi
moja katika kuimarisha stadi ya
kuzungumza;
(b) Kutambua haki za watoto bila tatizo
ili kukabiliana na maisha vilivyo;
(ch) Kutaja haki zake ili kuimarisha ujuzi
wa masuala yanayomwathiri;
(d) Kutambua picha kuhusu haki za
watoto ili kuifahamu hadithi vizuri;
(e) Kutambua matumizi ya vizuri na
vibaya katika mawasiliano.
Mwanafunzi aweza kutambua sauti
/p/, /f/, na /v/ katika maneno.
Mwanafunzi afafanue msamiati
kuhusu haki za watoto k.v. ajira,
kuishi, haki, kuelimishwa, kupewa
malezi bora, matibabu, kutoteswa,
kupewa jina, chakula na mavazi.
Mwanafunzi ataje haki zake k.v.
kuishi, kuelimishwa, kupewa malezi
bora, matibabu, kutoteswa, kupewa
jina, chakula na mavazi.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi aweza kujaza mapengo
kwa kutumia vizuri na vibaya.
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
(a) Kazi ya vikundi.
(b) Michezo.
(ch) Nyimbo na mashairi kuhusu haki za watoto.
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Mazingira.
Mada Kuu 2: Haki Zangu
Idadi ya vipindi: 16
Sura ya
2
37
Nyenzo:
Rekodi za masimulizi mbalimbali;
Rekodi za nyimbo/mashairi kuhusu haki za watoto;
Kadi za herufi p, f na v;
Michoro au picha kuonyesha haki za watoto;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 34;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Mada hii inashughulikia sauti tatu za herufi p, f na v, msamiati wa haki za
watoto, masimulizi kuhusu haki za watoto pamoja na kusoma hadithi kuhusiana
na masuala ya haki za watoto. Pia, kipengele cha sarufi kuhusu matumizi ya
vizuri na vibaya yameangaziwa katika mada hii.
Lengo kuu la mada hii ni kumsaidia mwanafunzi kujenga stadi yake ya kusikiliza,
kufahamu msamiati kuhusu haki za watoto, kusimulia hadithi, kusoma hadithi,
pamoja na kufahamu matumizi ya vizuri na vibaya katika sentensi na
mazungumzo kwa jumla.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
• Uraia: haki za watoto wanafunzi wanahamasishwa kuhusu haki zao.
• Utangamano wa kijamii - wanafunzi watangamane na kufanya kazi
pamoja.
Msamiati maalum
Baadhi ya msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao
katika mada hii ni kama vile:
Msamiati
Maana
1.
haki
kitu unachostahili
2.
elimu
mafundisho shuleni na hata nyumbani
3.
makao
mahali pa kuishi
4.
mavazi
nguo za kuvaa
5.
watoto
watu walio na umri wa miaka isiyozidi kumi na minane
38
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Ili kuwashirikisha wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali, mwalimu
awe na vifaa maalum vya kuwasaidia wanafunzi wa aina hii katika ujifundishaji
wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri au
wajuzi wa lugha ya ishara.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kuona, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya breli pamoja na vifaa vya kunasia sauti. Haya yatawawezesha
wanafunzi hawa kusoma kama wanafunzi wenzao bila vikwazo vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya vipindi
Mada Ndogo 1: Sauti na majina ya herufi za Kiswahili
6
Mada Ndogo 2: Msamiati
3
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya vizuri na vibaya
2
JUMLA: 16
Mada Ndogo 1: Sauti na majina ya heru za Kiswahili
(Idadi ya vipindi: 6)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
(a) Kutamka sauti tatu za herufi moja katika kuimarisha stadi ya kuzungumza;
(b) Kutambua sauti za herufi moja zilizofunzwa katika maneno ili kuimarisha
stadi ya kuzungumza;
(ch) Kutambua majina ya herufi zinazowakilisha sauti lengwa katika
kuimarisha stadi ya kusoma;
(d) Kusoma herufi za sauti moja kwa ufasaha ili kuimarisha stadi ya kusoma;
(e) Kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa ili
kuimarisha stadi ya kusoma;
39
(f) Kusoma vifungu vilivyo na maneno yenye sauti lengwa ili kuimarisha
stadi ya kusoma;
(g) Kuandika herufi zinazowakilishwa na sauti lengwa ili kuimarisha stadi ya
kuandika;
(h) Kuchangamkia kutumia maneno yanayojumuisha sauti zilizofunzwa
katika mawasiliano ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
• Mwanafunzi aweza kutambua sauti /p/, /f/ na /v/ katika maneno.
• Mwanafunzi atamke sauti lengwa baada ya mwalimu, kisha watamke
pamoja na mwalimu na mwishowe atamke akiwa peke yake, wawili
wawili na katika darasa.
• Mwanafunzi atambue sauti alizosoma katika maneno.
• Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia (papaya) kutamkia sauti.
• Mwanafunzi atambue herufi zinazowakilisha sauti lengwa kwa kutumia
kadi za herufi.
• Mwanafunzi aambatanishe silabi kusoma maneno yanayotokana na
sauti lengwa.
• Mwanafunzi atenganishe silabi katika kutambua sehemu mbalimbali za
maneno.
• Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
• Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi au kuchanganua yaliyo
marefu zaidi.
• Mwanafunzi aandike herufi za sauti alizosoma hewani au vitabuni.
• Mwanafunzi aweza kufinyanga maumbo ya herufi.
• Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa
wakiwa wawili wawili.
• Mwanafunzi aweza kutumia vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi,
projekta na kinasasauti kusikiliza na kusoma hadithi.
40
• Mwanafunzi anakili herufi na maneno yanayotokana na sauti
alizofunzwa.
• Mwanafunzi asikilize imla inayojumuisha maneno yaliyo na herufi za
sauti lengwa na kuyaandika.
III. Nyenzo:
ØKadi za herufi p, f na v;
ØRekodi za sauti /p/, /f/ na /v/,
ØMgeni mwalikwa mwenye matamshi mazuri na sahihi;
ØWanafunzi wenyewe;
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 35 - 44;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Mada hii inahusu sauti na majina ya herufi za Kiswahili. Herufi na sauti
zitakazoangaziwa katika funzo hili ni: /p/, /f/ na /v/. Matamshi mazuri na
sahihi ya wanafunzi yatazingatiwa hapa na kukuzwa zaidi.
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi. Vifaa
hivi ni kama vile: rekodi za matamshi ya sauti husika, mgeni mwalikwa mwenye
matamshi mazuri na sahihi, kadi zenye herufi na sauti husika pamoja na vyombo
vingine maalum vya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa alivyovileta darasani. Mwalimu akumbuke kuwa matumizi
ya michoro, picha, vifaa halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha
ufundishaji wa wanafunzi; hasa wale ambao wana matatizo mbalimbali katika
kuelewa na kufahamu haraka yale wanayofundishwa darasani au wale walio na
kiwango cha chini katika ujifunzaji wao.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, mwalimu awasaidie
kuvionyesha vifaa vilivyopo kwa wao kuvigusa huku wakiandika maelezo yake
41
ubaoni. Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi
kuandaa maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii
kujifundisha kama wanafunzi wengine.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa
katika Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize somo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu salamu za
mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kuchunguza michoro iliyo katika
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 35. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa
kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na mchoro huo. Baadhi ya maswali
ambayo mwalimu anaweza kuuliza ni kama vile: Mnaona nini kwenye mchoro
huu? Mwalimu awaelekeze wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo na
kuelewa kinachoendelea katika mchoro waliopewa.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Vipindi 2
i) Sauti /p/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 35.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti za kwanza za majina hayo pekee. Wanafunzi
watamke sauti /p/ baada ya mwalimu kisha wakiwa wawili wawili na hatimaye
42
atamke sauti hii akiwa pekee yake. Mwalimu awaombe wanafunzi waandike
sauti /p/ katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi ‘p’, ambazo ni: pa, pe, pi, po, pu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ‘p’. Kwa mfano: papa, penda, popo, pika, punda, panda, paka, pesa, potea,
pumua n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno
yenye silabi za herufi ‘h’ kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia
maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Mama anapika wali.
2. Paka amelala.
3. Huyu ni punda.
4. Kaka anapenda kucheza.
5. Hizi ni pesa.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ‘p’.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /p/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) paka pa ka
ii) pesa pe sa
iii) popo po po
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi ‘p’.
43
Vipindi 2
ii) Sauti /f/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa
38-39. Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro
iliyopo. Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya
michoro hii. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti za kwanza za majina hayo pekee. Wanafunzi
watamke sauti /f/ baada ya mwalimu kisha wakiwa wawili wawili na hatimaye
kila mwanafunzi atamke sauti hii akiwa pekee yake. Mwalimu awaombe
wanafunzi waandike sauti /f/ katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi
ndogo.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o,
u kisha watambue silabi za herufi ‘f’, ambazo ni: fa, fe, fi, fo, fu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ‘f’. Kwa mfano: farasi, feri, fimbo, foleni, foronya, futa, faida, fedha, fika n.k.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye silabi
za herufi ‘f kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Hii ni fulana.
2. Mgeni amefika kwetu.
3. Huyu ni fundi wa redio.
4. Biashara hii ina faida.
5. Watoto wamepanga foleni.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ‘f’.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /f/, kwa mfano:
44
Neno Silabi
i) fulana fu la na
ii) fika fi ka
iii) foleni fo le ni
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi ‘f ’.
Vipindi 2
iii) Sauti /v/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 41.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti za kwanza za majina hayo pekee. Wanafunzi
watamke sauti /v/ baada ya mwalimu kisha wakiwa wawili wawili na hatimaye
atamke sauti hii akiwa pekee yake. Mwalimu awaombe wanafunzi waandike
sauti /v/ katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi ‘v’, ambazo ni: va, ve, vi, vo, vu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ‘v’. Kwa mfano: vaa, vua, valiwa, vuka, veli, vokali, vita, vurugu, vuma n.k.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye silabi
za herufi ‘v’ kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Mama amevaa rinda.
2. Habari zake zilivuma.
3. Mwanafunzi anavua nguo.
45
4. Watoto wanavuka daraja.
5. Hizi ni vokali.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ‘v’.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /v/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) vuka vu ka
ii) vita vi ta
iii) vuma vu ma
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi ‘v’.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo hili kuhusu sauti /p/, /f/ na /v/ kwa
kuwauliza wanafunzi maswali tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali haya yatilie mkazo uwezo wa wanafunzi wa kutamka sauti /p/, /f/
na /v/ kwa usahihi, kutambua na kutamka maneno yenye sauti hizi kwa
usahihi pamoja na kutunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno yenye sauti
hizi walizojifundisha. Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza
kuandika sauti hizo kwa usahihi.
VI. Majibu
Maswali, ukurasa35
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali, ukurasa 36
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
46
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 38
1. pe te
2. pa ta
3. po te a
4. pu a
5. pe nda
Maswali, ukurasa 39
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 41
1. fe ri
2. fa ha mu
3. fi ka
4. fu a
5. fa gi a
Maswali, ukurasa 42
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
47
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 44
1. va li sha 2. vu ka 3. vi ta
4. va mi a 5. vu ta
Mada Ndogo 2: Msamiati
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua haki za watoto bila tatizo ili kukabiliana na maisha vilivyo;
b) Kusoma msamiati kuhusu haki za watoto ili kuimarisha stadi ya kusoma;
ch) Kutunga sentensi akitumia msamiati wa haki za watoto ili kuwasiliana
ifaavyo;
d) Kuandika maneno na sentensi akitumia msamiati wa haki za watoto ili
kuimarisha stadi ya kuandika;
e) Kuthamini haki za watoto katika maisha ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi afafanue msamiati kuhusu haki za watoto k.v. ajira, kuishi,
haki, kuelimisha, kupewa malezi bora, matibabu, kutoteswa, kupewa jina,
chakula na mavazi.
Mwanafunzi ajadiliane na wenzake kuhusu maana za msamiati wa haki za
watoto.
Mwanafunzi aandike msamiati wa haki za watoto.
Mwanafunzi atunge sentensi kwa kutumia msamiati wa haki za watoto.
48
Mwanafunzi aweza kushirikishwa katika kuimba nyimbo na kukariri
mashairi yanayohusu haki za watoto.
II. Nyenzo:
Kadi zenye kuonyesha haki za watoto;
Michoro ya matendo ya haki kwa watoto;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 44 - 47;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
III. Maandalizi ya somo
Ni muhimu kwa kila mtoto kufahamu kuhusu haki zake katika kiwango hiki.
Kama tunavyojua, mtoto ni mtu yeyote aliye na umri wa miaka isiyozidi kumi
na minane. Kwa hivyo, funzo hili ni muhimu sana kwa wanafunzi katika kiwango
hiki kwa sababu litawasaidia kujitambua na kujithamini zaidi.
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama
vilivyotajwa hapo juu. Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati
mwafaka wa kuweka hadharani vifaa alivyovileta darasani kwa kukumbuka
kuwa matumizi ya michoro, picha na kadi ni mbinu bora ambayo hutumika
kufanikisha ufundishaji wa wanafunzi.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, wavionyeshe vifaa vilivyopo
kwa kuvigusa huku wakiandika maelezo yake ubaoni. Ikiwa kuna wanafunzi
wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa maelezo yake kwenye
breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha kama wanafunzi
wengine.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwenye vitabu vyao.
49
IV. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu awaamkue wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu maamkuzi
ya mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusu
maisha yao, kwa mfano: Wewe hulala wapi? Wewe hula wapi? Nani hukununulia
nguo? Nani hukununulia chakula? n.k. Mwalimu ahakikishe anawashirikisha
wanafunzi wote katika shughuli hii. Hii itakuwa namna nzuri ya kutanguliza
funzo hili kuhusu haki za watoto.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 44.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Unaona nini? Watu hawa wanafanya nini? Wanafunzi wajibu
maswali ya mwalimu kulingana na wanayoyaona kwenye michoro waliyopewa.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne
wanne, waimbe wimbo kuhusu haki zao ulio katika vitabu vyao. Wanafunzi wote
washirikishwe katika shughuli hii. Wanafunzi waelekezwe kufahamu baadhi
ya haki zao kutokana na wimbo huo, kwa mfano: kupewa matibabu, makazi,
chakula, mavazi n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kujibu maswali
ya wimbo waliyopewa katika vitabu vyao.
Mwalimu awaombe wanafunzi katika makundi yao waimbe tena wimbo huo
wa haki kwa mahadhi mbalimbali katika makundi. Wanafunzi wajadiliane zaidi
kuhusu haki zao na iwapo wanazipokea au la. Mwalimu awe makini ili awasaidie
wanafunzi ambao huenda wanateseka katika jamii.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu haki zao kama watoto.
50
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 45
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali ya wimbo, ukurasa 46
1. Mtoto akiwa mgonjwa ana haki ya kupata matibabu.
2. Mtoto mwenye njaa ana haki ya kupata chakula.
3. Mtoto akizaliwa, ana haki kupewa jina.
4. Mtoto ana haki kupelekwa shuleni apate elimu.
5. Mtoto mdogo ana haki ya kupata mavazi.
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
a) Kutaja haki zake ili kuimarisha ujuzi wa masuala yanayomwathiri;
b) Kueleza umuhimu wa haki za watoto ili kujitetea haki zake zinapokiukwa;
ch) Kusimulia kuhusu haki zake ili kujenga stadi ya kuzungumza;
d) Kusikiliza masimulizi kuhusu haki za watoto ili kuimarisha umakinifu;
e) Kuthamini haki za watoto ili kuzitetea maishani.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ataje haki zake k.v. kuishi, kuelimishwa, kupewa malezi bora,
matibabu, kutoteswa, kupewa jina, chakula na mavazi;
Wanafunzi wajadili michoro, chati au picha zinazozingatia haki za watoto;
Mwanafunzi asimulie kisa kuhusu haki za watoto;
Mwanafunzi aweza kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu haki za
watoto;
Mwanafunzi aweza kutazama video kuhusu haki za watoto;
Mwanafunzi aweza kusikiliza mgeni mwalikwa akizungumza kuhusu haki
za watoto;
Wanafunzi waweza kujadilana kuhusu haki za watoto.
51
III. Nyenzo:
Rekodi za hadithi bunifu mbalimbali;
Michoro au picha za hadithi bunifu mbalimbali;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 47 - 48;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano, wanafunzi
wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusoma masimulizi bunifu
ili kujenga stadi yao ya kusikiliza na kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba
ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji
wake. Mwalimu anaweza kuwaonyesha wanafunzi michoro au picha za
masimulizi bunifu ambayo atawasomea wanafunzi darasani. Mwalimu anaweza
hata kumwalika mtambaji au msomaji mashuhuri akawasomea wanafunzi
masimulizi bunifu kisha wanafunzi wakasoma baada yake katika makundi na
hatimaye mmoja mmoja. Mwalimu ahakikishe kuwa mwalikwa huyu ana uwezo
wa kusoma kwa sauti ya kusikika na kwa matamshi sahihi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwaamkua wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
matamshi ya herufi ‘v’. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na
maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wasahihishe zoezi
walilopewa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wenye matatizo katika
zoezi hili wasaidiwe.
52
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza pamoja na kusoma masimulizi bunifu. Mwalimu awagawe
wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha awaombe watazame
michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 47. Wanafunzi wachunguze
michoro hiyo na kuijadili katika makundi yao. Mwalimu anaweza kuwauliza
wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro hiyo kama vile: Unaona nini
kwenye michoro hii? Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu
maswali waliyoulizwa. Mwalimu ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote
katika majadiliano haya. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na
wanayoona katika michoro waliyopewa.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi masimulizi yafuatayo.
Ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa makini. Pia, mwalimu ahakikishe
kuwa anasoma kwa matamshi sahihi na sauti ya kusikika.
Mfano wa masimulizi
HAKI ZA MTOTO
Kila mtoto ana haki zake. Mtoto ana haki ya kuishi. Ana haki ya kupelekwa shule
ili kupata elimu. Apate malezi bora. Apate matibabu bora. Mtoto anapozaliwa
ni haki apewe jina. Ni haki kupewa chakula bora cha kutosha. Ni haki kupewa
mavazi mazuri.
Sio haki kumchapa mtoto. Mtoto akifanya makosa, zungumza na yeye. Mwambie
matendo mazuri ya kutenda. Kumchapa mtoto ni unyama. Sio haki kamwe. Watoto
wanastahili kulindwa. Watoto wanastahili kupendwa. Watoto wawe salama.
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi walisikiliza masimulizi ya mwalimu kwa makini,
mwalimu awashirikishe katika kujibu maswali ya masimulizi waliyopewa katika
vitabu vyao. Mwalimu azunguke darasani akiwasaidia wanafunzi wanaotatizika
katika makundi yao.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi wote katika kusoma masimulizi
aliyowasomea katika makundi kisha mmoja mmoja. Mwalimu anaweza
kuandika masimulizi aliyosoma kwenye ubao, chati au hata kwenye tarakilishi
kisha wanafunzi wakajisomea. Mwalimu ahakikishe anakosoa makosa ya
kimatamshi pindi tu yanapotokea.
53
Shughuli hii itawawezesha wanafunzi kukuza stadi yao ya kusikiliza pamoja na
kusoma kwa ufasaha. Wanafunzi wenye matatizo mbalimbali wasaidiwe.
Mwalimu awe makini kwa kutambua wanafunzi ambao wanaweza kuwa
hawatendewi haki. Anaweza kuwasaidia kadri ya uwezo wake.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya kuchunguza
iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma masimulizi bunifu. Pia, mwalimu
achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kujibu maswali ya masimulizi
waliyosomewa.
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 47
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusiana na michoro waliyopewa
katika vitabu vyao.
Maswali ya masimulizi, ukurasa 48
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano:
1. Mtoto ana haki kadhaa kama vile: haki ya kuelimishwa, kula, kuishi,
kupewa matibabu, malezi bora, kupewa jina anapozaliwa n.k.
2. Mtoto asichapwe.
3. Kumtesa mtoto kwa kumchapa.
4. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
5. Sio haki bali ni unyama.
6. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
54
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua picha kuhusu haki za watoto ili kuifahamu hadithi vizuri;
b) Kusikiliza hadithi za mwalimu kuhusu haki za watoto katika kuimarisha stadi
ya kusikiliza na kusoma;
ch) Kusoma hadithi kuhusu haki za watoto katika kuimarisha stadi ya kusoma;
d) Kufahamu hadithi aliyoisoma mwenyewe au aliyosomewa ili kupata mafunzo
yanayolengwa;
e) Kuchangamkia kusoma hadithi kuhusu haki za watoto ili kuendeleza stadi
ya kusoma.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi;
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi;
Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi;
Mwanafunzi adhihirishe ufahamu wa matumizi ya msamiati uliotumika
kwenye hadithi;
Mwanafunzi aweza kusikiliza mwalimu anaposoma hadithi kisha asome na
mwalimu na baadaye asome peke yake, wakiwa wawili wawili au katika
vikundi;
Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kwa kutumia vifaa vya
teknolojia k.v. tarakilishi na projekta;
Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kutoka kwa jitabu mbele ya darasa;
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali yanayotokana na hadithi aliyosoma
na kusomewa;
Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.
III. Nyenzo:
Rekodi za hadithi bunifu;
55
Michoro au picha za hadithi bunifu mbalimbali;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu, projekta;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 48 - 49;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano, wanafunzi
wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu ili kujenga stadi ya wanafunzi
ya kusikiliza na kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa
vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake kama
vilivyotajwa hapo juu. Mwalimu anaweza kumwalika mtambaji au msomaji
mashuhuri akawasomea wanafunzi hadithi bunifu kisha wanafunzi wakasoma
baada yake katika makundi makubwa na hatimaye kila mwanafunzi kusoma
mmoja mmoja. Mwalikwa huyu sharti awe na uwezo wa kusoma kwa sauti ya
kusikika na kwa matamshi sahihi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwaamkua wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi wajibu maamkuzi ya mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
funzo la hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao
ya kusoma pamoja na kusikiliza hadithi bunifu. Mwalimu awagawe wanafunzi
56
katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha awaombe watazame mchoro
ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 48. Wanafunzi wachunguze mchoro
huo na kuujadili katika makundi yao. Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi
maswali mepesi kuhusiana na mchoro huo kama vile: Unaona nini kwenye
mchoro huu? Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu maswali
waliyoulizwa kwa kuwapa kitangulizi kama vile “Mimi ninaona….. Mwalimu
ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote katika majadiliano haya.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kujadili kuhusu
suala la ajira za watoto. Wanafunzi wafahamu kuwa sio haki kwa watoto wadogo
kuajiriwa ila ni haki yao kuelimishwa hadi wanapofikisha umri wa kujitegemea
wenyewe. Wanafunzi washirikishwe katika kusimulia mifano ya watoto ambao
wamewahi kukumbana nao walioajiriwa wangali wadogo. Waeleze hatima
ya watoto hao. Mwalimu awe makini kuwasaidia wanafunzi ambao huenda
wamekumbwa na suala hili la ajira za watoto.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika kusoma hadithi bunifu iliyo
vitabuni mwao kuhusu haki za mtoto. Wanafunzi wasome hadithi hiyo katika
makundi kisha wasome wakiwa wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi
apewe fursa ya kusoma pekee yake. Mwalimu ahakikishe anakosoa makosa
yoyote ya matamshi pindi tu yanapotokea.
Baada ya kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi amesoma hadithi hiyo kwa
usahihi, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao kujibu maswali
waliyopewa katika vitabu vyao. Maswali hayo yanahusu hadithi waliyoisoma
darasani. Wanafunzi wanaotatizika wasaidiwe.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusoma pamoja na kusikiliza hadithi
bunifu. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa
kusoma hadithi na kuweza kujibu maswali ya hadithi hiyo kwa usahihi kulingana
na muktadha wa hadithi hiyo.
