
95
mbalimbali ambazo zina tamaduni mbalimbali zenye utajiri mkubwa ambao
unakuwa kivutio kikubwa. Ikiwa pato linalotokana na sekta hii ya utalii
litatumiwa vyema, upo uwezekano wa nchi zinazohusika kupiga maendeleo
makubwa ya kiuchumi.
Kiwango cha kukua kwa sekta ya utalii miongoni mwa nchi zinazoendelea
kinatazamiwa kukua kwa asilimia tano kwa mwaka hadi kukia mwaka wa
2020. Hali hii inaonyesha kuwa dalili za kuboreka kwa sekta hii siku za usoni
ni nzuri. Ili kuhakikisha kuwa sekta hii inaendelea kuwa kivutio kikubwa
cha pato la nchi, pana umuhimu wa mataifa yanayohusika kuhakikisha
kuwa yanaimarisha sekta hiyo. Uimarishaji huo ni kwa kupanua soko la
utalii kwa kuwahimiza wananchi wenyewe kutembelea sehemu mbalimbali,
yaani kuhimiza utalii wa ndani kwa ndani. Njia nyingine ni kuboresha
muundo msingi kama barabara, mahoteli na maeneo yanayopendwa na
watalii wenyewe ili kuwavuta wengine zaidi. Pana haja pia ya kuhakikisha
usalama umedumishwa katika maeneo yanayotembelewa na watalii. Sekta
hii haitafanikiwa vyema pasipokuwa na juhudi za kuitangaza nchi na vivutio
vyake vya utalii ili kuwavuta watalii wengi.
Fedha zinazotokana na sekta ya utalii zinaweza kutumiwa kwa
maarubu mbalimbali. Kwa mfano, fedha za kigeni zinazopatikana zinaweza
kusaidia kupunguza mzigo wa madeni ambao unazirudisha nyuma nchi
nyingi. Fedha hizi huweza pia kutumiwa kulipia bidhaa ambazo huagizwa
kutoka nje na ambazo kwa kawaida hulipiwa kwa fedha za kigeni. Tatu,
fedha hizi huweza kutumiwa kuimarisha muundo msingi wa ndani katika
nchi inayohusika ili kuhakikisha kuwa baadhi ya matatizo kama uhaba wa
barabara za kutegemewa yameondolewa. Aidha, hutumiwa kuboresha na
kuimarisha huduma za jamii katika nyanja mbalimbali kama elimu na afya
ambazo ni muhimu kama nguzo ya taifa lolote lile.
Kati ya nchi 49 zinazojulikana kama maskini sana, nyingi ziko barani
Afrika na utalii ni moja kati ya sekta muhimu zinazoziingizia fedha za kigeni.
Licha ya faida za utalii ambazo tumeziona hapo juu, kuna matatizo
kadha yanayoweza kuhusishwa na sekta hii ya utalii. Kwa mfano, miongoni
mwa nchi nyingi zinazoendelea, sehemu kubwa ya biashara ya utalii
imetawaliwa na makampuni na waendeshaji wa nje. Kwa mfano, hoteli nyingi
na mashirika yanayohusiana na utalii humilikiwa na wawekezaji wa nje, hali
ambayo inazinyima serikali na nchi zinazohusika kipato fulani. Pili, kutokana
na kutokuwepo kwa mipango mizuri, sekta hii ya utalii haiunganishwi vizuri
na sekta nyingine kama uvuvi, kilimo, viwanda, utamaduni na burudani hali
ambayo ingeweza kuipanua sekta yenyewe.
Isitoshe, kuibuka, siku hizi, kwa milolongo ya mahoteli ya kimataifa,
usarishaji wa watalii kwa njia za barabara na usari wa anga kunatishia
na kwa kiasi kikubwa hata kuondolea mbali uwezo wa hoteli ndogo na
makampuni ya wazalendo kushiriki katika biashara hii. Hoteli hizo ndogo,
kwa mfano, hazina uwezo wa kuumudu ushindani mkubwa kutoka kwa
hoteli hizo kubwa.
Katika sehemu iliyotangulia tumeona faida zinazotokana na utalii na
mchango wake katika kukua kwa uchumi. Je, kwa upande ule mwingine,