
91
Ndoto yake Roda ilikuwa imetimia! Ama
kweli Mungu akikupa kilema hukupa na
mwendo wake. Ndugu yangu Sambo naye
alikuwa mwalimu mkuu katika shule ya upili
ya Ziwani ambayo ilikuwa hatua chache kutoka
nyumbani kwetu. Kila mmoja wetu alikuwa
amejiwekezea mali si haba. Awali safu za majengo
ya misonge zilikuwa zimekitawala kijiji chetu
ndani na nje. Kwa sasa kuliona jengo la msonge
kwenye vijiji vya Mabatini na Tupe ingalikuwa
ni sawa na kuiona barafu ya kukaangwa! Vifo
vilikuwa vimepunguka kwa kiwango kikubwa
huku usalama nao ukidhibitiwa kikamilifu.
Wakati wa likizo, Roda na familia yake Bwana
Kilemba wangalirejea Mabatini kuiendeleza
miundombinu kuko huko. Barabara, majengo,
nguvu za nishati, mifumo ya mawasiliano
iliyohitajika katika uendeshaji wa kijamii na
kibiashara zilikuwa zimeimarishwa vilivyo.
Wazazi wetu waliishi maisha ya kitajiri.
Baiskeli hazikuonekana tena! Utajiri ulikuwa
umezipiga marufuku kote kijijini. Mashangingi