57
VI. Majibu
Maswali ya hadithi, ukurasa 49
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali ya hadithi, ukurasa 49
1. Tamaa alitaka pesa za kunywa pombe.
2. Matibabu
3. Kazi ya kupasua mawe
4. Kwa polisi
5. Polisi
6. Daktari
7. Ndio
8. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Mada Ndogo 5: Saru: Matumizi ya ‘vizuri’ na ‘vibaya’
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua matumizi mazuri ya vizuri na vibaya katika mawasiliano;
b) Kutumia vizuri na vibaya katika sentensi sahili ili kuimarisha mawasiliano;
ch) Kusoma sentensi zinazojumuisha vizuri na vibaya ili kuimarisha usomaji
bora;
d) Kuandika sentensi kwa kujumuisha vizuri na vibaya ili kuimarisha uandishi
mwafaka;
e) Kuchangamkia matumizi ya vizuri na vibaya katika kuimarisha mawasiliano.
58
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia vizuri na vibaya.
Mwanafunzi aweza kubainisha matumizi ya vielezi vya jinsi vinavyofunzwa
kwa kutumia vifaa vya teknolojia.
Mwanafunzi arejelee vitu mbalimbali kwa kutumia vizuri na vibaya k.m
Mtoto amesoma vizuri.
Mwanafunzi aandike sentensi zinazojumuisha vizuri na vibaya.
III. Nyenzo:
Chati zenye sentensi zilizojumuisha matumizi ya vizuri na vibaya;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 50;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Kama tunavyofahamu, sarufi ni kipengele muhimu katika ujifundishaji wa
wanafunzi. Mwalimu anastahili kutilia maanani dhana hii ili kuweza kuwahusisha
wanafunzi kwa ukamilifu katika somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema
na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi. Wanafunzi wenyewe watumiwe sana katika
funzo hili la kuonyesha matumizi ya vizuri na vibaya.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa
maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha
kama wanafunzi wengine. Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia
mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya lugha ya ishara. Mwalimu anaweza
pia kumshirikisha mtaalamu wa lugha ya ishara katika kuwasaidia wanafunzi
wa aina hii.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba amewagawa wanafunzi katika makundi yanayotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi katika vitabu vya
wanafunzi.
59
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu awasalimie wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu salamu za
mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awashirikishe katika kusoma sentensi walizopewa katika vitabu vyao kuhusu
matumizi ya vizuri na vibaya. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi katika
makundi yao. Shughuli hii itawawezesha wanafunzi kufahamu matumizi ya
vizuri na vibaya. Wanafunzi wasimulie katika makundi yao kuhusu mambo
ambayo wao huyatenda vizuri na yale wanayoyatenda vibaya.
Kwa mfano:
1. Mimi ninaandika vizuri.
2. Baba analima vizuri.
3. Mtoto analia vibaya.
4. Mbwa anabweka vibaya.
Katika hatua hii ya wanafunzi kusimulia na kutunga sentensi kwa kutumia
vizuri na vibaya, wanafunzi watapata fursa ya kujifundisha kuhusu matumizi
ya vizuri na vibaya katika mawasiliano.
Wanafunzi waelekezwe kutambua kuwa vizuri ni kielezi cha kurejelea kufanya
jambo kwa jinsi inayotakikana na vibaya ni kielezi cha kurejelea kufanya jambo
kwa jinsi isiyotakikana.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mzoezi waliyopewa
katika vitabu vyao. Mwalimu awasaidie wanafunzi wanaotatizika katika kufanya
mazoezi haya.
60
ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa katika kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana
kwa kutumia vizuri na vibaya. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wanaweza kutunga sentensi sahihi kwa kutumia vizuri na vibaya.
VI. Majibu
Zoezi, ukurasa 50
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Zoezi, ukurasa 50
1. Fisi anakula vibaya.
2. Rafiki yangu anasoma vibaya.
3. Kasuku anaimba vizuri.
4. Shule yao ilijengwa vibaya.
5. Mzazi anataka niishi vizuri.
Zoezi la masimulizi, ukurasa 50
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kupitia kwa majadiliano yao kuhusu
mambo ambayo wao huyafanya vibaya na yale wanayoyafanya vizuri.
61
Matokeo maalum yanayotarajiwa Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kukia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutambua sauti za herufi mbili
zilizofunzwa ili kuimarisha stadi ya
kusikiliza na kuzungumza;
(b) Kutambua baadhi ya majina
ya vyombo vya usafiri katika
kuimarisha mawasiliano;
(ch) Kutambua kwa kutaja vyombo
mbalimbali vya usafiri ili kuimarisha
mawasiliano;
(d) Kutambua picha za vyombo
mbalimbali vya usafiri ili kuimarisha
ufahamu wa hadithi;
(e) Kubainisha matumizi ya herufi
kubwa ili kuimarisha mawasiliano
andishi.
Mwanafunzi atamke sauti lengwa
/ch/ na /dh/ baada ya mwalimu,
kisha watamke na mwalimu na
mwishowe atamke akiwa peke
yake, wawili na katika darasa.
Mwanafunzi atunge sentensi sahihi
akitumia msamiati wa vyombo
vya usafiri k.v. matatu, basi, lori,
pikipiki, garimoshi, gari ndogo,
ndege na meli.
Mwanafunzi atambue aina
mbalimbali za vyombo vya usafiri
k.v. matatu, basi, lori, pikipiki,
garimoshi, gari ndogo, ndege na
meli kwa kutumia picha au vyombo
vya teknolojia.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi aeleze matumizi ya
herufi kubwa.
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kazi ya vikundi.
Michezo.
Mada Kuu 3: Usari
Idadi ya vipindi: 13
Sura ya
3
62
Uhusiano na masomo mengine:
Somo kuhusu Mazingira na somo la Kiingereza.
Nyenzo:
Michoro au picha za vyombo mbalimbali vya usafiri;
Kadi zenye sauti /ch/na /dh/;
Mtambaji au msimulizi mwalikwa;
Rekodi ya masimulizi bunifu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 51;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Usafiri ni muhimu sana katika maisha ya binadamu kwa sababu huwawezesha
watu kutoka katika sehemu moja hadi nyingine. Kupitia kwa usafiri, watu
pia huweza kusafirisha mizigo kutoka mahali pamoja hadi mahali pengine.
Ni vyema kwa wanafunzi katika kiwango hiki kufundishwa kuhusu vyombo
mbalimbali vya usafiri kwa kuwa wanavitumia kila siku. Mwalimu ahakikishe
kuwa wanafunzi wote wanashirikishwa kupata maarifa haya.
Pia, mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kujenga stadi yake ya kutamka
sauti za herufi mbili ambazo ni: /ch/ na /dh/, kutamka maneno yenye sauti hizi
pamoja na kutunga sentensi kwa kutumia maneno yenye sauti hizi.
Mada hii itaangazia pia kukuza stadi ya kusoma na kusikiliza kupitia kwa
masimulizi na hadithi bunifu mbalimbali ambazo wanafunzi watasomewa na
nyingine watajisomea wenyewe.
Kipengele cha sarufi pia kitashughulikiwa katika mada hii ambapo wanafunzi
watafahamu matumizi ya herufi kubwa.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
• Elimu ya maendeleo endelevu usalama katika usafiri wanashughulikia
vyombo vya usafiri.
63
• Utangamano wa kijamii,
• Uzalendo: ushirikiano katika vikundi,
• Amani na maadili.
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii ni kuhusu vyombo mbalimbali vya usafiri kama vile:
Msamiati Maana
1.
meli
chombo cha kusafiria majini
2.
pikipiki
chombo chenye magurudumu mawili na chenye injini
3.
lori
aina ya gari kubwa la kubeba hasa mizigo mikubwa na mizito
4.
eropleni
chombo cha kusafiri angani au hewani
5.
basi
aina ya gari kubwa la kubebea abiria wengi
6.
garimoshi
chombo cha kusafiria kwenye reli na huwa na mabogi
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Mwalimu ahakikishe anawashughulikia na kuwashirikisha wanafunzi walio na
ulemavu na matatizo mbalimbali, kwa kuwa na vifaa maalum vya kuwasaidia
wanafunzi hawa katika ujifundishaji wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa
kuona, mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya breli pamoja na vifaa vya
kunasia sauti.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri wa
lugha ya ishara. Maandalizi haya yatawawezesha wanafunzi hawa kusoma kama
wanafunzi wenzao bila vikwazo vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya vipindi
Mada Ndogo 1: Sauti za herufi mbili za Kiswahili
4
Mada Ndogo 2: Msamiati
2
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya herufi kubwa
2
JUMLA: 13
64
Mada Ndogo 1: Sauti za heru mbili za Kiswahili
(Idadi ya vipindi: 4)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua sauti za herufi mbili zilizofunzwa ili kuimarisha stadi ya
kusikiliza na kuzungumza;
b) Kutamka sauti lengwa za herufi mbili ili kuimarisha stadi ya kuzungumza;
ch) Kusoma herufi za sauti mbili ili kuimarisha usomaji bora;
d) Kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa ili
kuimarisha usomaji bora;
e) Kusoma hadithi fupi zilizo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kuimarisha
usomaji bora;
f) Kuandika maneno kutokana na herufi alizofunzwa ili kuimarisha stadi ya
kuandika;
g) Kufurahia kutumia sauti zilizofunzwa katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atamke sauti lengwa /ch/ na /dh/ baada ya mwalimu, kisha
watamke na mwalimu na mwishowe atamke akiwa peke yake, wawili na
katika darasa.
Mwanafunzi atambue sauti lengwa katika maneno.
Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia kama vile papaya kutamkia sauti.
Mwanafunzi atambue herufi zinazowakilisha sauti lengwa kwa kutumia
kadi za herufi.
Mwanafunzi aambatanishe silabi kusoma maneno yanayotokana na sauti
lengwa.
Mwanafunzi atenganishe silabi katika kutambua sehemu mbalimbali za
maneno.
Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
Mwanafunzi aandike herufi za sauti alizosoma hewani na vitabuni.
65
Mwanafunzi aweza kufinyanga maumbo ya herufi inayowakilisha sauti
lengwa.
Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi na kuchanganua yaliyo
marefu zaidi.
Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa
wakiwa wawili wawili.
Mwanafunzi aweza kutumia vifaa vya teknolojia kama vile tarakilishi,
projekta na kinasasauti kusikiliza na kusoma hadithi.
Mwanafunzi anakili herufi na maneno yanayotokana na sauti alizofunzwa.
III. Nyenzo:
Kadi za herufi ‘ch’ na ‘dh’;
Rekodi za sauti /ch/ na /dh/,
Kadi zenye maneno yenye sauti /ch/ na /dh/,
Mgeni mwalikwa mwenye matamshi mazuri na sahihi;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 52 - 58;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano, wanafunzi
wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Mada hii inahusu sauti za herufi mbili za Kiswahili kwa kurejelea vyombo
mbalimbali vya usafiri. Herufi na sauti zitakazoangaziwa katika funzo hili ni:
ch, dh, /ch/ na /dh/. Matamshi mazuri na sahihi ya wanafunzi yatazingatiwa
hapa na kukuzwa zaidi. Wanafunzi walio na matatizo ya matamshi wasaidiwe
wakuze uwezo wa kutamka kwa usahihi. Wanafunzi wa aina hii washirikishwe
katika kufanya mazoezi ya utamkaji. Mwalimu awaongoze. Pia, wanafunzi
wengine wenye matamshi mazuri wanaweza kuwasaidia hawa wanaolemewa.
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi
kama vilivyotajwa hapo juu. Vyombo maalum vya kuwasaidia wanafunzi wenye
ulemavu na matatizo mbalimbali pia viandaliwe mapema.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa alivyovileta darasani. Mwalimu akumbuke kuwa matumizi ya
66
michoro, picha na vifaa halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha
ufundishaji wa wanafunzi; hasa wale ambao wana matatizo mbalimbali katika
kuelewa na kufahamu haraka yale wanayofundishwa darasani.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwenye vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize somo hili kwa kuwaamkua wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichopita. Wanafunzi wajibu
maamkuzi ya mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu
wachunguze michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 52-53
Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusiana
na michoro hiyo. Baadhi ya maswali ambayo mwalimu anaweza kuuliza ni
kama vile: Mnaona nani kwenye michoro hii? Mwalimu awaelekeze wanafunzi
ili waweze kujibu maswali hayo na kufahamu aina mbalimbali ya vyombo vya
usafiri katika michoro hiyo kama vile: basi, garimoshi, baiskeli, eropleni, pikipiki
na tuktuk.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
i) Sauti /ch/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 52-
53. Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kama vile: chakula, chura, choo, cherehani na chipsi kisha watamke
sauti ya kwanza pekee ya majina hayo. Wanafunzi watamke sauti /ch/ baada
ya mwalimu katika darasa zima kisha wakiwa wawili wawili na hatimaye kila
67
mwanafunzi atamke sauti hii akiwa pekee yake. Mwalimu awaombe wanafunzi
waandike sauti /ch/ katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
Yaani: ch na CH.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi ‘ch’, ambazo ni: cha, che, chi, cho, chu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ‘ch’. Kwa mfano: chama, cheka, chimba, choka, chungu, chapa, cheza,
chura n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno
yenye silabi za herufi ‘ch’ kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia
maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Mama anacheka.
2. Mlango wetu ni wa chuma.
3. Chungu kiko motoni.
4. Huyu ni chura.
5. Watoto wanakula chipsi.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ‘ch’.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /ch/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) cheza che za
ii) chura chu ra
iii) cherehani che re ha ni
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi ‘ch’.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusoma kifungu walichopewa
katika vitabu vyao kisha watambue maneno yenye sauti /ch/ katika kifungu
hicho.
68
ii) Sauti /dh/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaelekeze kutazama mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 56.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na mchoro uliopo.
Maswali kama vile: Unaona nini kwenye mchoro huu? Wanafunzi wajibu maswali
ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua jina sahihi la mchoro
waliopewa kisha watamke sauti ya kwanza ya jina hilo pekee. Wanafunzi
watamke sauti /dh/ baada ya mwalimu katika darasa zima kisha wakiwa
wawili wawili na hatimaye atamke sauti hii akiwa peke yake. Mwalimu awaombe
wanafunzi waandike sauti /dh/ katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi
ndogo. Yaani: dh na DH.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi ‘dh’, ambazo ni: dha, dhe, dhi, dho, dhu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ‘dh’. Kwa mfano: dhahabu, dhamani, dhehebu, dhoruba, dhani, dhoofika
n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye
silabi za herufi ‘dh’ kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno
hayo.
Kwa mfano:
1. Afya ya babu imedhoofika.
2. Tajiri anauza dhahabu.
3. Nilidhani unajua kusoma.
4. Hili ni dhehebu gani?
5. Kijiji hiki kilikumbwa na dhoruba kali.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ‘dh’.
69
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /dh/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) dhahabu dha ha bu
ii) dhani dha ni
iii) dhiki dhi ki
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi ‘dh’.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kusoma kifungu
walichopewa katika vitabu vyao kisha watambue herufi ‘dh’ katika maneno ya
kifungu hicho.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo hili kuhusu sauti /ch/ na /dh/ kwa
kuwauliza wanafunzi maswali tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali haya yatilie mkazo uwezo wa wanafunzi wa kutamka sauti /ch/ na
/dh/ kwa usahihi, kutambua na kutamka maneno yenye sauti hizi kwa usahihi
pamoja na kutunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno yenye sauti hizi
walizojifundisha. Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza
kuandika sauti hizo kwa usahihi kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 52
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali, ukurasa 53
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
70
Zoezi la makundi, ukurasa 55
1. Chungwa
2. Chupa
3. Chokaa
4. Chafua
5. Cheka
6. Chawa
Zoezi, ukurasa 56
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watambue sauti /ch/
katika hadithi waliyosoma.
Maswali, ukurasa 56
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali, ukurasa 58
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 58
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watambue sauti /dh/
katika hadithi waliyopewa.
71
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua baadhi ya majina ya vyombo vya usafiri katika kuimarisha
mawasiliano;
b) Kusoma majina ya vyombo vya usafiri na msamiati mwingine wa usafiri
katika sentensi ili kuimarisha usomaji bora;
ch) Kutumia msamiati wa usafiri kutungia sentensi katika kuimarisha stadi ya
kuzungumza na kuandika;
d) Kuandika majina ya vyombo vya usafiri na msamiati mwingine wa usafiri ili
kuimarisha stadi ya kuandika;
e) Kuthamini vyombo vya usafiri katika maisha ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atunge sentensi sahihi akitumia msamiati wa vyombo vya
usafiri k.v. matatu, basi, lori, pikipiki, garimoshi, gari dogo, ndege na meli.
Mwanafunzi atoe maana ya msamiati unaohusu usafiri.
Mwanafunzi aweza kutazama michoro na picha zinazolenga usafiri.
Mwanafunzi achore baadhi ya vyombo vya usafiri na kuvitambua kwa
majina.
Wanafunzi wajadiliane kuhusu umuhimu wa vyombo vya usafiri.
III. Nyenzo:
Kadi zenye majina ya vyombo mbalimbali vya usafiri;
Michoro au picha za vyombo mbalimbali vya usafiri;
Vifaa halisi vya usafiri;
Wanafunzi wenyewe;
Mada Ndogo 2: Msamiati - Usari
(Idadi ya vipindi: 2)
72
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 59 - 60;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Msamiati wa vyombo mbalimbali vya usafiri ni muhimu kwa sababu vyombo
hivi hutumika kila siku kuwasafirisha watu pamoja na mizigo. Mwalimu aandae
vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama vilivyotajwa
hapo juu pamoja na vyombo vingine maalum vya kuwasaidia wanafunzi wenye
ulemavu na matatizo mbalimbali.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, wavionyeshe vifaa
vilivyopo kwa kuvigusa huku wakiandika maelezo yake ubaoni. Mwalimu
anaweza kuhusisha matumizi ya lugha ishara katika kuwafundisha wanafunzi
wa aina hii. Pia, ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu
ajitahidi kuandaa maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi hawa
kujifundisha kama wanafunzi wengine bila vikwazo vyovyote.
Ni vyema mwalimu ahakikishe kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi
ya wanafunzi wanaotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwa kila
shughuli ya wanafunzi katika vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu awaamkue wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu vyombo
vya usafiri ambavyo wamewahi kuviabiri. Wanafunzi wajibu maamkuzi ya
mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne wanne kisha
awashirikishe katika kuchunguza michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi,
ukurasa 59. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali
mepesi kuhusiana na michoro hiyo. Baadhi ya maswali ambayo mwalimu
anaweza kuuliza ni kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii?
73
Mwalimu awaelekeze wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo na kuelewa
vifaa vilivyo katika michoro iliyopo kama vile: lori, helikopta, meli, matatu na
pikipiki.
Mwalimu awaelekeze wanafunzi katika makundi yao watambue majina ya aina
mbalimbali za vyombo vya usafiri pamoja na vinakosafiria, kwa mfano: helikopta
- hewani, matatu barabarani, meli majini n.k.
Wanafunzi katika kila kundi wapewe muda wa kusimuliana kuhusu vyombo
vya usafiri ambavyo wamewahi kuabiri, waseme walikuwa wakienda wapi na
vyombo hivyo vilisafiria maeneo gani.
Mwalimu awaonyeshe wanafunzi picha au michoro ya vyombo mbalimbali vya
usafiri. Iwapo kuna baadhi ya vyombo hivi shuleni kama vile basi, pikipiki n.k.
mwalimu ahakikishe amewaonyesha wanafunzi vyombo hivyo halisi. Wanafunzi
wanaweza kuvigusa na ikiwezekana wakabebwa kwavyo. Mwalimu ahakikishe
anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu vyombo mbalimbali vya usafiri wa barabarani,
majini, angani na kwenye reli.
Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza kuandika kwa usahihi
majina ya vyombo mbalimbali vya usafiri.
VI. Majibu
Zoezi la makundi, ukurasa 60
1. Meli huendea majini.
2. Ukitaka kubeba mizigo mingi utatumia lori.
3. Helikopta huendea angani.
4. Anayeendesha gari huitwa dereva.
5. Anayeongoza meli majini huitwa nahodha.
74
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua kwa kutaja vyombo mbalimbali vya usafiri ili kuimarisha
mawasiliano;
b) Kuzungumza kuhusu vyombo vya usafiri ili kuimarisha uwezo wa kujieleza;
ch) Kusikiliza visa kuhusu usafiri ili kuimarisha umakinifu;
d) Kusimulia kisa kuhusu usafiri ili kuimarisha ukakamavu katika kujieleza;
e) Kufurahia masimulizi kuhusu vyombo vya usafiri ili kuimarisha mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atambue aina mbalimbali za vyombo vya usafiri k.v. matatu,
basi, lori, ndege, gari dogo, garimoshi, pikipiki na meli kwa kutumia picha
au vyombo vya teknolojia.
Mwanafunzi asimulie kuhusu vyombo vya usafiri. Kwa mfano: Mimi nilisafiri
kwa matatu.
Mwanafunzi ashiriki katika mjadala darasani kuhusu vyombo vya usafiri
kwa kutumia video au kinasasauti.
III. Nyenzo:
Rekodi za masimulizi bunifu mbalimbali kuhusu usafiri;
Michoro au picha za vyombo vya usafiri;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Mgeni mwalikwa (dereva);
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 61 - 62;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano, wanafunzi
wasioweza kuona, kusikia n.k.).
75
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusikiliza masimulizi bunifu
yanayohusu vyombo mbalimbali vya usafiri ili kujenga stadi yao ya kusikiliza
na kuzungumza. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika
kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake kama vilivyotajwa hapo
juu. Mwalimu anaweza kumwalika mgeni kama vile dereva wa magari makubwa,
madogo, pikipiki au hata baiskeli. Rubani, nahodha na kandawala wanaweza
pia kualikwa wakaja kuzungumzia kuhusu vyombo vya usafiri ambavyo wao
huendesha.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza masimulizi bunifu pamoja na stadi ya kuzungumza kupitia
kwa wao wenyewe kuwasimulia wenzao. Masimulizi haya yatahusu vyombo
mbalimbali vya usafiri.
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu
kisha awaombe watazame mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa
61. Wanafunzi katika makundi yao waeleze wanachoona katika mchoro huo
ambapo kuna wasafiri wanaoabiri basi jekundu la kwenda Pwani.
76
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
Wanafunzi wajibu maswali waliyopewa kwenye kitabu chao kuhusu michoro
waliyopewa.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi hadithi bunifu ifuatayo
inayohusu vyombo vya usafiri. Ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa
makini. Pia, mwalimu ahakikishe kuwa anasoma kwa ufasaha, kwa matamshi
sahihi na sauti ya kusikika na ya kuvutia. Iwapo mwalimu ana matatizo
ya kimatamshi, anaweza kumwalika msomaji stadi atakayewasomea au
kuwasimulia wanafunzi hadithi kuhusu vyombo mbalimbali vya usafiri.
Mfano wa hadithi
Likizo ya Aprili
Mimi ni Julia. Wakati wa likizo sisi husafiri. Likizo ya Aprili tulisafiri kwenda
kwa nyanya yetu. Tulienda kwenye kituo cha mabasi. Katika kituo hicho, tuliona
mabasi mengi sana. Watu walikuwa na mizigo yao. Kando ya kituo kulikuwa na
pikipiki. Hizi zilisafirisha watu waliokuwa wakienda karibu. Kondakta alituambia
tuabiri basi moja. Basi lilitupeleka hadi kwa nyanya. Kijakazi wa nyanya ana
baiskeli nzuri. Yeye huenda sokoni kwa baiskeli hiyo. Akitoka sokoni, sisi huendesha
baiskeli hiyo uwanjani. Babu ana gari dogo. Gari lake lilitubeba siku ya kurudi
kwetu. Sisi tunapenda kusafiri.
