
32
Kamusi yangu
amani: hali ya utulivu bila vita
bendera: kitambaa chenye rangi au alama
inayowakilisha nchi
gwaride: sehemu wanakosimama wanafunzi
na penye mlingoti wa bendera ili
kuhutubiwa na walimu
flamingo:ndege mwenye miguu mirefu
myekundu, shingo ndefu na mwili
mweupe wenye wekundu kiasi,
hupatikana kwenye ziwa
kandanda: mchezo wa mpira wa miguu
mbuga: mahali ambapo wanyama wa mwitu
hutunzwa
mlingoti:kipande cha mti au chuma
kilichosimamishwa ardhini ili kushika
bendera
mwanariadha: mtu anayecheza michezo ya
riadha kama kukimbia au kuogelea
riadha: mchezo wa mazoezi kama kukimbia,
kuruka na kuogelea
simama wima: simama sawasawa bila kujipinda
talanta: uwezo wa kufanya jambo fulani
vizuri
tarakilishi: mashine ya elektroniki