Baada ya kusomewa hadithi, wanafunzi wajaribu katika makundi yao kuelezana
kuhusu hadithi waliyoisikia. Watoe muhtasari wa hadithi hiyo katika makundi
yao. Wanafunzi waelezane kuhusu vyombo mbalimbali vya usafiri vilivyotajwa
katika masimulizi waliyosomewa na mwalimu wao. Baadaye, mwalimu
awashirikishe katika kujibu maswali ya masimulizi waliyopewa. Mwalimu
ahakikishe anawasaidia wanafunzi wanaotatizika katika makundi yao.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma masimulizi
bunifu pamoja na kufahamu vyombo mbalimbali vya usafiri. Pia, mwalimu
achunguze iwapo wanafunzi wameweza kupata maarifa ya kujibu kwa usahihi
maswali ya masimulizi. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kufanya
mazoezi yaliyo katika vitabu vyao.
77
VI. Majibu
Maswali ya masimulizi, ukurasa 61 - 62
1. Wakati wa likizo Julia husafiri.
2. Basi
3. Baiskeli nzuri
4. Gari dogo
Zoezi la masimulizi, ukurasa 62
Mwalimu atathmini masimulizi ya wanafunzi katika makundi yao.
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua picha za vyombo mbalimbali vya usafiri ili kuimarisha ufahamu
wa hadithi;
b) Kuelezea maana ya maneno yaliyotumiwa katika hadithi ili kuimarisha
ufahamu wa hadithi;
ch) Kusikiliza hadithi inaposomwa na mwalimu ili kuimarisha umakinifu;
d) Kusoma hadithi zinazohusu usafiri ili kujenga stadi ya kusoma;
e) Kufahamu hadithi aliyoisoma kuhusu usafiri ili kupata ujumbe katika
hadithi;
f) Kuchangamkia kusoma hadithi katika maisha ya kila siku ili kujenga ari ya
usomaji huru.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi;
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi;
78
Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi;
Mwanafunzi aweza kusikiliza mwalimu anaposoma hadithi kisha asome na
mwalimu na baadaye asome peke yake, wakiwa wawili wawili au katika
vikundi;
Mwanafunzi asimulie hadithi aliyoisoma au kusomewa kwa kutumia
maneno yake mwenyewe;
Mwanafunzi aweza kurekodiwa akisoma vizuri kwa video au kinasasauti
ili wanafunzi waweze kutazama na kusikiliza jinsi ya kusoma hadithi kwa
ufasaha;
Mwanafunzi aweza kufanya ziara ya kwenda kuona vyombo vya usafiri
kwenye vituo vya usafiri;
Mwanafunzi ajibu maswali ya ufahamu akiwa peke yake, wawili wawili au
katika vikundi.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za vyombo vya usafiri;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu usafiri;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 62 - 65;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu inayohusu usafiri kwa kutaja vyombo
mbalimbali vya usafiri ili kujenga stadi ya wanafunzi ya kusikiliza na kusoma.
Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo
hili kama vilivyoorodheshwa hapo juu. Hili litamsaidia kufanikisha ufundishaji
wake. Mwalimu anaweza kurekodi hadithi kuhusu usafiri ili wanafunzi waisikilize
darasani.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika lililotolewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
79
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wasahihishe zoezi walilopewa katika funzo
la hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi yao
ya kusoma pamoja na ya kusikiliza hadithi bunifu. Mwalimu awagawe wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha awaombe watazame michoro
iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 62-65. Wanafunzi wachunguze
michoro hiyo na kuijadili katika makundi yao.
Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na
michoro hiyo kama vile: Unaona nini kwenye michoro hii? Mwalimu awaelekeze
wanafunzi kuhusu namna ya kujibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu ahakikishe
amewashirikisha wanafunzi wote katika majadiliano haya. Wanafunzi wajibu
maswali ya mwalimu kulingana na wanayoona katika michoro waliyopewa. Kisha,
mwalimu awaelekeze wanafunzi kusoma vifungu vifupivifupi vilivyotolewa baada
ya kila mchoro waliopewa kuhusu vyombo mbalimbali vya usafiri. Vifungu hivi
vifupivifupi vinahusu usafiri. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika
kujadili vyombo vya usafiri vilivyotajwa katika vifungu hivi vifupi walivyopewa.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kujibu maswali ya zoezi
walilopewa katika vitabu vyao.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi bunifu. Pia,
mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa aina mbalimbali
za vyombo vya usafiri.
80
VI. Majibu
Zoezi, ukurasa 65
1. Meli husafiri majini.
2. Garimoshi hutumia magurudumu kusonga.
3. Pikipiki na baiskeli.
4. Baiskeli
5. Utingo hukusanya nauli kwenye basi.
Mada Ndogo 5: Saru: Matumizi ya heru kubwa
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kubainisha matumizi ya herufi kubwa ili kuimarisha mawasiliano andishi;
b) Kusoma sentensi zilizo na matumizi ya herufi kubwa katika kuimarisha
stadi za kusoma na kuandika;
ch) Kuandika sentensi akitumia herufi kubwa katika kuimarisha uandishi
bora;
d) Kuthamini matumizi ya herufi kubwa katika kufanikisha mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aelezee matumizi ya herufi kubwa.
Wanafunzi waweza kushirikishwa kusoma sentensi zinazotumia herufi
kubwa wakiwa wawili wawili.
Mwanafunzi aweza kutofautisha kati ya herufi kubwa na herufi ndogo.
Mwanafunzi aakifishe sentensi kwa kutumia herufi kubwa.
Wanafunzi waweza kuakifisha sentensi mbalimbali wakitumia herufi kubwa
wakiwa wawili wawili katika vikundi.
81
III. Nyenzo:
Chati zenye sentensi zinazoonyesha matumzi ya herufi kubwa;
Chati zenye maumbo ya herufi kubwa na herufi ndogo;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 66-67;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Katika funzo hili, mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla
ya vipindi hivi. Chati mbalimbali zitumike kuonyesha maumbo sahihi ya herufi
kubwa na ndogo. Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati
mwafaka wa kuweka hadharani vifaa vyake kwa kukumbuka kuwa matumizi
ya michoro, picha na vifaa halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha
ufundishaji wa wanafunzi.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, mwalimu anaweza
kuhusisha mtafsiri wa lugha ya ishara kwa ajili ya kufanikisha ujifunzaji wao.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa
maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha
kama wanafunzi wengine.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa
katika vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu aanze funzo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe
wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika kipindi kilichotangulia.
82
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili
kisha awashirikishe wanafunzi wote katika kutazama kadi walizopewa katika
vitabu vyao zilizo na herufi kubwa na herufi ndogo. Mwalimu awachangamshe
wanafunzi kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na kadi hizo kama vile:
Onyesha herufi kubwa katika kadi ulizopewa. Onyesha herufi ndogo katika
kadi ulizopewa. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na herufi
walizopewa katika kadi hizo.
Kisha, wanafunzi washirikishwe katika zoezi la kujibu maswali waliyopewa
katika vitabu vyao kuhusu majina yao, jina la shule yao, majina ya mahali
wanaishi n.k.
Katika hatua hii, wanafunzi watapata fursa ya kujifundisha matumizi ya herufi
kubwa kwa kurejelea majina watakayotamka katika makundi yao. Wanafunzi
wafahamu kuwa herufi kubwa hutumika mwanzoni mwa:
1. Jina la mtu, kwa mfano: Maria, Joni, Yusufu n.k.
2. Jina la mahali, kwa mfano: Nairobi, Kisumu, Wajir n.k.
3. Mwanzo wa sentensi zote, kwa mfano: Mimi ni Nuhu.
Mwalimu awaongoze wanafunzi katika kutunga sentensi sahihi wakitumia herufi
kubwa, kwa mfano:
1. Amina anaenda shule. (herufi kubwa imetumika mwanzoni mwa sentensi
na kuonyesha jina la mtu)
2. Sisi tunaishi Nakuru. (herufi kubwa imetumika mwanzoni mwa sentensi
na kuonyesha jina la mahali)
3. Huyu ni Joni. (herufi kubwa imetumika mwanzoni mwa sentensi na
kuonyesha jina la mtu)
4. Nitaenda kumtembelea rafiki yangu Shiro. (herufi kubwa imetumika
mwanzoni mwa sentensi na kuonyesha jina la mtu)
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi zaidi ya
kutaja majina ambayo yanastahili kuanza kwa herufi kubwa.
83
ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa kuwau-
liza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa kwa kuchunguza ikiwa wamepata ufahamu wa
matumizi ya herufi kubwa hasa katika majina yao na majina ya mahali wanaishi
au wanasoma.
VI. Majibu
Zoezi la kadi, ukurasa 66
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Ahakikishe wanafunzi wanatambua
kwa usahihi herufi kubwa na herufi ndogo kutoka kwenye kadi walizopewa
kwenye vitabu vyao.
Zoezi, ukurasa 66
Mwalimu atathmini majadiliano ya wanafunzi.
Zoezi, ukurasa 67
1. Rafiki yangu anaitwa Anita.
2. Shule yangu inaitwa Heshima.
3. Nairobi ni mji mkubwa.
4. a) MELI
b) PIKIPIKI
ch) USAFIRI
d) ABIRIA
84
Matokeo maalum yanayotarajiwa Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kukia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutambua sauti za herufi mbili
zilizofunzwa ili kuimarisha stadi ya
kusikiliza na kuzungumza;
(b) Kutambua maneno ya heshima
na adabu ili kuimarisha stadi ya
kuzungumza;
(ch) Kutumia msamiati wa familia katika
mawasiliano ya kila siku;
(d) Kutaja majina ya watu wa
familia katika kujenga umilisi wa
kuzungumza;
(e) Kutambua picha za watu wa familia
ili kuimarisha ufahamu wa hadithi;
(f) Kutambua maneno yanayoashiria
vitendo ili kuimarisha mawasiliano.
Mwanafunzi atamke sauti lengwa
/gh/, /ny/, na /ng’/ baada ya
mwalimu, kisha watamke na
mwalimu na mwishowe atamke
akiwa peke yake, wawili na katika
darasa.
Mwanafunzi aeleze matumizi ya
maneno ya heshima na adabu k.v.
hodi, karibu, naomba, nisamehe na
nashukuru.
Mwanafunzi ataje majina ya watu
wa familia k.v. babu, nyanya,
mjomba, ami/amu, shangazi, binamu
na halati.
Mwanafunzi arejelee watu wa
karibu katika familia aliofunzwa
awali.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi aweza kuigiza vitendo
k.m. simama, tembea, andika, cheka
n.k.
Mada Kuu 4: Familia
Idadi ya vipindi: 18
Sura ya
4
85
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
• Kazi ya vikundi.
• Shughuli za vyama vya ushirika shuleni.
• Michezo.
Uhusiano na masomo mengine:
üSomo la Dini, somo la Kiingereza na somo la Mazingira.
Nyenzo:
üMichoro au picha zinazoonyesha vitendo vya heshima;
üKadi zenye sauti /gh/, /ny/ na /ng’/;
üKadi zenye maneno yenye sauti /gh/, /ny/ na /ng’/;
üRekodi za hadithi au masimulizi bunifu;
üWanafunzi wenyewe;
üKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 68;
üChombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Mada hii itashughulikia matamshi sahihi ya sauti zenye herufi mbili za Kiswahili
ambazo ni: sauti /gh/, /ny/ na /ng’/ pamoja na matumizi yazo katika
maneno na katika sentensi. Kutokana na mada hii, wanafunzi watafahamu
maneno ya heshima na adabu ya kutumia katika mawasiliano yao ya kila siku
wanapotangamana na watu wa aina mbalimbali katika jamii.
Pia, kipengele cha masimulizi na hadithi bunifu zinazohusisha maneno ya
heshima na adabu zitafundishwa hapa. Masimulizi na hadithi za kuvutia na
zenye msamiati wa kiwango cha wanafunzi wa gredi hii zibuniwe ili kuwafaa
wanafunzi katika ujifundishaji wao.
86
Pia, mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kufahamu matumizi ya maneno
yanayoashiria vitendo mbalimbali.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
• Uraia: kushirikiana katika vikundi,
• Utangamano wa kijamii,
• Uzalendo,
• Mahusiano katika familia.
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii kuhusu maneno ya heshima na adabu ni kama vile:
Msamiati Maana
1.
asante
neno la kuonyesha shukrani
2.
pole
neno la kumtuliza mtu
3.
tafadhali
neno la kusihi
4.
hodi
neno la kuomba ruhusa ya kuingia mahali
5.
nisamehe
neno la kuomba msamaha
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Katika ufundishaji wa mada hii, mwalimu ahakikishe kuwa ana vifaa maalum
vya kuwasaidia wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali ili kuweza
kuwashirikisha katika ujifundishaji wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa
kuona, mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya breli pamoja na vifaa vya
kunasia sauti.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri wa
lugha ya ishara.
Haya yatawawezesha wanafunzi wa aina hii kusoma kama wanafunzi wenzao
bila vikwazo vyovyote.
87
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya
vipindi
Mada Ndogo 1: Sauti za herufi mbili za Kiswahili
6
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza:
Maneno ya heshima na adabu
2
Mada Ndogo 3: Msamiati
3
Mada Ndogo 4: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 5: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 6: Sarufi:
Matumizi ya maneno ya kuashiria vitendo
2
JUMLA: 18
Mada Ndogo 1: Sauti za heru mbili za Kiswahili
(Idadi ya vipindi: 6)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua sauti za herufi mbili zilizofunzwa ili kuimarisha stadi ya
kusikiliza na kuzungumza;
b) Kutamka sauti lengwa za herufi mbili katika kuimarisha stadi ya
kuzungumza;
ch) Kusoma herufi za sauti mbili ili kuimarisha usomaji bora;
d) Kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa ili
kuimarisha usomaji bora;
e) Kusoma hadithi fupi zilizo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kuimarisha
usomaji bora;
f) Kuandika maneno kutokana na herufi alizofunzwa ili kuimarisha stadi ya
kuandika;
g) Kufurahia kutumia sauti zilizofunzwa katika mawasiliano.
88
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atamke sauti lengwa /gh/, /ny/ na /ng’/ baada ya mwalimu,
kisha watamke na mwalimu na mwishowe atamke akiwa peke yake, wawili
na katika darasa.
Mwanafunzi atambue sauti lengwa /gh/, /ny/ na /ng’/ katika maneno.
Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia kama vile papaya kutamkia sauti.
Mwanafunzi atambue herufi zinazowakilisha sauti lengwa kwa kutumia
kadi za herufi.
Mwanafunzi aambatanishe silabi kusoma maneno yanayotokana na sauti
lengwa.
Mwanafunzi atenganishe silabi katika kutambua sehemu mbalimbali za
maneno.
Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
Mwanafunzi aandike herufi za sauti alizosoma hewani au vitabuni.
Mwanafunzi aweza kufinyanga maumbo ya herufi inayowakilisha sauti
lengwa.
Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi na kuchanganua yaliyo
marefu zaidi.
Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa kama
darasa au wawili wawili.
Mwanafunzi anaweza kutumia vifaa vya teknolojia kama vile tarakilishi,
projekta na kinasasauti kusikiliza na kusoma hadithi n.k.
Mwanafunzi anakili herufi na maneno yanayotokana na sauti alizofunzwa.
III. Nyenzo:
Kadi za herufi ‘gh’, ‘ny’ na ‘ng’’;
Rekodi za sauti /gh/, /ny/ na /ng’/;
Kadi zenye maneno yenye sauti /gh/, /ny/ na /ng’/;
Mgeni mwalikwa mwenye matamshi mazuri na sahihi;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 69 - 76;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
89
I V. Maandalizi ya somo
Mada hii inahusu sauti za herufi mbili za Kiswahili kwa kurejelea maneno ya
heshima na adabu. Herufi na sauti zitakazoangaziwa katika funzo hili ni: /gh/,
/ny/ na /ng’/. Matamshi mazuri na sahihi ya wanafunzi yatazingatiwa na
kukuzwa zaidi.
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama
vilivyotajwa hapo juu bila kusahau vyombo vingine maalum vya kuwasaidia
wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa alivyovileta darasani. Mwalimu akumbuke kuwa matumizi ya
michoro, picha na vifaa halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha
ufundishaji wa wanafunzi.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi katika
vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize somo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichopita. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kuchunguza mchoro ulio katika
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 68. Mwalimu awachangamshe wanafunzi
kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na mchoro huo. Baadhi ya maswali
ambayo mwalimu anaweza kuuliza ni kama vile: Mnaona nani kwenye mchoro
huu? Mwalimu awaelekeze wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo na
kufahamu majina ya watu wa familia kama vile: baba, mama, kaka na dada
katika michoro waliyopewa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika shughuli hii ili waweze kutambua
msamiati wa familia.
90
Mwalimu atahadhari sana anapofundisha somo hili iwapo kuna wanafunzi
katika darasa lake ambao hawana baadhi ya watu wa familia.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Vipindi 2
i) Sauti /gh/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 69.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro hiyo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti ya kwanza pekee ya majina hayo. Wanafunzi
watamke sauti /gh/ baada ya mwalimu katika darasa zima, kisha wakiwa
wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi atamke sauti hii akiwa peke yake.
Mwalimu awaombe wanafunzi waandike sauti /gh/ katika madaftari yao kwa
herufi kubwa na herufi ndogo. Yaani: gh na GH.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi ‘gh’, ambazo ni: gha, ghe, ghi, gho, ghu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ‘gh’. Kwa mfano: ghala, ghuni, gharama, gharika, ghera, ghorofa, ghilibu
n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye
silabi za herufi ‘gh’ kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno
hayo.
Kwa mfano:
1. Kijiji chao kilikumbwa na gharika kubwa.
2. Mama anaweka mahindi kwenye ghala.
3. Hii ni nyumba ya ghorofa.
91
4. Gharama ya kazi hii ni pesa nyingi.
5. Tapeli alimghilibu muuzaji.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ‘gh’.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /gh/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) gharika gha ri ka
ii) ghala gha la
iii) ghorofa gho ro fa
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi ‘gh’.
ii) Sauti /ny/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 71.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Wanafunzi wajibu maswali
ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti za kwanza za majina hayo pekee. Wanafunzi
watamke sauti /ny/ baada ya mwalimu katika darasa zima kisha wakiwa wawili
wawili na hatimaye atamke sauti hii akiwa peke yake. Mwalimu awaombe
wanafunzi waandike sauti /ny/ katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi
ndogo. Yaani: ny na NY.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi ‘ny’, ambazo ni: nya, nye, nyi, nyo, nyu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ‘ny’. Kwa mfano nyanya, nyani, nyembamba, nyimbo, nyuma, nyororo,
92
nyumba, nyaraka, nyasi, nyusi, nyuzi n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi
wote katika kutamka maneno yenye silabi za herufi ‘ny’ kwa usahihi. Hatimaye
watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Nyanya anatusimulia hadithi.
2. Mama anapika chakula kwa kutumia nyanya.
3. Nyumba yetu ni kubwa.
4. Huyu ni nyani.
5. Mtoto ameketi nyuma ya nyumba.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ‘ny’.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusoma kifungu
walichopewa katika vitabu vyao kisha watambue herufi ‘ny’ katika maneno ya
kifungu hicho.
iii) Sauti /ng’/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaelekeze kutazama mchoro ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 74.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na mchoro uliopo.
Maswali kama vile: Unaona nini kwenye mchoro huu? Wanafunzi wajibu maswali
ya mwalimu.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua jina sahihi la mchoro
waliopewa kisha watamke sauti ya kwanza ya jina hilo pekee. Wanafunzi watamke
sauti /ng’/ baada ya mwalimu katika darasa zima kisha, wakiwa wawili wawili
na hatimaye atamke sauti hii akiwa peke yake. Mwalimu awaombe wanafunzi
waandike sauti /ng’/ katika madaftari yao kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
Yaani: ng’ na NG’.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi ng’, ambazo ni: ng’a, ng’e, ng’i, ng’o, ng’u.
93
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ng’. Kwa mfano: ng’ara, ng’ombe, ng’arisha, ng’ambo, ng’oa, ng’ang’ania
n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye
silabi za herufi ng’ kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno
hayo.
Kwa mfano:
1. Ng’ombe huyu anatoa maziwa mengi.
2. Ndovu aling’oa mti ule.
3. Nyota zinang’aa angani.
4. Tulivuka ng’ambo ya mto.
5. Nyani ananing’inia juu ya mti.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ng’.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /ng’/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) ng’ombe ng’o mbe
ii) ng’ara ng’a ra
iii) ng’oa ng’o a
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi ng’.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusoma kifungu walichopewa
katika vitabu vyao kisha watambue herufi ng’ katika maneno ya kifungu hicho.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo hili kuhusu sauti /gh/, /ny/ na
/ng’/ kwa kuwauliza wanafunzi maswali tofauti kuhusu mambo muhimu
waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo uwezo wa wanafunzi wa kutamka
sauti /gh/, /ny/ na /ng’/ kwa usahihi, kutambua na kutamka maneno yenye
94
sauti hizi kwa usahihi pamoja na kutunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno
yenye sauti hizi walizojifundisha. Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi
wanaweza kuandika sauti hizo kwa usahihi kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
VI. Majibu
i) Sauti /gh/
Maswali, ukurasa 68
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na michoro waliyopewa
vitabuni mwao.
Maswali, ukurasa 70
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
6. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 71
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watambue sauti /gh/
katika sentensi walizopewa.
i) Sauti /ny/
Maswali, ukurasa 72
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
95
5. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
6. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 73
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watambue sauti /ny/
katika sentensi walizopewa.
Zoezi la kusoma, ukurasa 74
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.Wanafunzi watambue sauti /ny/
katika hadithi waliyopewa.
iii) Sauti /ng’/
Maswali, ukurasa 74
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
Zoezi, ukurasa 76
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watambue sauti /ng’/
katika sentensi walizopewa.
Zoezi la kusoma, ukurasa 76
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watambue sauti /ng’/
katika hadithi waliyope
96
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Maneno ya heshima
na adabu (Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua maneno ya heshima na adabu ili kuimarisha stadi ya kuzungumza;
b) Kutumia maneno ya heshima na adabu katika mawasiliano;
ch) Kuonyesha vitendo vya heshima na adabu anapowasiliana katika mazingira
yake;
d) Kuthamini matumizi ya maneno ya heshima na adabu katika mazingira
yake;
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aeleze matumizi ya maneno ya heshima na adabu k.v. hodi,
karibu, naomba, nisamehe na nashukuru.
Wanafunzi waigize vitendo vya heshima na adabu wakiwa watatu watatu
au katika vikundi.
Mwanafunzi atazame michoro na picha za watu wakidhihirisha vitendo
vya heshima na adabu.
Wanafunzi wajadili maneno ya heshima na adabu katika vikundi.
Mwanafunzi aweza kutazama video inayowasilisha vitendo vya heshima
na adabu.
Mwanafunzi asome maneno ya heshima na adabu.
Mwanafunzi aeleze maneno ya heshima na adabu.
III. Nyenzo:
Kadi zenye maneno ya heshima na adabu;
Rekodi au video za vitendo vinavyodhihirisha heshima na adabu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 77 - 78;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
97
IV. Maandalizi ya somo
Mwalimu aandae mapema vifaa atakavyohitaji katika kufundisha funzo hili
na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama vilivyotajwa hapo juu bila kusahau
vyombo vingine maalum vya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali.
Mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri wa lugha ishara iwapo kuna wanafunzi
walio na matatizo ya kusikia ili kufanikisha ujifundishaji wao. Ikiwa kuna
wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa maelezo
yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha kama
wanafunzi wengine.
Ni vyema mwalimu ahakikishe kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi
ya wanafunzi wanaotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwa kila
shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa katika Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu awasalimie wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu salamu za
mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu
kisha awashirikishe wanafunzi wote katika kuchunguza michoro iliyo katika
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 77. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa
kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na michoro hiyo. Baadhi ya maswali
ambayo mwalimu anaweza kuuliza ni kama vile: Watu hawa wanafanya nini?
Watu hawa wanasema nini? Wanafunzi waelekezwe na mwalimu kujibu maswali
ya mwalimu na kueleza kinachoendelea katika michoro iliyopo. Wanafunzi
wachunguze vitendo katika michoro waliyopewa na wajadili kuhusu maneno
ya heshima na adabu ambayo yanatumika katika miktadha ya michoro husika.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao kuigiza vitendo
mbalimbali kama vile: kuomba kalamu, kubisha mlango, kushukuru kwa zawadi,
kumkaribisha mgeni n.k. Wanafunzi watambue katika maigizo yao matumizi ya
maneno ya heshima kama vile: hodi, karibu, naomba, asante n.k.
98
Mwalimu azunguke darasani kuhakikisha wanafunzi wote wanashiriki katika
shughuli hii. Baadaye, kila kundi lipewe muda wa kuigiza vitendo hivi mbalimbali
vinavyodhihirisha matumizi ya maneno ya heshima na adabu. Shughuli hii
itawasaidia wanafunzi kupata ujasiri wa kusimama na kuzungumza mbele ya
watu. Mwalimu ahakikishe anakosoa makosa ya kimatamshi pindi yanapotokea.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu matumizi ya maneno ya heshima na
adabu.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu na kutumia maneno ya heshima na adabu
katika mawasiliano yao ya kila siku wanapotangamana na watu wa kila aina.
VI. Majibu
Zoezi la maigizo, ukurasa 78
Mwalimu atathmini maigizo ya wanafunzi ambapo watahitajika kutumia
maneno ya heshima na adabu waliyopewa baada ya kila kitendo cha kuigiza.
Kwa mfano:
1. Naomba kalamu. - Asante / Nashukuru.
2. Hodi huku! - Karibu!
3. Karibu mgeni. - Asante /Nashukuru.
4. Nisamehe kwa kosa nililotenda. - Nimekusamehe.
5. Asante kwa zawadi nzuri. - Karibu!
Zoezi, ukurasa 78
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watumie maneno ya
heshima na adabu waliyopewa kujibu maswali zoezi hili.
1. Naomba
2. Hodi
3. Nashukuru
4. Nisamehe
5. Karibu
99
Mada Ndogo 3: Msamiati - Familia
Idadi ya vipindi: 3
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutumia msamiati wa familia katika mawasiliano ya kila siku;
b) Kutunga sentensi akitumia msamiati wa familia uliofunzwa ili kuimarisha
stadi ya mazungumzo na uandishi;
ch) Kusoma maneno na sentensi kuhusu familia ili kuimarisha stadi ya
kusoma;
d) Kuandika maneno na sentensi kuhusu familia ili kuimarisha stadi ya
kuandika;
e) Kufurahia kuwarejelea watu wa familia kwa majina yao mwafaka ili
kuimarisha mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
• Mwanafunzi ataje majina ya watu wa familia k.v. babu, nyanya, mjomba,
ami/amu, shangazi, binamu na halati.
• Mwanafunzi atazame picha au michoro ya watu wa familia.
• Wanafunzi wasome majina ya watu wa familia kwenye kadi au chati.
• Wanafunzi waweza kushiriki katika nyimbo na mashairi kuhusu watu
wa familia.
• Mwanafunzi aandike majina ya watu wa familia.
• Mwanafunzi asome msamiati wa watu wa familia katika kadi na chati.
• Mwanafunzi atunge na kusoma sentensi wakitumia msamiati wa familia.
100
III. Nyenzo:
ØKadi zenye majina ya watu wa familia;
ØMichoro au picha za watu wa familia;
ØWatu halisi wa familia;
ØChati zenye majina ya watu wa familia;
ØWanafunzi wenyewe;
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 79 - 81;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Msamiati kuhusu majina ya watu wa familia ni muhimu sana kwa sababu kila
mtu hutangamana na watu wa familia kila siku. Mwalimu aandae vifaa vyake
mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama vilivyotajwa hapo juu
pamoja na vyombo vingine maalum vya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu
na matatizo mbalimbali.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia mwalimu anaweza
kuhusisha matumizi ya lugha ishara katika kuwafundisha. Pia, ikiwa kuna
wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa maelezo
yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi hawa kujifundisha kama wanafunzi
wengine bila vikwazo vyovyote.
Ni vyema mwalimu ahakikishe kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi
ya wanafunzi wanaotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwa kila
shughuli ya wanafunzi katika vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu awaamkue wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu watu wa
familia zao. Wanafunzi wajibu maamkuzi ya mwalimu kisha wajibu maswali
waliyoulizwa.
101
Mwalimu atahadhari anapofundisha funzo hili iwapo kuna wanafunzi katika
darasa lake wasio na baadhi ya watu wa familia.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awashirikishe katika kuchunguza michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi,
ukurasa 79. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali
mepesi kuhusiana na michoro hiyo. Baadhi ya maswali ambayo mwalimu
anaweza kuuliza ni kama vile: Mnaona nani kwenye michoro hii? Mwalimu
awaelekeze wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo na kuelewa watu wa
familia walio katika michoro iliyopo kama vile: nyanya, babu, binamu, kaka,
dada, shangazi n.k.
Mwalimu awaelekeze wanafunzi katika makundi yao watambue majina ya watu
mbalimbali wa familia, kwa mfano: nyanya, babu, mama, baba, kaka, dada,
shangazi, mjomba, binamu, halati, ami/amu n.k.
Wanafunzi katika kila kundi wapewe muda wa kuelezana kuhusu watu wa
familia yao kwa kueleza familia yao ina watu wangapi, yeye ni mtoto wa ngapi
kuzaliwa, majina ya baba na mama yake, majina ya ndugu zake n.k.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi kusoma hadithi waliyopewa katika
vitabu vyao kuhusu majina ya watu wa familia. Wanafunzi wasome hadithi hiyo
kama darasa zima kisha wakiwa wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi
asome peke yake. Mwalimu ahakikishe anakosoa makosa ya kimatamshi
ya wanafunzi pindi tu yanapotokea. Mwalimu ahakikishe anawashirikisha
wanafunzi wote katika shughuli hii. Baada ya shuguli hii ya usomaji, wanafunzi
wajibu maswali ya hadithi waliyopewa katika vitabu vyao.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu majina ya watu mbalimbali wa familia.
Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza kuandika kwa usahihi
majina ya watu mbalimbali wa familia.
102
VI. Majibu
Zoezi la ufunguzi, ukurasa 79
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na michoro waliyopewa.
Maswali ya hadithi, ukurasa 81
1. Dada wa baba ni shangazi.
2. Mtoto wa mjomba ni binamu.
3. Kaka wa mama ni mjomba.
4. Baba mzazi wa baba ni babu.
5. Dada wa mama ni halati/hale.
6. Mama mzazi wa mama au baba ni nyanya.
Mada Ndogo 4: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutaja majina ya watu wa familia katika kujenga umilisi wa kuzungumza;
b) Kusikiliza kwa makini masimulizi kuhusu watu wa familia ili kujenga
umakinifu;
ch) Kuelezea kuhusu watu wa familia katika kuimarisha uwezo wa kuwaelezea
watu katika mazingira yake;
d) Kuthamini umuhimu wa familia katika kuendeleza mshikamano wa kijamii.
103
II Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi arejelee watu wa karibu katika familia aliofunzwa awali.
Mwanafunzi asimulie kuhusu familia.
Mwanafunzi aelezee maana ya majina ya watu wa familia.
Mwanafunzi aweza kushirikishwa katika nyimbo au mashairi kuhusu watu
wa familia.
Mwanafunzi aweza kutazama video, picha au michoro inayoonyesha watu
wa familia ili wajadiliane katika vikundi.
III. Nyenzo:
ØMichoro ya matukio ya masimulizi bunifu;
ØRekodi za masimulizi mbalimbali,
ØVideo za masimulizi mbalimbali;
ØWanafunzi wenyewe;
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 82 - 84;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusoma masimulizi bunifu
ili kujenga stadi yao ya kusikiliza na kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba
ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji
wake bila kusahau vyombo vya kuwezesha ufundishaji wa wanafunzi walio na
matatizo na ulemavu mbalimbali.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
104
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza pamoja na ya kusoma masimulizi bunifu. Mwalimu awagawe
wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha awaombe watazame
michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 82. Wanafunzi wachunguze
michoro hiyo na kuijadili katika makundi yao. Mwalimu anaweza kuwauliza
wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro hiyo kama vile: Unaona nani
kwenye michoro hii? Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu
maswali waliyoulizwa. Mwalimu ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote
katika majadiliano haya. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na
wanayoona katika michoro waliyopewa.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi masimulizi yafuatayo.
Ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa makini. Pia, mwalimu ahakikishe
kuwa anasoma kwa matamshi sahihi na sauti ya kusikika.
Mfano wa hadithi
Hadithi ya babu
Mimi ninaitwa Babu Koza. Nilizaliwa miaka sabini iliyopita. Miaka yangu ni
mingi sana. Nilizaliwa katika mji wa Mombasa. Baba na mama yangu waliishi
huko. Mimi nina ndugu watatu. Kaka wawili na dada mmoja. Familia yetu ina
watu sita. Mimi, kaka wawili, dada mmoja, baba na mama. Dada ya baba yangu
ambaye ni shangazi anaishi katika mji wa Nakuru. Kaka mmoja wa baba yangu
alienda ng’ambo kusomea udaktari. Ninamshukuru Mungu kwa kunipa familia
yenye upendo. Sisi tumezeeka lakini tunapendana sana.
105
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi walisikiliza masimulizi ya mwalimu kwa makini,
mwalimu awashirikishe katika kusimulia kwa maneno yao wenyewe masimulizi
hayo. Wanafunzi wasimulie masimulizi haya katika makundi yao. Mwalimu
azunguke darasani ili kuwasaidia wanafunzi wanaotatizika katika makundi yao.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao kusoma
masimulizi yaliyo katika kitabu chao na wajibu maswali waliyopewa kwa
ufasaha. Wanafunzi wanaotatizika wasaidiwe.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma masimulizi bunifu.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kusoma
masimulizi yaliyoandikwa na kujibu maswali ya masimulizi hayo kwa ufasaha.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi yaliyo katika vitabu
vyao.
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 83
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kwa kurejelea michoro waliyopewa.
Maswali ya hadithi, ukurasa 84
1. Babu na nyanya
2. Halati hupika.
3. Dada ya mama
4. Binamu wawili
106
Mada Ndogo 5: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua picha za watu wa familia ili kuimarisha ufahamu wa hadithi;
b) Kusikiliza hadithi za mwalimu kuhusu watu wa familia ili kuimarisha
umakinifu;
ch) Kusoma hadithi kuhusu watu wa familia ili kuimarisha usomaji bora;
d) Kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa ili kupata ujumbe;
e) Kuchangamkia kusoma ujumbe kuhusu watu wa familia katika kujenga ari
ya usomaji bora.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi;
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi;
Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi;
Mwanafunzi asikilize mwalimu anaposoma hadithi kisha asome na
mwalimu na baadaye asome peke yake, wawili wawili au katika vikundi;
Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kwa kutumia tarakilishi na
projekta;
Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kutoka kwa jitabu mbele ya darasa;
Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kutokana na hadithi;
Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za hadithi bunifu mbalimbali;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu, projekta;
Mtambaji mwalikwa;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 84 - 85;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
107
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu ili kujenga stadi ya wanafunzi
ya kusikiliza na kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa
vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake bila
kusahau vyombo maalum vya kuwafundishia wanafunzi wenye matatizo na
ulemavu mbalimbali. Mwalimu anaweza hata kumwalika mtambaji au msomaji
mashuhuri akawasomea wanafunzi hadithi bunifu kisha wanafunzi wakasoma
baada yake katika makundi makubwa hadi kusoma mwanafunzi mmoja mmoja.
Mwalikwa huyu sharti awe na uwezo wa kusoma kwa sauti ya kusikika na kwa
matamshi sahihi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao ya
kusoma hadithi bunifu pamoja na ya kusikiliza. Mwalimu awagawe wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha awaombe watazame mchoro
ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 84. Wanafunzi wachunguze mchoro
huo na kuujadili katika makundi yao. Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi
maswali mepesi kuhusiana na mchoro huo kama vile: Unaona nani kwenye
mchoro huu? Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu maswali
waliyoulizwa kwa kuwataja watu anaowaona katika mchoro waliopewa kama
vile: watoto, babu n.k.
108
Mwalimu ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote katika majadiliano haya.
Wanafunzi wajadili zaidi kuhusu watu wa familia zao.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi hadithi iliyo katika
Kitabu cha Mwanafunzi huku wanafunzi wakimsikiliza. Mwalimu ahakikishe
anasoma kwa matamshi sahihi na kwa sauti ya kusikika na wanafunzi wote.
Iwapo mwalimu ana matatizo ya matamshi, anaweza kumwalika msomaji stadi
akawasomea wanafunzi hadithi hiyo. Kisha wanafunzi wasome hadithi hiyo
pamoja na mwalimu, halafu wasome wakiwa wawili wawili na hatimaye kila
mwanafunzi asome hadithi hiyo peke yake. Mwalimu ahakikishe anawashirikisha
wanafunzi wote katika shughuli hi.
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi walielewa hadithi ya mwalimu, mwalimu
awashirikishe katika kujibu maswali waliyopewa katika vitabu vyao. Mwalimu
azunguke darasani ili kuwasaidia wanafunzi wanaotatizika katika makundi yao.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi bunifu. Pia,
mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kusoma hadithi
na kuweza kujibu maswali ya hadithi hiyo kwa usahihi kulingana na muktadha
wa hadithi hiyo.
VI. Majibu
Maswali ya hadithi, ukurasa 85
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano:
1. Kwa sababu mguu wake ulikuwa umeumia.
2. Mamake Saidia.
3. Binamu wa Saidia ni Pokea na Patia.
4. Nyanya aliwapatia Patia na Pokea matunda wampelekee Saidia.
Zoezi la imla, ukurasa 85
Mwalimu awasomee wanafunzi maneno yafuatayo kisha wanafunzi wayaandike
katika madaftari yao.
1. nyanya 2. babu 3. mjomba 4. shangazi
5. halati 6. ami 7. binamu
109
Mada Ndogo 6: Saru: Matumizi ya maneno yanayoashiria
vitendo (Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua maneno yanayoashiria vitendo ili kuimarisha mawasiliano;
b) Kusoma maneno yanayoashiria vitendo ili kujenga usomaji bora;
ch) Kutumia maneno yanayoashiria vitendo katika sentensi ili kuimarisha
mawasiliano;
d) Kuandika sentensi sahihi akitumia maneno yanayoashiria vitendo katika
kuimarisha uandishi bora;
e) Kufurahia kutumia maneno yanayoashiria vitendo katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aweza kuigiza vitendo k.m. simama, tembea, andika, cheka
n.k.
Mwanafunzi atunge sentensi zenye matumizi ya maneno yanayoashiria
vitendo k.m. simama, oga, chana n.k.
Mwanafunzi aandike sentensi zinazohusisha vitendo.
Mwanafunzi asome sentensi zinazohusisha vitendo.
Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa maneno yanayoashiria vitendo.
Mwanafunzi anakili sentensi kwa kutumia maneno yanayoashiria vitendo.
Wanafunzi watunge sentensi katika makundi.
Mwanafunzi aweza kupewa zoezi la kujaza mapengo kwa tarakilishi
(mchezo wa kuvuta na kutia kapuni).
III. Nyenzo:
Michoro au picha za watu wakitenda vitendo mbalimbali;
Chati zenye maneno ya kuashiria vitendo mbalimbali;
Kadi zenye maneno ya kuashiria vitendo mbalimbali;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 86 - 89;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
110
IV. Maandalizi ya somo
Kwa kuwa sarufi ni kipengele muhimu katika ujifundishaji wa wanafunzi,
mwalimu anastahili kutilia maanani dhana hii ili kuweza kuwahusisha wanafunzi
kwa ukamilifu katika somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na
kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi bila kusahau vyombo vingine vitakavyofanikisha
ufundishaji wa wanafunzi walemavu na walio na matatizo mbalimbali.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, mwalimu ahusishe matumizi
ya lugha ishara. Mwalimu anaweza kumshirikisha mtaalamu wa lugha ishara.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa
maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha
kama wanafunzi wengine.
Ni vyema mwalimu ahakikishe kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi
ya wanafunzi wanaotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwa kila
shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa katika Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu aanze funzo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wenye matatizo wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awaombe wanafunzi wote kwa pamoja wasimame, waketi, wacheke,
wainame, waruke, waimbe na walale. Shughuli hii itakuwa njia bora ya kutanguliza
funzo hili kuhusu maneno ya vitendo mbalimbali.
Baadaye, mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu
watatu kisha awashirikishe katika kuchunguza michoro iliyo katika Kitabu cha
Mwanafunzi, ukurasa 86.
111
Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusiana
na michoro hiyo kama vile: Unaona nini kwenye michoro hii? Wanafunzi wajibu
maswali ya mwalimu kulingana na wanayoona kwenye michoro waliyopewa
vitabuni mwao. Kisha, wanafunzi waelekezwe kufahamu maneno mbalimbali ya
kuashiria vitendo mbalimbali, kwa mfano: cheka, lia, simama, keti, kula, amka,
imba, kimbia, chora, cheza, pika, osha, fua, ruka, oga n.k. Wanafunzi wataje
mifano zaidi ya maneno yanayoashiria vitendo mbalimbali. Wanafunzi waigize
vitendo hivyo.
Baada ya wanafunzi kupata ufahamu kuhusiana na maneno ya kuashiria vitendo,
mwalimu awaelekeze katika kutunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno ya
kuashiria vitendo.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kutunga sentensi sahihi kwa kutumia
maneno ya kuashiria vitendo mbalimbali, kwa mfano:
1. Baba anakula.
2. Mama anafua nguo.
3. Sisi tunafuta ubao.
4. Mtoto anakunywa maziwa.
5. Mwalimu anaandika ubaoni. n.k.
Katika hatua hii, wanafunzi watapata fursa ya kujifundisha jinsi ya kutunga
sentensi sahihi kwa kutumia majina ya watu wa familia. Mwalimu ahakikishe
anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa katika kuchunguza ikiwa wanaweza kutunga
sentensi sahihi kwa kutumia majina ya watu mbalimbali wa familia.
112
VI. Majibu
Zoezi la maigizo, ukurasa 87
Mwalimu atathmini maigizo ya wanafunzi. Wanafunzi waigize vitendo
walivyopewa katika vitabu vyao.
Zoezi la kusoma, ukurasa 88
Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi. Wanafunzi wasome maneno ya
kuashiria vitendo waliyopewa katika vitabu vyao.
Zoezi, ukurasa, 89
1. Mwalimu ameandika ubaoni.
2. Mimi nitakula wali.
3. Nyanya ameshona mkeka.
4. Shangazi atatupikia chapati.
5. Baba amesoma gazeti.
113
Matokeo maalum yanayotarajiwa Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kukia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutamka sauti za herufi mbili katika
kuimarisha matamshi bora;
(b) Kutambua msamiati ambao
hutumiwa katika usalama ili
kuwasiliana kuhusu masuala
yanayohusu usalama wake;
(ch) Kutambua jinsi ya kuepukana na
baadhi ya ajali katika mazingira
yao;
(d) Kutambua picha zinazohusu
usalama ili kuimarisha ufahamu wa
hadithi;
(e) Kufahamu matumizi ya huyo na
hao katika mawasiliano.
Mwanafunzi atambue sauti /sh/ na
/th/ katika maneno.
Mwanafunzi atoe maana ya
msamiati wa usalama.
Mwanafunzi asimulie baadhi ya
mambo yanayoweza kuhatarisha
usalama wake kupitia kwa mgeni
mwalikwa.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi asome sentensi zenye
kudhihirisha matumizi ya huyo na
hao kama vile: Huyo ni nani?
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kazi ya vikundi.
Shughuli za vyama vya ushirika shuleni.
Michezo.
Uhusiano na masomo mengine:
Somo kuhusu Mazingira.
Mada Kuu 5: Usalama Wangu
Idadi ya vipindi: 18
Sura ya
5
114
Nyenzo:
Michoro au picha za vitendo vya usalama au hatari;
Kadi zenye sauti /sh/ na /th/;
Mtambaji au msimulizi mwalikwa;
Rekodi ya masimulizi bunifu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 90;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Usalama ni kipengele muhimu sana katika maisha ya binadamu. Ni vyema
kwa kila mtu wakiwemo wanafunzi hata wa kiwango hiki kufundishwa kuhusu
vitendo mbalimbali vya kudumisha usalama wao kila wakati ili kuepuka hatari.
Mada hii inashughulikia kukuza ujuzi wa wanafunzi kuhusu njia mbalimbali za
kulinda usalama wao, msamiati kuhusiana na usalama, masimulizi na hadithi
kuhusu shughuli za usalama. Kama tujuavyo, hakuna binadamu anayependelea
kukumbwa na hatari ya aina yoyote. Hivyo, funzo hili ni muhimu sana kwa
wanafunzi ili kuwawezesha kujilinda na kuwa salama. Mwalimu ahakikishe
kuwa wanafunzi wote wanashirikishwa kupata maarifa haya.
Pia, mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kupata maarifa kuhusiana na
matumizi ya huyo na hao katika mawasiliano yao ya kila siku.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
Elimu endelevu somo la usalama: kueleza jinsi ya kujiepusha na vitendo
vinavyoweza kumdhuru maishani,
Stadi za maisha: uwajibikaji,
Uzalendo: ushirikiano katika vikundi,
Amani na maadili.
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii ni kuhusu vitendo vya usalama ni kama vile:
115
Msamiati Maana
1.
hatari
kitu au jambo la kumdhuru mtu
2.
ajali
chochote cha kudhuru kinachotokea bila kutarajiwa
3.
moto
mwako unaochoma
4.
kutekwa nyara
kushikwa kwa nguvu na kukosa uhuru
5.
kivukomilia
sehemu salama ya kuvukia barabara
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Ili kuweza kuwashirikisha wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali,
mwalimu awe na vifaa maalum vya kuwasaidia wanafunzi hawa katika
ujifundishaji wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kuona, mwalimu anaweza
kuhusisha matumizi ya breli pamoja na vifaa vya kunasia sauti.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri wa
lugha ya ishara. Haya yatawawezesha wanafunzi hawa kusoma kama wanafunzi
wenzao bila vikwazo vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya vipindi
Mada Ndogo 1: Sauti na herufi mbili za Kiswahili
4
Mada Ndogo 2: Msamiati
3
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya huyo na hao
2
JUMLA: 14
116
Mada Ndogo 1: Sauti na heru mbili za Kiswahili
(Idadi ya vipindi: 4)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua sauti za herufi mbili katika kuimarisha matamshi bora;
b) Kutamka sauti za Kiswahili za herufi mbili katika kuimarisha matamshi bora;
ch) Kusoma silabi za sauti zinazoundwa kutokana na sauti mbili ili kuimarisha
usomaji;
d) Kuunda silabi na maneno kwa kutumia sauti lengwa katika kuimarisha
umilisi wa kusoma maneno;
e) Kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa ili
kuimarisha stadi ya kusoma;
f) Kusoma hadithi fupi fupi zilizo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili
kuimarisha stadi ya kusoma;
g) Kuandika maneno kutokana na herufi za sauti lengwa katika kuimarisha
uandishi;
h) Kufurahia kutumia sauti zilizofunzwa katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atambue sauti /sh/ na /th/ katika maneno.
Mwanafunzi atamke sauti lengwa baada ya mwalimu, kisha watamke na
mwalimu na mwishowe atamke akiwa peke yake, wawili na katika darasa.
Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia kama vile, tarakilishi na projekta
kutamkia sauti.
Mwanafunzi atambue herufi zinazowakilisha sauti lengwa kwa kutumia
kadi za herufi.
Mwanafunzi aambatanishe silabi kusoma maneno yanayotokana na sauti
lengwa.
Mwanafunzi atenganishe silabi katika kutambua sehemu mbalimbali za
maneno.
117
Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa mwenye umahiri katika
kutamka sauti lengwa.
Mwanafunzi aweza kufinyanga maumbo ya herufi inayowakilisha sauti
lengwa.
Mwanafunzi aandike herufi za sauti alizosoma hewani au vitabuni.
Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi na au sehemu zenye maana
kwa yale yaliyo marefu zaidi.
Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa
wakiwa wawili wawili.
Mwanafunzi anakili herufi na maneno yanayotokana na sauti alizofunzwa.
III. Nyenzo:
Kadi za herufi sh na th;
Rekodi za sauti /sh/ na /th/;
Kadi zenye maneno yenye sauti /sh/ na /th/;
Mgeni mwalikwa mwenye matamshi mazuri na sahihi;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 91;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Katika mada hii, mwalimu alenge kuwafundisha wanafunzi kuhusu sauti na
herufi mbili za Kiswahili kwa kurejelea vitendo mbalimbali vya usalama. Herufi
na sauti zitakazoangaziwa katika funzo hili ni: /sh/ na /th/. Matamshi mazuri
na sahihi ya wanafunzi yatazingatiwa hapa na kukuzwa zaidi.
Mwalimu aandae mapema vifaa atakavyohitaji na kuvihifadhi kabla ya vipindi
hivi. Vifaa hivi ni kama vile: kadi za herufi sauti sh na th, rekodi za matamshi
sahihi ya sauti husika, mgeni mwalikwa mwenye matamshi mazuri na sahihi
ya sauti lengwa, kadi zenye maneno yenye herufi na sauti husika pamoja na
vyombo vingine maalum vya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu na matatizo
mbalimbali.
118
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na mazoezi waliyopewa.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu aanze somo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichopita. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kuchunguza mchoro ulio katika
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 90. Mwalimu awachangamshe wanafunzi
kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na mchoro huo. Baadhi ya maswali
ambayo mwalimu anaweza kuuliza ni kama vile: Unaona nini kwenye mchoro
huu? Mwalimu awaelekeze wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Vipindi 2
i) Sauti /sh/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 91.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Unaona nini kwenye michoro hii? Taja majina ya michoro hii.
Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu katika makundi yao.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
waliyopewa kisha watamke sauti ya kwanza pekee ya majina hayo. Wanafunzi
watamke sauti /sh/ baada ya mwalimu katika darasa zima kisha wakiwa
wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi atamke sauti hii akiwa pekee yake.
Mwalimu awaombe wanafunzi waandike sauti /sh/ katika madaftari yao kwa
herufi kubwa na herufi ndogo. Yaani: sh na SH.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watambue silabi za herufi ‘sh’, ambazo ni: sha, she, shi, sho, shu.
119
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ‘sh’. Kwa mfano: shati, shule, shimo, shuka, sherehe, shilingi, shika, shona,
shungi n.k. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno
yenye silabi za herufi ‘sh’ kwa usahihi.
Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Hii ni shule yetu.
2. Hili ni shati la kaka.
3. Shida ya huku kwetu ni usalama.
4. Mama anashona nguo.
5. Tutaenda kwenye sherehe.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ‘sh’.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /sh/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) shule shu le
ii) sherehe she re he
iii) shoka sho ka
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa
ya kutamka silabi za herufi ‘sh’. Pia, wanafunzi washirikishwe kusikiliza rekodi
ya mwalimu ya utamkaji sahihi wa sauti /sh/. Mwalimu ahakikishe ameandaa
rekodi hii mapema kabla ya kipindi hiki.
ii) Sauti /th/
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kutazama michoro ya nambari iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi,
ukurasa 94. Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na nambari
hizo. Maswali kama vile: Mnaona nambari ngapi kwenye michoro hii? Taja majina
ya nambari hizo. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu.
120
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua majina sahihi ya michoro
ya nambari walizopewa kisha watamke sauti ya kwanza ya majina hayo pekee.
Wanafunzi watamke sauti /th/ baada ya mwalimu katika darasa zima kisha
wakiwa wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi atamke sauti hii akiwa peke
yake. Mwalimu awaombe wanafunzi waandike sauti /th/ katika madaftari yao
kwa herufi kubwa na herufi ndogo. Yaani: th na TH.
Wanafunzi waelekezwe katika kutamka irabu za Kiswahili ambazo ni: a, e, i, o, u
kisha watamke silabi za herufi ‘th’, ambazo ni: tha, the, thi, tho, thu.
Baada ya shughuli hii, wanafunzi watambue maneno kadhaa yenye silabi za
herufi ‘th’. Kwa mfano: thelathini, themanini, thumni, theluji, thurea, thieta n.k.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kutamka maneno yenye silabi
za herufi ‘th’ kwa usahihi. Hatimaye watunge sentensi wakitumia maneno hayo.
Kwa mfano:
1. Hawa ni wanafunzi thelathini.
2. Hii ni thurea ya nyota.
3. Sukari kilo moja ni shilingi themanini.
4. Mgonjwa amepelekwa thieta.
5. Naomba thumni ya mali yako.
Wanafunzi washirikishwe katika kufanya mazoezi kadhaa ya kutamka silabi za
herufi ‘th’.
Wanafunzi washirikishwe katika kufahamu jinsi ya kutenganisha silabi katika
maneno yaliyo na sauti /th/, kwa mfano:
Neno Silabi
i) thurea thu re a
ii) themanini the ma ni ni
iii) thelathini the la thi ni
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi kadhaa ya
kutamka silabi za herufi ‘th’.
121
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kusoma hadithi
waliyopewa katika vitabu vyao. Wanafunzi watambue sauti /sh/ na /th/ katika
maneno ya hadithi hiyo.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo hili kuhusu sauti /sh/ na /th/ kwa
kuwauliza wanafunzi maswali tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali haya yatilie mkazo uwezo wa wanafunzi wa kutamka sauti /sh/ na
/th/ kwa usahihi, kutambua na kutamka maneno yenye sauti hizi kwa usahihi
pamoja na kutunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno yenye sauti hizi
walizojifundisha. Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza
kuandika sauti hizo kwa usahihi kwa herufi kubwa na herufi ndogo.
VI. Majibu
i) Sauti /sh/
Maswali ya makundi, ukurasa 92
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
6. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
i) Sauti /th/
Maswali ya makundi, ukurasa 94-95
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
2. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
3. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
4. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
5. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
6. Mwalimu atathmini matamshi ya kila mwanafunzi.
122
Zoezi la kusoma hadithi, ukurasa 96
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi watambue sauti /sh/ na
/th/ katika hadithi waliyopewa.
Mada Ndogo 2: Msamiati: Usalama wangu
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati ambao hutumiwa katika usalama ili kuwasiliana
kuhusu masuala yanayohusu usalama wake;
b) Kueleza maana ya msamiati wa usalama katika kuimarisha mawasiliano;
ch) Kutumia msamiati wa usalama katika kuimarisha mawasiliano;
d) Kuthamini usalama wake katika maisha ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atoe maana ya msamiati wa usalama.
Mwanafunzi atunge sentensi sahihi kwa kutumia msamiati wa usalama
kama vile: kivuko cha barabara, moto, vidaraja, ajali michezoni, kuzama
majini na vita.
Wanafunzi waweza kuchora baadhi ya vifaa vinavyohusiana na usalama
wao kama vile kivuko cha barabarani na vidaraja;
Wanafunzi waweza kutazama video, michoro au picha zinazolenga usalama
wake;
Wanafunzi wajadiliane kuhusu umuhimu wa usalama wao kwenye makundi.
III. Nyenzo:
Kadi zenye majina ya vifaa vinavyohusiana na usalama;
Michoro ya vifaa vinavyohusiana na usalama;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 97;
123
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Maarifa kuhusu njia za kudumisha usalama ni muhimu kwa sababu binadamu
hujishughulisha na masuala mengi hivyo anahitaji kuwa salama. Mwalimu
anastahili kutilia maanani dhana hii wakati wa uandalizi wa funzo hili.
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi
kama vilivyoorodheshwa hapo juu bila kusahau vyombo vingine maalum vya
kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo na ulemavu mbalimbali.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa alivyovileta darasani kwa kukumbuka kuwa matumizi ya
michoro, picha na kadi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha ufundishaji
wa wanafunzi; hasa wale ambao wana matatizo mbalimbali katika kuelewa na
kufahamu haraka yale wanayofundishwa darasani au wale walio na kiwango
cha chini katika ujifunzaji wao.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa
maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha
kama wanafunzi wengine. Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia
mwalimu ahusishe matumizi ya lugha ishara.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa
katika vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu awaamkue wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kwa kurejelea
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia kuhusu utamkaji wa sauti za
herufi mbili za Kiswahili. Wanafunzi wajibu maamkuzi ya mwalimu kisha wajibu
maswali waliyoulizwa.
124
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awaelekeze kuchunguza michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa
97. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali mepesi
kuhusiana na michoro hiyo. Baadhi ya maswali ambayo mwalimu anaweza
kuuliza ni kama vile: Unaona nini kwenye michoro hii? Mwalimu awaelekeze
wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo na kuelewa ujumbe wa michoro
iliyopo.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Watu hawa wanafanya nini?Unaona ishara gani za barabarani?
Unaona taa gani za barabarani? Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kwa
kurejelea michoro waliyopewa katika vitabu vyao.
Baadaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kutambua njia kadhaa
za kuwa salama hasa katika kuvuka barabara zenye magari. Wanafunzi
wafahamishwe kuhusu ishara kadhaa za barabarani pamoja na eneo salama la
kuvukia barabara ambalo huitwa kivukomilia. Wanafunzi wafahamishwe kuwa
taa za trafiki husaidia sana wenye magari pamoja na wapitanjia kuwa salama
barabarani na hivyo kupunguza ajali na madhara mengine ya barabarani.
• Taa nyekundu huashiria kuwa magari yasimame;
• Taa za rangi ya chungwa huashiria kuwa magari yawe tayari kuondoka;
• Taa za kijani huashiria kuwa magari yanaweza kuondoka.
Mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wamepata uelewa wa matumizi ya taa za
trafiki pamoja na kujua maeneo salama ya kuvukia barabara.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi wasome hadithi waliyopewa katika
vitabu vyao kama darasa zima halafu wasome wawili wawili na kisha kila
mwanafunzi apate fursa ya kusoma peke yake. Wanafunzi wote washirikishwe
katika usomaji huu. Mwalimu ahakikishe anakosoa makosa ya kimatamshi ya
wanafunzi pindi tu yanapotokea. Baada ya usomaji wa wanafunzi, mwalimu
awaongoze wanafunzi wajibu maswali ya hadithi waliyopewa katika vitabu
vyao.
125
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu njia kadhaa za kudumisha usalama wao hasa
wa barabarani.
VI. Majibu
Zoezi la makundi, ukurasa 98
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na michoro waliyopewa.
Zoezi, ukurasa 98
1. Ukiwa hutaki kuchomeka, usiuchezee moto.
2. Kama hutaki kuzama, usiyachezee maji.
3. Unapovuka barabara pitia kwenye vidaraja.
4. Sehemu salama ya kuvukia barabara ni kwenye michoro ya
kivukomilia.
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua jinsi ya kuepukana na baadhi ya ajali katika mazingira yao;
b) Kujiepusha na vitendo vinavyoweza kumdhuru maishani;
ch) Kusimulia kuhusu mambo yanayoweza kuhatarisha usalama wake ili
kuimarisha stadi ya kuzungumza;
d) Kusikiliza masimulizi kuhusu usalama wake katika maisha ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asimulie baadhi ya mambo yanayoweza kuhatarisha usalama
wake kupitia kwa mgeni mwalikwa.
126
Mwanafunzi aweza kutazama video, picha au michoro inayoashiria usalama
wa watoto.
Wanafunzi waigize namna ya kuepuka ajali mbalimbali kama vile: moto,
kuvunjika viungo, kugongwa barabarani na kupigana.
Mwanafunzi aandike baadhi ya mambo muhimu kuhusu usalama wake.
III. Nyenzo:
Rekodi za masimulizi bunifu mbalimbali;
Michoro au picha za masimulizi bunifu mbalimbali;
Video za jinsi ya kuepuka ajali mbalimbali;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 99;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusikiliza masimulizi bunifu
yanayohusu jinsi ya kulinda au kudumisha usalama wa mtu binafsi dhidi ya
hatari nyingi zilizotuzunguka kila mahali. Ili kufanikisha ufundishaji wake,
mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia funzo
hili kama vilivyotajwa hapo juu bila kusahau vyombo maalum vya kuwafundishia
wanafunzi wenye matatizo au ulemavu mbalimbali.
Mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika makundi ya wanafunzi
yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi husika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
msamiati kuhusiana na usalama. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja
na maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha
zoezi walilopewa katika kipindi cha hapo awali.
127
Wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza masimulizi bunifu pamoja na stadi ya kuzungumza kupitia
kwa wao wenyewe kuwasimulia wenzao katika shughuli mbalimbali za vikundi.
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu
kisha awaombe watazame michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa
99. Wanafunzi katika makundi yao watabiri matendo katika michoro hiyo na
wajaribu kutunga masimulizi kuyahusu matendo hayo. Mwalimu ahakikishe
anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii. Wanafunzi wajibu maswali
waliyopewa kwenye kitabu chao kuhusu michoro waliyopewa. Mwalimu
awaongoze wanafunzi katika kuchambua michoro waliyopewa na kubaini kuwa
inahusu ajali mbalimbali ambazo huweza kutokea na kuhatarisha maisha ya
binadamu, kwa mfano, jengo kuporomoka, kushambuliwa na nyuki na hata
kuteleza na kuanguka chini. Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufahamu
njia kadhaa za kujizuia dhidi ya hatari kama vile kuepuka maeneo yenye hatari
mbalimbali.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi hadithi bunifu iliyo katika
vitabu vya wanafunzi. Wanafunzi wasikilize kwa makini. Mwalimu ahakikishe
anasoma kwa matamshi sahihi na kwa sauti ya kusikika. Baada ya mwalimu
kusoma, wanafunzi wasome pamoja na mwalimu kwa mara ya pili halafu
wanafunzi wasome wakiwa wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi apate
fursa ya kusoma mmoja mmoja.
Baada ya shughuli hii ya usomaji, wanafunzi wajaribu katika makundi yao
kuelezana kuhusu hadithi waliyosoma. Watoe muhtasari wa hadithi hiyo
katika makundi yao. Baadaye, mwalimu awashirikishe katika kujibu maswali
ya masimulizi bunifu waliyopewa. Mwalimu ahakikishe anawasaidia wanafunzi
wanaotatizika katika makundi yao.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma masimulizi bunifu.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wameweza kupata maarifa ya kujibu
maswali ya masimulizi kwa usahihi kulingana na muktadha wa masimulizi
husika. Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi yaliyo katika
vitabu vyao.
128
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 100
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali ya hadithi, ukurasa 101
1. Nyuki
2. Mtu anaweza kuvunjika viungo vya mwili kama vile mguu na mkono.
3. Mtu akicheza barabarani.
4. Kando ya barabara
5. Nyuki humpatia binadamu asali iliyo tamu sana.
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua picha zinazohusu usalama ili kuimarisha ufahamu wa hadithi;
b) Kusoma hadithi kuhusu usalama ili kujenga stadi ya kusoma;
ch) Kusikiliza hadithi inayosomwa na mwalimu kuhusu usalama ili kujenga
usikivu wake;
d) Kufahamu hadithi aliyoisoma au kusomewa kuhusu usalama wake ili kupata
ujumbe wa hadithi;
e) Kuchangamkia kusoma hadithi kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi;
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi;
Mwanafunzi adhihirishe ufahamu wa matumizi ya msamiati uliotumika
kwenye hadithi;
129
Mwanafunzi asikilize mwalimu anaposoma hadithi kisha asome na
mwalimu na baadaye asome peke yake, wawili wawili au katika vikundi;
Wanafunzi waweza kusikiliza hadithi ikisomwa kwa kutumia tarakilishi na
projekta;
Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kutoka kwa kitabu mbele ya darasa;
Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi;
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kutokana na hadithi.
Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za hadithi bunifu mbalimbali;
Rekodi za hadithi bunifu mbalimbali;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu, projekta;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 102;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu ili kujenga stadi ya wanafunzi ya
kusikiliza pamoja na ya kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa
vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake. Mwalimu
anaweza kuwaonyesha wanafunzi michoro au picha za hadithi bunifu ambazo
atawasomea wanafunzi darasani na nyingine ambazo watajisomea wenyewe.
Mwalimu anaweza kumwalika mtambaji, msimulizi au msomaji mashuhuri
akawasomea wanafunzi hadithi bunifu kisha wanafunzi wakasoma baada
yake katika makundi makubwa hadi kusoma kwa mwanafunzi mmoja mmoja.
Msimulizi mwalikwa huyu sharti awe na uwezo wa kusoma kwa sauti ya kusikika,
ya kuvutia na kwa matamshi sahihi na ufasaha.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
130
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
funzo la hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao
ya kusikiliza pamoja na kusoma hadithi bunifu. Mwalimu awagawe wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha awaombe watazame mchoro
ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 102. Wanafunzi wachunguze
mchoro huo na kuujadili katika makundi yao. Mwalimu anaweza kuwauliza
wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na mchoro huo kama vile: Unaona nini
kwenye mchoro huu? Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu
maswali waliyoulizwa. Mwalimu ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote
katika majadiliano haya.
Baada ya shughuli hii ya kuchunguza mchoro uliopo, mwalimu awaombe
wanafunzi wafunge vitabu vyao kisha wamsikilize akiwasomea hadithi iliyo
katika vitabu vyao. Mwalimu ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa
makini. Pia, mwalimu ahakikishe kuwa anasoma hadithi hiyo kwa matamshi
sahihi, kwa ufasaha na kwa sauti ya kusikika na kuvutia. Baada ya mwalimu
kusoma hadithi hiyo, wanafunzi wasome baada yake kisha katika makundi
ya wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi apewe fursa ya kusoma pekee
yake. Mwalimu ahakikishe anakosoa makosa yoyote ya matamshi pindi tu
yanapotokea. Shughuli hii ya kila mwanafunzi kusoma pekee yake itasaidia
katika kukuza uwezo na stadi ya kusoma ya kila mwanafunzi. Kupitia kwa zoezi
hili, ni rahisi kwa mwalimu kufahamu matatizo ya kila mwanafunzi kibinafsi.
Kila mwanafunzi ashughulikiwe kibinafsi.
131
Baada ya kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi amesoma hadithi hiyo kwa
usahihi na ufasaha, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao
kujibu maswali waliyopewa katika vitabu vyao. Maswali hayo yanahusu hadithi
waliyoisoma darasani. Wanafunzi wanaotatizika wasaidiwe.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi bunifu. Pia,
mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kusoma hadithi
na kuweza kujibu maswali ya hadithi hiyo kwa usahihi kulingana na muktadha
wa hadithi hiyo.
VI. Majibu
Maswali ya makundi, ukurasa 103
1. Sofia alikuwa mtoto mtukutu.
2. Alivuka barabara bila kutazama pande zote.
3. Sofia alipona baada ya wiki tatu.
4. Mama na dada ya Sofia.
5. Daktari
Zoezi la makundi, ukurasa 103
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Mada Ndogo 5: Saru: Matumizi ya huyo na hao
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kufahamu matumizi ya huyo na hao katika mawasiliano;
b) Kutumia huyo na hao katika sentensi kwa usahihi ili kuimarisha mawasiliano;
ch) Kusoma sentensi zinazojumuisha huyo na hao ili kujenga stadi ya kusoma;
132
d) Kuandika sentensi zinazojumuisha huyo na hao katika kuimarisha uandishi;
e) Kuchangamkia matumizi ya huyo na hao katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome sentensi zenye kudhihirisha matumizi ya huyo na hao
kama vile: Huyo ni nani?
Mwanafunzi aandike sentensi zinazodhihirisha matumizi ya huyo na hao
kama vile: Huyo ni nani? Huyo ni kaka.
Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia huyo na hao.
Mwanafunzi aigize vitendo vya kuwaashiria watu mbalimbali kwa kutumia
huyo na hao.
Mwanafunzi aweza kukamilisha mafungu yanayohusu matumizi ya huyo
na hao wakiwa wawili wawili k.m.
Mtoto ________ (huyo); Watoto _______(hao).
III. Nyenzo
Michoro ya watu wakiashiria viumbe mbalimbali;
Chati zenye sentensi za kurejelea viashiria vya mbali kidogo;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 104;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Sarufi ni kipengele muhimu katika ujifundishaji wa wanafunzi. Mwalimu
anastahili kutilia maanani dhana hii ili kuweza kuwahusisha wanafunzi kwa
ukamilifu katika somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi
kabla ya vipindi hivi. Wanafunzi watumiwe sana katika funzo hili la matumzi ya
huyo na hao, hali ya umoja na wingi.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa
maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha
133
kama wanafunzi wengine. Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia
mwalimu ahakikishe anatumia au anamwalika mtaalamu wa lugha ishara.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi iliyopendekezwa
katika Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu aanze funzo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu
awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika kipindi
kilichotangulia.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu
kisha awashirikishe wanafunzi wote katika kuchunguza michoro iliyo katika
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 104. Mwalimu awachangamshe wanafunzi
kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusiana na michoro hiyo kama vile: Unaona
nini kwenye michoro hii? Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na
wanayoona kwenye michoro waliyopewa vitabuni mwao. Katika zoezi hili la
kuchunguza michoro waliyopewa, wanafunzi watunge sentensi sahihi kwa kila
mchoro waliopewa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote. Kisha, wanafunzi
walinganishe kwa usahihi sentensi walizopewa na michoro iliyopo.
Katika hatua hii, wanafunzi watapata fursa ya kujifundisha kuhusu matumizi ya
huyo na hao katika mazungumzo na katika mawasiliano kwa jumla. Wanafunzi
waelezwe kuwa matumizi ya huyo na hao huathiri majina ya viumbe hai pekee.
Huyo na hao hutumika kama maneno ya kuonyesha au kuashiria umbali wa
kiumbe. Hutumika kuonyesha kuwa kiumbe husika yuko mbali kidogo na
msemaji au mzungumzaji.
134
Kwa mfano:
Umoja Wingi
1. Huyo ni mbwa. Hao ni mbwa.
2. Huyo ni mtoto. Hao ni watoto.
3. Mwanafunzi huyo amechelewa. Wanafunzi hao wamechelewa.
Wanafunzi wafahamu na waweze kutunga sentensi kwa kutumia huyo na hao.
Mwalimu awaelekeze wanafunzi katika ujifundishaji wao.
Wanafunzi wafanye mazoezi zaidi ya kutunga sentensi sahihi kwa kutumia huyo
na hao, hali ya umoja na wingi.
ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa kwa kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana
kwa kutumia huyo na hao, umoja na wingi. Pia, mwalimu achunguze iwapo
wanafunzi wanaweza kutunga sentensi sahihi katika umoja na wingi kwa
kutumia huyo na hao.
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 104
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi wabuni na kuandika
sentensi kwa kila mchoro waliopewa katika vitabu vyao.
Zoezi, ukurasa 105
1. Kaka huyo anakuja.
2. Mwalimu wetu ni huyo.
3. Watoto wazuri ni hao.
4. Rafiki yako ni huyo.
5. Wageni hao ni wetu.
135
Matokeo maalum yanayotarajiwa Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kufikia mwisho wa mada, mwanafun-
zi aweze:
(a) Kutambua alfabeti za Kiswahili ili
kuimarisha usomaji;
(b) Kutambua msamiati ambao
hutumiwa katika hali ya anga ili
kuelezea hali ya anga ifaavyo;
(ch) Kutambua msamiati unaotumika
kuonyesha hali ya anga ili
kuimarisha mawasiliano;
(d) Kutambua picha za kuonyesha hali
ya anga ili kuimarisha ufahamu;
(e) Kutambua maneno na viambishi
vinavyowakilisha nafsi ya pili wakati
uliopita ili kumarisha mawasiliano.
Mwanafunzi asome alfabeti za
Kiswahili kwa mfuatano: a, b, ch, d,
dh, e, f, g, gh, h, i, j, k, l, m, n, ny, ng,
ng’, o, p, r, s, sh, t, th, u, v, w, y, z.
Mwanafunzi atoe maana ya
msamiati unaohusu hali ya anga.
Mwanafunzi asimulie visa kuhusu
hali mbalimbali za anga.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi atumie nafsi ya pili
wakati uliopita hali ya umoja na
wingi katika mazungumzo.
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kazi ya vikundi.
Shughuli za vyama vya ushirika shuleni.
Michezo.
Uhusiano na masomo mengine:
Somo kuhusu Mazingira.
Mada Kuu 6: Hali ya Anga
Idadi ya vipindi: 12
Sura ya
6
136
Nyenzo:
Michoro au picha za hali mbalimbali za anga;
Kadi zenye alfabeti za Kiswahili;
Mtambaji au msimulizi mwalikwa;
Rekodi ya masimulizi bunifu;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 106;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Alfabeti za Kiswahili ni herufi muhimu sana katika matamshi ya kila mtu. Maneno
yote ambayo watu huzungumza katika Kiswahili huwa yameundwa kwa kutumia
herufi za Kiswahili. Mwalimu atilie maanani wazo hili ili kufanikisha ufundishaji
wake wa wanafunzi katika kiwango hiki. Kwa kufanya hivi, wanafunzi wataweza
kupata maarifa na uwezo wa kutamka herufi kwa usahihi pamoja na kubaini
zilikotumika kwenye maneno na sentensi.
Mada hii inashughulikia kuwafahamisha wanafunzi kuhusu hali mbalimbali
za anga. Mabadiliko ya anga huathiri binadamu wote wawe watu wazima au
watoto. Ni muhimu kwa wanafunzi kufahamu hali mbalimbali za anga na namna
ya kujiandaa kihali. Mwalimu ahakikishe kuwa wanafunzi wote wanashirikishwa
kupata maarifa haya.
Pia, mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kujenga stadi yake ya kusikiliza
na kuzungumza pamoja na kusoma kupitia kwa masimulizi pamoja na hadithi
bunifu zinazohusu hali za anga.
Kipengele cha sarufi pia kitashughulikiwa katika mada hii ambapo wanafunzi
watafahamu matumizi ya viambishi vya nafsi ya pili, wakati uliopita ili kuimarisha
mawasiliano yao ya jumla.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
Elimu ya Maendeleo Endelevu,
Elimu ya Mazingira hali ya anga,
Uzalendo: ushirikiano katika vikundi,
Amani na maadili.
137
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii ni kuhusu hali za anga ni kama vile:
Msamiati Maana
1.
jua kali
mwangaza mkubwa na mkali utokao angani mchana
2.
mvua
maji yatokayo angani
3.
upepo
hewa yenye nguvu nyingi
4.
mwavuli
kifaa cha kujikinga dhidi ya mvua au jua kali
5.
joto
hewa kuwa moto hadi mtu kutokwa na jasho
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Mwalimu ahakikishe anawashughulikia na kuwashirikisha wanafunzi walio na
ulemavu na matatizo mbalimbali, kwa kuwa na vifaa maalum vya kuwasaidia
wanafunzi hawa katika ujifundishaji wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa
kuona, mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya breli pamoja na vifaa vya
kunasia sauti.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri wa
lugha ya ishara. Maandalizi haya yatawawezesha wanafunzi hawa kusoma kama
wanafunzi wenzao bila vikwazo vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya vipindi
Mada Ndogo 1: Alfabeti za Kiswahili
2
Mada Ndogo 2: Msamiati
2
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 5: Sarufi: Matumizi ya huyu na hawa
3
JUMLA: 12
138
Mada Ndogo 1: Alfabeti za Kiswahili
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua alfabeti za Kiswahili ili kuimarisha usomaji;
b) Kusoma alfabeti za Kiswahili kwa mfuatano ufaao katika kuimarisha
matumizi ya kamusi baadaye;
ch) Kubainisha irabu za Kiswahili ili kuelewa jinsi silabi huundwa;
d) Kubainisha konsonanti za Kiswahili ili kuelewa jinsi silabi huundwa;
e) Kuandika alfabeti za Kiswahili katika kuimarisha uandishi bora;
f) Kuthamini alfabeti katika lugha.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome alfabeti za Kiswahili kwa mfuatano: a, b, ch, d, dh, e, f,
g, gh, h, i, j, k, l, m, n, ny, ng, ng’, o, p, r, s, sh, t, th, u, v, w, y, z.
Mwanafunzi aweza kusoma alfabeti kwenye chati.
Mwanafunzi aweza kuimba wimbo wa alfabeti.
Mwanafunzi ashiriki katika kikundi ili kutenganisha konsonanti na irabu
akitumia kadi za herufi.
Mwanafunzi aandike alfabeti za Kiswahili.
Wanafunzi washiriki katika mjadala kuhusu umuhimu wa alfabeti katika
lugha.
III. Nyenzo:
Kadi za alfabeti za Kiswahili;
Rekodi za sauti za alfabeti za Kiswahili;
Kadi zenye maneno yenye alfabeti za Kiswahili;
Mgeni mwalikwa mwenye matamshi mazuri na sahihi;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 107-113;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
139
IV. Maandalizi ya somo
Mada hii ndogo inahusu alfabeti za Kiswahili pamoja na majina ya herufi za
Kiswahili. Lugha ya Kiswahili ina irabu tano ambazo ni: a, e, i, o, u. Konsonanti
katika lugha ya Kiswahili ni ishirini na sita. Matamshi mazuri na sahihi ya
wanafunzi yatazingatiwa hapa na kukuzwa zaidi. Wanafunzi walio na matatizo
ya matamshi wasaidiwe kukuza uwezo wao wa kutamka kwa usahihi. Wanafunzi
hawa wafanye mazoezi kadhaa ya utamkaji wa alfabeti za Kiswahili. Mwalimu
awasaidie wakiwa na matatizo. Pia, wanafunzi wengine wenye matamshi mazuri
wanaweza kuwasaidia hawa wanaolemewa.
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama
vilivyotajwa hapo juu bila kusahau vyombo vingine maalum vya kuwasaidia
wanafunzi wenye ulemavu na matatizo mbalimbali.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa alivyovileta darasani. Mwalimu akumbuke kuwa matumizi ya
michoro, picha na vifaa halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha
ufundishaji wa wanafunzi; hasa wale ambao wana matatizo mbalimbali katika
kuelewa na kufahamu haraka yale wanayofundishwa darasani.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwenye vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize somo hili kwa kuwaamkua wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichopita. Wanafunzi wajibu
maamkuzi ya mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
a) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili
wachunguze sauti walizopewa katika vitabu vyao na wazitamke kwa awamu
kadhaa. Kwanza, wanafunzi waanze kwa kutamka irabu tano za Kiswahili
walizopewa ambazo ni a, e, i, o, u. Wanafunzi watamke irabu hizi wakiwa darasa
zima kisha katika makundi ya wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi apate
fursa ya kuzitamka irabu hizi.
140
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wanatamka kwa ufasaha. Akosoe makosa ya
kimatamshi pale yanapotokea.
Baada ya mwalimu kubaini kuwa wanafunzi wote wameweza kutamka irabu
hizo kwa usahihi, awaongoze kutamka konsonanti walizopewa katika vitabu
vyao. Wanafunzi watamke konsonanti hizi pamoja na mwalimu kisha baada ya
mwalimu. Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli
hii ya utamkaji. Baadaye, wanafunzi watamke konsonanti hizi katika makundi ya
wanafunzi wawili wawili na hatimaye kila mwanafunzi apate fursa ya kuzitamka
konsonanti hizi peke yake. Mwalimu awe makini kutambua unyonge wa kila
mwanafunzi na kuwasaidia. Wanafunzi walio na matamshi fasaha ya konsonanti
hizi wanaweza kuwasaidia wanafunzi wanaolemewa.
Baada ya shughuli hii ya utamkaji, mwalimu awashirikishe wanafunzi kuchunguza
michoro waliyopewa katika vitabu vyao. Michoro hii ni ya kuwakilisha kila
alfabeti ya Kiswahili kuanzia Aa hadi Zz. Wanafunzi wasome majina ya michoro
hiyo na kuichunguza ili kuelewa kila alfabeti.
Mwishowe, mwalimu awaelekeze wanafunzi katika kuziandika alfabeti za
Kiswahili katika madaftari yao. Mwalimu ahakikishe wanafunzi wanaandika kwa
usahihi alfabeti hizo.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi zaidi ya utamkaji wa
alfabeti za Kiswahili.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kutamka kwa ufasaha na mfuatano alfabeti za Kiswahili
kuanzia Aa hadi Zz. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza
kuziandika alfabeti za Kiswahili zote kwenye madaftari yao kwa usahihi.
141
VI. Majibu
Zoezi, ukurasa 107
1. Irabu/vokali
2. Konsonanti
3. Irabu na konsonanti
Zoezi la makundi, ukurasa 108
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Zoezi la kusikiliza, ukurasa 109
Mwalimu atathmini namna wanafunzi wanavyoimba alfabeti.
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Msamiati
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati ambao hutumiwa katika hali ya anga ili kuelezea hali ya
anga ifaavyo;
b) Kutambua hali ya anga ya siku husika ili kuimarisha mawasiliano;
ch) Kueleza maana ya msamiati unaohusu hali ya anga katika kuimarisha stadi
ya kuzungumza na kuandika;
d) Kutumia msamiati unaohusu hali ya anga katika sentensi sahihi ili kuimarisha
stadi ya kuzungumza na kuandika;
e) Kuthamini hali mbalimbali za anga ili kuelewa misimu.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atoe maana ya msamiati unaohusu hali ya anga.
Mwanafunzi atunge sentensi sahihi akitumia msamiati unaohusu hali ya
anga kama vile upepo, jua, mvua na mawingu.
Mwanafunzi aweza kutazama video inayoonyesha hali mbalimbali za anga.
Mwanafunzi atazame michoro na picha zinazolenga hali mbalimbali za
anga.
142
Mwanafunzi achore baadhi ya michoro inayoashiria hali mbalimbali za
anga kama vile mvua, mawingu na jua.
Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu umuhimu wa hali mbalimbali
za anga.
III. Nyenzo:
Kadi zenye majina ya hali mbalimbali za anga;
Michoro ya kuonyesha hali mbalimbali za anga,
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 114-115;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Msamiati kuhusu hali mbalimbali za anga ni muhimu kwa sababu shughuli za
binadamu hutegemea hali ya anga ilivyo. Mwalimu anastahili kutilia maanani
dhana hii wakati wa uandalizi wa funzo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake
mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama vilivyotajwa hapo. Mwalimu
ahakikishe ana vyombo maalum vya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu na
matatizo mbalimbali.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa alivyovileta darasani kwa kukumbuka kuwa matumizi ya
michoro, picha na kadi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha ufundishaji
wa wanafunzi; hasa wale ambao wana matatizo mbalimbali katika kuelewa na
kufahamu haraka yale wanayofundishwa darasani au wale walio na kiwango
cha chini katika ujifunzaji wao.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
watafsiri wa lugha ishara. Pia, ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni
lazima mwalimu ajitahidi kuandaa maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha
wanafunzi wa aina hii kujifundisha kama wanafunzi wengine.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi katika
vitabu vyao.
143
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu awaamkue wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu shughuli
zao mbalimbali za kila siku kuhusiana na hali mbalimbali za anga. Wanafunzi
wajibu maamkuzi ya mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awashirikishe katika kuchunguza michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi,
ukurasa 114. Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na
michoro hiyo. Baadhi ya maswali ambayo mwalimu anaweza kuuliza ni kama
vile: Unaona nini kwenye michoro hii? Watu hawa wanafanya nini? Taja majina
ya hali za anga unazoona. Mwalimu awaelekeze wanafunzi ili waweze kujibu
maswali hayo na kuelewa kinachoendelea katika michoro iliyopo.
Mwalimu awaelekeze wanafunzi katika makundi yao watambue hali mbalimbali
za anga zikiwemo mvua, jua kali, upepo na mawingu. Wanafunzi waelekezwe
kujadiliana katika makundi yao kuhusu hali hizi za anga na shughuli ambazo
hufanyika katika hali hizi. Wanafunzi wajadili hata na mavazi ambayo watu
huvaa katika hali mbalimbali za anga kama vile kuvaa nguo zenye joto wakati
wa mvua na kuvaa nguo nyepesi wakati wa jua kali.
Baadaye, wanafunzi wajadili kuhusu umuhimu wa hali mbalimbali za anga kwa
binadamu. Kwa mfano, msimu wa mvua huwasaidia wakulima kwa kuinyunyizia
mimea yao maji na kuifanya inawiri. Watu pia huweza kupata maji ya kutumia
nyumbani. Kando na uzuri wa mvua, mvua pia ina madhara inaponyesha kupita
kiasi.
Kila kundi lipewe muda wa kujadiliana na kuwasilisha mbele ya wenzao.
Shughuli hii ya kuwasilisha mbele ya wenzao itakuza ujasiri wa wanafunzi wa
kusimama na kuongea mbele ya watu.
Kabla ya kukamilisha funzo hili, mwalimu awe ameandaa mapema video
inayoonyesha hali mbalimbali za anga. Wanafunzi watazame video hii kwa
pamoja darasani. Mwalimu ahakikishe kila mwanafunzi anaweza kuona vizuri
video hiyo. Wanafunzi wajaribu kubaini hali mbalimbali za anga katika video
hiyo. Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli
hii. Hatimaye, wanafunzi washirikishwe katika kujibu maswali kuhusu video
waliyopewa katika vitabu vyao.
144
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 114
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi waeleze wanachoona
kwenye michoro waliyopewa kwenye vitabu vyao. Pia, waeleze mambo
ambayo wao huyafanya wakati wa mvua kunyesha.
Zoezi, ukurasa 115
1. jua
2. mawingu
3. upepo
Wanafunzi wote washirikishwe katika kufanya mazoezi waliyopewa katika
vitabu vyao.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu hali mbalimbali za anga, umuhimu wake
pamoja na madhara yake kwa maisha ya binadamu.
Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza kuandika kwa usahihi
majina ya hali mbalimbali za anga.
Mada Ndogo 3: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati unaotumika kuonyesha hali ya anga ili kuimarisha
mawasiliano;
b) Kubainisha hali mbalimbali za anga ili kuimarisha stadi ya kuzungumza;
ch) Kusimulia kuhusu hali mbalimbali za anga ili kuimarisha stadi ya kuzungumza;
d) Kusikiliza masimulizi kuhusu hali ya anga ili kujenga umakinifu;
e) Kuthamini umuhimu wa hali ya anga katika maisha ya kila siku.
145
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asimuliwe visa kuhusu hali mbalimbali za anga.
Mwanafunzi aweza kutazama video inayohusu hali ya anga.
Wanafunzi waweza kupewa nafasi kwenda nje ya darasa na kujadiliana
kuhusu hali ya anga wakati huo.
Mwanafunzi ashiriki katika majadiliano kuhusu hali za anga tofauti kama
vile upepo, jua, mvua na mawingu katika makundi.
Mwanafunzi aeleze hali mbalimbali za anga kwa kutumia michoro au picha.
III. Nyenzo:
Rekodi za masimulizi bunifu mbalimbali kuhusu hali za anga;
Michoro au picha za vitendo vya hali mbalimbali za anga;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Mgeni mwalikwa (mtaalamu wa hali ya anga);
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 115-117;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusikiliza masimulizi
bunifu yanayohusu hali mbalimbali za anga ili kujenga stadi yao ya kusikiliza
na kuzungumza. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika
kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake. Mwalimu anaweza
kumwalika mgeni kama vile mtaalamu wa hali ya anga atakayezungumza
kuhusu hali mbalimbali za anga pamoja na mabadiliko yake mwakani.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi
146
wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza masimulizi bunifu pamoja na stadi ya kuzungumza kupitia kwa
wao wenyewe kuwasimulia wenzao. Masimulizi haya yatahusu hali mbalimbali
za anga.
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awaombe watazame michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 116-
117. Wanafunzi katika makundi yao waeleze wanachoona katika michoro hiyo
na wajaribu kusimuliana kuhusu hali mbalimbali za anga.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
Wanafunzi wajibu maswali waliyopewa kwenye kitabu chao kuhusu michoro
waliyopewa.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awaongoze wanafunzi kusoma vifungu
vifupivifupi vilivyo katika kitabu cha mwanafunzi kuhusu hali mbalimbali za
anga. Mwalimu asome kwanza kisha wanafunzi wasome na yeye na hatimaye
wasome wakiwa wawili wawili hadi kusoma mmoja mmoja. Anaposoma,
mwalimu ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa makini. Pia, mwalimu
ahakikishe kuwa anasoma kwa ufasaha, kwa matamshi sahihi na sauti ya
kusikika na ya kuvutia. Iwapo mwalimu ana matatizo ya kimatamshi, anaweza
kumwalika msomaji stadi atakayewasomea au kuwasimulia wanafunzi hadithi
kuhusu hali mbalimbali za anga. Baadaye, mwalimu awashirikishe katika kujibu
maswali ya masimulizi waliyopewa. Mwalimu ahakikishe anawasaidia wanafunzi
wanaotatizika katika makundi yao.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma masimulizi bunifu
pamoja na kufahamu hali mbalimbali za anga. Pia, mwalimu achunguze
iwapo wanafunzi wameweza kupata maarifa ya kujibu kwa usahihi maswali ya
masimulizi kulingana na muktadha husika.
147
IV. Majibu
Maswali, ukurasa 116
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kulingana na wanayoona kwenye
michoro husika.
Zoezi la makundi, ukurasa 116 -117
1. Kitu hicho ni jua.
2. Matone ya maji yanayotoka angani ni mvua.
3. Vitu vyeupe ambavyo vinafunika jua kama blanketi kubwa huitwa
mawingu.
4. Husukumwa na upepo.
Mada Ndogo 4: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua picha za kuonyesha hali ya anga ili kuimarisha ufahamu;
b) Kutambua maneno yanayohusiana na hali ya anga ili kuimarisha usomaji;
ch) Kusoma hadithi zinazohusu hali ya anga ili kuimarisha usomaji;
d) Kusikiliza hadithi za mwalimu kuhusu hali ya anga ili kujenga stadi ya
kusoma na kusikiliza;
e) Kufahamu hadithi aliyoisoma kuhusu hali ya anga ili kupata ujumbe;
f) Kuchangamkia kusoma hadithi katika maisha ya kila siku.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi;
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi;
Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi;
Mwanafunzi asikilize mwalimu anaposoma hadithi kisha asome na
mwalimu na baadaye asome peke yake, wakiwa wawili wawili au katika
vikundi;
Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kwa kutumia tarakilishi na
projekta;
148
Mwanafunzi asome hadithi kutoka kwa kitabu mbele ya darasa;
Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi;
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali baada ya kusoma hadithi;
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kutokana na hadithi;
Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za kuonyesha hali za anga;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Rekodi za hadithi bunifu kuhusu hali ya anga;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 118;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu inayohusu hali ya anga kwa kutaja
mabadiliko mbalimbali ya anga ili kujenga stadi ya wanafunzi ya kusikiliza na
kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika kufundishia
funzo hili kama vilivyoorodheshwa hapo juu. Hili litamsaidia kufanikisha
ufundishaji wake. Mwalimu anaweza kurekodi hadithi kuhusu hali ya anga au
hata video ambazo wanafunzi wanaweza kuzitazama na kuzisikiliza darasani.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika lililotolewa kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi kusahihisha zoezi walilopewa katika funzo
la hapo awali. Iwapo kuna wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe.
149
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusoma pamoja na ya kusikiliza hadithi bunifu. Mwalimu awagawe
wanafunzi katika makundi kisha awaombe watazame mchoro ulio katika Kitabu
cha Mwanafunzi, ukurasa 118. Wanafunzi wachunguze mchoro huo na kuujadili
katika makundi yao.
Mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na
mchoro huo kama vile: Unaona nini kwenye mchoro huu? Mwalimu awaelekeze
wanafunzi kuhusu namna ya kujibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu ahakikishe
amewashirikisha wanafunzi wote katika majadiliano haya. Wanafunzi wajibu
maswali ya mwalimu kulingana na wanayoona katika mchoro waliopewa.
Kisha, mwalimu awaombe wanafunzi wote wawe makini naye awasomee
hadithi bunifu ifuatayo. Wanafunzi wasikilize kwa makini. Mwalimu ahakikishe
anasoma kwa matamshi sahihi na kwa sauti ya kusikika na wanafunzi wote.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kujadili kuhusu hali mbalimbali
za anga zilizotajwa katika hadithi bunifu ya mwalimu.
Mfano wa masimulizi
MVUA KUBWA YA KISIRANI
Ilikuwa siku ya Jumamosi. Sisi tulikuwa ndani ya nyumba. Tulikuwa tukitazama
runinga. Upepo mkali ulikuwa unavuma nje. Baada ya dakika chache, mawingu
meusi yalijaa angani. Jua lilianza kupotea. Hii ilikuwa dalili ya mvua kunyesha.
Nilitazama nje kupitia kwa dirisha. Manyunyu yalidondoka. Upepo ulikuwa
unavuma. Matawi ya miti yaliyumba. Niliyaona mawingu mengi meusi. Mawingu
hayo yakalifunika jua. Jua lilipotea. Mvua ilianza kunyesha. Paa ya nyumba
yetu iling’olewa na upepo mkali. Miti ilivunjika. Majani yalianguka ardhini. Hii
ilikuwa mvua ya kisirani. Maji yalijaa kila mahali. Nyumba yetu ilibebwa na maji.
Wasamaria wema walituokoa. Hatukuzama majini.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kujibu maswali ya hadithi
aliyowasomea waliyopewa katika vitabu vyao.
150
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi bunifu. Pia,
mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa hali mbalimbali
za anga.
VI. Majibu
Maswali ya hadithi, ukurasa 118
1. Walikuwa ndani ya nyumba
2. Meusi
3. Matawi
4. Mawingu
5. Paa la nyumba liling’olewa.
Mada Ndogo 5: Saru: Nafsi ya pili wakati uliopita
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua maneno na viambishi vinavyowakilisha nafsi ya pili wakati
uliopita ili kuimarisha mawasiliano;
b) Kusoma vifungu vya maneno yanayoashiria nafsi ya pili wakati uliopita ili
kuimarisha usomaji;
ch) Kutumia nafsi ya pili wakati uliopita hali ya umoja na wingi katika sentensi
ili kuimarisha mawasiliano;
d) Kuandika vifungu vya maneno vinavyoashiria nafsi ya pili wakati uliopita
katika hali ya umoja na wingi ili kuimarisha uandishi bora;
e) Kufurahia kutumia nafsi ya pili wakati uliopita hali ya umoja na wingi
katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
• Mwanafunzi atumie nafsi ya pili wakati uliopita hali ya umoja na wingi
katika mazungumzo.
151
• Mwanafunzi atumie nafsi ya pili wakati uliopita hali ya umoja na wingi
katika sentensi.
• Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia maneno na viambishi
vinavyowakilisha nafsi ya pili wakati uliopita kama vile: wewe, u, li,
nyinyi (ninyi) na m hali ya umoja na wingi.
• Mwanafunzi aigize nafsi ya pili wakati uliopita hali ya umoja na wingi
katika makundi kwa kutumia mafungu kama vile: wewe uliandika
nyinyi mliandika; wewe ulisoma nyinyi mlisoma.
• Mwanafunzi aweza kupewa zoezi katika tarakilishi ili atumie mbinu ya
kuburuta majibu sahihi na kutia kapuni.
III. Nyenzo:
ØMichoro ya watu wakitenda vitendo kwa kurejelea nafsi ya pili;
ØChati zenye sentensi katika umoja na wingi za nafsi ya pili;
ØWanafunzi wenyewe;
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 119;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Mwalimu anastahili kutilia maanani kuwa sarufi ni kipengele muhimu katika
ujifundishaji wa wanafunzi ili kuweza kuwahusisha wanafunzi kwa ukamilifu
katika somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla
ya vipindi hivi. Wanafunzi wenyewe kwa wenyewe watumiwe katika funzo hili
kuonyesha matumizi ya nafsi ya pili hali ya umoja na wingi.
Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati mwafaka wa kuweka
hadharani vifaa vyake kwa kukumbuka kuwa matumizi ya michoro, picha na vifaa
halisi ni mbinu bora ambayo hutumika kufanikisha ufundishaji wa wanafunzi.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo au ulemavu wa kutosikia au kutoona,
mwalimu ahakikishe ana vifaa au vyombo maalum vya kuwafundishia kama
vile watafsiri wa lugha ishara pamoja na breli.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, mwalimu ahakikishe kwamba
wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana kulingana
na maelekezo yaliyopendekezwa katika vitabu vyao.
152
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu aanze funzo hili kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza maswali
mepesi kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu
salamu za mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe
wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika kipindi kilichotangulia.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha
awashirikishe wanafunzi wote katika kuchunguza michoro iliyo katika Kitabu cha
Mwanafunzi, ukurasa 119. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza
maswali mepesi kuhusiana na michoro hiyo kama vile: Mnaona nini kwenye
michoro hii? Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na wanayoona
kwenye michoro waliyopewa vitabuni mwao. Kisha, wanafunzi wasome kwa
usahihi sentensi walizopewa katika vitabu vyao zilizotumia nafsi ya pili hali ya
umoja na wingi katika wakati uliopita.
Katika hatua hii, wanafunzi watapata fursa ya kujifundisha matumizi ya wewe
na nyinyi, hali ya umoja na wingi kwa kurejelea hali mbalimbali za anga katika
wakati uliopita. Wanafunzi wafahamu na waweze kutunga sentensi sahihi kwa
kutumia nafsi ya pili, umoja na wingi katika wakati uliopita.
Kwa mfano:
Umoja Wingi
1. Wewe uliyaona mawingu. - Nyinyi mliyaona mawingu.
2. Wewe uliketi juani. - Nyinyi mliketi juani.
3. Wewe ulinyeshewa jana. - Nyinyi mlinyeshewa jana.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi kutambua kuwa wewe na nyinyi ni maneno
ya kuonyesha au kuashiria mtu katika nafsi ya pili. Kiambishi -li- hutumika
kuonyesha wakati uliopita.
Wanafunzi wafanye mazoezi zaidi ya kutunga sentensi sahihi kwa kutumia nafsi
ya pili hali ya umoja na wingi katika wakati uliopita.
153
VI. Majibu
Zoezi, ukurasa 120
1.
Nyinyi mlioga vizuri.
2.
Wewe ulifua nguo.
3.
Wewe ulivaa viatu.
4.
Nyinyi mlikuja shuleni.
5.
Wewe na dada mlisoma jana.
ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa kwa kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana
kwa kutumia nafsi ya pili hali ya umoja na wingi katika wakati uliopita. Pia,
mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza kutunga sentensi sahihi katika
umoja na wingi kwa kutumia nafsi ya pili.
154
Matokeo maalum yanayotarajiwa Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kukia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kutambua msamiati kuhusu lishe
bora ili kuimarisha mawasiliano;
(b) Kutambua vyakula vinavyofaa
mwili ili kuimarisha stadi ya
kuzungumza;
(ch) Kusikiliza hadithi ya mwalimu ili
kuimarisha stadi za kusikiliza na
kusoma;
(d) Kutambua matumizi ya hiki na hivi
katika kuimarisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelezee maana ya
msamiati unaohusiana na lishe bora
kama vile: afya, protini, vitamini,
wanga (vyakula vinavyopatia mwili
nguvu) chumvi, ukosefu, upungufu
na baadhi ya vyakula vinavyofaidi
mwili.
Mwanafunzi ataje baadhi ya
vyakula kwa kuonyeshwa michoro
na vyakula halisi.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi asome vifungu
vinavyojumuisha hiki na hivi kama
vile: Kitabu hiki Vitabu hivi;
Kifutio hiki Vifutio hivi.
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
• Kazi ya vikundi.
• Michezo.
• Vyama vya ushirika shuleni.
Mada Kuu 7: Lishe Bora
Idadi ya vipindi: 12
Sura ya
7
155
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Afya na Lishe Bora.
III. Nyenzo:
Picha au michoro ya vyakula mbalimbali;
Aina mbalimbali za vyakula halisi;
Rekodi za masimulizi mbalimbali;
Kadi zenye majina ya vyakula mbalimbali;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 122;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Mada hii inashughulikia lishe bora kwa kurejelea aina mbalimbali ya vyakula
ambavyo hufaidi mwili wa binadamu, msamiati wa vyakula mbalimbali,
masimulizi kuhusu lishe bora pamoja na kusoma hadithi kuhusiana na
masuala lishe bora. Pia, kipengele cha sarufi kuhusu matumizi ya hiki na hivi
yameangaziwa katika mada hii.
Lengo kuu la mada hii ni kumsaidia mwanafunzi kujenga stadi yake ya
kusikiliza, kufahamu msamiati kuhusu vyakula mbalimbali, kusimulia hadithi,
kusoma hadithi, pamoja na kufahamu matumizi ya hiki na hivi katika sentensi
na mazungumzo kwa jumla.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
Elimu ya Afya: Magonjwa yanayohusiana na vyakula kuthamini lishe
bora.
Utangamano wa kijamii, wanafunzi watangamane na kufanya kazi pamoja.
156
Msamiati maalum
Baadhi ya msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao
katika mada hii kuhusu lishe bora ni kama vile:
Msamiati Maana
1.
chakula
kitu kinacholiwa ili kufaidi mwili
2.
protini
vyakula vya kujenga mwili
3.
vitamini
vyakula vya kuzuia magonjwa mwilini
4.
wanga
vyakula vya kuupa mwili nguvu
5.
vyakula
wingi wa ‘chakula’
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Ili kuwashirikisha wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali, mwalimu
awe na vifaa maalum vya kuwasaidia wanafunzi wa aina hii katika ujifundishaji
wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri au
wajuzi wa lugha ya ishara.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kuona, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya breli pamoja na vifaa vya kunasia sauti. Haya yatawawezesha
wanafunzi hawa kusoma kama wanafunzi wenzao bila vikwazo vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada Idadi ya vipindi
Mada Ndogo 1: Msamiati
3
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi
3
Mada Ndogo 4: Sarufi: Matumizi ya hiki na hivi
2
JUMLA: 10
157
Mada Ndogo 1: Msamiati Lishe Bora
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua msamiati kuhusu lishe bora ili kuimarisha mawasiliano;
b) Kusoma maneno yanayohusiana na lishe bora ili kuimarisha usomaji;
ch) Kuandika maneno yanayohusu lishe bora katika kuimarisha uandishi bora;
d) Kutumia msamiati uliosomwa katika kutunga sentensi ili kuimarisha
mawasiliano;
e) Kuthamini kula chakula kinachofaidi mwili ili kujikinga kutokana na
madhara ya ukosefu wa lishe bora.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi aelezee maana ya msamiati unaohusiana na lishe bora kama
vile: afya, protini, vitamini, wanga (vyakula vinavyopatia mwili nguvu) chumvi,
ukosefu, upungufu na baadhi ya vyakula vinavyofaidi mwili.
Wanafunzi wajadiliane katika makundi au wakiwa wawili kuhusu vyakula
vinavyodhuru afya.
Mwanafunzi atazame picha za vyakula vinavyoashiria msamiati unaorejelewa
kwenye vyombo vya teknolojia na kuvijadili;
Mwanafunzi asome majina mbalimbali ya vyakula kwenye kadi za maneno.
Mwanafunzi anakili msamiati unaofunzwa kwenye kitabu.
III. Nyenzo:
Kadi zenye majina ya vyakula mbalimbali;
Michoro au picha za vyakula mbalimbali;
Vyakula halisi;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 123;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
158
IV. Maandalizi ya somo
Msamiati wa aina mbalimbali za vyakula ni muhimu kwa sababu kila binadamu
hutegemea chakula ili kupata nguvu, kukingwa dhidi ya magonjwa pamoja
na mwili wake kujengwa. Chakula humsaidia binadamu kuwa hai na kufanya
viungo vyake vya mwili kuweza kufanya kazi. Mwalimu aandae vifaa vyake
mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama vilivyotajwa hapo juu
pamoja na vyombo vingine maalum vya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu
na matatizo mbalimbali.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ishara katika kuwafundisha. Pia, ikiwa kuna wanafunzi
wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa maelezo yake kwenye
breli ili kuwawezesha wanafunzi hawa kujifundisha kama wanafunzi wengine
bila vikwazo vyovyote.
Ni vyema mwalimu ahakikishe kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi
ya wanafunzi wanaotakikana kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwa kila
shughuli ya wanafunzi katika vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu awaamkue wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu aina ya
vyakula mbalimbali ambavyo wamewahi kula. Wanafunzi wajibu maamkuzi
ya mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa. Wanafunzi wataje vyakula
mbalimbali ambavyo wamewahi kuvila.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awashirikishe katika kuchunguza michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi,
ukurasa 123. Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali
mepesi kuhusiana na michoro hiyo. Baadhi ya maswali ambayo mwalimu
anaweza kuuliza ni kama vile: Mnaona nini kwenye michoro hii? Mwalimu
awaelekeze wanafunzi ili waweze kujibu maswali hayo na kuelewa aina ya
vyakula vilivyo katika michoro iliyopo kama vile: wali, mayai, maharage na
ugali.
159
Mwalimu awaelekeze wanafunzi katika makundi yao watambue majina ya
aina za vyakula mbalimbali pamoja na kazi zake katika miili ya binadamu, kwa
mfano: wali huongeza nguvu mwilini, maharage hujenga mwili n.k.
Wanafunzi katika kila kundi wapewe muda wa kusimuliana kuhusu vyakula
mbalimbali ambavyo wamewahi kula, kununua, kutayarisha, waseme walikula
vyakula hivi wapi na iwapo walivifurahia.
Mwalimu awaonyeshe wanafunzi picha au michoro ya vyakula mbalimbali.
Iwapo kuna baadhi ya vyakula hivi shuleni kama vile wali, maharage, ugali n.k.
mwalimu ahakikishe amewaonyesha wanafunzi vyakula hivyo halisi. Wanafunzi
wanaweza kuvigusa na ikiwezekana wakavionja. Mwalimu ahakikishe
anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu vyakula mbalimbali pamoja na matumizi
yake mwilini.
Vilevile, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza kuandika kwa usahihi
majina ya vyakula mbalimbali.
VI. Majibu
Maswali (kuhusu michoro), ukurasa 124
1. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Wanafunzi wataje vyakula
ambavyo wanaviona katika michoro waliyopewa.
2. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi, kwa mfano: mayai, wali,
ugali na maharage.
3. Mayai, maharage.
4. Maembe
5. Ugali
160
Zoezi, ukurasa 125
1. Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
2. Vyakula vinavyoliwa kwa wingi kupita kiasi kama vile: sukari,
chumvi, mafuta n.k.
3. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Kwa mfano, ukosefu wa
lishe bora huweza kudhoofisha afya.
4. Vyakula hivi viliwe kwa uchache sana au viepukwe kabisa.
Zoezi, ukurasa 125
Nyama ya kuku
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua vyakula vinavyofaa mwili ili kuimarisha stadi ya kuzungumza;
b) Kuzungumza juu ya chakula anachokipenda ili kuimarisha mazungumzo;
ch) Kuzungumza juu ya chakula kinachodhuru afya ili kuelewa madhara ya
vyakula hivyo;
d) Kusikiliza masimulizi kuhusu lishe bora ili kujenga stadi ya kusikiliza;
e) Kuthamini vyakula vinavyofaidi mwili ili kuchagua vyakula kwa uangalifu.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ataje baadhi ya vyakula kwa kuonyeshwa michoro na vyakula
halisi.
Wanafunzi wajadiliane kuhusu umuhimu wa vyakula mbalimbali k.m.
vinavyompa mtu nguvu, vinavyomkinga mtu kutokana na magonjwa,
vinavyoleta joto mwilini, vinavyomwezesha mtu kukua n.k.
Mwanafunzi ashiriki katika mazungumzo kuhusu chakula akipendacho.
161
Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu chakula kinachodhuru afya
k.m. vibanzi, biskuti.
Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akisimulia kuhusu lishe
bora na madhara ya vyakula vinavyodhuru afya.
Mwanafunzi aweza kuonyeshwa video kuhusu lishe bora na madhara ya
vyakula hasi na baadaye washiriki katika mijadala ya vikundi.
III. Nyenzo:
Rekodi za masimulizi bunifu mbalimbali kuhusu lishe bora;
Michoro au picha za vyakula mbalimbali;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Mgeni mwalikwa (mtaalamu wa lishe bora);
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 126;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusikiliza masimulizi
bunifu yanayohusu vyakula mbalimbali ili kujenga stadi yao ya kusikiliza na
kuzungumza. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika
kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake kama vilivyotajwa hapo
juu. Mwalimu anaweza kumwalika mgeni kama vile mtaalamu wa lishe bora,
daktari au nesi ili awazungumzie wanafunzi kuhusu lishe bora.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
162
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza masimulizi bunifu pamoja na stadi ya kuzungumza kupitia
kwa wao wenyewe kuwasimulia wenzao. Masimulizi haya yatahusu vyakula
mbalimbali pamoja na umuhimu wavyo.
Wanafunzi wakiwa darasa zima waonyeshwe video ya aina mbalimbali za
vyakula, namna vinavyoandaliwa, vinavyopandwa, kuvunwa na kusafirishwa
na michakato yote inayohusu utayarishaji wa vyakula mbalimbali. Mwalimu
ahakikishe ameandaa video hii mapema kabla ya somo hili. Video hiyo inaweza
pia kuonyesha madhara ya kula vyakula fulani na faida ya kula vingine. Mwalimu
ahakikishe wanafunzi wote wanashirikishwa katika ujifundishaji kupitia kwa
vyombo vya teknolojia.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika zoezi la
masimulizi ambapo kila mmoja atasimama mbele ya wenzake na kusimulia
kuhusu chakula anachokipenda na sababu za kukipenda chakula hicho.
Hatimaye, wanafunzi washirikishwe katika makundi watazame michoro ya
vyakula waliyopewa katika vitabu vyao kisha waeleze sababu za kuviepuka.
Wanafunzi waelezane kuhusu vyakula hivyo ambavyo ni sukari, chumvi, mafuta,
chipsi, biskuti n.k. Mwalimu ahakikishe anawasaidia wanafunzi wanaotatizika
katika makundi yao.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma masimulizi bunifu
pamoja na kufahamu vyakula mbalimbali.
163
VI. Majibu
Zoezi la masimulizi, ukurasa 126
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Zoezi la makundi, ukurasa 127
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kusikiliza hadithi ya mwalimu ili kuimarisha stadi ya kusikiliza na kusoma;
b) Kusoma hadithi kwa mtiririko ufaao ili kuimarisha stadi ya kusoma;
ch) Kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa ili kuelewa ujumbe katika hadithi;
d) Kuchangamkia kusoma hadithi ili kuendelea kujenga stadi ya kusoma.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
Mwanafunzi asikilize mwalimu anaposoma hadithi, asome pamoja na
mwalimu kisha asome peke yake, wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kupitia kwa kinasasauti.
Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma na kusomewa
hadithi.
Mwanafunzi aweza kutazama video ya mtu au mtoto akisoma hadithi
husika kwa ufasaha kisha aige usomi huo.
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kuhusu hadithi.
Mwanafunzi asimulie hadithi kutokana na picha alizopewa za lishe bora.
164
III. Nyenzo:
Rekodi za hadithi bunifu;
Michoro au picha za hadithi bunifu mbalimbali;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu, projekta;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 129;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu ili kujenga stadi ya wanafunzi
ya kusikiliza na kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa
vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake kama
vilivyotajwa hapo juu. Mwalimu anaweza kumwalika mtambaji au msomaji
mashuhuri akawasomea wanafunzi hadithi bunifu kisha wanafunzi wakasoma
baada yake katika makundi makubwa na hatimaye kila mwanafunzi kusoma
mmoja mmoja. Mwalikwa huyu sharti awe na uwezo wa kusoma kwa sauti ya
kusikika na kwa matamshi sahihi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwaamkua wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia.
Wanafunzi wajibu maamkuzi ya mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
funzo la hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika ujifundishaji wao
wasaidiwe.
165
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao
ya kusoma pamoja na kusikiliza hadithi bunifu. Mwalimu awagawe wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha awaombe watazame mchoro
ulio katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 129. Wanafunzi wachunguze
mchoro huo na kuujadili katika makundi yao. Mwalimu anaweza kuwauliza
wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na mchoro huo kama vile: Unaona nini
kwenye mchoro huu? Mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu
maswali waliyoulizwa. Mwalimu ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote
katika majadiliano haya.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusoma hadithi
iliyo katika vitabu vyao kuhusu afya ni mali. Mwalimu awasomee wanafunzi
hadithi hiyo kisha wanafunzi waisome wakiwa wawili wawili na hatimaye kila
mmoja apate fursa ya kusoma peke yake. Wanafunzi wajadiliane kuhusu afya zao
na vyakula vya kuboresha afya pamoja na vile vya kudhoofisha afya. Mwalimu
ahakikishe anakosoa makosa yoyote ya matamshi pindi tu yanapotokea.
Baada ya kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi amesoma hadithi hiyo kwa
usahihi, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi yao kujibu maswali
waliyopewa katika vitabu vyao. Maswali hayo yanahusu hadithi waliyoisoma
darasani. Wanafunzi wanaotatizika wasaidiwe.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusoma pamoja na kusikiliza hadithi
bunifu. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa
kusoma hadithi na kuweza kujibu maswali ya hadithi hiyo kwa usahihi kulingana
na muktadha wa hadithi hiyo.
166
VI. Majibu
Maswali ya hadithi, ukurasa 130
1. Watu wa zamani walikula vyakula vya kuongeza nguvu mwilini.
2. Babu hakupata magonjwa.
3. Wao waliikausha nyama na kuihifadhi.
4. Vyakula vinavyopikwa kwa mafuta mengi huleta madhara mwilini.
5. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Babu anaonya tusikule
vyakula vilivyopikwa kwa mafuta mengi, tusikule sukari nyingi,
tusikule chumvi nyingi, tusikule vyakula vya jokofu n.k.
Mada Ndogo 4: Saru Matumizi ya ‘hiki’ na ‘hivi’
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua matumizi ya hiki na hivi katika kuimarisha mawasiliano;
b) Kutumia hiki na hivi katika sentensi katika kuimarisha mawasiliano;
ch) Kusoma vifungu vinavyojumuisha hiki na hivi katika kuimarisha ya kusoma;
d) Kuandika vifungu vinavyojumuisha hiki na hivi katika kuimarisha stadi ya
uandishi;
e) Kuchangamkia matumizi ya hiki na hivi katika mawasiliano.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi asome vifungu vinavyojumuisha hiki na hivi kama vile: Kitabu
hiki Vitabu hivi; Kifutio hiki Vifutio hivi.
Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwenye vifungu au sentensi
zinazojumuisha hiki na hivi.
Mwanafunzi aonyeshe vitu mbalimbali kama vile vyakula ili kuvitungia
sentensi katika vikundi k.m. chakula hiki vyakula hivi.
167
Mwanafunzi aweza kupewa vifungu vyenye mapengo wakamilishe kwa
kutumia hiki na hivi wakiwa wawili wawili k.m. chakula _________ (hiki),
vyakula _________ (hivi).
III. Nyenzo:
Chati zenye sentensi zilizojumuisha matumizi ya hiki na hivi;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 131;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Kama tunavyofahamu, sarufi ni kipengele muhimu katika ujifundishaji wa
wanafunzi. Mwalimu anastahili kutilia maanani dhana hii ili kuweza kuwahusisha
wanafunzi kwa ukamilifu katika somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema
na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi. Wanafunzi wenyewe watumiwe sana katika
funzo hili la kuonyesha matumizi ya hiki na hivi.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa
maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha
kama wanafunzi wengine. Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia,
mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya lugha ya ishara. Mwalimu anaweza
pia kumshirikisha mtaalamu wa lugha ya ishara katika kuwasaidia wanafunzi
wa aina hii.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba amewagawa wanafunzi katika makundi yanayotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi katika vitabu vya
wanafunzi.
168
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu awasalimie wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu salamu za
mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
awashirikishe katika kutazama michoro waliyopewa katika vitabu vyao pamoja
na kusoma sentensi kuhusu matumizi ya hiki na hivi zilizoambatanishwa na
michoro husika. Mwalimu atathmini majadiliano ya wanafunzi katika makundi
yao. Shughuli hii itawawezesha wanafunzi kufahamu matumizi ya hiki na hivi.
Wanafunzi wataje katika makundi yao vyakula ambavyo vinaweza kuashiriwa
kwa kutumia hiki na hivi k.m. kipande hiki cha mkate vipande hivi vya mikate;
kiazi hiki viazi hivi n.k.
Katika hatua hii ya wanafunzi kujadiliana na kutunga sentensi kwa kutumia hiki
na hivi, wanafunzi watapata fursa ya kujifundisha kuhusu matumizi ya hiki na
hivi katika mawasiliano.
Wanafunzi waelekezwe kutambua kuwa hiki na hivi ni viashiria au vionyeshi.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi waliyopewa
katika vitabu vyao. Mwalimu awasaidie wanafunzi wanaotatizika katika kufanya
mazoezi haya.
ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa kwa kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana
kwa kutumia hiki na hivi. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza
kutunga sentensi sahihi kwa kutumia hiki na hivi.
169
VI. Majibu
Zoezi la kusoma, ukurasa 132
Mwalimu atathmini usomaji na majadiliano ya wanafunzi.
Zoezi, ukurasa 133
1. Mama anapenda kisu hiki.
2. Chota maji ya kisima hiki.
3. Kiti hiki ni changu.
4. Naomba kitabu hiki kizuri.
5. Vichwa hivi vimeoshwa.
6. Vitanda hivi ni vikubwa.
170
Matokeo maalum yanayotarajiwa Mapendekezo ya shughuli za
ujifunzaji
Kukia mwisho wa mada, mwanafunzi
aweze:
(a) Kuwatambua wanyama wa
nyumbani kwa majina ili kujenga
stadi ya kuzungumza;
(b) Kumtambua mnyama ampendaye
ili kujenga stadi ya kuzungumza;
(ch) Kusikiliza hadithi ya mwalimu ili
kujenga usikivu;
(d) Kutambua matumizi ya hili na
haya ili kuimarisha mawasiliano.
Mwanafunzi awatambue wanyama
wa nyumbani kama vile ng’ombe,
mbuzi, kondoo, ngamia na punda
kwa majina yao kwa kutumia picha,
michoro na wanyama halisi.
Mwanafunzi atambue mnyama
ampendaye kupitia kwa maswali na
majibu.
Mwanafunzi ajadili picha
zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Wanafunzi wasome vifungu vyenye
matumizi ya hili na haya kama
vile: embe hili maembe haya;
dawati hili madawati haya; jani hili
majani haya.
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kushiriki katika vyama vya ushirika wa wanafunzi.
Kazi ya vikundi.
Uhusiano na masomo mengine:
Somo la Mazingira na somo la Kiingereza.
Mada Kuu 8: Mnyama Nimpendaye
Idadi ya vipindi: 11
Sura ya
8
171
Nyenzo:
Rekodi za masimulizi bunifu mbalimbali;
Wanyama halisi;
Michoro au picha za wanyama mbalimbali;
Rekodi za hadithi bunifu mbalimbali;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 134;
Chombo cha kunasia sauti na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia
wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalum na wenye ulemavu.
Maelezo kwa mwalimu
Mada hii inashughulikia aina mbalimbali za wanyama ambao hupendwa na
watu pamoja na masimulizi na hadithi kuhusu wanyama wanaopendwa na
watu. Pia, kipengele cha sarufi kuhusu matumizi ya hili na haya kitaangaziwa
katika mada hii.
Mada hii inalenga kumsaidia mwanafunzi kujenga stadi yake ya kusikiliza,
kufahamu aina mbalimbali za wanyama wanaopendwa pamoja na kusoma
hadithi kwa ufasaha. Hadithi za kuvutia na zenye msamiati wa kiwango cha
wanafunzi wa gredi hii zibuniwe ili kuwafaa wanafunzi katika ujifundishaji wao.
Uhusiano na masuala mtambuko
Masuala mtambuko ambayo yatashughulikiwa katika mada hii ni:
Elimu ya maendeleo endelevu: masilahi ya wanyama kujali na kutunza
mnyama,
Utangamano wa kijamii,
Amani na maadili.
Msamiati maalum
Msamiati maalum na muhimu ambao wanafunzi watapatana nao katika mada
hii ni kuhusu wanyama wanaopendwa ni kama vile:
172
Msamiati Maana
1.
ng’ombe
mnyama wa kufugwa atupatiaye nyama, maziwa, ngozi
n.k
2.
farasi
mnyama mwenye mkia wa singa
3.
mbwa
mnyama anayebweka wa nyumbani
4.
paka
mnyama wa jamii ya chui alaye panya
5.
mbuzi
mnyama wa nyumbani mfano wa swara mwenye pembe
Ushirikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali
Ili kuweza kuwashirikisha wanafunzi walio na ulemavu na matatizo mbalimbali,
mwalimu awe na vifaa maalum vya kuwasaidia wanafunzi hawa katika
ujifundishaji wao. Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kuona, mwalimu anaweza
kuhusisha matumizi ya breli pamoja na vifaa vya kunasia sauti.
Kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kusikia, mwalimu anaweza kuhusisha
matumizi ya lugha ya ishara. Pia, mwalimu anaweza kuwahusisha watafsiri wa
lugha ya ishara. Haya yatawawezesha wanafunzi hawa kusoma kama wanafunzi
wenzao bila vikwazo vyovyote.
Orodha ya mada na vipindi
Mada
Idadi ya vipindi
Mada Ndogo 1: Msamiati
3
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
2
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi
4
Mada Ndogo 4: Sarufi: Matumizi ya hili na haya
2
JUMLA: 11
Mada Ndogo 1: Msamiati
(Idadi ya vipindi: 3)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kuwatambua wanyama wa nyumbani kwa majina yao ili kujenga stadi ya
kuzungumza;
173
b) Kueleza maana ya msamiati unaotumiwa katika kutunza wanyama ili
kuimarisha mawasiliano;
ch) Kutumia majina ya wanyama katika sentensi ili kuimarisha mawasiliano;
d) Kutumia msamiati unaotumiwa katika kutunza wanyama katika sentensi ili
kujenga mapenzi ya kuwatunza wanyama wa nyumbani;
e) Kuthamini umuhimu wa kuwatunza wanyama wa nyumbani.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi awatambue wanyama wa nyumbani kama vile ng’ombe,
mbuzi, kondoo, ngamia na punda kwa majina yao kwa kutumia picha,
michoro na wanyama halisi.
Mwanafunzi atunge sentensi sahihi akitumia msamiati wa utunzaji wa
wanyama kama vile lishe, zizi n.k.
Mwanafunzi aeleze msamiati unaotumiwa katika kutunza wanyama.
Mwanafunzi achore baadhi ya wanyama na kuandika majina yao.
Mwanafunzi aweza kuonyeshwa video ya utunzaji wa wanyama.
Mwanafunzi aweza kutazama michoro na picha za wanyama wa nyumbani
na wanyama wakitunzwa.
III. Nyenzo:
Kadi zenye majina ya wanyama wa nyumbani;
Michoro au picha za wanyama wa nyumbani;
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 135;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Ni muhimu kwa kila mtu kufahamu kuhusu wanyama wa nyumbani pamoja na
jinsi ya kuwatunza na kuwapa ‘haki zao’.
Mwalimu aandae vifaa vyake mapema na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi kama
vilivyotajwa hapo juu. Wakati wa kuendesha funzo hili, mwalimu atambue wakati
mwafaka wa kuweka hadharani vifaa alivyovileta darasani kwa kukumbuka
174
kuwa matumizi ya michoro, picha na kadi ni mbinu bora ambayo hutumika
kufanikisha ufundishaji wa wanafunzi.
Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia wavionyeshe vifaa vilivyopo
kwa kuvigusa huku wakiandika maelezo yake ubaoni. Ikiwa kuna wanafunzi
wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa maelezo yake kwenye
breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha kama wanafunzi
wengine.
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba wanafunzi wamejigawa katika makundi ya wanafunzi wanaotakikana
kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwenye vitabu vyao.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu awaamkue wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu maamkuzi ya
mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awachangamshe wanafunzi kwa kuwauliza maswali mepesi kuhusu
wanyama wa nyumbani ambao wanawafahamu na wamewahi kuwaona kwa
macho yao wenyewe. Wanafunzi wataje majina ya wanyama hao. Mwalimu
ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii. Hii itakuwa
namna nzuri ya kutanguliza funzo hili kuhusu wanyama wa nyumbani.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wanne wanne kisha
awaelekeze kutazama michoro iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 135.
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali mepesi kuhusiana na michoro iliyopo.
Maswali kama vile: Unaona nini? Hawa ni wanyama gani? Wanafunzi wajibu
maswali ya mwalimu kulingana na wanayoyaona kwenye michoro waliyopewa.
Wanafunzi wapewe muda katika makundi yao wa kujadiliana kuhusu michoro
waliyopewa na wanyama wanaowaona.
Kabla ya somo hili, mwalimu awe ametayarisha kadi za majina ya wanyama
mbalimbali wa nyumbani ambazo atawaonyesha wanafunzi nao watatamka
175
kwa sauti majina hayo. Shughuli hii itawasaidia wanafunzi kufahamu majina
kadhaa ya wanyama wa nyumbani.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awe ameandaa mapema video kuhusu
wanyama wa kufugwa ambayo anaweza kuwaonyesha wanafunzi darasani.
Wanafunzi wachangamke na kutazama video hiyo kwa makini ili kupata ujumbe
uliokusudiwa.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika makundi kutaja na kueleza
kuhusu mnyama wanaompenda. Mwalimu atathmini majadiliano ya wanafunzi
katika makundi yao.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu ahitimishe funzo kwa kuwauliza wanafunzi maswali
tofauti kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha. Maswali haya yatilie mkazo
uwezo wa wanafunzi wa kufahamu majina ya wanyama wa nyumbani.
VI. Majibu
Maswali, ukurasa 135
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
Maswali, ukurasa 136
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Kwa mfano:
1. Ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda, mbwa, paka n.k.
2. Simba, ndovu, nyani, fisi n.k.
3. Mwalimu atathmini michoro ya wanafunzi.
176
Mada Ndogo 2: Kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi
(Idadi ya vipindi: 2)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kumtambua mnyama ampendaye ili kujenga stadi ya kuzungumza;
b) Kusimulia kuhusu mnyama ampendaye ili kujenga stadi ya kuzungumza;
ch) Kusikiliza masimulizi kuhusu utunzaji wa wanyama ili kujenga usikivu;
d) Kuthamini wanyama ili kushiriki katika kuwatunza.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi atambue mnyama ampendaye kupitia kwa maswali na majibu.
Mwanafunzi asimulie kuhusu mnyama ampendaye katika darasa, wakiwa
wawili wawili na katika vikundi.
Mwanafunzi aweza kusimuliwa jinsi ya kutunza wanyama kupitia kwa
mgeni mwalikwa.
Mwanafunzi aweza kuwatambua wanyama wa nyumbani kwa kutumia
michoro na picha halisi.
Mwanafunzi aweza kuonyeshwa video inayohusu utunzaji wa wanyama
mbalimbali.
Mwanafunzi aweza kushiriki katika mjadala kuhusu jinsi wanavyowatunza
wanyama wawapendao.
III. Nyenzo:
Rekodi za masimulizi bunifu mbalimbali kuhusu wanyama wa nyumbani;
Michoro au picha za wanyama wa nyumbani;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Mgeni mwalikwa (daktari wa mifugo);
Wanafunzi wenyewe;
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 136;
177
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linawashirikisha wanafunzi kusomewa na kusikiliza masimulizi
bunifu yanayohusu wanyama wa nyumbani ili kujenga stadi yao ya kusikiliza
na kuzungumza. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa vinavyohitajika
kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake kama vilivyotajwa
hapo juu. Mwalimu anaweza kumwalika mgeni kama vile daktari wa mifugo
akawaeleza wanafunzi kuhusu njia mbalimbali za kuwatunza wanyama wetu.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mepesi kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi
wajibu salamu za mwalimu pamoja na maswali waliyoulizwa.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kusahihisha zoezi walilopewa katika
kipindi cha hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika zoezi hili wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi katika kujenga stadi
yao ya kusikiliza masimulizi bunifu pamoja na stadi ya kuzungumza kupitia
kwa wao wenyewe kuwasimulia wenzao. Masimulizi haya yatahusu kuwatunza
wanyama wa nyumbani.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika darasa zima kujadili kuhusu wanyama
wawapendao. Kila mwanafunzi apewe fursa ya kusimama mbele ya wanafunzi
wengine na kueleza kuhusu wanyama wanaopenda pamoja na sababu za
kuwapenda wanyama hao.
178
Shughuli hii itawasaidia wanafunzi kukuza ujasiri wao wa kusimama na
kuzungumza mbele ya watu.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya
wanafunzi watatu watatu kisha wachunguze michoro ya wanyama waliyopewa
katika vitabu vyao. Wanafunzi wawatambue wanyama hao pamoja na majina
yao.
Mwalimu ahakikishe anawashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii.
Wanafunzi wajibu maswali waliyopewa kwenye kitabu chao kuhusu michoro
waliyopewa.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi hadithi bunifu ifuatayo
inayohusu mnyama nimpendaye. Ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza
kwa makini. Pia, mwalimu ahakikishe kuwa anasoma kwa ufasaha, kwa
matamshi sahihi na kwa sauti ya kusikika na ya kuvutia. Iwapo mwalimu ana
matatizo ya kimatamshi, anaweza kumwalika msomaji stadi atakayewasomea
au kuwasimulia wanafunzi hadithi kuhusu mnyama nimpendaye.
Mfano wa hadithi
MBWA
Mbwa ni mnyama wa nyumbani. Mbwa ana manyoya kwenye ngozi yake.
Yeye hula ugali na mifupa. Mbwa humlinda binadamu. Akichafuka, yeye huoshwa
kwa maji safi yenye dawa. Dawa ya kuosha mbwa huua viroboto. Viroboto hukaa
kwenye ngozi na manyoya yake. Mbwa pia hupewa dawa. Dawa ya mbwa
humfanya awe na afya nzuri. Ni vizuri kumtunza mbwa.
Baada ya kusomewa hadithi, wanafunzi wajaribu katika makundi yao kuelezana
kuhusu hadithi waliyoisikia. Watoe muhtasari wa hadithi hiyo katika makundi
yao. Wanafunzi waelezane kuhusu mnyama wa nyumbani aliyetajwa katika
masimulizi waliyosomewa na mwalimu wao. Baadaye, mwalimu awashirikishe
katika kujibu maswali ya masimulizi waliyopewa. Mwalimu ahakikishe
anawasaidia wanafunzi wanaotatizika katika makundi yao.
179
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma masimulizi bunifu
pamoja na kufahamu wanyama mbalimbali wa nyumbani.
Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wameweza kupata maarifa ya kujibu
kwa usahihi maswali ya masimulizi.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi wote katika kufanya mazoezi yaliyo katika
vitabu vyao.
VI. Majibu
Maswali ya masimulizi, ukurasa 136
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi kuhusu wanyama wawapendao.
Zoezi la kusikiliza, ukurasa 137
Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi.
180
Mada Ndogo 3: Kusoma: Hadithi
(Idadi ya vipindi: 4)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
a) Kusikiliza hadithi ya mwalimu ili kujenga usikivu;
b) Kusoma hadithi kwa mtiririko ufaao ili kuimarisha usomaji;
ch) Kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa ili kuelewa ujumbe;
d) Kupenda kusoma hadithi kuhusu wanyama wa nyumbani ili kuendeleza
usomaji.
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
Mwanafunzi asikilize mwalimu anaposoma hadithi, asome pamoja na
mwalimu kisha asome peke yake, wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kupitia kwa kinasasauti.
Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma na kusomewa
hadithi.
Mwanafunzi aweza kutazama video ya mtu au mtoto akisoma hadithi
husika kwa ufasaha kisha aige usomi huo.
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kuhusu hadithi aliyosoma na
kusomewa.
Mwanafunzi aweza kusimulia hadithi kutokana na picha kuhusu wanyama
wa nyumbani.
III. Nyenzo:
Michoro au picha za hadithi bunifu mbalimbali;
Vifaa vya teknolojia kama vile: tarakilishi, simu;
Wanafunzi wenyewe;
181
Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 138;
Chombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Somo hili linahusu kusoma hadithi bunifu ili kujenga stadi ya wanafunzi
ya kusikiliza na kusoma. Mwalimu ahakikishe kwamba ameleta vifaa
vinavyohitajika kufundishia funzo hili ili kufanikisha ufundishaji wake. Mwalimu
anaweza kutumia michoro au picha za hadithi bunifu ambazo atawasomea
wanafunzi darasani na nyingine watajisomea wenyewe. Mwalimu anaweza hata
kumwalika mtambaji au msomaji mashuhuri akawasomea wanafunzi hadithi
bunifu kisha wanafunzi wakasoma baada yake. Mwalikwa huyu sharti awe na
uwezo wa kusoma kwa sauti ya kusikika na kwa matamshi sahihi.
Ili kufanikisha funzo hili, mwalimu ahakikishe amewagawa wanafunzi katika
makundi ya wanafunzi yanayotakikana kulingana na shughuli ya kila zoezi
husika.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu atangulize sehemu hii kwa kuwasalimia wanafunzi na kuwauliza
maswali mbalimbali kuhusu waliyosoma katika kipindi kilichotangulia kuhusu
wanyama wawapendao. Wanafunzi wajibu salamu za mwalimu pamoja na
maswali waliyoulizwa. Mwalimu awashirikishe wanafunzi wasahihishe zoezi
walilopewa katika funzo la hapo awali. Wanafunzi wenye matatizo katika
ujifundishaji wao wasaidiwe.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Katika hatua hii, mwalimu alenge kuwaelekeza wanafunzi kujenga stadi yao
ya kusikiliza pamoja na kusoma hadithi bunifu. Mwalimu awagawe wanafunzi
katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha awaombe watazame michoro
iliyo katika Kitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 136 - 140. Wanafunzi wachunguze
michoro hiyo ya wanyama wa nyumbani na kuijadili katika makundi yao.
Mwalimu awaelekeze katika kusoma vifungu vifupi walivyopewa baada ya kila
mchoro wa mnyama wa nyumbani.
182
Wanafunzi wasome vifungu hivi wakiwa wawili wawili kisha kila mmoja asome
akiwa peke yake.
Hatimaye, mwalimu awaelekeze wanafunzi kuhusu namna ya kujibu maswali
waliyoulizwa. Mwalimu ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote katika
majadiliano haya. Wanafunzi wajibu maswali ya mwalimu kulingana na
wanayoona katika michoro ya wanyama waliyopewa.
Baada ya shughuli hii, mwalimu awasomee wanafunzi hadithi ifuatayo.
Ahakikishe wanafunzi wote wanamsikiliza kwa makini. Pia, mwalimu ahakikishe
kuwa anasoma hadithi hiyo kwa matamshi sahihi na sauti ya kusikika.
Mfano wa hadithi
Wanyama ni muhimu sana katika maisha yetu. Wanyama hutupa maziwa na
nyama. Wengine hutupa ngozi na mbolea. Wanyama hufugwa nyumbani. Kuna
wanyama wa porini pia. Mfano ni simba. Wanyama wa nyumbani ni: mbuzi,
ng’ombe, kondoo, punda na ngamia. Wanyama hawa wanakula nyasi. Ni muhimu
kuwatunza wanyama hawa.
Ili kuchunguza iwapo wanafunzi walisikiliza hadithi ya mwalimu kwa makini,
mwalimu awashirikishe katika kujibu maswali waliyopewa katika vitabu vyao.
Mwalimu azunguke darasani ili kuwasaidia wanafunzi wanaotatizika katika
makundi yao.
ch) Tathmini
Katika hatua hii, mwalimu awaulize wanafunzi maswali mbalimbali ya
kuchunguza iwapo wamepata ujuzi wa kusikiliza na kusoma hadithi bunifu. Pia,
mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wamepata ufahamu wa kusoma hadithi
na kuweza kujibu maswali ya hadithi hiyo kwa usahihi kulingana na muktadha
wa hadithi hiyo.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi yaliyo katika vitabu
vyao.
183
VI. Majibu
Maswali ya makundi, ukurasa 140
1. Mnyama anayefugwa katika mahali kame ni ngamia.
2. Mnyama aliye na manyoya mengi sana ni kondoo.
3. Mnyama wa kurusha mateke ni punda.
4. Ng’ombe hutupatia maziwa, nyama na ngozi.
5. Mbuzi ana mkia mfupi.
Maswali ya hadithi, ukurasa 141
1. Mbuzi, ng’ombe, kondoo, punda na ngamia
2. Simba
3. Mwalimu atathmini majibu ya wanafunzi. Kwa mfano, kuna wanyama
ambao hutupatia maziwa na nyama, wengine hutupatia ngozi n.k.
Mada Ndogo 4: Saru: Matumizi ya ‘hili ’ na ‘haya
(Idadi ya vipindi: 4)
I. Matokeo maalum yanayotarajiwa:
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:
a) Kutambua matumizi ya hili na haya ili kuimarisha mawasiliano;
b) Kutumia hili na haya katika sentensi sahili ili kuimarisha mawasiliano;
ch) Kusoma vifungu vinavyojumuisha matumizi ya hili na haya ili kujenga
usomaji;
d) Kuandika vifungu vinavyojumuisha matumizi ya hili na haya ili kuimarisha
uandishi bora;
e) Kuchangamkia matumizi ya hili na haya katika mawasiliano.
184
II. Mapendekezo ya shughuli za ujifunzaji
Wanafunzi wasome vifungu vyenye matumizi ya hili na haya kama vile:
embe hili maembe haya; dawati hili madawati haya; jani hili majani
haya.
Wanafunzi waweza kujaza mapengo kwa kutumia hili na haya.
Mwanafunzi aonyeshwe vitu mbalimbali kama vile tunda kwa kurejelea
hili na haya kwa mfano: tunda hili matunda haya; embe hili maembe
haya n.k.
Wanafunzi waweza kukamilisha mafungu yanayohusu matumizi ya hili na
haya wakiwa wawili wawili k.m. tunda ____(hili), matunda ____ (haya).
Mwanafunzi aweza kufanya mazoezi mbalimbali katika tarakilishi kuhusu
mada.
III. Nyenzo:
ØChati zenye sentensi zilizojumuisha matumizi ya hili na haya;
ØWanafunzi wenyewe;
ØKitabu cha Mwanafunzi, ukurasa 141;
ØChombo cha kunasia sauti, breli pamoja na vifaa vingine vinavyoweza
kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji uangalifu maalumu (kwa mfano,
wanafunzi wasioweza kuona, kusikia n.k.).
IV. Maandalizi ya somo
Kama tunavyofahamu, sarufi ni kipengele muhimu katika ujifundishaji wa
wanafunzi. Mwalimu anastahili kutilia maanani dhana hii ili kuweza kuwahusisha
wanafunzi kwa ukamilifu katika somo hili. Mwalimu aandae vifaa vyake mapema
na kuvihifadhi kabla ya vipindi hivi.
Ikiwa kuna wanafunzi wasioweza kuona, ni lazima mwalimu ajitahidi kuandaa
maelezo yake kwenye breli ili kuwawezesha wanafunzi wa aina hii kujifundisha
kama wanafunzi wengine. Iwapo kuna wanafunzi walio na matatizo ya kusikia
mwalimu anaweza kuhusisha matumizi ya lugha ya ishara. Mwalimu anaweza
pia kumshirikisha mtaalamu wa lugha ya ishara katika kuwasaidia wanafunzi
wa aina hii.
185
Ili kutimiza malengo yake katika somo hili, ni vyema mwalimu ahakikishe
kwamba amewagawa wanafunzi katika makundi yanayotakikana kulingana
na maelekezo yaliyotolewa kwa kila shughuli ya wanafunzi katika vitabu vya
wanafunzi.
V. Utaratibu wa somo
a) Utangulizi
Mwalimu awasalimie wanafunzi na kuwauliza maswali mepesi kuhusu
waliyofundishwa katika kipindi kilichotangulia. Wanafunzi wajibu salamu za
mwalimu kisha wajibu maswali waliyoulizwa.
b) Uwasilishaji wa funzo lenyewe
Mwalimu awagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi wawili wawili
kisha awashirikishe katika kutazama michoro waliyopewa pamoja na kusoma
sentensi walizopewa katika vitabu vyao kuhusu matumizi ya hili na haya.
Mwalimu atathmini majadiliano ya wanafunzi katika makundi yao. Shughuli hii
itawawezesha wanafunzi kufahamu matumizi ya hili na haya.
Katika hatua hii ya wanafunzi kujadiliana kuhusu matumizi ya hili na haya,
wanafunzi watapata fursa ya kujifundisha zaidi kuhusu majina ambayo hutumiwa
pamoja na hili na haya, kwa mfano: embe, dawati, dirisha, tunda n.k.
Mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kutunga sentensi sahihi kwa kutumia
hili na haya, kwa mfano:
1. Embe hili limeiva. Maembe haya yameiva.
2. Tunda hili ni la mtoto. Matunda haya ni ya watoto.
3. Dawati hili ni langu. Madawati haya ni yetu.
Wanafunzi waelekezwe kutambua kuwa hili na haya ni viashiria au vionyeshi.
Mwalimu ahakikishe amewashirikisha wanafunzi wote katika shughuli hii ya
kutunga sentensi sahihi kwa kutumia hili na haya.
Hatimaye, mwalimu awashirikishe wanafunzi katika kufanya mazoezi waliyopewa
katika vitabu vyao. Mwalimu awasaidie wanafunzi wanaotatizika katika kufanya
mazoezi haya.
186
ch) Tathmini
Katika hatua hii ya mwisho wa funzo hili, mwalimu ahitimishe somo kwa
kuwauliza wanafunzi maswali kadhaa kuhusu mambo muhimu waliyojifundisha.
Maswali hayo yaegemee haswa katika kuchunguza ikiwa wanaweza kuwasiliana
kwa kutumia hili na haya. Pia, mwalimu achunguze iwapo wanafunzi wanaweza
kutunga sentensi sahihi kwa kutumia hili na haya.
VI. Majibu
Zoezi la kusoma, ukurasa 143
Mwalimu atathmini matamshi ya wanafunzi.
Zoezi, ukurasa 143
1. Darasa hili ni letu.
2. Meno haya yanauma.
3. Masikio haya yameumia.
4. Tunda hili lilioshwa.
5. Tumbo hili linauma.